Maagano Mawili
(Wagalatia 4:21-31, Warumi 4)
Swahili
Year:
2011
Quarter:
4
Lesson Number:
10
Utangulizi: Majuma kadhaa yaliyopita tulijifunza kuwa ahadi ya Mungu ya kuhesabiwa haki kwa imani kwa Abrahamu iliendelea kuwepo sambamba na uelewa wa Abrahamu wa amri za Mungu. Tuliona kwamba sababu iliyofanya vitu hivi viwili (neema na sheria) viwepo bega kwa bega ilikuwa ni kwa sababu vilikuwa na malengo tofauti. Juma hili Paulo anawajumuisha wanawake na watoto kwenye mjadala. Je, hii itatupatia mtazamo sahihi zaidi kwenye uchaguzi wetu wa kuitegemea sheria na kuitegemea neema? Hebu tuzame kwenye somo letu la Wagalatia na kujifunza zaidi!
- Sheria Inazungumza
- Soma Wagalatia 4:21. Swali hili linaelekezwa kwa wale wanaoamini kwamba lazima tuitii sheria ili tuweze kuokolewa. Je, kuna mtu yeyote hapa anayeamini hivyo? Hata kama huamini hivyo, kwa ajili ya mjadala hebu tuchukulie kwamba tunaamini hivyo. Kwa hiyo, Paulo anauliza kuwa, je, sheria inasemaje? (Sheria inasema kuhusu mambo mengi sana. Mara kwa mara nimesikia ikisemwa kwamba sheria “ni nakala ya tabia ya Mungu.” Hilo linapaswa kuwa jema!
- Je, ni kweli kwamba Paulo anahitaji jibu kutoka kwa wasikilizaji wake kuhusiana na swali lake la kile ambacho sheria inasema? (Hapana. Anasema kuwa wasikilizaji wake hawana habari/utambuzi wa kile sheria inachokisema, na anataka kutuambia kile ambacho sheria inasema.)
- Soma Wagalatia 4:22-24. Je, Paulo anapendekeza kuwa sheria inasema nini? (Inasema, “mimi ni Hajiri na wanae.”)
- Hebu subiri kidogo! Sioni mahali popote hilo likiwa limeandikwa kwenye Amri Kumi. Je, Paulo anasema kuwa hili limeandikwa wapi? (Paulo anasema “mambo haya husemwa kwa mfano.” Kiyunani hutafsiri neno “kwa mfano” kuwa “allegoreo” – istiari, usambamba, maelezo. Paulo anatuambia kuwa kisa cha Hajiri ni kisa cha sheria.)
- Soma Wagalatia 4:21. Swali hili linaelekezwa kwa wale wanaoamini kwamba lazima tuitii sheria ili tuweze kuokolewa. Je, kuna mtu yeyote hapa anayeamini hivyo? Hata kama huamini hivyo, kwa ajili ya mjadala hebu tuchukulie kwamba tunaamini hivyo. Kwa hiyo, Paulo anauliza kuwa, je, sheria inasemaje? (Sheria inasema kuhusu mambo mengi sana. Mara kwa mara nimesikia ikisemwa kwamba sheria “ni nakala ya tabia ya Mungu.” Hilo linapaswa kuwa jema!
- Kisa cha Hajiri
- Hebu tugeukie kisa cha Hajiri. Soma Mwanzo 15:2-6. Hili ni fungu ambalo huwa tunalirejea mara kwa mara: Mungu alimwahidia Ibrahimu uzao mkubwa, Ibrahimu alimwamini Mungu, na imani hiyo ilimfanya Mungu “amzawadie” Ibrahimu haki.)
- Soma Mwanzo 16:1-2. Je, Sarai (Sara) alimwamini Mungu? (Alimwamini Mungu – kwa kuwa alidhani kuwa Mungu alimfunga tumbo ili asizae.)
- Je, hakuwa akimheshimu Mungu? (Nilirudi nyuma na kuziangalia ahadi alizopewa Ibrahimu kuhusiana na kuwa na uzao mkubwa. Ahadi hizi ni kwa Ibrahimu, sio kwa Sara. Sara alikuwa tu akimsaidia Mungu.)
- Hebu tujadili hili kidogo. Paulo anatuambia kuwa Hajiri ni kisa kinachohusiana na sheria. Hajiri alijitokeza kwenye mchakato kwa sababu ya maamuzi yaliyofanywa na Sara na Ibrahimu. Hebu tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusiana na huu ulinganifu:
- Je, haikuwa sahihi kwa Sara kuwa na lengo la kupata watoto kwa ajili ya Ibrahimu? (Hapana.)
