Somo la 8: Uhuru wa Kuchagua, Upendo, na Majaliwa ya Mungu
Somo la 8: Uhuru wa Kuchagua, Upendo, na Majaliwa ya Mungu
(Mwanzo 22, Zaburi 81, Waebrania 11, Waefeso 1)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Unadhani “majaliwa ya Mungu” yanamaanisha nini? Masomo yetu ya hivi karibuni yananikumbusha mashine ya kukata vipande vyembamba (slices) vya nyama niliyoishuhudia nilipokuwa kijana mdogo. Mashine ilikuwa na uwezo wa kukata vipande vya nyama vyembamba sana kiasi cha macho kutoweza kuamini. Katika masomo machache yaliyopita tulijadili juu ya mada zinazohusiana kama vile endapo Mungu anawajibika kwa uovu, endapo Mungu ni mwenye haki, na endapo Mungu anatekeleza hukumu. Kwa ujumla mada hizi zote zinazungumzia jambo moja kuhusu jinsi Mungu anavyoshughulika na wanadamu. Juma hili “kipande chetu chembamba” ni endapo Mungu, sambamba na majaliwa yake, anadhibiti mambo yote yanayotokea duniani. Ikiwa anayadhibiti, kwa nini hakomeshi matukio ya kutisha? Kwa nini haondoshi shida/dhiki/taabu maishani mwetu? Kwa mara nyingine, hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu Mungu wetu!
- Nani Aliye Msimamizi (Who Is In Charge)?
-
- Soma Mwanzo 22:1-2. Majaliwa ya Mungu yanaonekanaje katika maelekezo haya kwa Ibrahimu? (Hayana mantiki. Katika Mwanzo 21:12 Mungu alimuahidi Ibrahimu kwamba uzao wake utatokana na Isaka. Kwa muktadha wa kiteolojia, 2 Wafalme 16:3 inatuambia kuwa kumtoa mwanao kama sadaka ya kuteketezwa kilikuwa kitendo “cha machukizo” kwa mataifa ambayo Mungu aliyafukuza kutoka katika nchi ya ahadi.)
-
- Tutaruka vifungu vinavyotuambia kuwa Ibrahimu alichukua hatua kumtii Mungu. Soma Mwanzo 22:9-12. Ni yepi yaliyo mapenzi ya Mungu katika kisa hiki? (Mapenzi yake ni kwamba Isaka asiuawe. Hii si dhahiri kwa msomaji hadi tuingie kwenye kifungu hiki.)
-
- Soma tena Mwanzo 22:12. Kama Mungu anajua kila kitu, anawezaje kusema, “Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu?” (Jibu rahisi ni kwamba Mungu anaturuhusu kufanya uchaguzi, na hadhibiti au kujua uchaguzi wetu kabla hatujaufanya.)
-
-
- Kisa hiki kinaletaje mantiki? (Mwanzo 22:1 inatuambia kuwa hili ni “jaribu.” Jambo la muhimu sana ni kwamba hii inafafanua jinsi ilivyokuwa vigumu kwa Mungu Baba kumtoa Yesu kwa ajili ya mateso na kifo.)
-
-
-
- Mungu anatufanyaje kuchagua unyofu kwa Mungu kuwa mdhibiti? Na kwa nini Mungu Baba amtoe Mwanaye kwa ajili ya mateso na mauaji? (Mungu, kwa sababu ya dhambi yetu, analazimika kufanya chaguzi asizozitaka.)
-
-
-
- Tunapatanishaje kifungu hiki na dhana ya kwamba Mungu anaufahamu mustakabali wa siku zijazo? (Ninaliangalia suala hili kama ubao wa sataranji (chess board.) Mungu anajua yote tutakayoyacheza kwenye mchezo wa sataranji, na anajua matokeo ya uchezaji. Katika muktadha huo Mungu ni mdhibiti. Lakini hilo pia linasababisha matatizo kwenye majaliwa yake kama tutakavyoona katika sehemu inayofuata.)
