Somo la 4: Mungu ni Mwenye Shauku na Huruma

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Zaburi 103, Hosea 9, 1 Wakorintho 13
Swahili
Year: 
2025
Quarter: 
1
Lesson Number: 
4

Somo la 4: Mungu ni Mwenye Shauku na Huruma

(Zaburi 103, Hosea 9, 1 Wakorintho 13)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, Mungu ana hisia? Mara kwa mara Agano la Kale linarejelea jinsi Mungu anavyojisikia. Je, hisia za Mungu zinaathiri uamuzi wake? Ninawafahamu watu ambao kimsingi uamuzi wao umejengwa juu ya hisia, badala ya mantiki, na ninawachukulia kuwa na mbinu hafifu (inferior) za kufanya uamuzi. Wakati huo huo mara nyingi huwa ninabarikiwa watu wanaponitendea kwa hisia chanya badala ya namna mantiki itakavyoongoza. Kitabu cha Mwanzo kinatuambia kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Ikiwa hilo linajumuisha hisia, na ninadhani linajumuisha, hisia zetu zinafananaje na hisia za Mungu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

  1.    Upendo wa Mzazi
    1.    Soma Zaburi 103:13. Natumaini kwamba wewe, kama ilivyo kwangu, ulikuwa na baba mzuri. Ikiwa ndivyo, unaweza kuamini kuwa baba wako angekupenda na kukujali? (Ninapokabiliana na tatizo, huku nikijua kuwa Mungu ananijali kama ambavyo baba wangu alinijali hunipa tulizo.)
      1.    Je, wewe ni mzazi? Mojawapo ya mambo bora kabisa kutokana na kuwa na watoto ni kwamba wanatufundisha zaidi kuhusu uhusiano wetu na Mungu. Kuwa mzazi kumekufundisha nini kuhusu Mungu?
    1.    Muktadha ni muhimu. Soma Zaburi 103:8-10. Je, watu hawa ni watiifu? (Hii inafafanua jinsi mwitiko (reaction) wa Mungu unavyokuwa pale tunapotenda jambo lisilo sahihi.)
    1.    Soma Zaburi 103:11-13. Dhambi yetu ni jaribu kwa uhusiano wetu na Mungu. Mungu anaahidi kwa kina kiasi gani kutatua tatizo letu la dhambi? (Anaondoa dhambi zetu milele.)
      1.    Zaburi zote mbili, yaani Zaburi 103:13 na Zaburi 103:11 zinasema kuwa mtazamo wa upendo wa Mungu ni kwa ajili ya wale “wamchao.” Unakielewaje kipengele hiki? (Kwa kulitafakari somo letu majuma mawili yaliyopita, ninadhani inamaanisha wale wanaotaka kumpendeza Mungu.)
    1.    Soma Zaburi 103:14. Ulipokuwa unatafakari kuhusu jinsi ya kufanya kutokana na utovu wa nidhamu wa watoto wako, je, ulizingatia umri wao? (Hii inaonesha kuwa Mungu anazingatia hali inayopunguza uzito wa makosa/dhambi. Hayo yanatufanya tuwe na huruma zaidi.)
    1.    Soma Isaya 49:14-16. Je, Mungu anaweza kukusahau? Je, hana habari na matatizo yanayokusumbua? (Mungu anasema kuwa yeye ni mwaminifu zaidi kuliko mama anyonyeshaye!)
      1.    Unaelewaje Mungu anaposema kuwa “amekuchora” katika vitanga vya mikono yake? (Wanamaoni kadhaa wanasema kuwa jina lako limechorwa mikononi mwake.)
        1.    Hiyo ni ishara ya jambo gani? (Mara zote anakumbushwa juu yako.)
      1.    “Kuta” zetu ni zipi ambazo mara kwa mara Mungu anazitafakari? (Ukuta huulinda mji. Mara kwa mara Mungu anafahamu hatari inayokukabili.)
