Kafara

(Mwanzo 3, 4 & 22; Mambo ya Walawi 2, 4 & 7)
Swahili
Year: 
2013
Quarter: 
4
Lesson Number: 
3
 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: “Kafara” si dhana maarufu. Nani atakaye kutoka kafara kitu fulani? Inamaanisha kukitoa kitu fulani, sawa? Sote huwa tunatazamia kupokea vitu, na si kutoa vitu! Au je, hatufanyi hivyo? Je, umewahi kuhisi furaha ya kutoa msaada? Furaha ya kumpatia mtu kitu ambacho anakihitaji zaidi yako? Je, Mungu anataka nini kutoka kwetu linapokuja suala la kafara? Je, kafara ndio njia ya sisi kupata vitu? Somo letu la Biblia juma hili linahusu kafara, hebu tuzame kwenye Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!

radhi kutoa kafara kwa ajili ya azimio jema? (Hapana. Adamu ni mbaya zaidi. Kimsingi anamlaumu Mungu na yuko radhi kumtupa mkewe chini ya basi! Angalao Hawa alikuwa na busara kwa kutomlaumu Mungu.)

ya hii kanuni ni ipi? (Damu ni uhai na inaleta upatanisho wa dhambi ili kwamba usiweze kufa. Damu ni kafara ya dhambi. Kwa hiyo, huwezi kutumia damu kwa jambo lolote lile.)

taarifa hizi za kina? (Ninashawishika kwamba hapa jambo zima si la kawaida na la kushtusha, kuchukiza hisia zetu za haki na usawa. Kwa nini? Kwa sababu ni jambo lisilo la kawaida na la kushangaza kwamba Mwana wa Mungu alikufa kifo cha kutisha kwa ajili ya dhambi zetu. Kisa cha Ibrahimu kinaelekeza kisa cha Mungu. Kafara ya Yesu kwa ajili yetu ni jambo lisilo la kawaida na la kushangaza. Upendo wake kwa watu wanaokataa kupokea lawama kwa ajili ya dhambi zao si wa kawaida na wa kushangaza!

