Nasaha Kutoka Patakatifu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, umefurahia kujifunza mfulilizo wa masomo haya yanayohusu patakatifu? Habari njema katika huu mfululizo inahusu kuhesabiwa haki kwa imani! Hukumu inaendelea mbinguni ambapo Yesu, Kuhani wetu Mkuu, anajitoa yeye mwenyewe kama kafara kwa wale wanaompokea kwa imani. Je, hii inamaanisha nini katika maisha ya kila siku? Somo letu la mwisho katika huu mfululizo linamalizia kwa kuangalia uhusiano kati ya neema, matendo na ujasiri tulionao katika wokovu wetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!
- Kufanywa Wakamilifu
- Soma Waebrania 10:1. Je, inamaanisha nini kwa kusema kuwa torati ni kivuli na si sura halisi? (Inamaanisha kwamba torati inatupatia wazo la kile alichonacho Mungu mawazoni mwake, lakini kimsingi si kile alicho nacho Mungu mawazoni mwake.)
- Soma Waebrania 10:2-4. Unadhani kuwa ni torati gani inazungumziwa hapa? Je, inarejea Amri Kumi? (Nadhani Amri Kumi ni kivuli cha kile Mungu alichonacho mawazoni mwake kwa ajili yetu, lakini hapa ninaamini kuwa hii ni rejea mahsusi ya mfumo wa kafara.)
- Soma Waebrania 10:5-7. Kama Mungu alianzisha mfumo wa kafara, inawezekanaje asipendezwe nao? (Nadhani mfumo wa kafara ulikuwa na malengo mawili: kuashiria kile ambacho Yesu atatutendea na kutukumbusha (Waebrania 10:3) juu ya asili ya kutisha ya dhambi. Sidhani kama Mungu alipendezwa na vifo vya wanyama wengi au ukweli kwamba haikuwa tiba ya kweli ya dhambi.)
- Soma Waebrania 10:8-10. Je, mfumo wa kafara bado upo? (Hapana. Yesu alipokufa kwa ajili yetu, aliuweka kando mfumo wa zamani.)
- Kwa nini hiyo ni habari njema? (Kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yetu, tukiikubali kafara hiyo, “tumepata utakaso … mara moja tu.”)
- Je, hiyo inamaanisha nini – kwa wewe kupata utakaso mara moja tu?
- Kwa nini hiyo ni habari njema? (Kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yetu, tukiikubali kafara hiyo, “tumepata utakaso … mara moja tu.”)
- Soma Waebrania 10:11-14. Angalia jinsi jambo hili linavyobainisha mambo kwa namna tofauti kidogo. Jambo hili linatuambia kuwa Yesu “amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.” Je, hiyo inafafanuaje swali kuhusu utakaso wetu? (Tunapoyategemea maisha, kifo na ufufuo wa Yesu, tunakuwa wakamilifu. Tunakuwa wakamilifu kwa sababu Yesu ni mkamilifu, na si kwa sababu sisi ni watu wakamilifu. Lakini, hii inatuweka kwenye njia inayouelekea utakaso – uamuzi wa kuishi maisha kulingana na kile ambacho Yesu ametutendea – ukamilifu.)
- Soma Waebrania 10:15-16. “Baada ya siku zile.” Ni siku gani hizo? (Baada ya Yesu kutufanya wakamilifu.)
- Kitu gani kinatokea baada ya Yesu kutufanya wakamilifu? (Anazitia sheria zake mioyoni mwetu na kuziandika katika nia zetu kwa njia ya Roho Mtakatifu.)
- Je, hiyo inamaanisha nini – kuwa na sheria mioyoni mwetu na katika nia zetu? (Kwanza, kwa sababu tunao moyo kwa ajili ya Mungu. Tunatamani kuyatenda mapenzi yake. Pili, inamaanisha kwamba tumefanya uamuzi wa busara kuyatenda mapenzi yake.)