  1.   Hisia za Mungu Dhidi ya Hisia Zetu
    1.    Soma Hosea 11:8-9. Kwa umahsusi Mungu anasema kuwa hisia zake si kama zetu. Vifungu hivi viaashiriaje kuwa hilo ni kweli? (Huruma ya Mungu kwetu hutuliza “ukali wa hasira” yake.)
      1.    Wanadamu wanafanya nini ambacho Mungu hakifanyi? (Hapotezi udhibiti. Haruhusu hisia zake hasi zidhibiti hisia zake chanya kwetu.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:23-26. Mungu anasema kuwa ana mkataba na watu wake. Mkataba huo unasema kuwa hawawezi kufanya nini? Matendo gani kwa upande wao humfanya Mungu kuwa na wivu, moto ulao, na mwangamizaji? (Kutengeneza sanamu.)
      1.    Hakuna mtu ninayemfahamu ambaye anatengeneza sanamu. Je, bado hilo ni tatizo? Kwa nini linamfanya Mungu awe na wivu?
    1.    Soma Kutoka 32:4. Jambo gani kwenye kauli hii lingekufanya ujisikie wivu kama ungekuwa Mungu? (Wanahusianisha mafanikio yao juu ya Misri na kitu walichokitengeneza.)
    1.    Soma Kutoka 20:17. Watu walio na tatizo la kutamani wanadai kuwa magari, nyumba, au mali za watu wengine ni sanamu. Je, Mungu atakuwa na wivu wa gari au nyumba?
      1.    Mioto ya kutisha iliyotokea Los Angeles, California imedhihirisha upande wa kidhambi wa mwanadamu. Watu wanataarifiwa kusema kuwa kwa sababu miji ya watu iliyoungua ni ya ghali sana, basi kuangamia kwa nyumba hizo ni jambo sahihi. Je, kuna ufafanuzi wa kutosha wa jambo hilo zaidi ya kutamani?
      1.    Jambo gani, tofauti na magari au nyumba, tunaweza kulifanya hii leo ambalo linaakisi uovu wa Kutoka 32:4? (Kujitwalia sifa kwa kile ambacho Mungu amekitenda. Kuhusianisha mafanikio yetu maishani na juhudi zetu wenyewe. Kutegemea kitu tulichokitengeneza (kama vile fedha zetu) katika nyakati za taabu.)
        1.    Je, kuna uhusiano kati ya mtazamo huu na magari na nyumba nzuri? (Kama mtu anasema kuwa anastahili vitu vizuri kutokana na juhudi zake binafsi, badala ya kumshukuru Mungu kwa baraka zake, hilo ni tatizo la uabudu sanamu.)
    1.    Soma Mathayo 12:24 na Mathayo 12:31-32. Je, dhambi isiyosameheka inafanana na uabudu sanamu? (Ndiyo. Inatoa sifa kwa pepo kwa kazi ya Roho Mtakatifu.)
      1.    Kwa nini Mungu asikitishwe na hili? (Je, unapenda watu wengine wasifiwe kwa kile unachokitenda? Mungu anatupenda na anatusaidia. Kwa nini tujisifie au kuzisifu pepo?)
      1.    Unakwenda hospitali, unapewa dawa, unapona, na unawasifu madaktari na dawa ulizotumia. Je, ni jambo baya? (Si madaktari wala dawa ambazo huponya. Zinawezesha tu mwili kujiponya wenyewe – uwezo utokao kwa Mungu.)
        1.    Je, Mungu anatupinga kutoa sifa shirikishi? (Mungu anashirikiana na wanadamu kutenda mema.)
    1.    Soma 1 Wakorintho 13:4-6. Je, Mungu ni upendo?
      1.    Kama umejibu, “Ndiyo,” kama tunavyotakiwa kujibu, je, Mungu anaweza kudhihirisha hisia zozote kati ya hizi? (Tumejadili kuwa kuna nyakati Mungu anakuwa na wivu na hasira.)
