Somo la 12: Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 18-20
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
4
Lesson Number: 
12

Somo la 12: Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo

(Yohana 18-20)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umewahi kukataliwa na mtu uliyempenda? Je, umewahi kusema, au hata kudhani, “Ukinikataa basi nami nitakutaa?” Ni tabia ya kawaida ya kibinadamu kuonesha kipimo cha upendo kwa kiwango ambacho umeoneshwa. Tumshukuru Mungu kwamba Yesu hakuwa hivyo! Katika somo letu la injili ya Yohana juma hili tutaona kuwa Yesu ana upendo usiofananishwa na kitu chochote kile. Upendo unaozidi fedheha au madhara aliyoyapitia kutoka kwetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Kutelekezwa na Wanafunzi
    1.    Soma Yohana 18:15. Kifungu hiki kinarejelea kipindi ambacho Yesu anaingizwa kwenye mashtaka ambayo hatima yake ni kifo chake. Kuna ujumbe gani ambao haujaandikwa kuhusu uaminifu wa wanafunzi wa Yesu? (Wanafunzi wawili pekee kati ya wanafunzi wote wa Yesu ndio waliomfuata katika mashtaka yake.)
      1.    Unadhani ni kwa nini?
    1.    Soma Yohana 18:25-27. Petro anasema nini kuhusu uhusiano wake na Yesu? (Anakana kwamba yeye si mwanafunzi wa Yesu.)
      1.    Wanafunzi wa Yesu wanaamini kuwa Yesu ni Masihi. Licha ya hayo, wanafunzi wote isipokuwa mmoja wanamtelekeza katika kipindi ambacho anawahitaji kuliko wakati wowote. Ungekuwa na mwitiko gani kama ungekuwa Yesu?
  1.   Kukataliwa na Watu
    1.    Soma Yohana 18:38-40. Tumesoma kwamba Pilato anafikia uamuzi kuwa Yesu hana hatia, lakini badala ya kutekeleza wajibu wake kama hakimu, anatumaini kwamba kundi lile la watu litaonesha mantiki na kumwachia Yesu badala ya “mnyang’anyi.” Watu wanachukua uamuzi gani?
      1.    Jiweke kwenye nafasi ya Yesu. Wewe ni Mungu na umeshuka kutoka mbinguni ili kuwakomboa watu kwa sababu unawapenda. Ungekuwa na mwitiko gani kwa watu kumchagua mnyang’anyi badala ya kukuchagua wewe? Yesu hawafanyii unyang’anyi, bali anautoa uhai wake kwa ajili yao!
    1.    Soma Yohana 19:3-5. Je, unapenda kutoheshimiwa? Je, unapenda kupigwa kichwani, au kupigwa kwa ujumla wake?
      1.    Yesu alioneshwa kutoheshimiwa kupi ikiwa ni pamoja na kuumizwa? (Walikuwa wanamdhihaki kwa kusema kuwa hakuwa mfalme. Kimsingi, alikuwa Mungu wao na Muumbaji wao.)
      1.    Fikiria kipindi fulani maishani mwako ambapo hukuheshimiwa na mtu ambaye ulimchukulia kuwa alikuwa na hadhi ya chini kuliko wewe. Ulikuwa na mwitiko gani?
      1.    Hivi karibuni, mwenzangu mmoja aliyekuwa akiendesha gari kuukuu chafu aina ya “pickup” la rangi ya kahawia alinifuata katika eneo la maegesho ya magari katika chuo kikuu ninachofundisha na kuanza kunidhihaki kwa sababu nilikuwa ninaendesha gari la zamani aina ya Corvette na si Corvette jipya. Ungekuwa na mwitiko gani kwenye dhihaka ya namna hiyo? (Je, mtu yule mwenye gari kuukuu la kahawia ana haki ya kuwadhihaki wengine kwa aina ya magari yao? Ninakumbuka miaka mingi iliyopita nilipokuwa ninaendesha gari kuukuu (mini-van), nilikuwa nikiangaza angaza na kuhitimisha kwamba kila mtu alikuwa akiendesha gari la thamani zaidi. Sikuwaza hata kidogo kuwadhihaki! Kudhihakiwa ni jambo baya, lakini Yesu alikuwa anadhihakiwa na wale aliowaumba! Wale ambao kwa dhahiri walikuwa na hadhi ya chini kuliko yeye.)
    1.    Soma Yohana 19:6-7. Utakuwa na mwitiko gani ikiwa kundi la watu linashinikiza kifo chako kwa sababu wamekataa kuamini ukweli wa utambulisho wako? (Kudhihaki ni jambo moja, kukuua kwa sababu ya kutokuwa mtiifu ni jambo baya zaidi.)
    1.    Soma Yohana 19:14-15. Mfalme wa Wayahudi ni Kaisari? Hii ni dharau (kutokumtii) gani ya ziada anayooneshwa Yesu? (Hawa ni viongozi wa taifa la Kiyahudi, taifa ambalo lengo lake ilikuwa liwe nuru kwa mataifa! Sasa wanamtaka mpagani kuwa mfalme wao badala ya Yesu?)
    1.    Soma Mathayo 26:39-40. Huu ni mfano mwingine wa Yesu kuangushwa na wanafunzi wake. Je, Yesu angeweza kuamua kwamba “kikombe hiki” kimetosha kutoka kwa watu hawa wasio na shukrani ambao wanamkataa kwa kurudiarudia na kumsikitisha mara kwa mara?
  1.      Kusulubiwa
    1.    Soma Yohana 19:16-18. Yesu alipitia mateso makali sana ambayo Injili ya Yohana haiyajadili. Unadhani kwa nini Yohana hajumuishi taarifa za maumivu? (Yohana anadai kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yesu. Nadhani ilikuwa vigumu sana kwake kuandika kwa kina mateso ya Yesu.)
    1.    Soma Yohana 19:23-24. Unaona dhihaka gani kwenye maelezo haya? (Yesu anasulubiwa uchi. Anawekwa wazi ili watu wote wamwone, ikiwemo na wale wanaomtukana. Udhalilishaji mkubwa namna gani!)
    1.    Soma Yohana 19:26-27. Nani ambaye hajamtelekeza Yesu? (Mama yake na mwanafunzi Yohana. Tunafahamu kwamba Yohana anajirejelea kwenye kifungu hiki kwa kile anachokiandika katika Yohana 21:20-24 mwishoni mwa injili yake.)
      1.    Kama ungekuwa Yesu, uwapo wa Yohana na mama yako ungeifanyia nini roho yako? (Hawajamtelekeza. Nitatiwa moyo. Hata hivyo, nisingependa mama yangu ayaone haya.)
      1.    Maneno ya Yesu kuhusu kujali kwa mama yake yanatufundisha nini? (Katikati ya mateso haya na udhalilishaji huu, bado Yesu anamwangalia mama yake.)
    1.    Soma Yohana 19:30. Kitu gani kimekwisha? (Yesu ameishinda dhambi. Alikuja duniani kama mwanadamu, akaishi maisha makamilifu, na sasa amekufa kifo cha kutisha kwa ajili yetu ili kwamba tuweze kwenda mbinguni. Ushindi mkubwa kiasi gani! Sehemu ya “Matumizi Mishani” inataarifu neno hili la Kiyunani linaweza kumaanisha, “imelipwa kikamilifu.” Yesu alilipa adhabu yetu kikamilifu, hata kama tulikuwa tukimuumiza, kumdhihaki, na kumkataa. Upendo wa namna gani huu!)
  1.   Ufufuo
    1.    Soma Yohana 20:1-2. Kwa nini Mariamu anasema, “Wala hatujui walikomweka?” (Uwingi huu unaashiria kuwa Mariamu alikuwa pamoja na wanawake wengine. Hii inathibitishwa na Marko 16:1.)

