Somo la 2: Kristo na Sheria ya Musa
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Juma lililopita tulijadili sheria ya asili, sheria ya maadili, sheria ya madai, na sheria ya mapokeo. Ipi kati ya hizo ni “Sheria ya Musa?” Musa aliwapa watu wa Mungu sheria ya maadili na sheria ya mapokeo katika mfumo wa maandishi walipokuwa safariki kuelekea Kaanani. Hata hivyo, je, sheria hizo zilikuwepo kabla Moses hajaziandika? Je, sheria hizo bado zinatumika leo? Hebu tuzame kwenye Biblia zetu ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Kujitoa kwa Mungu
- Soma Luka 2:21. Jambo gani liliwatokea wana wazaliwa wachanga katika siku ya nane? (Walitahiriwa na kupewa jina.)
- Kwa nini? (Soma Mwanzo 17:12. Hii ilikuwa ni sehemu ya sheria.)
- Sheria ya nani? Je, towara iliwakilisha nini? (Soma Mwanzo 17:9-11. Hilo lilikuwa ni agizo la Mungu kwa Ibrahimu. Tendo hilo lilikuwa linawakilisha ukweli kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa na uhusiano maalum na Mungu. Hata hivyo, tunaona katika Mambo ya Walawi 12:3 na Yohana 7:22 kwamba baadaye jambo hili lilijumuishwa kama sehemu ya sheria ya Musa.)
- Katika Mwanzo 17:9-10, tohara inapewa jina la “agano” (mkataba) kati ya wanadamu na Mungu. Kwa nini tendo hili linafanyika siku ya nane, kabla mtoto hajawa na uwezo wa kuelewa kinachoendelea au ridhaa yake kwenye huu mkataba na Mungu?
- Soma Wagalatia 5:2-4 na Wagalatia 5:6. Utakumbuka kuwa juma lililopita tulijadili sheria ya asili, sheria ya madai, sheria ya maadili na sheria ya mapokeo. Je, tohara inawakilisha sheria ya aina gani? (Paulo anapendekeza kwamba sheria ya tohara ilitimizwa kwa Yesu, kwa hiyo lazima sheria hiyo itakuwa ni sheria ya mapokeo.)
- Soma Mwanzo 17:13. Paulo anawezaje kutuambia kuwa sheria hii haina maana wakati kwa dhahiri Mungu aliiita kuwa ni “agano la milele?”
- Soma Wakolosai 2:9-12. Je, mafungu haya yanatusaidiaje kuelewa vizuri agano hili la milele? (Hii inatuambia kuwa sheria ya Mungu ya maadili inahusika. Agano (mkataba) kati ya Mungu na uzao wa Ibrahimu (Wayahudi) lilikuwa ni kwamba wataiendeleza sheria yake ya maadili. Kama tulivyojadili juma lililopita, hii iliwasaidia kuepuka matatizo yaliyoelezewa na sheria ya asili.)
- Je, ni kwa jinsi gani, sisi tusio Wayahudi, tunalitunza agano la milele na Mungu? (Kwa njia ya ukubali, kwa njia ya ubatizo, wa uzima, kifo na ufufuo wa Yesu.)
- Soma Warumi 2:29. Je, ni kwa njia gani nyingine tunaweza kushiriki katika agano la milele? (Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu “hututahiri” mioyo yetu, ili tuweze kuyatii mapenzi ya Mungu.)
- Soma Luka 2:22-24. Je, jambo gani jingine lilimtokea Yesu kwa mujibu wa sheria ya mapokeo? (Walimpeleka kwa Mungu na sadaka ilitolewa kwa niaba yake.)
- Je, unaweza kutumia kanuni hizi kwa mwana mzaliwa mchanga leo? (Kumkabidhi kwa Mungu. Ikiwa ubatizo, neema na Roho wa Mungu akaaye ndani yetu vinachukua nafasi ya tohara, basi inaonekana kuleta mantiki kumwomba Mungu kwa kutumia vyote vitatu.)
- Soma Luka 2:21. Jambo gani liliwatokea wana wazaliwa wachanga katika siku ya nane? (Walitahiriwa na kupewa jina.)
- Kuihusianisha Sheria
- Soma Mathayo 17:24. Hii ilikuwa ni kodi kwa ajili ya kulisaidia hekalu. Je, sheria ya aina gani inahitaji kodi hii? (Soma Kutoka 30:13-16. Kodi hii ilianza kama sehemu ya sheria ya Musa!)
