Somo la 3: Kumpendeza Mungu
Somo la 3: Kumpendeza Mungu
(Waefeso 5, 1 Petro 5, Zaburi 149, Marko 9)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Ni nini mtazamo wako juu ya kuwafurahisha watu wengine? Kwa sababu mimi ni profesa, wanafunzi wangu wanataka kunifurahisha. Kwa kuwa mimi ni mzee kiasi kwamba sina haja ya kufanya kazi, ninaweza kusema kuwa nimeshamfurahisha mwajiri wangu kiasi cha kutosha. Lakini huo si mtazamo wangu. Ninataka kuwafurahisha wanafunzi wangu, mwajiri wangu, na kwa ujumla kila mtu ninayechangamana naye. Kwa nini hilo ni kweli? Watu wengi hawajali mawazo ya watu wengine. Sababu yangu ni kwamba ninaamini maisha yangu yanakuwa mazuri zaidi pale ninapoyafanya maisha ya wengine kuwa mazuri. Je, hii ni kanuni ya Kibiblia? Hebu tuzame kwenye somo letu na Biblia na tujifunze zaidi!
- Kuwafurahisha Wengine
-
- Soma Waefeso 5:22. Unakielewaje kifungu hiki? Je, wake wanapaswa “kuwatii” waume wao kwa namna inayowachukulia waume wao kufanana na Mungu? Je, hilo litakuwa jambo la kuwapendeza/kuwafurahisha?
-
-
- Au, wanapaswa tu kuwatii waume wao kwa namna inayoendana na jinsi wanavyomtii Mungu?
-
-
-
- Au, hii ni kusema kwamba stahili ya mume si ya muhimu, kwa kuwa hili ni suala la utii kwa Mungu?
-
-
-
- Je, kwa ujumla kifungu hiki kinatoa amri ya wanawake kuwatii wanaume? (Kwa umahsusi ukomo wake ni kwa “mume wako.”)
-
-
-
- Unalielewaje neno, “kutii?”
-
-
- Hebu turejee nyuma na kuutafakari muktadha. Soma Waefeso 5:15-16. Unawezaje kuufanya ushauri huu kuwa sehemu ya maisha yako? (Paulo anatuambia kutafakari kwa umakini kuhusu mwelekeo wa maisha yetu. Kuwa mwerevu. Tumia muda wako vizuri.)
-
- Soma Waefeso 5:17. Je, tunapaswa kujiuliza tunapotafakari mwelekeo wa maisha yetu, kwamba Mungu ataashiria kitu gani?
-
- Soma Waefeso 5:18. Unapokuwa umelewa, jambo gani hutokea kwenye utashi wako? (Unadhibitiwa na ulevi wako.)
-
-
- Utaona kwamba kujawa Roho Mtakatifu kunaelezewa kama kitendo pingamizi. Je, unadhani mambo haya mawili yanakinzana? (Roho Mtakatifu anayaongoza matendo yako kinyume na ulevi wako.)
-
-
- Soma Waefeso 5:19-20. Je, hili linafafanua mtazamo? (Hii ni njia chanya ya uhusiano wako na watu wengine. Unashiriki na wengine mambo ya kufurahisha na una shukurani.)
-
- Soma Waefeso 5:21. Ushauri huu unaendanaje na ushauri mbalimbali tuliouangalia hivi punde? (Ushauri wa kwanza unahusu maisha yetu na unaendelea hadi jinsi tunavyopaswa kuhusiana na watu wengine.)
-
-
- Watu wengi wanakichukulia kifungu cha 21 kama mwelekeo wa kuwatii walio kwenye mamlaka, lakini kifungu hakisemi chochote kuhusu mamlaka. Hata hivyo, usipoingiza mamlaka kwenye kifungu hiki, je, inaleta mantiki yoyote?
-
-
-
-
- Watu wawili wanawezaje kuheshimiana ikiwa wana mawazo tofauti juu ya nini cha kufanya? (Muktadha unatuambia kuwa na mtazamo wa uchangamfu na shukurani. Mtazamo huu unaboresha maisha ya watu wengine, na kwa namna hiyo ni kuwatii watu wengine bila kuhafifisha (compromising) mawazo yetu juu ya mada mahsusi.)
-
-
-
-
- Maneno ya mwisho, “katika kicho cha Kristo” yanaongezea nini kwenye kile kinachomaanishwa? (Utii ni matokeo ya uelewa wetu wa mapenzi ya Mungu. Matokeo yanapaswa kuendana na mafundisho ya Kristo.)
-
-
- Soma 1 Petro 5:5. Je, Petro anakubaliana kwamba wazee wanapaswa kuwatii vijana? Je, hakubaliani na kauli ya Paulo katika kitabu cha Waefeso?
-
- Soma Mithali 14:7. Vipi kama mtu mwingine ni “mpumbavu,” je, tunapaswa kumtii mpumbavu?
-
- Hebu tuangalie tena 1 Petro 5:5. Petro anawapendekezea nini “ninyi nyote?” (Anaashiria mtazamo wa unyenyekevu.)
-
-
- Hebu tuliingize hili kwenye Waefeso 5:21. Unadhani utii humaanisha kutenda kile anachokisema mtu mwingine? (Utii ni mtazamo unaoboresha maisha ya watu wengine. Muktadha unaashiria kuwa hatuzungumzii juu ya masuala mahsusi ambayo tunaweza tusikubaliane nayo.)
-
- Kumfurahisha Mwenzi Wako
-
- Sasa hebu tutumie uelewa wetu wa “utii” kwenye Waefeso 5:22. Kwa kuwa neno lile lile la Kiyunani limetumika katika Waefeso 5:21, je, hii inamaanisha wake wanapaswa kuwa na mtazamo wa unyenyekevu kwa waume wao?
