Somo la 11: Ningeweza Kufanya Nini Zaidi?
Somo la 11: Ningeweza Kufanya Nini Zaidi?
(Isaya 5, Mathayo 21, Warumi 3)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Yakobo 3:10-11 inatuambia kuwa chemchemi haiwezi kutoa maji matamu na machungu kwa wakati mmoja. Kutokana na hilo Yakobo anajenga hoja kwamba kinywa kimoja hakiwezi kutoa baraka na laana. Je, Yakobo yuko sahihi? Si kwa uzoefu wangu. Vipi kuhusu uzoefu wako? Watu wema wangapi unaowafahamu walio na tabia mbaya? Watu wabaya wangapi unaowafahamu wanaotenda maovu tu? Watu wengi wana mchanganyiko wa mambo yote mawili. Yakobo analielewa tatizo la mchanganyiko huo na anajenga hoja kwamba kilicho kweli kwa maji kinapaswa kuwa kweli pia kwa Wakristo. Yakobo anatoa wito wa kuwa na kiwango cha hali ya juu. Kiwango cha Mungu. Ugumu iliopo kiuhalisia ni kwamba watu wengi wanawachukulia wengine kwa namna “mchanganyiko” na pia wanautumia mtazamo huu wa “mchanganyiko” kwenye uelewa wao wa Mungu. Juma hili tunaliangalia suala hilo na kujibu swali la Mungu, “Ningeweza kufanya nini zaidi?” Imetosha kuwashawishi wanadamu kwamba tabia ya Mungu ni safi, na safi pekee. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia!
- Mmiliki wa Shamba la Mizabibu
-
- Soma Isaya 5:1. Huu ni wimbo wa namna gani? (Wimbo wa mapenzi.)
-
-
- Kitu gani kinapendwa hapa? Mmiliki wa shamba la mizabibu au shamba la mizabibu? (Inaonekana ni vyote viwili. Mmiliki wa shamba la mizabibu anapendwa, lakini wimbo wa mapenzi unahusu shamba la mizabibu.)
-
-
- Soma Isaya 5:2. Je, kazi iliyofanyika kwenye shamba la mizabibu imefanyika kwa umakini? (Tunaambiwa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika. Tunaambiwa “mizabibu iliyo mizuri” ilipandwa. Inaonekana kazi ilifanyika kwa umakini.)
-
-
- Jambo gani linaweza kuanzisha mjadala kuhusu ubora wa uandaaji wa shamba la mizabibu? (Lilizaa zabibu-mwitu.)
-
-
- Soma Isaya 5:3. Kwa nini wananchi wa Yerusalemu na wa Yuda wanapewa wito wa kutoa uamuzi? (Swali, kama lilivyogusiwa hapo juu, ni “Nani anayewajibika kwa zabibu-mwitu? Kwa nini kazi hii ya ukulima ilifeli?”)
-
- Soma Isaya 5:4. Mmiliki wa shamba la mizabibu anatoa hoja gani kwamba hana kosa? (Anataka kujua angetakiwa kufanya nini zaidi? Kwa nini palikuwepo na zabibu-mwitu?)
-
-
- Ungejibuje swali hili? (Ningejibu kwamba mimi si mtaalamu wa suala hilo, na sina taarifa za kutosha kutoa uamuzi kwamba nani ana kosa.)
-
-
-
- Mtazamo wa mmiliki wa shamba la mizabibu ni upi kuhusu mtu aliye na kosa? (Anasema kuwa hajui chochote cha ziada ambacho angeweza kufanya. Si kosa lake. Jambo la ajabu ni kwamba anawakaribisha watu wengine kutoa uamuzi wa nani ana kosa.)
-
-
-
-
- Au anawataka wakubali kuwa yeye hana kosa?
-
-
-
- Soma Isaya 5:5-6. Je, mwitiko wa mmiliki wa shamba la mizabibu una mantiki? (Mambo mawili. Ni shamba lake la mizabibu, anaweza kulitendea vyovyote atakavyo. Pili, kama lisingekuwa na uzio, ukuta, hakuna kupogolea, na hakuna kupalilia, ungetarajia zabibu za namna gani? (Zabibu-mwitu. Mmiliki wa shamba la mizabibu anasema kuwa sasa zabibu zinapokea aina ya matunzo inayozalisha zabibu-mwitu.)
-
- Hebu turudi kwenye Isaya 5:1. Ni kwa jinsi gani huu ni wimbo wa mapenzi? Nani anayependwa? (Mmiliki wa shamba la mizabibu ndiye “mpendwa” ambaye ndiye kiini cha wimbo. Mwimbaji anamwambia mmiliki wa shamba la mizabibu, “Ninakaupenda hata kama ukulima huu haukuzaa kama ilivyotarajiwa.”)
-
- Soma Isaya 5:7. Wimbo huu unahusu nini hasa? (Mungu na watu wake. Taifa la Mungu ndilo shamba la mizabibu na watu ni mizabibu iliyo mizuri iliyopandwa katika ardhi yenye rutuba sana.)
-
-
- Kitu gani kinazifanya ziwe zabibu mwitu? (Badala ya hukumu ya haki, wanatenda mambo ya umwagaji damu. Badala ya haki, wanampigia Mungu kelele.)
-
-
-
- Nani ana kosa? (Watu, si Mungu.)