- Kama ungekuwa Petro, ungejibuje swali hili? (Musa aliamuru! Hekalu lilikuwa kitovu cha shughuli za kidini. Huenda kulipa kodi ile kilikuwa ni kipimo cha imani ya kidini. Kulipa kodi zako kunaonesha uaminifu. Jibu la dhahiri ni “Ndiyo, Yesu analipa kodi ya hekalu!”)
- Soma Mathayo 17:25. Je, Petro alishindwa kufikiria jambo gani? (Wafalme hawawatozi kodi wana wao. Ikiwa Yesu ni Mwana wa Mungu, hapaswi kulipa kodi.)
- Soma Mathayo 17:26. Je, suala gani la kidini la msingi linahusika katika ulipaji wa kodi hii? (Swali la muhimu kabisa kwa kila kizazi: je, Yesu ni nani? Je, yeye ni Mungu au yeye ni mwanadamu tu?)
- Ikiwa Yesu alilipa kodi ya hekalu, je, angekuwa akisema nini kuhusu kama yeye ni Mungu? (Ingekuwa ni kukana kile ambacho yeye alicho.)
- Hebu ngoja tukuweke kwenye nafasi ya Petro tena, je, Yesu anapaswa kuwa akilipa kodi ya hekalu?
- Soma Mathayo 17:27. Je, Yesu analipa kodi ya hekalu?
- Nadhani wakusanyaji wa pesa ya kale ya kiyunani (drachma) walimfuata Petro hadi baharini ili waweze kuikusanya. Je, unaifikiriaje njia ambayo Petro aliipata ile shekeli? (Kimsingi huu ni muujiza. Je, kuna samaki wangapi baharini? Yesu anasema, enenda baharini ukatupe ndoana, samaki wa kwanza utakayemkamata atakuwa na kiasi kamili cha shekeli mdomoni mwake!)
- Je, njia ambayo ilitumika kuipata ile shekeli inasema nini kuhusu uungu wa Yesu? (Inathibitisha uungu wake.)
- Yesu anasema “ili tusije tukawakwaza.”)
- Katika Mathayo 12:34 Yesu anawaita baadhi ya viongozi wa dini kuwa ni “wazao wa nyoka.” Je, tunaweza kuhitimisha kuwa Yesu alijali sana kuhusu kuwakwaza watu? (Ukiyaangalia mazungumzo yote katika Mathayo 12, viongozi wa dini walisema kwamba Yesu alikuwa kwenye pambano dhidi ya pepo. Inaonekana wakusanyaji wa kodi ya hekalu walikuwa tu wakitenda jambo jema – kuifuata sheria ya Musa.)
- Nadhani wakusanyaji wa pesa ya kale ya kiyunani (drachma) walimfuata Petro hadi baharini ili waweze kuikusanya. Je, unaifikiriaje njia ambayo Petro aliipata ile shekeli? (Kimsingi huu ni muujiza. Je, kuna samaki wangapi baharini? Yesu anasema, enenda baharini ukatupe ndoana, samaki wa kwanza utakayemkamata atakuwa na kiasi kamili cha shekeli mdomoni mwake!)
- Katika kisa cha kodi ya hekalu, je, Yesu anatufundisha nini kuhusu sheria? (Mfumo wa hekalu pamoja na vyote vilivyolitegemeza vilikuwa vinakaribia kukoma kutokana na kazi ya Mungu hapa duniani. Pamoja na hayo, Yesu anatenda kwa kadri awezavyo ili kuepuka kuwakwaza, bila kuhatarisha kanuni ya msingi ya maadili.)
- Je, tunachojifunza katika kodi ya hekalu kinahusiana kivyovyote vile na fundisho la Paulo kuhusu tohara? (Paulo anajaribu kuepuka “kuwakwaza” waumini wapya kwa kuwaambia kuwa wanatakiwa kutahiriwa.)
- Je, tunalichukulia kwa makini somo la kuepuka kuwakwaza watu wengine wanaomtafuta Mungu? (Hatuwezi kulegeza masharti kwenye kanuni za msingi, lakini tunapaswa kutenda kila lililo ndani ya uwezo wetu kuepuka kuwakwaza wale wanaodhani kuwa wanatenda mapenzi ya Mungu.)