- Je, haikuwa sahihi kwa Sara kumsaidia Ibrahimu kupata watoto? Je, kwani mke hapaswi kuwa wa msaada?
- Je, kulikuwa na kitu chochote kibaya kutokana na kile alichokifanya Sara? (Sara aliamua kufanya kazi ya Mungu. Natambua kuwa utamaduni wa wakati ule ulitambua kwamba Hajiri alikuwa ni mali ya Sara, kama vile ambavyo angeweza kumiliki motokaa hivi leo. Sara angeweza kuchukulia ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu kuwa ahadi kwake kwa sababu mbele za macho ya Mungu wanandoa ni kitu kimoja (wawili wanapokuwa kitu kimoja – Mwanzo 2:24). Kwa vile alimmiliki Hajiri, angeweza kutafakari kuwa hakuwa akikiuka sheria ya ndoa ya “wawili kuwa kitu kimoja” kwa kuwa Hajiri alikuwa ni mali yake. Kwa hiyo, angetenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.)
- Je, hii ni sawa - taswira ya wale wanaoishika sheria? (Ndiyo! Kwa hakika hii ndio hali halisi. Badala ya kumwamini Mungu (kama ambavyo Ibrahimu alifanya) na kumwacha Mungu atimize ahadi yake, Sara alikuwa akijishughulisha sana na kile ambacho Mungu tayari alikwisha ahidi kuwa atakifanya. Kama tu angemwamini Mungu, hiyo ingetosha.)
- Je, tuna tatizo dogo la kimantiki hapa – Biblia (Wagalatia 4:24) inasema kuwa “wanawake wanawakilisha maagano mawili.” Hajiri anawakilisha sheria, lakini ni Sara aliyefanya jambo lisilo sahihi. Je, tunapaswa kulielewaje hili? (Tunahitajika kuliangalia hili kwa mujibu wa mtazamo wa Ibrahimu. Mungu alimwahidi watoto na ingeendana na Biblia kama watoto hao wangetokana na Sara. Sara alibadili hili kwa kumwingiza Hajiri kwenye mchakato mzima. Kwa hiyo, Hajiri anawakilisha wokovu unaopatikana kwa matendo ya mwanadamu.)
- Soma Wagalatia 4:25. Je, kwa nini Hajiri analinganishwa na Mlima Sinai na Yerusalemu? (Sinai ndipo mahali ambapo Amri Kumi zilitolewa. Yerusalemu ni chanzo cha wale wanaohoji kwamba sheria lazima itunzwe/ishikwe ili kuweza kuokolewa. Hajiri na mwanae ni watumwa. Wale walio chini ya sheria ni watumwa wa adhabu ya kifo.
- Je, kuna dini kubwa inayoshadadia wokovu kwa matendo, inayohusianishwa na Arabuni na Hajiri?
- Licha ya uhasama kati ya Uislamu na dini ya Kiyahudi, je, kuna mtazamo unaofanana kati yao kuhusu wokovu? (Kila dini hivi leo, isipokuwa Ukristo, inaamini katika “wokovu kwa matendo.”)
- Soma Wagalatia 4:26-27. Je, ni nani aliyekuwa akiishi katika Yerusalemu iliyokuwa mbinguni kwa wakati ule? (Yesu! Yesu, huku akiwa ameshatimiza matakwa ya sheria kwa ajili yetu , sasa yupo mbinguni. Hayo ndio makao yetu ya kweli ya kiroho, sio Yerusalemu ya duniani iliyomkataa Yesu kama Masihi.)
- Utabaini kuwa fungu la 27 ni nukuu kutoka Isaya 54:1. Je, “mwanamke tasa” ni nani? (Sara!)
- Je, mwanamke “aliye na mume” ni nani? (Kumbuka kuwa Sara alimtoa Hajiri kwa Ibrahimu. Ni Hajiri ambaye sasa “ana mume.” Paulo bado anawaongelea wanawake wawili.)
- Je, ni sahihi kiasi gani kusema kuwa, “watoto wa mwanamke aliyeachwa pekee ni wengi?” (Hatimaye Sara ndiye ambaye angemzaa Isaka, na kwa hiyo kuwa mama wa taifa la Kiyahudi na mwishowe, Masihi.)
