Pambano la Ulimwengu Kuhusu Tabia ya Mungu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Sote tunafahamu kwamba Mungu ni mwema, sawa? Kimsingi, katika kanisa langu la zamani tuliongezea maneno “wakati wote, na wakati wote, Mungu ni mwema.” Kwa hiyo je, kuna jambo gani la kujifunza juma hili? Unaweza kufahamu kwamba Mungu ni mwema, lakini ni ukweli kabisa kuwa watu wengi hawana uhakika. Jambo baya kabisa kwenye hilo tatizo ni kwamba wewe unaweza kuwa msingi ambao watu hao wanajenga dhana yao kumhusu Mungu. Hebu tuone kile Biblia inachokisema juu ya suala hili na kile tunachopaswa kukifanya!
- Tatizo la Ulimwengu
- Soma Ayubu 1:1-3. Tunajifunza nini juu tabia ya Ayubu? (Alikuwa “mkamilifu na mwelekevu.” Alikuwa mtu mkuu.)
- Tunajifunza nini juu ya masuala ya kifedha? (Alikuwa tajiri.)
- Tunajifunza nini juu ya hadhi yake? (Alikuwa “mkuu sana kuliko watu wote.”)
- Tunajifunza nini juu ya ukubwa wa familia yake? (Familia yake ilikuwa kubwa!)
- Soma Ayubu 1:4-5. Je, Ayubu alikuwa na mtazamo gani dhidi ya maisha ya kiroho ya watoto wake? (Alijihusisha nayo kikamilifu. Alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa kwa ajili yao na kimsingi aliungama dhambi zao.)
- Je, wazazi wanaweza kuungama dhambi za watoto wao? (Soma 1 Yohana 5:16-17. Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana mwenendo wa Ayubu pamoja na haya mafungu kwa muda mrefu. Sidhani kama ninaelewa kikamilifu kinachoendelea – lakini inaonekana kwamba baadhi ya dhambi zinaweza kusamehewa kwa njia ya maombi ya watu wengine.)
- Soma Ayubu 1:6-7. Kwa nini Shetani anakuwa sehemu ya hii kamati katika huu mkutano?
- Je, swali la Mungu linamaanisha nini? Je, Mungu anatilia mashaka juu ya mahali ambapo Shetani anakaa/anaishi? Je, Mungu anautia changamoto uwepo wa Shetani?
- Soma Ezekieli 28:13-14. Je, huyu kiumbe mwenye utukufu anaishi wapi? (Mbinguni. “Katika mlima mtakatifu wa Mungu.”)
- Soma Ezekieli 28:15-16. Kitu gani kilimtokea huyu kiumbe mwenye utukufu? (Kwa sababu ya uovu, alifukuzwa kutoka mbinguni.)
- Soma Ezekieli 28:17. Je, chanzo cha uovu wa huyu kiumbe kilikuwa ni kipi? (Kiburi kilichotokana na uzuri wake. Kiburi hicho kiliharibu fikra ya huyu mtu.)
- Soma Ufunuo 12:7-9. Je, hii inaashiria kuwa sura halisi ya kiumbe mwenye utukufu ni yupi? (Shetani.)
- Hebu tusome tena Ayubu 1:6-7 kisha uingize kile tulichojifunza katika maelezo ya utangulizi kutoka katika kitabu cha Ezekieli na Ufunuo. Kwa nini Shetani yupo duniani? (Kwa sababu alitupwa kutoka mbinguni hadi duniani.)
- Je, Mungu alilitambua jambo hili? (Ndiyo! Kulikuwa na pambano kuu kati ya Mungu na Shetani.)
- Unadhani basi ni kitu gani ambacho kimsingi Mungu alikuwa akikiuliza? (Sidhani kama Mungu anauliza jambo lolote. Inaonekana mkutano ulikuwa unaendelea mbinguni. Mungu anamdhihaki Shetani kwa kumkumbusha kuwa yeye si mkaazi tena wa mahali penye kustahili mbinguni, badala yake yeye ni mkaazi wa duniani.)
- Je, Mungu alilitambua jambo hili? (Ndiyo! Kulikuwa na pambano kuu kati ya Mungu na Shetani.)
- Soma tena jibu la Shetani katika sehemu ya mwisho ya Ayubu 1:7. “Dunia” ndilo lingekuwa jibu sahihi. Je, asili ya jinsi Shetani alivyojibu inaashiria nini? (Shetani anajivuna kwamba ingawa alifukuzwa na kwenda duniani, sasa yeye ndio mtawala wa dunia.)
