Somo la 12: Upendo na Haki: Amri Kuu Mbili

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mathayo 5, 19, 22 & 25, Mambo ya Walawi 19
Swahili
Year: 
2025
Quarter: 
1
Lesson Number: 
12

Somo la 12: Upendo na Haki: Amri Kuu Mbili

(Mathayo 5, 19, 22 & 25, Mambo ya Walawi 19)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unajua “haki” maana yake ni nini? Watu wengi watajibu, “Ndiyo,” lakini nina mashaka juu ya usahihi wa majibu yao. Kwa sasa nipo kwenye mjadala na watu kisasa sana kuhusu “haki.” Wamedhamiria kuondoa ubaguzi dhidi ya mbari (race) yao, lakini watu hao hao ni wanatetea ubaguzi dhidi ya mbari nyinginezo. Hiyo si haki. Sote tuna hatia ya kosa hili kwa kiwango fulani au kingine. Tunamtaka polisi amwadhibu dereva anayeendesha kwa kasi ambaye ametupita barabarani. Kwa upande mwingine, hatupendi kuadhibiwa pale tunapokuwa tumeendesha kwa mwendo wa kasi. Biblia inazungumzia kwa kina kuhusu kuwasaidia maskini na wanyonge katika jamii. Je, hiyo ni kwa sababu Mungu anawapendelea maskini na wanyonge, au kwa sababu hao ni watu ambao kuna uwezekano mkubwa jamii ikawanyanyasa kwa kuwaonea? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile inachokisema kuhusu “haki,” na endapo hilo lina chochote cha kujihusianisha na upendo!

  1.    Usawa (Equality) Dhidi ya Haki (Usawa wa Fursa)
    1.    Soma Mambo ya Walawi 19:15. Kwa nini Biblia inafundisha kuwa tusiwapendelee maskini? Kwani matajiri hawana vitu zaidi ya mahitaji yao? (Kuna dhana ya kiutamaduni inayohuzunisha, inayoitwa “usawa wa fursa” inayoashiria kuwa wanadamu wanapaswa kubagua kwa kuwapendelea wengine na kutowapendelea wengine ili kutengeneza jamii yenye “haki” zaidi. Badala yake Biblia inaidhinisha “usawa,” katika vifungu kama hiki ambacho kimsingi kinasema, “tenda haki kwa kila mtu.”)
      1.    Unadhani kwa nini kifungu hiki kinarejelea “kumstahi (diferring)” mwenye nguvu?
    1.    Soma Mathayo 25:14-18. Huu ni mfano. Unadhani “talanta” zimekusudiwa kufafanua jambo gani? (Zinaakisi “uwezo” wa watumwa, manufaa ya asili maishani.)
    1.    Bwana anarejea na watumwa wenye talanta tano na mbili wana kiasi mara mbili zaidi ya kile walichopewa. Wanasifiwa kwa usawa. Soma Mathayo 25:24-28. Je, mtumwa mwenye talanta moja anadai kuwa bwana wake hatendi haki?
      1.    Jambo gani mahsusi ni msingi wa madai ya kutotendewa haki? (Kwamba bwana alitumia mali yake kutengeneza fedha zaidi bila kufanya kazi yoyote.)
    1.    Angalia tena Mathayo 25:28. Je, kisa hiki kinaunga mkono usawa wa fursa? Dhana ya kwamba jamii inapaswa kuachana na dhana ya ustahili (merit) na kutendeana kwa usawa na kujaribu kutufanya sote tuwe sawa? (Hiki ni kisa kinachohusu kuzawadia ustahili (sifa njema) na kukataa mawazo ya usawa wa fursa. Hata kama awali watumwa hawakupewa talanta sawa maishani, bwana aliwatarajia watumie talanta walizopewa. Kama kisa hiki kingekuwa na chembechembe ya usawa wa fursa ndani yake, talanta moja angepewa mtumwa mwenye talanta mbili, si mtumwa mwenye talanta tano.)
  1.   Upendo na Haki
    1.    Soma Mathayo 22:34-36. Je, mwanasheria huyu ana udadisi wa kweli kuhusu jibu la swali lake? (Hapana. Lengo la kuuliza swali ilikuwa ni “kumjaribu” Yesu.)
