Kristo na Utamaduni wa Kidini
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unakumbuka mjadala wetu uliopita kuhusu sheria ya asili, sheria ya maadili, sheria ya madai na sheria ya mapokeo? Nadharia tunayoifanyia kazi ni kwamba kila sheria (sheria ya asili ikiwa ya kwanza) inalenga kusaidia au kuelezea kiwango cha juu cha sheria. Hata hivyo, tunafahamu kwamba jambo hili halidhoofishi kile tunachokishuhudia maishani. Baadhi ya sheria za madai zinakinzana kwa wazi kabisa na sheria ya asili. Wanadamu wanabadili mawazo yao wenyewe dhidi ya mawazo ya Mungu. Tunaona mitafaruku inayofuatia baada ya hapo. Je, tunakabilianaje na kushindwa kwa watunga sheria za kibinadamu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Kujaza Nafasi ya Musa
- Soma Mathayo 23:1-2. Je, Yesu anamaanisha nini kwa kusema “kiti cha Musa?” Je, Musa alikuwa ameukalia ufalme na bado walikuwa na ufalme? (Hapana. Yesu alikuwa kiongozi wa kidini na kisiasa kwa watu wa Mungu. Walimu wa sheria na Mafarisayo walikuwa na nafasi kama ya Musa katika kipindi cha Yesu.)
- Soma Mathayo 23:3-4. Je, viongozi wa kipindi hiki wanastahili heshima/cheo? (Hapana!)
- Je, wana tatizo gani? (Matendo yao hayaendani na maneno yao.)
- Sote tunafahamu kwa nini ni vizuri kufuata mafundisho sahihi hata kama mwalimu atashindwa kuyazingatia mafundisho yake mwenyewe. Lakini je, kwa nini Yesu anawaambia wanafunzi “watii” suala hili linalohusisha “mizigo mizito?” Mizigo ambayo katika muktadha huo inaonekana kutokuwa ya haki?
- Soma Mathayo 15:1-2. Je, mashtaka gani yanaletwa dhidi ya wanafunzi? (Hawabebi “mzigo mzito” wa utamaduni wa wazee.)
- Soma Mathayo 15:3-6. Je, unaelezeaje jibu la Yesu? Mtu anapokuambia kuwa unatenda jambo baya, je, unajibu kuwa, “Wewe pia unatenda mambo mabaya!”
- Je, hicho ndicho anachokifanya Yesu hapa – wewe pia ni mvunja sheria? (Hapana. Tunapokiangalia kwa undani zaidi kile kilichosemwa, tunaona kwamba viongozi wa dini wanatoa hoja za utamaduni wao. Yesu anasema utamaduni wao unakiuka sheria ya Mungu.)
- Rejea mjadala wetu wa juma lililopita. Je, sheria za mapokeo zilipaswa kufanya nini? (Zilitakiwa kutusaidia kuelewa mpango wa Mungu wa wokovu. Zilipaswa kutusaidia kuepuka kukiuka sheria za maadili na sheria za asili. Yesu anasema kuwa utamaduni huu unakinzana na malengo yake.)
- Soma Mathayo 15:10-11. Je, ingekuwa ni ukiukaji wa sheria ya Mungu kwa wanafunzi kunawa mikono yao? (Hapana, lakini ingewafanya watu wasiielewe sheria ya Mungu. Wangezingatia zaidi unawaji wa mikono na kubadili umakini wao kutoka kwenye tatizo halisi – kile kiwatokacho vinywani mwao. Je, unaweza kuona jinsi sheria zilizotungwa na wanadamu zinavyokiuka kinachopaswa kuwa malengo ya sheria hizo – ili kuendana na sheria ya maadili?)
- Je, hicho ndicho tunachopaswa kujifunza leo? Je, tunasisitiza mambo yasiyo ya msingi yanayotuzinga ili tusiyaangalie mambo ya msingi zaidi?
- Soma Mathayo 15:12. Je, tulijifunza nini katika somo la juma lililopita kuhusu kuwakwaza watu? (Soma Mathayo 17:27. Yesu alilipa kodi ya hekalu ili asiweze kuwakwaza.)