- Soma Ayubu 1:8. Je, Mungu anataka kufahamu kama Shetani amekutana na Ayubu? (Hapana. Mungu anayatia changamoto madai ya Shetani kwamba yeye ndio mtawala wa dunia. Mungu anamkumbusha Shetani kwamba mtu mkuu aliyepo katika upande wa Mashariki ni mfuasi wa Mungu, na si mfuasi wa Shetani. Kiukweli, Ayubu anamheshimu Mungu, bali “anamwepuka” Shetani.)
- Soma Ayubu 1:9-11. Shetani angeweza kujibu kuwa, “Ninalishughulikia tatizo hilo.” Kwa nini alijibu vile alivyojibu? (Shetani anamdhihaki Mungu. Anamfananisha Ayubu na kahaba – anamtumikia Mungu ili apate fedha, na si kwa sababu ya upendo wake kwa Mungu au kwa sababu ya kupenda kutenda kilicho sahihi.)
- Kwa nini Shetani alisema hivi? Je, hili ni lengo tu la kumdhihaki Mungu, au unadhani kuwa Shetani anaamini jambo hili?
- Soma Mwanzo 3:1-5. Je, Shetani alishindaje nafasi yake duniani? (Alimwahidi Hawa jambo alilodai kuwa Mungu asingempatia. Alimpa rushwa.)
- Pitia kwa harakaharaka Kumbukumbu la Torati 28 na usome Malaki 3:10-11. Je, mashtaka ya Shetani ni ya kweli? (Ukweli uliochanganywa ndio njia ya utendaji wa Shetani. Ndiyo, ni kweli kwamba kwa ujumla kumfuata Mungu huleta mibaraka. Swali kwa Ayubu na kwa kila mmoja wetu ni hili: je, unamfuata Mungu kwa sababu ya mibaraka yake?)
- Soma Ayubu 1:12. Je, ni nani anayejaribiwa hapa? Je, hii ni changamoto kwa tabia ya Mungu au ni changamoto kwa tabia ya Ayubu? (Angalao ni jaribu kwa Ayubu. Je, anafanana na kahaba? Au, je, anamtumikia Mungu kwa upendo na uaminifu kwa mambo ya Mungu? Kwa upande mwingine, Mungu aliyatia changamoto mamlaka ya Shetani duniani kwa kumbainisha Ayubu.)
- Je, tabia ya nani isiyo ya muhimu? (Tabia ya Shetani! Tunafahamu mambo mabaya yatatokea Ayubu atakapokuwa “mikononi” mwa Shetani.”)
- Ukisoma kitabu chote cha Ayubu (au hata sehemu iliyosalia ya sura ya kwanza ya kitabu cha Ayubu), utaona kwamba mambo ya kutisha yanamtokea Ayubu. Kama wewe ndio ungekuwa Ayubu, je, ungesema nini endapo ungefahamu sababu halisi ya mambo ya kutisha yaliyokuwa yakikutokea maishani mwako?
- Je, huu ni “utunishianaji vifua” kati ya Mungu na Shetani – na Ayubu anateseka?
- Au, je, hii ni changamoto ya msingi kuliko zote kwa tabia ya Mungu?
- Je, unadhani kuwa hili ni jambo la “mara moja?” Au, je, unadhani kuwa mustakabali wa Ayubu unaendelea kurudiwarudiwa hapa duniani?
- Chukulia kwamba umejibu kuwa, “Ndiyo, nadhani unarudiwa mara nyingi sana zisizoweza kuhesabika, na mustakabali huo unaweza kuwa unaendelea maishani mwangu sasa hivi!” Kama jambo linalohusika ni tabia ya Ayubu (tofauti na tabia ya Mungu), je, jambo hili linaendanaje na neema? Je, jambo hili linaendanaje na kuhesabiwa haki kwa imani?
- Soma Ayubu 1:1-3. Tunajifunza nini juu tabia ya Ayubu? (Alikuwa “mkamilifu na mwelekevu.” Alikuwa mtu mkuu.)
- Jibu la Ulimwengu
- Soma Mathayo 20:17-19. Je, hii inafunua nini kuhusu endapo kafara ya Yesu kwa ajili yetu ilikuwa ni ya hiari? (Aliitabiri. Yesu angeweza kuepuka kwenda Yerusalemu.)