  1. Dhambi inaingia
    
    1. Soma Mwanzo 3:1-5. Je, suala gani la kafara unaloliona kwenye mazingira haya ya kuutengeneza ukweli? (Wanadamu wanatoa kafara ya mti mmoja kisha wanafurahia yote yaliyosalia.)
      1. Je, nyoka anampa nini Hawa? (Kuwa kama Mungu.)
      2. Je, huo ni wito wa kujikana nafsi? (Ni kinyume chake tu, ni wito wa kujitwalia zaidi.)
    2. Soma Mwanzo 3:6-7. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu. Je, walipata au kutoa kitu? (Walipoteza jambo kubwa sana, ikiwemo kufunikwa kwao.)
      1. Hebu angalia huu muunganiko. Kwa kutafuta kupata faida, hawakuipata na pia walipoteza.
    3. Soma Mwanzo 3:11-12. Je, Adamu anaonekana kusikitikia dhambi yake?
      1. Je, Adamu yu radhi kutoa kafara? (Sasa yu radhi kumtoa mkewe kafara!)
    4. Soma Mwanzo 3:13. Je, Hawa anaonekana kusikitikia dhambi yake?
      1. Je, nani kati ya hawa wawili, Adamu au Hawa, anaonekana kutubu zaidi?
    5. Soma Mwanzo 3:14-15. Sehemu ya mwisho ya haya mafungu mawili ina ahadi kwamba kichwa cha nyoka kitapondwa katika muktadha wa kusababisha maumivu na adha (kero) kwa wanadamu. Je, hii ni ahadi ya namna gani? (Ahadi hii ni juu ya dhambi na ni ahadi kwamba hatimaye wanadamu watalishinda tatizo la dhambi.)
      1. Angalia jambo hili katika muktadha wa Mungu. Je, wanadamu ni kundi la kupendeza lililopo kwa ajili ya jambo jema? Je, wataamsha huruma yako kwa kutenda kosa, lakini wanatubu kwa usahihi? Je, wanadamu wako
  2. Mwitikio wa Dhambi
    1. Soma Mwanzo 4:1-3. Je, Kaini anafanya nini anapoleta sadaka kwa Mungu? (Hii ni sadaka ya kujitoa mwenyewe.)
    2. Soma Mwanzo 4:4-6. Wana wote wawili wanaleta sadaka inayoakisi asili ya kazi zao. Kwa nini Mungu anamwitikia Habili kwa upendeleo zaidi, lakini hafanyi hivyo kwenye sadaka ya Kaini? (Fungu halisemi chochote. Lakini, kwa sababu fulani fulani, sadaka ya Habili i sahihi.)
    3. Soma Mwanzo 4:6-7. Je, hili linaashiria nini kuhusu sadaka ya Kaini? (Haikuwa sahihi. Ilishindwa kufikia viwango ambavyo havikubainishwa.)
    4. Soma Kutoka 12:21-23. Je, damu ya mnyama inaitendea nini familia? (Inamwepusha “mwenye kuharibu” asiiangamize familia.)
    5. Soma Mambo ya Walawi 4:27-29. Hatimaye, tunaanza kuona taswira ya kile kinachoendelea. Je, sababu ya kumchinja mbuzi ni ipi? (Ni sadaka kwa ajili ya dhambi.)
      1. Katika jambo hili hebu tusome kisa cha Kaini na kisa cha Pasaka. Kwa nini sadaka ya Kaini haitoshi? Kwa nini damu ya kondoo wa Pasaka n+i ya msingi? (Mnyama anakufa kwa ajili ya dhambi za mtu. Kwa namna fulani damu ya mnyama inamlinda mdhambi. Tunaona wazo hili katika kumbukumbu ya historia ya kale kwenye Biblia kuhusu programu ya Mungu ya kuishinda dhambi linahusisha kafara ya mnyama na ukweli kwamba damu inawaokoa wanadamu.)
        1. Je, hii ni kafara binafsi? (Kama unammiliki mnyama, angekuwa kafara, lakini kama mnyama amekufa badala yako, itaepusha sadaka nyingine kubwa.)
        2. Je, kila sadaka/kafara ni njema? (Hapana! Kaini alikuwa akitoa sadaka, lakini hakuwa akitoa sadaka kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.)
    6. Soma Mambo ya Walawi 4:1-3 na Mambo ya Walawi 6:1-3. Sura ya 4 ya kitabu cha Mambo ya Walawi ni ya mfano hasa kwa rejea nyingi zinazozungumzia utendji wa dhambi bila kukusudia na kafara inayohitajika kwa ajili ya dhambi hiyo. Je, ni aina gani za dhambi tunazozisoma katika sura ya 6 ya kitabu cha Mambo ya Walawi? (Hizi ni dhambi za makusudi. Kwa hakika, hizi ni dhambi zinazohusisha si dhamira tu, bali pia kwa namna fulani zinahusisha mpango wa kuzitenda.)
