Who is the Man of Romans 7?

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Warumi 7)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
4
Lesson Number: 
8

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Warumi 7 ni mojawapo ya sura za Biblia ninazozipenda sana. Hilo linawezekana likawa jambo la ajabu kwako. Kwa nini nisichague sura inayommiminia Mungu sifa? Kwa nini nisichague sura inayotoa ahadi ya amani na furaha? Ninapenda sura za aina hiyo pia. Sababu inayonifanya niipende Warumi 7 sana ni kwamba inanitia moyo katika mapambano yangu na dhambi. Baadhi ya watu watasema kuwa sipaswi kutiwa moyo na sura hiyo. Wengine watasema kuwa sura hiyo ni kwa ajili ya Wakristo wachanga, na sio watu wazima kama mimi ambao wamekuwa kwenye imani kwa miongo kadhaa. Hebu tufanye kile tukifanyacho kila juma – tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi kile ambacho Mungu anatufundisha!

 

  1. Mamlaka ya Kisheria

 

    1. Soma Warumi 7:1-3. Kitu gani kimebadilika kwenye hiki kisa anachokielezea Paulo kwenye vifungu hivi? (Mume amefariki.)

 

      1. Je, sheria imebadilika? (Hapana.)

 

      1. Tuhitimishe nini kutokana na hili? Hii inatufundisha nini kuhusu sheria? (Sheria haibadiliki, lakini mazingira yanabadilisha uhusiano wetu na sheria.)

 

    1. Soma Warumi 7:4. Uhusiano wetu na sheria umebadilikaje kutokana na mazingira kubadilika? (Kama ilivyo kwa mke aliyewekwa huru dhidi ya sheria ya uzinzi kutokana na kifo cha mkewe, vivyo hivyo tunawekwa huru dhidi ya sheria kwa kifo cha Yesu kwa ajili (niaba) yetu.)

 

      1. Kwenye kisa chetu, mwanamke ameolewa na mwanaume mwingine. Au, angalao, alikuwa huru kufanya hivyo. Tumewekwa huru kufanya nini? (“Kumzalia Mungu matunda.”)

 

        1. Unaweza kuelezea jambo hili? Kwa nini kuwekwa kwetu huru dhidi ya sheria kutufanye tumzalie Mungu matunda?

 

  1. Tunda

 

    1. Soma Warumi 7:5-6. Nadhani hili ni jibu la swali letu lililopita. Lakini, tunatakiwa kuchimbua zaidi ili kuelewa jibu! Je, sheria ya Mungu inaamsha “tamaa za dhambi?” (Haifanyi hivyo kwa yenyewe. Angalia viungo vingine muhimu – “kudhibitiwa na asili ya dhambi.”)

 

      1. Je, kuwa “chini ya sheria” kunatufanya tudhibitiwe na asili yetu ya dhambi? (Liangalie suala hili kwa namna hii. Asili yetu ya kibinadamu ni ya kidhambi. Tunapoona kauli za sheria za “Msifanye hivi,” asili yetu ya uasi inachipuka na tunatamani kutenda kile kinachozuiliwa na sheria.)

 

 

    1. Angalia tena Warumi 7:6. Njia mpya ya kutumika ni ipi? (Kwa njia ya Roho Mtakatifu. Mara hii, “roho” inayotusukuma sio asili yetu ya kibinadamu, bali Roho wa Mungu. Kwa “kuwekwa huru” dhidi ya hukumu ya sheria, tuko huru kuchagua maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu.)

 

      1. Je, sheria imebadilika? (Hapana.)

 

      1. Kitu gani kimebadilika? (Mazingira yako. Unaongozwa kuishi maisha yanayoendana na sheria ya Mungu kupitia uongozi na uhamasisho wa Roho Mtakatifu. Husukumwi tena na asili yako ya dhambi kuwa muasi dhidi ya sheria ya Mungu.)

 

    1. Soma Warumi 7:7. Sheria inaendelea kutumikia lengo gani? (Kututahadharisha katika kilicho dhambi.)

 

      1. Watu wengine wanafundisha kwamba Paulo anaandika kuhusu “sheria ya mapokeo” ya Musa. Tuliwekwa huru dhidi ya sheria hiyo na si Amri Kumi. Kifungu hiki kinasema nini kuhusu fundisho hilo? (Hakipo sahihi kutokana na sababu mbili. Kwanza, mfano anaoutumia Paulo ni mmojawapo wa Amri Kumi (Kutoka 20:17). Pili, Paulo anasema kuwa sheria inatufundisha kuhusu dhambi. Manufaa hayo (uelewa sahihi wa dhambi) yanahusiana kwa usahihi zaidi na Amri Kumi kuliko sheria yoyote ya mapokeo. Ikiwa Paulo alikuwa anazungumzia kuhusu sheria ya mapokeo pekee, ungekuwa na taswira gani ya dhambi?)

 

      1. Sababu inayowafanya watu wengine wafundishe kuwa Paulo hazungumzii Amri Kumi ni kwamba wana wasiwasi kuwa Wakristo hawataijali sheria, hususani amri ya Sabato. Soma tena Warumi 7:5-6. Je, unataka kufungwa kwenye kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo kwa ajili ya amri ya Sabato – au amri nyingine zozote zile? (Rafiki, ninataka kuokolewa kwa neema katika sheria zote! Ninataka kuongozwa kwenye njia mpya ya Roho Mtakatifu katika sheria zote! Dhana ya kwamba Paulo anaacha kujumuisha sehemu ya sheria (Amri Kumi) inahafifisha neema.)