-
-
-
- Je, Mungu anawaadhibu watu? (Hapana. Anachukua tu faida za pekee (zaidi ya mvua) alizowapatia.)
-
- Smamba la Mizabibu Lililokodishwa
-
- Soma Mathayo 21:33. Yesu anasimulia mfano huu. Je, anaonekana kama anafafanua Isaya 5? (Matendo ya mmiliki wa shamba la mizabibu yanaonekana kukaribia kufanana kabisa. Kilicho tofauti ni kwamba mmiliki analiacha shamba la mizabibu mikononi mwa watu waliolikodisha.)
-
- Soma Mathayo 21:34-35. Tunaona mkengeuko (deviation) gani mkubwa kutoka katika kisa cha Isaya 5? (Zabibu zinaonekana kuwa nzuri tu. Zinastahili kuvunwa.)
-
-
- Tatizo ni lipi? (Wapangaji wanataka kumiliki zabibu, na wako radhi kuua ili kutimiza azma hiyo.)
-
-
- Soma Mathayo 21:36. Je, mauaji ya kundi la kwanza la watumwa yalikuwa na dosari? Kwamba wapangaji waliona kosa lao na kubadilika? (Hapana. Hii inaakisi tabia ile ile ya wapangaji.)
-
- Soma Mathayo 21:37-39. “Mwana” ni nani katika mfano huu? (Ni Yesu.)
-
-
- Jambo gani linawahamasisha wapangaji kumwua mwana wa mmiliki? (Wanataka “urithi.”)
-
-
-
-
- Unadhani hii inamaanisha nini?
-
-
-
- Hebu turuke vifungu kadhaa na tusome Mathayo 21:45. Je, viongozi wa Kiyahudi wako sahihi? (Ndiyo. Na hii inajibu swali linalohusu urithi. Walitaka kuhusudiwa, kusifiwa, na kuabudiwa na watu. Kile kilichokuwa cha Mungu peke yake ndicho walichokitaka. Hilo pia lilikuwa lengo la Shetani.)
- Kuyaunganisha Mashamba ya Mizabibu
-
- Kitu gani kilikuwa na kasoro katika kisa cha Isaya 5? (Zabibu.)
-
- Kitu gani kilikuwa na kasoro katika kisa cha Mathayo 21? (Wale waliotakiwa kuzitunza zabibu kwa niaba ya mmiliki ambaye hakuwepo.)
-
- Kuviunganisha visa hivi viwili vya mashamba ya mizabibu kunatoa fundisho gani? (Watu wa Mungu na viongozi wa kiroho – wote wana kasoro.)
-
- Rejea nyuma kwenye sehemu ya utangulizi. Visa hivi viwili vya mashamba ya mizabibu vinazungumza nini kuhusu asili ya Mungu? (Anaweka vigezo vyote kwa ajili ya zabibu kamilifu. Asili ya zabibu na kufeli kwa viongozi wa kiroho halikuwa kosa la Mungu.)
-
-
- Mmiliki wa shamba la zabibu angeweza kufanya nini zaidi?
-
-
-
- Tunapaswa kuhitimisha nini kuhusu washiriki wenzetu wa kanisa na viongozi wetu wa kanisa? (Sote tunafeli, lakini hakuna hata moja kati ya haya ni kosa la Mungu.)
-
- Wimbo wa Mapenzi
-
- Soma Warumi 3:21-24. Hitimisho la visa viwili vya mashamba ya mizabibu linakatisha tamaa sana. Sisi ni lundo la zabibu zilizooza, na viongozi wetu vivyo hivyo. Tunalo tumaini gani? (Mwana aliyeuliwa na wapangaji ametukomboa sisi sote tunaomwamini Yeye.)
-
- Soma Warumi 3:25-26. Hili linafanya nini kwenye hadhi ya Yesu? (Inaonesha haki ya Mungu. Inaonesha kuwa Mungu anatenda haki na ni mthibitishaji wetu sote tunaoiweka imani yetu kwake.)
-
- Soma Warumi 3:27-31. Wapangaji waovu walitaka kitu gani kilichokuwa milki ya mwana? (Urithi wake. Kamwe hatupaswi kudai kuwa sisi ni wenye haki. Kamwe hatupaswi kudai kuwa mitazamo yetu iko juu ya mitazamo ya Mungu na haki ya Mungu. Hatupaswi kujivunia matendo yetu ya haki. Yupo Mmoja pekee ambaye ni mwenye haki.)
-
- Mungu angeweza kufanya nini zaidi?
-
- Rafiki, je, umechanganyikiwa kuhusu asili ya Mungu? Je, umechanganyikiwa kuhusu asili ya mwanadamu? Sisi ni “zabibu-mwitu.” Viongozi wetu wa kiroho si wakamilifu. Mungu pekee ndiye mkamilifu na alionesha upendo wake kwetu kwa kuja duniani, akaishi maisha makamilifu, akafa kifo cha mateso makali, na akarejea mbinguni kama Mtu aliyeishinda dhambi na mauti. Je, kwa imani utamtegemea Mungu, na si kujitegemea wewe mwenyewe? Kwa nini usitubu kwa kutoelewa kwako asili yetu na asili ya Mungu, na kumgeukia Mungu sasa hivi?
- Juma lijalo: Upendo na Haki: Amri Kuu Mbili.