 

      1.    Jambo gani lingekuwa mawazoni mwako kama ungekuwa Mariamu? (Zaidi ya matusi yote aliyoyapitia Yesu, sasa mwili wake umeondolewa.)
      1.    Kwa nini waamini kwamba mwili wa Yesu umeibwa badala ya kuamini kuwa Yesu amefufuka?
    1.    Soma Yohana 20:3-7. Je, taarifa hii ya eneo linalohusika inaunga mkono dhana ya kwamba kuna mtu ameuiba mwili wa Yesu? (Wezi hawakunji vitu vizuri pale wanapoondoka.)
    1.    Soma Yohana 20:8. “Mwanafunzi mwingine” anaamini nini? (Yohana ndiye “mwanafunzi mwingine” anayeona vitambaa vilivyolala. Anahitimisha kuwa Yesu amefufuka kutoka katika wafu.)
    1.    Soma Yohana 20:9-10. Je, hii inasahihisha hitimisho nililopendekeza kwamba Yohana aliamini kuwa Yesu alifufuka kutoka katika wafu? (Sidhani kama Yohana anajijumuisha na wanafunzi wengine. Badala yake, nadhani anatuambia kuwa aliamini, lakini wengine bado hawajafikia hitimisho hili.)
    1.    Soma Yohana 20:11-13. Kwa nini malaika wawili wanazungumza na Mariamu na si Petro na Yohana? (Wanafunzi waliondoka. Kama Yohana aliamini kuwa Yesu alifufuliwa kutoka katika wafu, anafanya nini akiwa anarejea nyumbani? Anapaswa kuwa anawaambia wengine habari hizo.)
    1.    Soma Yohana 20:14-16. Kwa nini Yesu anamtokea Mariamu kwanza na si mwanafunzi “ambaye Yesu alimpenda?” (Mariamu bado alidhani kuwa mwili wa Yesu umeibwa. Hiyo inaweza kuwa sababu. Au, Yohana na Petro walikuwa wamekwenda nyumbani, lakini Mariamu hakuondoka. Kwa dhahiri Mariamu alikuwa amejitoa kwa Yesu.)
    1.    Soma Yohana 20:17. Kauli ya Yesu inatuambia nini kuhusu anachokifanya Mariamu? (Anamng’ang’ania Yesu. Anamshikilia. Hii inasisitiza taswira ya kujitoa kwake kwa dhati kwa Yesu.)
      1.    Mtazamo wa Mariamu umebadilikaje? (Amehama kutoka kwenye huzuni kuu na kuvunjika moyo, na kuingia kwenye furaha kamili.)
        1.    Je, hili ni jibu bora la kwa nini Yesu alimtokea Mariamu kwanza?
    1.    Soma Yohana 20:18. Je, Yesu anajishughulisha (concerned) na wanafunzi wake? Wanafunzi waliomtelekeza?
    1.    Rafiki, maneno hayatoshi kuelezea upendo alionao Yesu kwetu. Upendo wake haupimwi kwa upendo wako kwake. Hata matatizo yatakapokujia, fikiria juu ya kile ambacho Yesu alikitenda ili kukuokoa. Je, utaahidi kuweka wasiwasi (concerns) na matatizo yako yote binafsi katika muktadha wa kile ambacho Yesu alikutendea?
  1.    Juma lijalo: Hitimisho: Kumjua Yesu na Neno lake.