- Je, wanafunzi wanamkumbusha Yesu juu ya mafundisho yake mwenyewe?
- Soma Mathayo 15:13-14. Yesu anatuambia tufanye nini kuhusu mafundisho ya uongo ya dini? (Tuyaepuke. Tusiyafuate.)
- Soma tena Mathayo 23:2-4. Yesu hakujikanganya mwenyewe, kwa hiyo lazima tutafute suluhisho kwenye mzozo wa wazi katika suala la “kukwaza” na kufuata “kila kitu” kinachofundishwa na viongozi wa dini. Je, unapendekeza jambo gani? (Nadhani jambo hili linafanana na mjadala wetu wa sheria ya madai. Mungu ndiye mwanzilishi wa mamlaka na mipango ya madai, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anadhamiria kwamba tunapaswa kufuata sheria za wanadamu zinazokiuka sheria za asili au sheria za maadili. Kwa hiyo, ninamwelewa Yesu akisema kuwa tunapaswa kufuata mafundisho ya watu walioshika nafasi za mamlaka ya dini, tuepuke kuwakwaza kwa kadri inavyowezekana, lakini tunapaswa kukataa yale mambo yasiyoendana na sheria ya maadili. Hii inajumuisha mafundisho yasiyo na maadili ndani yake (kama vile kunawa mikono), lakini yanaondoa usikivu/umakini wetu kwenye mambo ya msingi.)
- Majivuno
- Soma Mathayo 23:5-7. Je, tatizo kubwa la wale wanaochukua nafasi ya Musa ni lipi? (Wamesahau kwamba wanawasilisha tu mapenzi ya Mungu kwa watu. Wanaanza kufikiri kwamba wanaweza kuwa kama Mungu. Wameanza “kujivuna [kuvimba vichwa].”)
- Soma Mwanzo 3:4-5. Je, Shetani ana orodha ya viwango vya majaribu anavyovitumia mara kwa mara?
- Soma Mathayo 23:8-10. Miaka ya nyuma mshiriki mmoja wa kanisa langu alikuwa akiniita “Rabi” na kitendo hicho kilinikumbusha fungu hili. Kwa kawaida wanafunzi wananiita “profesa,” wengi wananiita “mwalimu” na wanangu wananiita “baba.” Je, huu ni ukiukaji wa wazi wa fundisho la Yesu?
- Je, wanao wanakuitaje? (Linganisha na Kutoka 20:12.)
- Soma 1 Wakorintho 12:28. Je, Mungu anapingana na muundo na vyeo vya kanisa?
- Kama hivyo ndivyo, kwa nini wanafunzi walijiita (Matendo 15:23) “mitume?”
- Soma Mathayo 23:11-12. Je, Yesu anamaanisha nini? (Mamlaka ya kibinadamu yanatufanya tujivune. Katika uhusiano kati ya sheria ya asili, sheria ya maadili na sheria ya madai, ni upotovu wa sheria kuwafanya wale wanaowasilisha mapenzi ya Mungu dhidi ya mambo mengine yote. “Ninyi nyote ni ndugu.”)
- Unadhani Yesu alimaanisha kile alichokisema, kwamba maneno ya “Rabi, mwalimu na baba” hayapaswi kutumika? (Sidhani kama Yesu anasema kuwa hatuwezi kuwaita watu kutokana na wajibu wao maishani au kanisani. Je, “mtume,” na “nabii” yanakubalika, na “Rabi” na “baba” hayakubaliki? Je, jina “mwalimu” linatajwa kimakosa katika Mathayo 23, lakini ni sahihi katika 1 Wakorintho 12? Nadhani anachomaanisha Yesu ni kwamba tunapaswa kuepuka “heshima” – vyeo ambavyo ni zaidi ya maelezo ya kawaida ya kazi.)
- Je, unaweza kufikiria chochote kati ya hivyo? (Vipi kuhusu “Mheshimiwa Mchungaji/Padri” au “Mheshimiwa Sana Mchungaji/Padri?” Hivi havionekani kuwa vyeo vya kikazi, vinadhamiria kuwasilisha mambo mengi zaidi.)
