Somo la 1: Mungu Hupenda Bure
Somo la 1: Mungu Hupenda Bure
(Mathayo 22, Kutoka 33, na Yohana 10)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Unalielewaje neno, “upendo?” Katika nchi za Magharibi, watu wengi wamepoteza uelewa wote kabisa wa maneno “upendo” na “chuki.” Ulipokuwa katika urafiki wa kimapenzi (dating), je, ulikuwa na uhakika kama ulikuwa unampenda huyo rafiki wako wa kiume au wa kike? Baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka hamsini, ninajua kwamba ninampenda mke wangu! Kichwa cha habari cha somo letu, “Mungu Hupenda Bure,” kinauelezea upendo wa Mungu. Wakati mwingine kuuona upendo wa Mungu katika Agano la Kale ni jambo gumu. Juma hili tunaangalia mjadala wa upendo wa Mungu katika Agano la Kale na Agano Jipya. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone, katika miktadha tofauti, jinsi Mungu anavyotupenda!
- Ukaribisho
-
- Soma Mathayo 22:2-4. Unadhani mfalme huyu alimpenda mwanaye?
-
-
- Je, aliwapenda wale aliowakaribisha kwenye karamu ya harusi? (Kwa kuwa huyu ni mfalme, angekuwa na sababu ndogo za kuwaalika watu ambao wangefanya mfalme aonekane wa muhimu zaidi. Lazima alikuwa amewaalika watu ambao alitaka kuwaalika. Au alikuwa na sababu za kibiashara za kuwaalika.)
-
-
- Soma Mathayo 22:5-6. Je, wale walioalikwa kwenye karamu ya harusi walimpenda mfalme? (Ama walizipenda kazi zao zaidi, au walimchukia mfalme kwa sababu waliwaua watumwa wa mfalme.)
-
-
- Je, mfalme hakuwaelewa vizuri watu aliowaalika?
-
-
- Soma Mathayo 22:7. Je, sasa mfalme anawapenda wale walioudharau mwaliko wake? (Mfalme si tu kwamba aliwaua, bali pia aliuangamiza mji wao. Huo hauonekani kuwa upendo.)
-
- Soma Mathayo 22:8-10. Je, mfalme analipenda kundi la pili ambalo sasa limealikwa kwenye karamu ya harusi? (Hapana. Hata hawafahamu. Huu ni ukaribisho ulio na upofu.)
-
-
- Kwa nini mfalme awakaribishe watu hata asiowafahamu, achilia mbali kuwapenda? (Mfalme anataka sherehe, na yuko tayari kuwapokea wale walio tayari kuukubali mwaliko wake.)
-
-
- Soma Mathayo 22:11. Hebu tuliangalie hili katika sehemu mbili. Kwanza, tunaambiwa kuwa mfalme alikuja “kuwatazama” wageni, si kula pamoja nao. Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Mfalme alikuwa anaangalia hali ya wageni wake. Je, wanafurahia karamu ya harusi?)
-
-
- Pili, mfalme anamgundua mtu asiye na vazi la harusi. Je, mtu huyu alishindwa kuvaa koti rasmi (tuxedo)? (Lazima itakuwa mavazi yalitolewa na mfalme kwa sababu wageni walikusanywa “kutoka njia panda za barabara.” Hawakuwa na mawazo yoyote walipoianza siku yao kwamba watakwenda kwenye harusi ya kifalme.)
-
-
-
-
- Kama mfalme alitoa vazi la harusi, hiyo inakuambia nini kuhusu mtu huyu? (Ama alidhani mavazi yake ni mazuri kiasi cha kutosha, au hakujali kuhusu harusi ile.)
-
-
-
- Soma Mathayo 22:12. Kwa nini mtu huyu ametekewa? (Lazima alidhani kuwa mavazi yake ni mazuri kiasi cha kutosha. Kwa hakika asingeshindwa kutambua kuwa kila mtu alikuwa amevaa vazi la harusi lililogawiwa kwa wageni.)
-
- Soma Mathayo 22:13. Je, mtu huyu anauawa? (Kifungu hakisemi, lakini anafungwa na kutupwa gizani, mahala pa kutisha.)
-
- Kisa cha Yesu ni ufafanuzi wa kuangamizwa kwa Yerusalemu kunakotarajiwa katika siku za mbeleni. Lakini ni zaidi ya hayo. Hebu tuone kama tunaweza kuelewa maana iliyokusudiwa kuhusu “ufalme wa mbinguni” (Mathayo 22:2). Je, kuna mfanano wowote kati ya waalikwa wa Mathayo 22:5 ambao “hawakujali,” na mtu asiye na vazi la harusi? (Kama mtu aliyetupwa katika giza la nje alikuwa anajali, alidhani hakuwa na haja ya kuvaa vazi. Waalikwa walioshindwa kwenda walidhani hawakuwa na haja ya kwenda.)
-
-
- Kwa hiyo basi kuna mfanano gani kati yao? (Hawatoi kipaumbele kumfurahisha mfalme.)
-
-
-
- Je, hili linahusu tabia? (Mathayo 22:10 inataarifu kuwa tabia, njema na mbaya, haikuwa kigezo cha kukaribishwa harusini.)
-
-
-
- Ni nini vigezo vya kuwa mgeni stahiki wa harusi, ikimaanisha mtu anayeustahili ufalme wa mbinguni? (Kwanza, kuwa na mwitikio chanya kwenye ukaribisho. Pili, kuvaa vazi la harusi linalotolewa na mfalme.)
-
-
- Tunajifunza nini kuhusu upendo wa Mungu kutoka kwenye kisa hiki? Hebu tuone kama tunaweza kulipambanua hili.