- Angalia fungu la 19 kisha uangalie mambo matatu ambayo Yesu alisema kuwa Mataifa watamtendea. Je, huwa unafurahia watu wanapokucheka – si kama matokeo ya utani, bali kwa sababu wanadhani kuwa hustahili heshima?
- Je, huwa unafurahia watu wanapokusababishia maumivu makali, na wanafanya hivyo kwa sababu tu wanaweza kufanya hivyo?
- Je, unafurahia kuuawa kwa njia yenye maumivu makali?
- Angalia fungu la 19 kisha uangalie mambo matatu ambayo Yesu alisema kuwa Mataifa watamtendea. Je, huwa unafurahia watu wanapokucheka – si kama matokeo ya utani, bali kwa sababu wanadhani kuwa hustahili heshima?
- Soma 1 Yohana 4:10. Kwa nini Yesu alipitia dhihaka, mateso na kifo kwa hiari? (Kwa sababu alitupenda. Alipatanisha dhambi zetu.)
- Soma Warumi 3:21-25. Je, kuhesabiwa kwetu haki kunategemeana na utii wa sheria? (Hapana! Huku ni “kuhesabiwa haki kutoka kwa Mungu, kinyume na sheria.”)
- Je, kuhesabiwa kwetu haki kunategemeana na nini? (Sote tumetenda dhambi, lakini Yesu alikufa kwa ajili yetu. Jambo hili linaakisiwa katika huduma ya patakatifu ambayo tumekuwa tukijifunza katika robo hii.)
- Je, tunatakiwa kufanya nini? (Kuwa na imani kwa damu yake. Hii ni kinyume na imani kwa matendo yetu mema.)
- Soma Warumi 3:26. Ni kwa namna gani kifo cha Yesu kwa ajili yetu ni tendo la haki? (Je, unakumbuka tulipojifunza 2 Samweli 14:4-9? Kisa hiki kinaakisi “utawala wa sheria.” Endapo mfalme alitangaza kwamba sheria haitafuatwa, basi aliwajibika yeye binafsi kwa uvunjaji wa sheria. Kwa upendo Yesu alipoamua kututoa kwenye adhabu ya kifo – kile ambacho sheria inakitaka kitendeke kwa ajili ya dhambi – aliichukua adhabu yeye mwenyewe. Hivi ndivyo ambavyo Warumi 3:26 inaweza kurejea kile kinachoonekana kutokutenda haki kukubwa kabisa kama “haki.”)
- Soma Mathayo 20:17-19. Je, hii inafunua nini kuhusu endapo kafara ya Yesu kwa ajili yetu ilikuwa ni ya hiari? (Aliitabiri. Yesu angeweza kuepuka kwenda Yerusalemu.)
- Utukufu kwa Mungu
- Hebu turejee kwa Ayubu. Utakumbuka kwamba tuliangalia maswali mawili: “Tabia ya nani inayohusika, ya Mungu au ya Ayubu? Na, “Kama tabia ya Ayubu ndio inayohusika, je, inaendanaje na kuhesabiwa haki kwa imani?” Soma Mathayo 5:16. Je, kujikita kwa Ayubu kunajibuje swali kuhusu tabia ya Mungu? (Matendo yetu yanamwakisi Mungu. Endapo Ayubu alikuwa mwaminifu, hilo lilimwakisi Mungu.)
- Soma 1 Yohana 4:11-12. Ayubu angewezaje kuonesha kuwa hoja ya Shetani juu ya ukahaba ilikuwa ya uongo? (Wafuasi wa Shetani wanamfuata kwa kile wanachodhani kuwa watakipata. Wafuasi wa Mungu wanamfuata kwa sababu ya upendo.)
- Je, matendo yetu yanajalisha? Je, kushika kwetu sheria ya Mungu kunajalisha? (Yote hayo hayana lolote katika kutupatia wokovu. Lakini, ni kiini katika kuakisi utukufu wa Mungu. Endapo tutakuwa watiifu, endapo tunawapenda wengine, basi tunafunua tabia ya Muumbaji na Mkombozi wetu.)
- Rafiki, je, utamwomba Roho Mtakatifu leo akusaidie ili umsifu Mungu kwa matendo yako? Kwa upendo wako?
- Juma lijalo: Ushawishi Kutoka Patakatifu.