      1.    Hili ni jaribu la namna gani? Mafarisayo wanatumaini kutimiza jambo gani kwa swali hili?
      1.    Je, unadhani kwamba baadhi ya amri ni kuu kuliko nyingine?
    1.    Soma Mathayo 22:37-39. Mungu anatutaka tuwe na upendo wa namna gani? (Sote tunapaswa” tujitoe kikamilifu” kwa upendo wetu kwake.)
      1.    Upendo wetu kwa Mungu unatofautianaje na upendo wetu baina yetu?
      1.    Vipi kama Yesu angesema kuwa tunapaswa kumpenda Mungu kama tunavyojipenda wenyewe? Upendo huo ungefananaje?
      1.    Wazazi wangu waliniwekea mazingira ya kufanya kazi ili kujipatia kipato kwa kuvuna stroberi nilipokuwa kijana mdogo. Sasa nina umri wa miaka 74 na bado ninafanya kazi. Ninapaswa kuwachukuliaje watu wanaoamua kutofanya kazi na badala yake kuwa ombaomba? Wajibu kwa upendo wangu kwao ni upi?
    1.    Soma Mathayo 5:43-45. Yesu anautafsirije “upendo” kwa wale ambao ni maadui wetu? (Yesu anamtumia Baba wake kama alama teule (benchmark) ya upendo. Alama hiyo ni kuwatendea watu kwa usawa. Haiwapendelei maadui wetu. Haitutaki tuwatendee chochote ambacho hatutamtendea mtu mwingine yeyote yule. Neno la kiteolojia ni “neema ya kawaida” (common grace).)
      1.    Je, neema ya kawaida ndio njia ambayo tunajipenda wenyewe? (Hapana. Tunajipendelea.)
        1.    Unalifafanuaje hili? (Maadui wetu wanapewa kipimo tofauti cha upendo.)
    1.    Soma Mathayo 19:21-22. Hebu subiri kidogo! Je, kijana huyu anaambiwa awapende wengine zaidi kuliko anavyojipenda mwenyewe? (Naam, ama kwa hakika. Watu hao watapata fedha zake zote naye hatabakiwa na chochote.)
      1.    Je, Yesu anakiuka vipimo vyake mwenyewe?
      1.    Je, tafsiri ya Yesu ya haki ni kuwapendelea maskini?
    1.    Jambo lisilo la kawaida kabisa linaendelea katika kisa hiki. Soma Mathayo 19:16-20. Kuna kasoro gani kwenye mazungumzo haya? (Yesu na kijana huyu wanajadili aina ya matendo yaliyo ya muhimu ili kuupata wokovu.)
    1.    Soma Wagalatia 3:10-11. Je, vifungu hivi vinakinzana? Je, Yesu analazimisha kuwa kijana huyu alaaniwe? (Vifungu hivi vinapatanishwa kiurahisi. Yesu anamwonesha kijana huyu kwamba hawezi kuupata wokovu kwa matendo. Yesu aliwasilisha tendo ambalo hakuwa tayari kulitenda.)
    1.    Soma Mathayo 19:23-25. Kwa nini haiwezekani kiuhalisia lakini si kwa ubayana kwa tajiri kuingia mbinguni? (Kwa sababu matajiri wanaelekea kuyategemea matendo yao. Wamefanikiwa katika mambo ya aina zote.)
    1.    Soma Mathayo 19:26 na Wagalatia 3:13. Hii inatufundisha nini kuhusu namna matajiri wanavyookolewa? (Wanaokolewa kama watu wengine – kwa maisha, kifo, na ufufuo wa Yesu.)
  1.      Neema ya Kawaida, Upendo, na Haki
    1.    Soma Zekaria 7:9-10. Unadhani kwa nini Biblia inatumia neno “usimdhulumu” tofauti na “kumpendelea” mjane, yatima, mgeni/msafiri, na maskini? (Amri ni kutenda kwa usawa. Neema ya kawaida. Ni kutakiwa kutenda haki, si upendeleo maalumu, na si usawa wa fursa.)