- Je, hilo linaendanaje na maisha yako? Binafsi ninajikuta kuvutiwa dhambini. Vipi kuhusu wewe? (Sidhani kama kamwe mvuto wa dhambi unatoweka katika upande huu wa mbinguni. Warumi 7:21-25 inaelezea mvuto wa dhambi, lakini pia inabainisha kwamba tunataka kutenda mambo mema. Moyo kwa ajili ya Mungu unamaanisha kwamba tunataka kutenda mambo mema hata kama asili yetu ya dhambi inatuvutia dhambini. Tunatakiwa kufanya uamuzi wa busara kila siku ili tuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu.)
- Kitu gani kinatokea baada ya Yesu kutufanya wakamilifu? (Anazitia sheria zake mioyoni mwetu na kuziandika katika nia zetu kwa njia ya Roho Mtakatifu.)
- Ujasiri wa Wokovu Wetu
- Soma Waebrania 10:19-21. Je, inamaanisha nini “kupaingia Patakatifu Sana?” (Soma Mambo ya Walawi 16:1-2. Mungu alionekana Mahali Patakatifu sana – na wanadamu wadhambi hufa wawapo mbele za Mungu. Lakini sasa, tunaweza kuingia katika uwepo wa Mungu kwa ujasiri kwamba hatutakufa kwa sababu Yesu ametufanya kuwa wakamilifu.)
- Soma Waebrania 10:22. Je, “miili yetu kuoshwa kwa maji safi” inamaanisha nini? (Ubatizo!)
- Soma Warumi 6:3-7. Je, ubatizo unamanisha nini kwetu? (“Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu … vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.” Tunapobatizwa, tunashiriki katika kifo cha Yesu kwa ajili ya dhambi zetu!)
- Angalia tena Waebrania 10:22. Je, moyo wa ukweli ulio katika utimilifu wa imani ni upi? (Wakati ambapo hatuwezi kuupata wokovu kwa njia ya matendo yetu, Yesu anawatafuta wale wanaomaanisha kile wanachokisema pale wanaposema kwamba kwa imani wanategemea kile alichowatendea.)
- Waebrania 10:22 inatuambia kuwa dhamiri ya hatia ni jambo ambalo pia linatakaswa, je, hiyo inamaanisha nini? (Inamaanisha kwamba huhitaji tena kujisikia hatia kutokana na dhambi zako. Shetani ndiye mshitaki, sio Mungu. Mungu alitutakasa, kwa hiyo unapaswa kuukubali msamaha wako na kuachana na hatia!)
- Soma Waebrania 10:25. Je, tatizo gani kubwa linabainishwa hapa? (Sote tunatakiwa kutiwa moyo katika imani yetu. Sote tunatakiwa kukumbushwa juu ya kile Yesu alichotutendea. Tunatakiwa kukutana pamoja na waumini wengine ili tuweze kutiwa moyo.)
- Je, hiyo inaashiria nini juu ya kusoma haya mafundisho ya Biblia? (Inamaanisha kwamba kusoma somo kwa njia ya mtandao tu bado haitoshi! Sote tunatakiwa kujifunza Biblia na waumini wengine. Tunatakiwa kuwa tunakutana na watu wengine ili tumsifu na kumwabudu Mungu.)
- Onyo
- Soma Waebrania 10:26-27. Hilo ni jambo baya sana! Natambua kwamba huenda umetenda dhambi leo. Nina uhakika dhambi yako haikuwa ya bahati mbaya – sio kama tendo la kujikwaa na kuanguka dhambini. Umetenda dhambi kwa kutambua na kwa makusudi. Pengine hukusema, “Nadhani leo nitatenda dhambi,” bali kwa asilimia kubwa dhambi yako haikuwa ya bahati mbaya. Je, sasa sote tunapaswa kuutarajia “moto utakaowala maadui wa Mungu?”
- Tunawezaje kutoka haraka haraka kwenye ujasiri wa kuingia katika uwepo wa Mungu hadi kuingia kwenye hofu ya kwamba tumekuwa maadui wa Mungu?
- Tunaielezeaje Warumi 7:21-25? Je, Paulo alikuwa adui wa Mungu?
