Unyenyekevu wa Wenye Hekima

(Mithali 30)
Swahili
Year: 
2015
Quarter: 
1
Lesson Number: 
12

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kitabu cha Mithali kinasema kwa kurudiarudia kwamba hekima huleta utajiri na furaha, wakati kuwa mpumbavu au mvivu huleta umaskini na huzuni. Watu wanapofanikiwa sana maishani, je, kwa ujumla huwa ni wanyenyekevu? Uchunguzi wangu binafsi umebainisha kwamba watu hao si wanyenyekevu, na ni kwa sababu rahisi sana. Kwa kuwa kile wanachokifanya maishani kinawanyookea na kuwapa mafanikio, wanadhani kwamba mawazo yao yako juu ya wale ambao maisha yao hayajawaendea vizuri. Huenda wako sahihi. Tatizo lililopo ni kwamba Biblia inanukuu unyenyekevu kama kuwa na maadili, na watu wenye majivuno si wanyenyekevu. Hebu tuchimbue somo letu la Mithali ili tuelewe maadili ya unyenyekevu vizuri zaidi!

6. Jina la Mungu ni lipi na jina la Mwanaye ni lipi?

  1. Mpumbavu na Ubaya
    1. Soma Mithali 30:1-2. Baadhi ya watu wanatoa maoni kwamba majina haya ni ishara ya wahusika wa Biblia, wengine wanasema kuwa yanamaanisha majina ambayo ni ya muhimu. Nani anayezungumza? (Aguru. Tutarahishisha mambo kwa kutumia jina hili pekee kama jina la mzungumzaji.)
      1. Mzungumzaji ana maoni gani kuhusu uelewa na elimu yake? (Anasema kuwa yeye ni mpumbavu zaidi kuliko watu wote. Huo ndio unyenyekevu!)
    2. Soma Mithali 30:3. Aguru anakiri upumbavu gani wa kipekee? (Hamjui Mungu. Hajajifunza hekima.)
    3. Soma Mithali 30:4. Hebu tuangalie upya maswali haya kwa kutumia lugha ya leo. Vipi kama yakiulizwa hivi:
      1. Mungu ni nani?
      2. Mbingu iko wapi?
      3. Nani anayedhibiti hali ya hewa?
      4. Nani anayeweka mipaka ya bahari?
      5. Nani aliyeweka mipaka ya nchi?
        1. Unadhani maswali haya yana upekee gani? (Ni baadhi ya maswali makuu maishani.)
        2. Maswali haya yanafikirisha jambo gani ambalo wanadamu wa sasa wanaweza wasiyafikirie? (Wanachukulia kwamba chombo (taasisi) chenye kufikiri ndicho kinachouongoza ulimwengu.)
    4. Soma Mithali 30:5. Hebu subiri kidogo! Je, hapa mtu mwingine ndiye anayeandika? Je, Aguru amepata kiwango fulani cha hekima? Nini kimemsababisha Aguru aelezee maneno ya Mungu “yasiyo na dosari?” (Ili jambo hili liwe na mantiki, lazima Aguru amwamini Mungu. Ujumbe wake ni kwamba majibu kwa maswali yote haya ya msingi maishani yanatoka kwa Mungu. Tunaweza tusitambue jambo hilo, lakini linapokuja suala la kujibu maswali haya ya msingi maishani, kama ilivyo kwa Aguru, sote tunafanana kabisa.)
      1. Ni kwa namna gani Mungu ni ngao yanapokuja masuala ya maswali ya msingi kabisa maishani? (Mungu anatupatia maarifa ya kina. Tunaweza tusiwe na ufahamu mkubwa, lakini kile tunachokifahamu ni cha muhimu.)