-
-
- Je, mfalme anampenda kila mtu? Je, anapenda “bure?” (Kama kuupokea mwaliko kunaakisi kiwango fulani cha upendo, basi jibu ni, “Ndiyo.”)
-
-
-
- Mtu anafanya nini ili kuvunja uhusiano wa upendo na mfalme? Kitu gani kinawafanya “wasiustahili” (Mathayo 22:8) upendo wake? (Kumpuuzia. Wale walio nje ya ufalme ama waliupuuzia (au walipigana kabisa) mwaliko au walilipuuzia vazi la harusi.)
-
- Jangwa
-
- Soma Kutoka 33:1-3. Mungu anamwambia Musa kuwa sasa ni wakati wa Mungu kutimiza ahadi yake kwa Ibrahimu. Musa atawaongoza watu wa Mungu kutoka Misri kwenda Kaanani. Ni nani ambaye hatashiriki safari hiyo? (Mungu hatashiriki safari hiyo.)
-
-
- Kwa nini? (Watu wana mtazamo wa uasi dhidi ya Mungu, na Mungu anaweza kuwaangamiza.)
-
-
- Soma Kutoka 32:10-12. Musa anataka kujua kwa nini Mungu haendi pamoja nao. Ni nini msingi wa Mungu kusema kwamba watu ni waasi na anaweza kuwaangamiza? (Soma Kutoka 32:8. Watu walijifanyia sanamu ya ndama na kusema hiki walichokitengeneza kimewatoa kutoka utumwani Misri!)
-
- Soma Kutoka 33:15. Ni nini mwitiko wa Musa kwa kauli ya Mungu kwamba hatashiriki katika safari hii kwa usalama wa watu? (Musa anasema kuwa kama Mungu hatakwenda, basi hawapaswi kuifanya hiyo safari.)
-
- Soma Kutoka 33:16-17. Musa anatoa sababu gani za Mungu kwenda pamoja nao katika safari?
-
-
- Je, wanamfanya Mungu kuamua kwenda pamoja nao? (Ndiyo.)
-
-
- Soma Kutoka 33:18-19. Ni kipi kigezo cha Mungu cha kuonesha rehema na neema? (Anaamua nani atakayepokea rehema na neema.)
-
-
- Nilisoma maoni juu ya kisa hiki yaliyosema kuwa kisa kinaonyesha mfano wa, “Mungu mwenyewe anampenda kila mtu, na anafanya hivyo bure.” Je, hivyo ndivyo unavyotafsiri jambo hili? Mungu anaonya, “Nikienda pamoja nanyi ninaweza kuwaangamiza. Mungu anasema “nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.” Huko ni kupenda bure?
-
-
- Hebu tusome kifungu tulichokiruka: Kutoka 33:14. Kitu gani huwapatia wanadamu pumziko? (Uwepo wa Mungu.)
-
-
- Ukijisikia amani, je, hizo ni hisia za kupendwa?
-
-
-
- Ili kuonesha tu kwamba hatupotezi kumbukumbu za muda mfupi, je, Mungu hakusema (Kutoka 33:3) kuwa nikienda pamoja nanyi ninaweza kuwaangamiza? Je, huo ni uwepo unaotoa pumziko?
-
-
-
- Jambo gani linafungua fumbo hili? (Ukipumzika kwa Mungu, ukimtegemea Mungu, na usipomwasi Mungu, unayo amani.)
-
-
- Soma Mathayo 11:29-30. Je, waasi hujitia nira vizuri sana? (Hapana. Nira ya Mungu hutunyanyulia mizigo ya maisha. Lakini hili linatutaka kumpokea na si kumwasi Mungu.)
-
-
- Je, unadhani mazungumzo yaliyopo katika kitabu cha Kutoka 33 ambayo tumekuwa tukiyajadili yanaendana na kisa tulichojifunza katika kitabu cha Mathayo 22? (Katika maeneo yote mawili watu walioupokea mwaliko wa Mungu na kuendana na programu yake walikuwa kiini cha upendo wake. Hawakuwa na haja ya kufanya kazi au kuupata upendo wake, walitakiwa tu kuichagua njia yake.)
-
- Msalaba
-
- Soma Yohana 10:7. Kwa kuzingatia mjadala wetu katika sehemu mbili zilizotangulia, ni kwa jinsi gani Yesu ni “mlango” wa wokovu na amani? (Mlango ni kielelezo kizuri kwa sababu mtu anaamua kufungua na kupita mlangoni ili kuingia mahala papya.)
-
- Soma Yohana 10:14-18. Yesu amefanya nini ili kutupatia njia ya uzima wa milele? (Alikufa kwa ajili yetu ili kutupatia njia ya uzima wa milele pamoja naye.)
-
- Tulianza kwa Mungu kuonesha nguvu kubwa dhidi ya wale waliomwasi na tumeishia kwa Mungu kufa ili kuwaokoa wale walioungana naye. Ni kwa jinsi gani hili linaendana? Ni kwa jinsi gani mambo yote haya mawili yanaweza kuwa ya kweli? (Yesu alionesha hatari ya dhambi. Jinsi ambavyo tungekuwa kama Shetani angekuwa kiongozi. Yesu anawaokoa na kuwapenda bure wale wanaomchagua Yeye na programu yake.)
-
- Rafiki, je, wewe ni muasi? Kwa nini usitubu sasa hivi na kuupokea wokovu wa Mungu unaotolewa bure? Nira ya Mungu ni laini na mzigo wake ni mwepesi.
- Juma lijalo: Upendo wa Agano.