      1. Soma Mambo ya Walawi 6:4-6. Je, dhambi ya makusudi inaweza kusamehewa? (Ndiyo. Shukrani kwa hilo. Utaona kwamba unapopanga kuchukua kitu kutoka kwa mtu, Mungu anataka ukirudishe pamoja na kuongezea adhabu ya asilimia 20.)
    7. Soma Mambo ya Walawi 17:10-12. Hebu chukulia mafungu haya kuwa kama vile ni kanuni ya hisabati au uhakiki (theorem) wa maumbo. Je, nadharia iliyo nyuma
    8. Je, tunapata taswira ya aina gani juu ya msamaha wa dhambi chini ya mfumo wa utoaji wa kafara? (Kafara ya uhai, damu ya mnyama inakuokoa kutoka mautini.)
  3. . Utoaji wa Sadaka kwa Ujumla
    1. Soma Mambo ya Walawi 2:1-3 na Mambo ya Walawi 2:14. Utakumbuka kuwa Kaini alileta tunda kama sadaka. Hapa, nafaka ndio sadaka. Kwa nini sadaka hii inakubalika wakati ile ya Kaini haikukubalika? (Sadaka tofauti tofauti zina malengo tofauti. Hii sadaka ya nafaka inaonekana kuakisi shukrani kwa mibaraka ya Mungu katika mavuno. Unatoa sadaka sehemu ya nafaka kwa sababu ya mbaraka mkubwa wa mavuno. Sadaka ya Kaini ilikuwa na kasoro kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya msamaha wa dhambi.)
    2. Soma Mambo ya Walawi 7:7-9. Je, sadaka inasaidia jambo gani jingine dogo? (Inawategemeza makuhani. Inategemeza mfumo wa upatanisho wa dhambi.)
    3. Soma Mambo ya Walawi 7:11-13. Je, sadaka hizi zilitokana na wazo gani? (Tunamrudishia Mungu sehemu ya mbaraka wake mkubwa. Hilo ndilo wazo la jumla lililopo katika hii mada inayohusu sadaka. Tunatoa sadaka ya mnyama, lakini maisha yetu yanaendelea. Tunatoa sadaka ya mavuno yetu ya kwanza, lakini tunaendelea kuyatunza mavuno.)
  4. Sadaka ya Ajabu
    1. Soma Mwanzo 22:1-2. Tafakari kuhusu maelekezo na namna maelekezo yalivyoandikwa. Je, maelekezo haya yanaendana na Mungu mwenye upendo? (Ni vigumu kabisa kuendana naye. Mungu hamwambii tu Ibrahamu kumuua mwana wa ahadi, bali pia analifanya jambo hilo liwe na machungu zaidi kwa kusema kuwa huyu ni mwana wako wa “pekee” “umpendaye.”)
      1. Je, haya maelekezo kwamba Isaka anapaswa kuwa sadaka ya “kuteketezwa” yanaongezea nini kwenye maumivu ya Ibrahamu?
    2. Soma Mwanzo 22:3. Unadhani ni kwa nini Ibrahimu aliondoka alfajiri? (Ubashiri wangu ni kwamba hakutaka kujadili jambo hili na mkewe, Sara.)
    3. Soma Mwanzo 22:6-8. Unafikiria nini hapa – je, Ibrahimu anamdanganya mwanaye, au Ibrahimu anadhani kuwa Mungu anao mpango mbadala?
    4. Soma Waebrania 11:17-19. Je, hii inaashiria kwamba Ibrahimu alikuwa akifikiria nini juu ya mpango mbadala?
    5. Soma Mwanzo 22:9-12. Je, hii inatuambia kuwa kisa hiki cha kikatili kinahusu nini? (Kumjaribu Ibrahimu. Mwanzo 22:1 inasemaa jambo hilo hilo.)
      1. Hebu tuwe wakweli kabisa hapa. Je, bado lingesalia kuwa jaribio la kweli endapo Mungu asingeongezea kwamba huyu alikuwa mwana wa Ibrahimu wa “pekee” na “apendwaye?”
      2. Kama umejibu, “ndiyo,” kwa swali hilo hapo juu, je, unakielezeaje hiki kisa? Roho Mtakatifu Ndiye anayetupatia hiki kisa, kwa nini kinajumuisha
    6. Rafiki, je, unaweza kuona wazo linaloendana na wito wa Mungu kwetu kuhusu kutoa sadaka? Si sadaka kabisa. Tunampa Mungu sehemu ndogo naye anatupatia yote yaliyosalia. Pale tu tunapojaribu kuchukua vyote (kama alivyofanya Hawa) ndipo tunapopoteza vyote. Je, utaamua leo kuingia mkataba dhidi ya wito wa Mungu wa kutoa sadaka?
  5. Juma lijalo: Masomo Kutoka Patakatifu.