-
-
- Je, inamaanisha zaidi ya hayo?
-
-
- Soma Waefeso 5:23-24. Je, unakubaliana kuwa tafsiri sahihi ya vifungu hivi ni kwamba tunapaswa kuwa na mtazamo wa unyenyekevu kwa Mungu? Je, hicho ndicho kinachomaanishwa? (Lazima kuna maana ya ziada.)
-
- Soma Waefeso 5:25-27. Mume anapaswa kumpa nini mkewe? (Yeye mwenyewe.)
-
-
- Je, unaweza kuuelezea uhusiano ambapo mshirika (partner) mmoja “anatii” na mwingine anatoa kila kitu kwa ajili ya mwingine?
-
-
- Soma Waefeso 5:28. Kwa kuwa mimi ni mume, ninauchukulia mwelekeo katika kifungu hiki kuwa ushauri wa muhimu sana kwa waume. “Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.” Je, mke atakuwa na matatizo yoyote akiwa na mume anayeliamini hili na kulitenda?
-
- Baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka hamsini, ninadhani amri za kutii na kupenda zinapaswa kuwa sehemu ya kawaida ya mtazamo ikiwa zinatakiwa kufanya kazi. Ikiwa mume atadai kuheshimiwa, au mke akidai kupendwa, basi kuna jambo ambalo halipo sawa kabisa. Roho Mtakatifu anaweza kubadili mtazamo wetu.
- Kumpendeza Mungu
-
- Soma Zaburi 149:1-3. Mtazamo gani kwa Mungu unaelezewa hapa? (Kusifu kwa furaha!)
-
-
- Je, umepitia uzoefu wa jambo hili? Ikiwa sivyo, kwa nini?
-
-
- Soma Zaburi 149:4. Je, Mungu anatufurahia? (Kifungu hiki kinasema kwa dhahiri kabisa kuwa anatufurahia.)
-
-
- Je, unataka Mungu akufurahie? Ikiwa ndivyo, hii inaashiria kuwa ni njia ipi ya kutimiza jambo hili? (Unyenyekevu.)
-
-
-
- Tafakari nyuma kwenye mjadala wetu wa utii wa pande zote mbili na utii wa mke. Unyenyekevu ni wa muhimu kiasi gani kwenye utii huo?
-
-
- Soma Zaburi 149:5. Utukufu wa nani unarejelewa hapa? (Kwa kuzingatia muktadha, lazima utakuwa utukufu wa Mungu.)
-
-
- Inamaanisha nini kuimba kwa furaha kitandani mwako? (Unaenda kulala ukiwa unamtukuza Mungu!)
-
-
- Soma Zaburi 149:6-9. Waaaao! Tumetokaje kwenye kumtukuza Mungu kwa unyenyekevu hadi kwenye kutekeleza adhabu na kuwafunga wafalme kwa nguvu ya upanga mkali?
-
-
- Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama Kuu ya Marekani kuhusiana na bunduki ulisema kuwa sababu ya msingi ya wananchi kuwa na haki ya kikatiba ya kumiliki bunduki ni kwamba ili waweze kuisahihisha serikali. Je, mjadala wa upanga kwenye vifungu hivi unaakisi dhana ile ile?
-
-
- Soma Yohana 18:36. Hii inahusikaje kwenye mjadala wetu? (Yesu alisema kuwa ufalme wake si wa ulimwengu huu, vinginevyo, watumishi wake wangekuwa wanapigana na Rumi kwa ajili ya uhuru wake. Kwa kuzingatia hili sina uhakika kamili wa kile kinachomaanishwa kwenye vifungu hivi vya kitabu cha Zaburi, lakini angalao lazima vinamaanisha kuwa kumtukuza na kumtii kwetu Mungu kwa unyenyekevu kunapaswa kuishia kwenye hatua halisi (tangible) za kuutangaza Ufalme wa Mungu hapa duniani.)
-
- Soma 2 Petro 2:2-5. Nani anayeudhibiti “upanga” hapa? (Mungu anatekeleza hukumu.)
-
- Soma 2 Petro 2:6-9. Nani anayewaokoa wenye haki kutoka kwenye “mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu?” (Mungu anamwokoa Lutu. Lutu hanyanyui upanga wake.)
-
-
- Tunapaswa kuhitimisha nini kutoka kwenye kisa cha Lutu cha kuishi kwenye mji wa waovu na Zaburi 149? (Kiini ni unyenyekevu. Roho Mtakatifu atatuongoza kuelewa kile tunachopaswa kukifanya ili kuiendeleza/kuitangaza kazi ya Mungu.)
-
- Mantiki ya Jambo Hili
-
- Soma Marko 9:17-19. Je, Yesu anawaita wanafunzi wake “wasio na imani?” (Wanaonekana kujumuishwa miongoni mwa wengine waliopo.)
-
- Soma Marko 9:28-29. Wanafunzi walishindwaje?
-
-
- Je, kushindwa kwao ni tatizo la kudumu? (Hii kimantiki inahusiana na mjadala wetu wa upanga. Wanafunzi walidhani wangeweza kutenda aliyokuwa akiyatenda Yesu. Yesu anawaambia kuwa kujifungamanisha na uwezo wa Mungu kwa njia ya maombi ni jambo la muhimu. Kwa mara nyingine, unyenyekevu ndio ufunguo wa mafanikio.)
-
-
- Rafiki, je, unataka kumpendeza Mungu, mwenzi wako, na marafiki wako? Mtazamo wa unyenyekevu ndio kiini cha mafanikio. Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu sasa hivi kukupatia mtazamo wa unyenyekevu?
- Juma lijalo: Mungu ni Mwenye Shauku na Huruma.