    5. Soma Mithali 30:6 na Kumbukumbu la Torati 4:2. Kumbukumbu la Torati 4:2 ni mojawapo ya mafungu ninayoyapenda sana kwa sababu fungu hilo linatukumbusha kwamba kutunga kanuni (sheria) mpya ni makosa tu kama ilivyo kusema kwamba ni sahihi kupuuzia kanuni (sheria) za Mungu zilizopo. Nadhani fungu hili linapaswa kubandikwa kwenye kila shule ya Kikristo! Je, Mithali 30:6 inarudia tu ukweli huu huu? (Nadhani tuna kitu tofauti kwenye Mithali. Mada inahusu baadhi ya maswali ya msingi sana maishani. Mungu anasema usiongezee kwenye kile ambacho kimeshafunuliwa.)
      1. Je, hii inamaanisha kuwa tunapaswa kupuuzia sayansi? (Zaburi 19:1-3 inabainisha kwamba mambo ya asili yanatufundisha habari za Mungu. Sidhani kama fungu hili linatuambia tupuuzie mambo ya asili na kile yanachofunua kwa njia ya sayansi.)
      2. Hebu tuweke kivitendo Mithali 30:6 katika umri wa dunia. Je, kwa dhahiri Biblia inabainisha umri wa dunia? (Sidhani. Mwanzo 1:2 inatuambia kwamba kuna kitu kilichokuwepo kabla ya juma la Mungu la uumbaji. Mwanzo 1:2 inatuambia kwamba Mungu aliumba miti na mimea mikubwa – ikimaanisha kwamba iliumbwa ikiwa na umri mkubwa. Sidhani, ingawa sina uhakika, kwamba wanafunzi wa dhati wa Biblia wanaamini kwamba vizazi vya Biblia vimekamilika na vilikusudiwa kuwa njia ya kubainisha umri wa dunia. Hili linaweza kuwa eneo ambalo ikiwa “tutaongezea kwenye maneno ya Mungu” tutathibitika kuwa waongo.)
      3. Ujumbe wa Aguru unaopaswa kutumiwa kivitendo ni upi hapa? (Kuna mambo mengi sana ambayo Mungu hajatufunulia. Usianze kutetea mambo ambayo Mungu hajayafunua kwa wazi – na kisha kuishia kuaibika pale utakapothibitika kuwa wewe ni mwongo.)
      4. Jambo hili linahusianaje na unyenyekevu? (Kuwa msikivu kwa kile usichokifahamu, na ukiri pale usipofahamu, badala ya kupindua mambo.)
      5. Unapoyafikiria maneno ya Aguru, je, yanatufundisha nini kuhusu uhusiano wetu na Mungu? (Mungu ndiye rejea yetu. Tunapaswa kuwa wanyenyekevu tunapolinganishwa na Mungu.
        1. Tunapoanza kupindua mambo, na kudai kwamba yako sahihi kwa sababu sisi ni Wakristo, hadhi ya nani inaathirika? (Tunadai kwamba tunazungumza kwa niaba ya Mungu! Mungu anasema, “Hawapindui mambo kwa Jina Langu!”)
  2. Manufaa ya Unyenyekevu
    1. Soma Mithali 30:7-8. Msemo wa kawaida unaotumika hapa Marekani unasema kuwa “orodha ya vitu ndani ya kapu.” Msemo huu unamaanisha orodha ya vitu unavyotaka kuvifanya kabla hujafariki. Kwa mfano, inaweza kuwa “kutembelea bonde refu jembamba lenye mkondo wa maji (the Grand Canyon),” au “kuruka angani kwa kutumia parachuti.” Sina uhakika kama nina chochote kwenye “kapu” langu, lakini Aguru ana vitu viwili kwenye kapu lake. Ni vitu gani hivyo? (Kuwa mkweli na mwaminifu. Kuwa “katikati ya barabara” katika masuala ya fedha.)