-
-
- Soma Zaburi 81:10-14. Hebu tupitie historia kwa ufupi. Watu wa Mungu walikuwa utumwani nchini Misri kwa mamia ya miaka. Mungu alipowaokoa kutoka utumwani, watu wawili pekee kati ya kundi la awali la maelfu ndio waliopona na kuingia katika nchi waliyoahidiwa. Vifungu hivi vinawajibuje wale wanaosema kuwa kumfuata Mungu ni sawa na biashara hatarishi? (Vinatuambia kuwa ingawa Mungu yupo (anapatikana) kwa ajili ya msaada na kuhakikisha mafanikio, watu walikuwa hawamfuati Mungu. Walichagua kuyafuata matamanio yao wenyewe. Matokeo yake ilikuwa ni majanga.)
-
- Soma Isaya 30:15. Je, Mungu ameweka njia kwa ajili ya kustarehe na mafanikio? (Ndiyo. Mungu anasema kuwa ukiufuata mpango wangu na kunirudia utafurahia pumziko, wokovu, na tumaini tulivu.)
-
-
- Je, watu waliufuata mpango wa Mungu? (Hapana. “Hawakuwa tayari.”)
-
-
- Soma Isaya 30:16. Jambo gani ni la pekee kukimbia (fleeing) kwa kutumia farasi? Je, ni kuendesha “swift steeds?” (Farasi walikuwa zana za kisasa za kijeshi. Farasi walimaanisha uliweza kwenda kwa haraka na kwa nguvu.)
-
-
- Watu wa Mungu wanawatumia farasi kufanya nini? (Kukimbia (fleeing)!)
-
-
-
- Je, hilo linafanikiwa? (Hapana. Wale wanaowafuatilia pia wana farasi.)
-
-
- Soma Isaya 30:17. Je, watu wana ujasiri juu ya ushindi? (Hapana. Ni waoga. Watu elfu moja kati yao wanamkimbia mtu mmoja. Askari watano adui wanawafanya wakimbie. Mwisho wa uoga wote huu ni kwamba hawako salama kabisa, wanaonekana kwa dhahiri kabisa, na adui hawezi kushindwa kuona mahali walipo.)
-
- Tunahitimisha nini kutoka Zaburi 81 na Isaya 30 kuhusiana na Mungu kutulinda dhidi ya uovu? (Anatulinda na kutupatia amani tukimgeukia. Tusipofanya hivyo, tunaangamizwa.)
-
-
- Vifungu hivi vinatufundisha nini kuhusu Mungu kuchukua njia yake? Majaliwa ya Mungu kutimizwa? (Alitaka watu wake washinde. Mungu hakupata kile alichokitaka.)
-
- Ugumu wa Majaliwa
-
- Soma Waebrania 11:32-34. Katika sehemu iliyotangulia tuliona kuwa watu hawakuyafurahia mambo makuu ambayo Mungu aliyapanga kwa ajili yao katika majaliwa yake kwa sababu hawakumsikiliza wala kumtii. Vipi kuhusu watu waliotajwa hapa? Je, walimtii Mungu? (Tunafahamu kwamba baadhi yao, kama vile Samsoni, walimtii Mungu lakini si kwa ukamilifu. Lakini kwa ujumla walikuwa watiifu. Hata Samsoni alikuwa mtiifu mwishoni.)
-
- Soma Waebrania 11:36-38. Je, hawa ni watu ambao hawakumtii Mungu na hivyo kupata matokeo ya kutokutii huko?
-
- Soma Waebrania 11:39. Hii inatufundisha nini kuhusu watu walioteseka? (Walikuwa waaminifu. Walisifiwa kwa imani yao.)
-
-
- Tunayaelezeaje majaliwa ya Mungu katika hili? Lilikuwa fundisho jepesi na la dhahiri kwamba usipomfuata Mungu, anajizuia kukupatia mambo makuu aliyoyapanga kwa ajili yako. Lakini hawa waliyafuata mapenzi ya Mungu na kuteseka kiasi cha kutisha. Hilo linawezekanaje?
-
-
- Soma Waebrania 11:40. Huu ni ufafanuzi wa sababu ya wafuasi waaminifu wa Mungu kulipitia mateso ya kutisha hata kama walikuwa waaminifu. Unauelewaje ufafanuzi huu? (Mungu ana mustakabali bora kwa ajili yao. Hatima ya majaliwa ya Mungu kwao inakuja.)