- Sikukuu
- Kamusi Mpya ya Biblia ya Unger inabainisha kwamba kila sikukuu “kwa namna fulani ilifungamanishwa na namba saba.” Kuna Sabato ya kila juma (Mwanzo 2:2-3; Kutoka 20:8-11), Mwaka wa Mapumziko (Kutoka 23:10-11), Mwezi wa Saba (Siku ya kupiga Tarumbeta – Hesabu 29:1), Mwaka wa Yubile (miaka saba mara saba – Mambo ya Walawi 25:8-12). Kisha kuna “sikukuu tatu kubwa za Israeli,” Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu (Mambo ya Walawi 23:5-6; Kutoka 12:1-28), Pentekoste (Sikukuu ya Majuma Kadhaa – Mambo ya Walawi 23:15-16), Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16:33-34).
- Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na sikukuu hizi ambazo ni sehemu ya sheria ya Musa?
- Je, tunapaswa kuzifuata sikukuu hizi leo? (Kwa dhahiri zile zilizomwelekeza Yesu, kama vile Pasaka na Siku ya Upatanisho zinatimizwa na Yesu. Pentekoste inaashiria kizazi kipya cha Roho Mtakatifu.)
- Vipi kuhusu sikukuu zilizosalia? (Wakristo wengi kwa kiasi fulani wanaitunza Sabato ya kila juma, kwenye baadhi ya sehemu chache za kazi, “Mapumziko” ya namna fulani hutolewa, lakini kwa ujumla si mwaka wa mapumziko. Wazo langu ni kwamba ninapenda ratiba ya Mungu ya likizo!)
- Je, kweli jambo hili linahusu likizo? (Kwa kiasi fulani, lakini angalia asili ya sikukuu za kidini. Tunatakiwa kutumia muda mwingi kupumzika na kumtafakari Mungu. Vipi kuhusu makambi?)
- Kamusi Mpya ya Biblia ya Unger inabainisha kwamba kila sikukuu “kwa namna fulani ilifungamanishwa na namba saba.” Kuna Sabato ya kila juma (Mwanzo 2:2-3; Kutoka 20:8-11), Mwaka wa Mapumziko (Kutoka 23:10-11), Mwezi wa Saba (Siku ya kupiga Tarumbeta – Hesabu 29:1), Mwaka wa Yubile (miaka saba mara saba – Mambo ya Walawi 25:8-12). Kisha kuna “sikukuu tatu kubwa za Israeli,” Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu (Mambo ya Walawi 23:5-6; Kutoka 12:1-28), Pentekoste (Sikukuu ya Majuma Kadhaa – Mambo ya Walawi 23:15-16), Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16:33-34).
- Kutafakari kwa Kina
- Soma Marko 3:1-4. Yesu anapouliza kuhusu sheria, je, anazungumzia sheria ipi? (Sheria zote mbili, sheria ya maadili (Kutoka 20:8-11) na sheria ya Musa (Mambo ya Walawi 23:3) zilizuia kufanya kazi siku ya Sabato.)
- Je, lengo la swali la Yesu ni lipi? (Anawauliza viongozi wa dini kuangalia sababu za kuwepo kwa sheria. Sheria ipo ili kuendeleza wema wa wanadamu.)
- Soma Marko 3:5. Je, Yesu alikuwa amekasirika? (Viongozi wa dini walikataa kutafakari kwa kina sababu ya kuwepo kwa sheria.)
- Zitafakari sheria za Musa tulizojifunza katika somo hili: tohara, kodi ya hekalu, na sikukuu. Je, mantiki gani la jumla iliyopo kwenye Biblia inayofundishwa na kila kipengele? (Angalia sababu ya kuwepo kwa sheria. Usiwakwaze watu wengine wanaomtafuta Mungu kwa sababu umeng’ang’ana kwenye masharti ya sheria badala ya sababu ya kuwepo kwa sheria.)
- Rafiki, je, utajitoa leo kuangalia mambo kwa kina linapokuja suala la sheria ya Mungu?
- Soma Marko 3:1-4. Yesu anapouliza kuhusu sheria, je, anazungumzia sheria ipi? (Sheria zote mbili, sheria ya maadili (Kutoka 20:8-11) na sheria ya Musa (Mambo ya Walawi 23:3) zilizuia kufanya kazi siku ya Sabato.)
- Juma lijalo: Kristo na Utamaduni wa Kidini.