    1.    Soma Kutoka 22:21-23 na Warumi 13:10. Kipimo gani cha upendo kinatolewa hapa? (Kwa mara nyingine, tunaambiwa tusimtendee “vibaya,” “kumtesa,” au “kumkandamiza” mgeni/msafiri, mjane, au mtoto yatima.)
    1.    Soma Warumi 13:1-5. Wakristo wanapaswa kufanya nini katika mazingira ambayo maskini au mgeni/msafiri anakiuka sheria? Vipi kama wanaiogopa serikali? (Sote tunapewa wito wa kuitii sheria. Tunaelekezwa tusipingane na mamlaka. Tunaonywa kwamba njia ya kuepuka kuiogopa serikali ni kutii. Kuitii serikali maana yake ni kumtii Mungu.)
      1.    Vipi kuhusu mazingira ambayo sheria ya kibinadamu inakiuka sheria ya Mungu? Vipi kama mtu atavunja na kuingia kwenye nyumba ya mtu mwingine kwa sababu ana njaa? (Jibu la dhahiri si kuelekea kwenye uvunjaji wa sheria. Sheria ya Mungu haihitaji uvunjaji na kuingia kwenye mali za watu.)
  1.   Kutoa Msaada
    1.    Soma Mithali 14:31, Mithali 19:17, Kumbukumbu la Torati 15:11, na Mathayo 25:34-36. Vifungu hivi vinatutia moyo (au kutuamrisha) kuwasaidia maskini. Je, vifungu hivi vinakinzana na kile tulichojifunza kabla katika somo hili? (Hapana. Hapo awali tulijadili upendo, haki, na utii wa sheria. Wakati tunapewa wito wa kuwahurumia maskini, hususan wanapokuwa katika taabu, hatupewi wito wa kukiuka sheria au kuwabagua wengine.)
      1.    Angalia Mathayo 25:40. Yesu anaporejelea kuwasaidia “ndugu,” je, kwa ujumla anawarejelea maskini? (Hii inawarejelea maskini na watakatifu wanaoteseka. Ndugu na dada walio kanisani. Angalia pia Kumbukumbu la Torati 15:11.)
    1.    Soma Mambo ya Walawi 19:9-10. Je, “mgeni/msafiri” anaweza kuwa “ndugu?” (Hapana.)
      1.    Je, maelekezo haya yahusuyo masazo ya mavuno ni mfano wa neema ya kawaida (Si kwa uhakika.)
      1.    Je, maelekezo haya yanaendana na kuzawadia ustahili? (Ndiyo. Mtu aliyelima shamba lake anapata takriban tuzo yote.)
      1.    Je, masazo ya mazao ni zawadi kwa maskini? (Wanatakiwa kufanya kazi kwa kukusanya masalia ya mavuno.)
    1.    Soma Luka 10:25-27. Kimsingi hili ni swali lile lile tuliloliangalia hapo awali katika Mathayo 19:16. Soma Luka 10:29. Ungejibuje swali hili kwa kuzingatia vifungu tulivyojifunza? (Watakuwa watakatifu wenzetu. Haitakuwa ulimwengu kwa ujumla.)
    1.    Kama hukifahamu kisa cha Msamaria Mwema, soma Luka 10:30-37. Kama unakifahamu kisa hicho soma Luka 10:36-37. Je, hapa ni kuweka neema ya kawaida kivitendo? (Hapana.)
      1.    Je, Yesu ametoa maelekezo mapya yaliyo na ukinzani? (Hebu tuyaite kuwa ni ufafanuzi. Hali ya dharura inarekebisha kanuni ya neema ya kawaida.)
    1.    Rafiki, wito wa msingi wa Mungu kwetu ni kuonesha upendo kwa kuwatendea wengine kwa usawa. Hatupewi wito wa kuwatendea vibaya matajiri ili tuweze kuwatendea maskini kwa kuwapendelea. Tunapewa wito wa kuwaonesha fadhila waumini wenzetu na kuwarehemu walio katika hali za dharura. Je, utaitikia wito wa Mungu wa kuwa na upendo na rehema?
  1.    Juma lijalo: Upendo ni utimilifu wa Sheria.