- Soma Waebrania 10:28-29. Je, matendo ya aina gani yanaelezewa hapa? Zingatia “maneno kwa vitendo” – “aliyekataliwa,” “aliyekanyagwa,” “kuihesabu damu [ya Yesu] ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo,” “kumfanyia jeuri Roho wa neema.” Je, haya maneno ya kivitendo yanaashiria nini? (Hii si dhambi ya “makusudi” kwa maana ya kwamba mambo mengi unayoyafanya unayafanya kwa makusudi. Badala yake, hii inamaanisha kwamba umemkataa Mungu. Umeikataa neema. Umekataa kile ambacho Yesu alikifanya kwa niaba yako. Mawazo yako yanapingana (yana uhasama) na yote yale aliyoyatenda Mungu.)
- Je, Mungu anatenda haki hapa? Je, kweli hili ni tendo la haraka haraka linalojiingiza kwenye ubaya? (Hapana! Kwa kuwa Mungu alitenda mambo yote kwa ajili yetu kwa kufa kifo cha kutisha na chenye maumivu makali badala yetu, je, Mungu hana haki ya kusikitika endapo tutakataa upendo na kafara yake? Endapo tutaukanyaga upendo wake na neema yake? Mimi ninasema kuwa, “Ndiyo.”)
- Je, kuna jambo lolote chanya katika haya mafungu? (Ndiyo. Hatupotei kwa bahati mbaya. Tunafanya uamuzi wa kuyakataa yale yote aliyotutendea Yesu. Watakatifu wote wanajikuta wakitenda dhambi kwa makusudi. Lakini, siamini kama hicho ndicho kinachomaanishwa hapa. Huku ni kuikataa kwa makusudi kafara ya Yesu kwa ajili yetu na kuyachagua maisha ya dhambi.)
- Vipi kama una mwana, binti, mzazi au mwenzi unayehofu kwamba amemkataa Yesu; je, kuna tumaini lolote? (Ndiyo. Utagundua kwamba Waebrania 10:26 inasema, “baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli.” Wengi wa wale wanaomkataa Yesu sasa kamwe hawauelewi ukweli kikamilifu. Nakumbuka wakati fulani nilipokuwa kijana mdogo, kwa sababu nilikuwa nimefundishwa kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo, nilihitimisha kwamba kamwe sikuwa mwema vya kutosha na vile vile naweza kumkataa Mungu. Sikuwa “nimeupokea ujuzi wa ile kweli.”)
- Soma Waebrania 10:26-27. Hilo ni jambo baya sana! Natambua kwamba huenda umetenda dhambi leo. Nina uhakika dhambi yako haikuwa ya bahati mbaya – sio kama tendo la kujikwaa na kuanguka dhambini. Umetenda dhambi kwa kutambua na kwa makusudi. Pengine hukusema, “Nadhani leo nitatenda dhambi,” bali kwa asilimia kubwa dhambi yako haikuwa ya bahati mbaya. Je, sasa sote tunapaswa kuutarajia “moto utakaowala maadui wa Mungu?”
- Ujasiri
- Soma Waebrania 10:32-34. Unalinganishaje mambo mabaya maishani mwako na hii orodha?
- Soma Waebrania 10:35. Je, tunazungumzia ujasiri wa namna gani? (Ujasiri kwa Mungu. Ujasiri kwamba tunatenda jambo jema hata kama linaweza kutusababishia mateso.)
- Soma Waebrania 10:36-39. Je, inamaanisha nini “kusita-sita?”
- Soma Ufunuo 21:8. Waoga wanaorodheshwa kabla ya wauaji? Je, Mungu anatupatia ujumbe gani katika hizi nukuu za kusita-sita na waoga? (Mungu anawatafuta wale wanaomtumaini. Anawatafuta waaminifu walio na ujasiri juu ya kile Yesu alichokitenda kwa ajili yao. Wale walio na ujasiri katika wokovu wao.)
- Rafiki, je, utadhamiria kumtumaini Mungu leo? Je, utaiweka imani yako kwake na katika neema yake? Je, utaachana na tabia ya kujitumainia mwenyewe?
- Juma lijalo: Tutaanza mfulilizo mpya wa masomo yanayohusu kuwa wanafunzi wa Yesu.