      1. Ninafahamu lengo la uaminifu, lakini kwa nini utafute kuwa na kitu cha wastani kwenye suala la utajiri?
    2. Soma Mithali 30:9. Hili hapa ndilo jibu linalohusu kulifanya jambo kwa wastani ndio liwe lengo. Kuna matatizo gani kwenye utajiri na umaskini? (Tatizo la utajiri ni kwamba unautegemea utajiri badala ya kumtegemea Mungu. “Unamkana” Mungu. Tatizo la umaskini ni kwamba unashawishika kuiba – na Mungu haupuuzii (hajifanyi kutouona) wizi hata kama wewe ni maskini.)
    3. Soma Mithali 30:10. Hii inahusianaje na unyenyekevu? (Kwa nini umkosoe mwajiriwa mwenzako? Je, lengo linaweza kuwa ni kukufanya uonekane kuwa wewe ni bora zaidi kwa bosi wako? Kama hivyo ndivyo, hilo ni tatizo la unyenyekevu.)
      1. Nani anayekulaani hapa? (Mwajiriwa mwenzako!)
    4. Soma Mithali 30:11-12. Watu wangapi wanawalaumu wazazi wao kutokana na matatizo waliyo nayo maishani mwao?
      1. Nani anayepaswa kubeba lawama katika haya mafungu? (Mtoto ana “uchafu,” lakini anadhani kwamba yu “msafi.” Hii inaashiria kwamba mtoto hafikiri kiuhalisia kuwahusu wazazi wake au yeye mwenyewe.)
    5. Soma Mithali 30:13-14. Je, kuna matatizo gani halisi katika maisha ya huyu mtoto? (Majivuno na maneno yakatayo. Huyu si mtu mwema.)
      1. Nani anaye athirika na huyu mtu mwovu? (Maskini na mhitaji.)
      2. Kwa nini maskini na wahitaji ndio wanaochaguliwa? (Wanaonekana kutokuwa na utetezi.)
    6. Soma Mithali 30:15-16. Je, tumebadili uelekeo? Je, sasa Aguru anazungumzia anguko la maskini? Kama sivyo, nani ambaye ni “mruba” na binti zake? (Hawa ni watu ambao wanataka uwapatie vitu.)
      1. Kwa nini Aguru anaingia kwenye orodha ya vitu “ambavyo kamwe haviridhiki?”
      2. Ikiwa Aguru alidhamiria kufikisha uumbe fulani kuhusu baadhi ya watu, kwa nini alitumia vitu visivyokuwa na uhai kama vile moto, maji na kuzimu? (Huenda anasema kuwa hiyo ndio asili ya baadhi ya watu. Huenda anasema kuwa hiyo ndio asili ya baadhi ya matatizo – kamwe hayatatuliwi hapa.)
        1. Je, kundi hili “lisiloridhika kamwe” linahusiana kivyovyote vile na unyenyekevu? (Hisia za haki ya umiliki ni tatizo la unyenyekevu.)
    7. Soma Mithali 30:20. Kwa nini mada inayohusu ulaji inaletwa hapa? (Inaonesha kwamba mwanamke huyu anaona kuwa ni kawaida sana kuhusu kile alichokitenda.)
      1. Unawezaje kutumia masomo haya hapa kwenye suala la uvumilivu? (Kama ambavyo mwana mwovu alivyowalaumu wazazi wake, lakini bado alikuwa “msafi (mwema) machoni pake, vivyo hivyo mwanamke mzinifu ana majivuno/majisifu mabaya kwamba hajatenda jambo lolote baya.)
    8. Soma Mithali 30:32-33. Ni katika hatua gani tunapaswa kushughulikia majivuno? (Mpambano upo akilini. Tunatakiwa kuzuia majivuno yetu hapo (weka mkono wako juu ya kinywa chako) na usiache maneno yakakuponyoka kutoka kinywani mwako na kusababisha ugomvi.)
  3. Rafiki, je, majivuno yana nafasi gani maishani mwako? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu sasa hivi ili akusaidie “kuweka mkono wako juu ya kinywa chako?”
  4. Juma lijalo: Wanawake na Mvinyo.