-
-
- Je, “ili wao wasikamilishwe pasipo sisi” inamaanisha nini? (Mungu anafanyia kazi suala la kuweka matokeo chanya ya majaliwa yake. Wakati fulani katika siku zijazo, wafuasi wote wa Mungu watakaosalia kuwa waaminifu na kumtumaini Mungu watafanywa kuwa wakamilifu. Mambo yote mazuri anayoyawaza Mungu kwa ajili yao yatatokea.)
-
-
-
- Hiyo inaacha swali la kwa nini jambo hilo linatendeka kikamilifu kwa baadhi na linakuwa na matokeo ya kutisha kwa wengine? (Jibu la dhahiri ni kwamba mambo yanakuwa mabaya kwa wale wanaoyafuata mapenzi yao wenyewe. Lakini kwa wale wanaoyafuata mapenzi ya Mungu, na bado wanateseka, tunaachwa na jibu alilopewa Ayubu: lazima tumtumaini Mungu.)
-
- Kuipata Nguvu ya Kuvutia kwa Ajili ya Majaliwa ya Mungu
-
- Soma Waefeso 1:9-10. Hii inatuambia kuwa Mungu ana mpango wa ajabu (mysterious). Je, kuuangalia uzoefu wa Yesu kunatufundisha nini kuhusu mpango huu? (Yesu alikufa na aliteswa na kupitia mateso makali ili hatimaye mpango wa Mungu uchukue nafasi. Hii inatuonesha kuwa mpango wa Mungu ni mchakato ambao kuna nyakati unahusisha mateso.)
-
-
- Tuuchukulieje ukweli kwamba mapenzi ya Mungu ni “fumbo” linalofafanuliwa katika Yesu? (Kama tumetilia shaka majaliwa ya Mungu, tunatakiwa tu kuangalia kile ambacho Yesu amekuwa akikifanya kwa ajili yetu.)
-
-
- Soma Waefeso 1:11-12. Ni yepi yaliyo majaliwa ya Mungu kwa ajili yetu sote? (Imeshaamuliwa kabla (predestined) kwamba tuyafuate mapenzi ya Mungu. Kupokea urithi aliotuandalia. Na kumtukuza.)
-
-
- Je, hii inamaanisha kuwa hatuna uhuru wa kuchagua katika hili? (Ni kinyume chake tu, tunaona kwamba wale waliokataa kuyafuata mapenzi ya Mungu hawakupokea manufaa ya mipango yake mikubwa kwa ajili yao. Mungu anatuwazia mambo makubwa kwa ajili yetu!)
-
-
- Soma Waefeso 1:13-14. Unaweza kuelezea kwa nini Wakristo wanajihusisha kwenye juhudi za kishujaa za kitabibu ili kuendelea kuwa hai? Au kurefusha maisha kwa miezi michache? (Huenda kuna mtu anayewategemea. Hata hivyo, kwa ujumla mtu aliye mgonjwa kiasi hicho hana uwezo wa kuwasaidia wengine. Nina shaka kama tatizo ni kwamba kwa dhati kabisa hawana uhakika kama wameokolewa.)
-
-
- Kifungu hiki kinatufundisha nini kuhusu hakikisho la wokovu? (Roho Mtakatifu anatutia mhuri kwa ajili ya wokovu. Kama Roho Mtakatifu anatenda kazi ndani yako, basi una “uhakika (guarantee)” wa urithi wako mbinguni.)
-
-
- Soma Yohana 16:33. Je, ungependa kuwa na amani katikati ya taabu? (Ikiwa jibu ni ndiyo, kifungu hiki kinatuambia kuwa tunaweza kuwa na amani kwa sababu Yesu “ameushinda ulimwengu.”)
-
- Rafiki, Mungu ana mpango kwa ajili yako. Mpango huo, yaani majaliwa ya Mungu kwa ajili yako, ni kutumia umilele pamoja na Mungu. Unaweza kuupinga mpango kwa kuyakataa mapenzi ya Mungu. Lakini kama utaukubali mpango wa Mungu basi uzima wa milele ni wako hata kama unaweza kukabiliana na magumu ya muda mfupi (temporary) hapa duniani. Kwa nini usiuchague mpango wa Mungu kwa ajili yako sasa hivi?
- Juma lijalo: Pambano la Ulimwengu Mzima.