- Je, Yesu anawataka wale walio kwenye nafasi za uongozi kufanya nini, wale wanaoangalia utekelezaji wa sheri? (Uongozi wa kuwatumikia watu – Mathayo 23:11.)
- Unadhani Yesu alimaanisha kile alichokisema, kwamba maneno ya “Rabi, mwalimu na baba” hayapaswi kutumika? (Sidhani kama Yesu anasema kuwa hatuwezi kuwaita watu kutokana na wajibu wao maishani au kanisani. Je, “mtume,” na “nabii” yanakubalika, na “Rabi” na “baba” hayakubaliki? Je, jina “mwalimu” linatajwa kimakosa katika Mathayo 23, lakini ni sahihi katika 1 Wakorintho 12? Nadhani anachomaanisha Yesu ni kwamba tunapaswa kuepuka “heshima” – vyeo ambavyo ni zaidi ya maelezo ya kawaida ya kazi.)
- Soma Mathayo 23:5-7. Je, tatizo kubwa la wale wanaochukua nafasi ya Musa ni lipi? (Wamesahau kwamba wanawasilisha tu mapenzi ya Mungu kwa watu. Wanaanza kufikiri kwamba wanaweza kuwa kama Mungu. Wameanza “kujivuna [kuvimba vichwa].”)
- Musa wa Kweli
- Soma Mathayo 5:17 na Wakolosai 2:9-12. Juma lililopita tulijifunza fungu hili katika Wakolosai na mtafaruku wa tohara. Je, hii inaendanaje na kile anachokisema Yesu katika Mathayo 5:17? (Huu ni mfano mzuri wa kile anachokisema Yesu. Alitimiza sheria ya tohara.)
- Soma Mathayo 5:18. Je, bado sheria inafanya kazi? (Unakumbuka mazungumzo yetu juu ya sheria ya asili na sheria ya maadili? Mungu anatupatia sheria ya maadili, kama ramani, ili kuepuka hatari ya kukiuka sheria ya asili. Sheria za asili hazipotei. Tunahitaji ramani yetu! Ramani yetu, kama neema, ni zawadi kutoka kwa Mungu.)
- Soma Mathayo 5:19. Je, Yesu anasema kuwa walimu wabaya watakwenda mbinguni? (Ndiyo. Neema inatuokoa, na sio kuwa walimu wazuri (wema) au watunza amri. Lakini, kuvunja amri za Mungu na kuwafundisha watu wengine kufanya hivyo ni upumbavu wa wazi usio na thawabu mbinguni.)
- Je, kuna mantiki gani katika jambo hili? (Anachokuambia mpumbavu kupuuzia ramani? Anachokuambia zuzu kukiuka sheria za asili? Mungu anatupatia sheria ya maadili ili kutuepusha na kutupatia uhuru!)
- Soma Mathayo 5:20. Je, tunatakiwa kuwazidi kiutendaji viongozi wa dini katika kipindi cha Yesu? Wale aliowaita (Mathayo 15:14) “viongozi vipofu wa vipofu!” (Ndiyo, na jukumu ni jepesi na lina mantiki. Ikiwa tunamkiri Yesu kama anayetuhesabia haki, basi tumezidi kuhesabiwa haki kwa mwanadamu yeyote yule. Kimantiki, tutayazingatia mambo makubwa na kukinzana na wale wanaotafuta kujikita kwenye mambo madogo yanayotuzinga dhidi ya mambo ya msingi.)
- Je, ni baadhi ya mambo gani basi yaliyo makubwa? (Soma Mathayo 15:17-20. Ulacho, usafi wa mikono yako, ni mambo madogo. Mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano ndio mambo makubwa.)
- Rafiki, wanadamu hufanya makosa kwenye sheria na kanuni zao. Je, utaikubali changamoto ya kuzingatia mambo ya muhimu?
- Juma lijalo: Kristo na Sheria Katika Mafundisho Pale Mlimani.