        1.    Je, hilo ni sawa – kwamba Mungu anazo hisia hizi? (Hali zote tulizozijadili zinahusisha Mungu kuwa na wivu au hasira kutokana na upendo wake kwetu. Vifungu vya 1 Wakorintho vyote ni mifano ya kutopenda.)
      1.    Asubuhi ya leo nimesoma kwenye jarida la Wall Street kuhusu tafsiri ya uamuzi wa kipumbavu. Makala yalisema kuwa watu wanaofurahia viwango mbalimbali vya mafanikio wanaweza kufanya uamuzi wa kipumbavu. Makala yalifafanua uamuzi wa kipumbavu kama ule ambao unawadhuru watu wengine bila kuwa na manufaa ya dhahiri kwa mtu anayefanya uamuzi wa kipumbavu.  Je, hisia hasi zilizoelezewa katika 1 Wakorintho 13:4-6 zinamnufaisha mtu anayezidhihirisha?
        1.    Kama Mungu anadhihirisha hisia hasi, je, hilo linamnufaisha? (Hiyo ni tofauti kati ya Mungu na wanadamu. Hisia zetu hasi, kwa kiasi kikubwa, hazitusaidii. Hisia hasi za Mungu hatimaye zinawanufaisha wanadamu.)
  1.      Hisia za Yesu
    1.    Soma Mathayo 9:35. Yesu anapeleka injili kwa watu. Anashiriki nao injili. Kwa nini awe na haja ya kuponya “kila” ugonjwa na “kila” udhaifu? (Soma Mathayo 9:36. Jibu lipo katika kifungu kinachofuata. Yesu aliwahurumia.)
    1.    Soma Yohana 5:2-9. Vifungu hivi vinadhihirisha kuwa watu wengi wagonjwa sana walikuwepo, lakini Yesu alimponya mgonjwa mmoja pekee. Kwa nini? Vipi kuhusu kuwahurumia wengine?
    1.    Soma Matendo 3:1-2. Unadhani ni mara ngapi Yesu aliingia katika hekalu hili na kumpita mtu huyu? (Kifungu kinasema alikuwepo mahali hapo “kila siku.”)
    1.    Soma Matendo 3:3-7. Kwa nini kamwe Yesu hakumponya mtu huyu lakini wanafunzi wake walimponya? (Tunafahamu Yesu anatuhurumia sote kwa sababu alikufa ili kila mtu aweze kuokolewa. Hitimisho pekee lenye mantiki ni kwamba Yesu alikuwa na sababu nyingine za kuwaponya baadhi na si wengine.)
      1.    Je, hilo linapaswa kubadili mitazamo yetu juu ya hisia za Yesu? (Hisia zake zinaguswa (tempered) na mazingatio mengine, kama ilivyo kwa mzazi mwenye busara.)
      1.    Nimegundua kuwa California imetumia dola bilioni 24 kwa muda wa miaka mitano iliyopita kukabiliana na tatizo la watu wasio na makazi. Idadi ya watu wasio na makazi ikaongezeka. Hilo linapaswa kutufundisha nini kuhusu huruma? (Kama ilivyo kwa Yesu, tunatakiwa kutafakari namna bora ya kuonesha upendo. Mwanamaoni mmoja aliyetumia muda mwingi kuongea na watu wasio na makazi anasema tatizo lipo sababu kubwa ikiwa ni tatizo la afya ya akili linalotokana na dawa za kulevya na vileo/pombe. Anasema aina hizi za kutokuwa na makazi zinapaswa kupewa uchaguzi kati ya jela na kujengwa upya (rehabilitation) ili waweze kuponywa.)
    1.    Rafiki, Mungu anakupenda kama mzazi mzuri. Hisia zake zinaongozwa na hekima yake. Je, utamwomba Roho Mtakatifu kuzifanya hisia zako ziendane na hisia za Mungu?
  1.   Juma lijalo: Ghadhabu ya Upendo wa Mungu.