- Utabaini kuwa fungu la 27 ni nukuu kutoka Isaya 54:1. Je, “mwanamke tasa” ni nani? (Sara!)
- Kisa cha Isaka
- Soma Wagalatia 4:28. Je, ni kwa namna gani sisi (wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa imani pekee) tu kama Isaka?
- Soma Warumi 4:18-21. Je, vitu muhimu vya imani ya Ibrahimu ni vipi? (Kwamba kile kilichoahidiwa hakikuwa kikiwezekana katika hali ya kibinadamu. Lakini, Ibrahimu aliiamini ahadi ya Mungu na alimpatia Mungu utukufu.)
- Soma Warumi 4:22-25. Sasa jibu swali langu la awali, “Je, ni kwa namna gani sisi tu kama Isaka?” (Isaka alipatikana ikiwa ni matokeo ya imani ya baba yake kwa ahadi ya Mungu. Mungu Baba yetu alituahidia Yesu. Tunao uzima kupitia kwa Yesu. Kama vile Ibrahimu alivyozawadiwa haki kwa sababu aliamini kumpata Isaka aliyeahidiwa, kwa hiyo tunazawadiwa haki kama tunaamini katika maisha, kifo na ufufuo wa Yesu kwa ajili yetu (kwa niaba yetu).)
- Hitimisho
- Tumeona kwamba malengo ya Sara kwa Ibrahimu kimsingi yalikuwa sawa na malengo ya Mungu kwa Ibrahimu. Je, hiyo inatufundisha nini kuhusiana na wale wanaoamini kwamba matendo ni ya muhimu katika kuupata wokovu? (Matendo mema ni jambo zuri! Kutenda mambo mema kimsingi ni mpango wa Mungu maishani mwetu. Tatizo sio lengo, bali njia. Kama tukifuata njia ya Ibrahimu na kumwamini na kumtumainia Mungu, njia yetu ni imara. Kwa upande mwingine, kama tukiyaangalia matendo yetu wenyewe, basi njia yetu sio tu kuwa itaishia kwenye kushindwa, bali pia ni dhambi.)
- Soma Wagalatia 4:29. Paulo anatuambia kuwa wale wanaoamini katika haki kwa imani wanateswa na wale wanaoamini katika haki kwa matendo. Kwa nini? (Je, unafurahia kazini kwako pale ambapo wewe peke yako ndiye unayefanya kazi kwa uaminifu kwa siku? Hapana! Unawaonea wivu wale wasiokuwa na maana na wavivu. Kama unaamini matendo yako yatakuokoa, basi unawaonea wivu wale wanaodai wanaokolewa kwa neema. Mioyo yetu (au tuseme wangu) ya asili inaamini katika kufanya kazi kwa bidii kwa sababu kwa asili mimi ni mchapa kazi. Kuikubali zawadi ya bure ya wokovu ni kinyume na mioyo yetu ya asili.)
- Soma Wagalatia 4:30-31. Kumbuka kwamba wale ambao wanaoshadadia matendo kwa asili wanawadharau wale wanaookolewa kwa neema. Je, Paulo anasema kuwa tunapaswa kufanya nini kwa watu wanaoshadadia haki kwa matendo? (Tuwaepuke!)
- Uuuuuuh! Hebu subiri kidogo! Nilidhani kwamba tulikubaliana na malengo ya wenye kushadadia matendo? Ya kwamba kuzishika Amri Kumi ilikuwa ni jambo jema? Je, kwa nini tuwatupe watu “wema” nje ya mahusiano yetu? (Soma Wagalatia 5:1-4. Hili ni suala zito sana. Wale wanaokana haki kwa imani pekee wanaikana kazi ya Yesu. Wanakana sehemu ya muhimu na ya msingi sana ya injili. Wanatenganishwa na Yesu na wanaelekezwa kwenye mauti ya milele kwa sababu lazima waishike sheria yote.)
- Rafiki, je, unaona jinsi swali hili lilivyo zito? Kama unayategemea matendo yako kwa ajili ya wokovu wako, basi umepotea. Umemkana Yesu. Kwa nini usitubu dhambi zako hivi leo, uyakubali kwa imani matendo ya Yesu kwa niaba (ajili) yako na kisha usalie kwenye uelewa wako mzuri kabisa wa wokovu kwa neema pekee!
- Juma lijalo: Uhuru Katika Kristo.