 

    1. Soma Warumi 7:8-11. Je, unaona kuwa jambo hili ni sahihi? Umewahi kugundua kwamba mtu anapoambiwa kuwa hawezi kumiliki kitu fulani, basi anaanza kukitaka kwa udi na uvumba? Kwa upande mwingine, kama kumiliki kitu fulani mara zote ni suala la uchaguzi, basi haijalishi kuwa nacho. Je, unaweza kuthibitisha, kwa uchunguzi wako binafsi, ukweli anaouandika Paulo?

 

    1. Soma Warumi 7:12. Asili ya Amri Kumi ni ipi? (Ni nzuri! Ni “takatifu, ya haki na njema.”)

 

      1. Ikiwa Amri Kumi ni nzuri sana, kuna tatizo gani? (Kisicho sahihi ni sisi! Kisicho sahihi ni asili yetu ya dhambi. Tunatakiwa kukibadilisha na mwongozo wa Roho Mtakatifu.)

 

      1. Kwa nini kuzifia Amri Kumi kunatusaidia kufikia hatua ya kuongozwa na Roho Mtakatifu? (Hatuna haja tena ya kuwa na wasiwasi kwamba kushindwa kuzishika Amri Kumi huleta mauti. Yesu ametufia. “Ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo” (Warumi 7:4). Tuko huru kuishi kwa mujibu wa Roho wake.)

 

 

      1. Je, hadi kufikia hapa mjadala wetu unaonekana kana kwamba unaelekezwa kwa waongofu wapya kwenye Ukristo? (Hakuna hata mjadala mmoja wenye mwelekeo huo. Hili wazo la utiifu wa sheria, wazo kwamba tunaweza kujiokoa wenyewe kwa kusaga meno yetu na mwenendo wetu, ni suala pana.)

 

    1. Soma Warumi 7:13. Vipi kuhusu sheria “kufanya mauti ndani yangu?” (Paulo anarudia kwamba sio sheria, bali dhambi. “Ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu.” Uzoefu wetu na dhambi unatufundisha kwamba dhambi huleta madhara. Huleta mauti. Kwa mara nyingine, Paulo anaonekana kutuasa tujaribu (kwa kuthibitisha) kile anachokisema kwa kulinganisha na uzoefu wetu wenyewe.)

 

  1. Pambano

 

    1. Soma Warumi 7:14-16. Unadhani Paulo anamwelezea nani hapa? Yeye mwenyewe au Mkristo mpya? (Kwa nini awe anamwelezea mtu mwingine wakati anatumia neno “mimi?”)

 

      1. Tafakari kauli ambayo Paulo amekuwa akiijenga kwenye somo letu majuma mawili yaliyopita. Ujumbe wake wa jumla ni upi? (Katika Warumi 5 tulijifunza kwamba tayari Yesu ameshalipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. Katika Warumi 6, Paulo anasema “usitoke chomboni,” na utarajie kwamba utaishinda dhambi. Kila sura inajenga juu ya mambo ya nyuma ili kuepuka mahitimisho makali. Paulo hawafundishi waumini wapya, anawafundisha Wakristo wote.)

 

    1. Soma Warumi 7:17-20. Paulo anatoa kisingizio gani kwa kutenda mambo ambayo hataki kuyatenda? Anatoa kisingizio gani kwa dhambi zake? (Anasema, “Nalaumu asili yangu ya dhambi!”)

 

      1. Je, tumesikia wazo hili kutoka kwa Paulo hapo awali kwenye sura hii?  (Hii inaenda mbali kwenya tatizo la sheria. Hakuna tatizo lolote kwenye sheria, bali asili yetu ya dhambi ndio inayotoa mjibizo kwenye Amri Kumi wenye tamaa ya kutenda dhambi (Warumi 7:4-12).

 

    1. Soma Warumi 7:21-24. Unaelewa vizuri hisia za Paulo? (Kila Mkristo mwaminifu nanapaswa kujisikia namna hii. Paulo anaelezea (anaonyesha) maoni yetu sote.)

 

    1. Soma Warumi 7:25. Nani ametuokoa? (Yesu! Yesu anatupatia neema!)

 

      1. Hebu tuangalie jambo hili kwa namna tofauti. Hebu tuseme kwamba Paulo anawaandikia Wakristo wachanga wasio wakomavu. Hiyo itakuwa inawazungumziaje Wakristo wakomavu? (Hawana kisingizio cha kutenda dhambi. Lakini, cha kukatisha tamaa zaidi ni kwamba, hawana tumaini la kuokolewa. Hii ni hoja nyingine ya kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo, na lazima ikataliwe.)

 

    1. Siwezi kuishia hapa. Tutajifunza Warumi 8 juma lijalo, lakini hebu tusome Warumi 8:1-4. Kuna habari gani njema kwetu ambao bado tunapambana na asili yetu ya dhambi? (Sisi, “kwa njia ya Yesu Kristo,” “tumewekwa huru dhidi ya sheria ya dhambi na kifo.” Ni furaha iliyoje!)

 

 

    1. Rafiki, Paulo hazishambulii Amri Kumi. Adui ni asili yetu ya dhambi. Asili yetu haiendani sana na sheria. Mapambano yetu dhidi ya asili yetu yanaendelea katika safari yetu ya Kikristo. Lakini, habari njema sana ni kwamba tuwapo ndani ya Yesu hatuna hukumu. Usiwaruhusu wale ambao kwa kujua ama kwa kutokujua wanajenga hoja kuunga mkono juu ya kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo wakuibie furaha yako. Wewe kubali tu karama ambayo Yesu anakupatia.

 

  1. Juma lijalo: Hakuna Hukumu.