Somo la 11: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu
Somo la 11: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu
(Mwanzo 1, Yohana 10 & 16)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, una mwanafamilia mzuri sana aliyefariki kabla watoto wako hawajazaliwa? Je, unatamani kama watoto wako wangeweza kujua baraka za kuwa na mtu huyo wa pekee? Kuwaonesha watoto wako picha inaweza isitoshe. Baada ya kubuniwa kwa picha mjongeo (videos) zinazotengenezwa kirahisi, hiyo inasaidia kuleta uelewa. Vipi kuhusu wewe? Kama ni mzazi wako, je unatosha kama mzazi wako kwamba watoto wako wanaweza kufahamu mambo ya muhimu kupitia kwako? Yesu alikabiliana na tatizo kama hilo katika kutufundisha kuhusu Baba wake wa Mbinguni. Hebu tuzame kwenye somo letu la Yohana ili tuone jinsi Yesu anavyotusaidia kumjua Baba wake na Roho Mtakatifu.
- Unachokidhihirisha Kumhusu Mungu
-
- Soma Mwanzo 1:26-28. Hii inatuambia kuwa tunaakisi “mfano” na “sura ya Mungu.” Unadhani hiyo inamaanisha nini?
-
-
- Zingatia uwingi. “Na tumfanye,” “kwa mfano wetu.” Mungu anazungumza na nani? (Huu ni ushahidi wa ziada wa Utatu Mtakatifu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Mungu anasema kuwa anawaumba wanadamu ili kuakisi uwingi wake.)
-
-
-
-
- Tafakari kwa kina zaidi. Je, hiyo inamaanisha sehemu za uwingi pia zinamuakisi kila mmoja? Kwa umahsusi, je, huu ni ushahidi kwamba Yesu na Roho wanatupatia taarifa kumhusu Mungu Baba?
-
-
-
-
-
- Chukulia kwamba mti, mwamba, na sili wa bahari mwenye pembe (walrus) wapo mahala pamoja wakiwa wamekaribiana. Sili wa bahari mwenye pembe anauambia mti na mwamba, “Hebu tutengeneze kitu kwa mfano wetu, kitakachoakisi sura yetu.” Je, hilo litafanyika?
-
-
-
-
- Je, wanadamu wanatofautiana na wanyama? (Hatufanani wala kufikiri kama wanyama. Mwanzo 1:26 inawapatia wanadamu “utawala” juu ya wanyama. Hiyo ndio sehemu ya namna tunavyomuakisi Mungu.)
-
-
- Soma Warumi 8:16. Je, wanadamu wana roho kama Roho Mtakatifu? (Kifungu hiki kinasema, “Ndiyo.”)
-
-
- Unaelewaje jinsi hili linavyofanya kazi? Je, roho zetu zinawasiliana?
-
-
-
- Unaposoma vifungu vya Biblia kwenye masomo haya, je, vinafanya nuru izimike kichwani mwako? Je, ghafla tu unaelewa jambo ambalo hapo awali halikuwa bayana kwako? (Huyo ni Roho Mtakatifu akizungumza na roho yako.)
-
-
-
- Mungu alipoamua kutuumba kwa mfano wake, je, roho yetu ni uthibitisho wa uumbaji wake? (Kiuhalisia tunafahamu kwamba sisi ni zaidi ya mfuko wa nyama.)
-
-
- Soma Yohana 3:34-35. Mwingiliano wa Roho Mtakatifu na roho zetu unasababisha jambo gani jingine maishani mwetu? (Tunashiriki na wengine maneno ya Mungu. Roho Mtakatifu anatupatia maneno hayo.)
-
-
- Au nimekosea? Je, kifungu hiki kinarejelea tu kile ambacho Mungu Baba amempa Yesu?
-
- Anachokidhihirisha Yesu Kumhusu Baba
-
- Soma Yohana 10:30-33. Yesu anamaanisha nini anaposema kuwa Yeye na Baba ni wamoja?
-
-
- Je, wasikilizaji wake wa Kiyahudi hawakumwelewa vizuri Yesu? (Walielewa, hawaamini.)
-
-
- Soma Yohana 10:34-36. Je, Yesu anajenga hoja kwamba wanadamu wote wanaweza kuwa “miungu?” (Kujibu hili soma Zaburi 82:6-8. Yesu anasema kuwa wanadamu wanaweza kuwa “miungu” na watoto wa Mungu.)
-
-
- Je, Yesu amekana Uungu wake? Je, anahafifisha kinachomaanishwa kwa yeye kutangaza, “Mimi na Baba tu umoja?” (Yesu anaonekana kushambulia mantiki ya Wayahudi walioamua kumwua. Sidhani kama Yesu anasema kuwa wanadamu wanaweza kuwa Mungu. Badala yake, anaonekana kuakisi kile ambacho Mwanzo 1 inakisema kuwahusu wanadamu.)
-
-
- Soma Yohana 10:37-38. Yesu anambainishaje Baba wake? (Matendo ya Yesu yanambainisha Baba.)
-
-
- Tunapaswa kuhitimisha nini kuhusu rejea ya Yesu ya Zaburi 82:6 na maisha yetu? (Tunapotenda kile ambacho Mungu anataka tukitende tunaifunua/tunaibainisha asili ya Baba.)
-
-
- Soma Yohana 7:15-17. Mafundisho ya Yesu yanabainisha nini kumhusu Baba wake? (Anafundisha kile ambacho Baba wake alitaka akifundishe.)
-
-
- Zingatia Yohana 7:17. Je, tunapaswa kuamini moja kwa moja kwamba Yesu anafundisha kile ambacho Baba wake alimfunulia? (Yesu anasema kuwa tunaweza kulijaribu hilo.)
-
-
-
- Hebu subiri kidogo. Tunawezaje “kujaribu” anachokisema Bwana wetu? (Hii inaturejesha kwenye roho yetu kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu. Yesu anasema kuwa tukitamani kuyatenda mapenzi ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atatupatia maarifa ya fundisho sahihi.)
-
-
- Soma Yohana 8:38. Je, Yesu anatupatia taswira pana ya wema na uovu? Tunamwelewa Mungu kwa kuangalia alichokitenda Yesu na tunamwelewa Shetani kutokana na kile wanachokitenda wafuasi wake? (Jibu ni, “Ndiyo.” Fikiria jinai ya kutisha uliyopata kuiona. Hiyo inakusaidia kumwelewa Shetani. Linganisha hilo na jinsi Yesu alivyoteseka kwa ajili yetu.)
- Anachokidhihirisha Roho Mtakatifu Kwetu
-
- Soma Yohana 14:24-26. Hebu tujadili anachokisema Yesu kuhusu “maneno.” Maneno ya Yesu yanatoka wapi? (Ni maneno ya Baba wake.)
-
-
- Kuna tatizo gani kwako na kwangu kuyasikiliza maneno ya wengine? (Tunaweza tusielewe. Tuna uwezekano mkubwa wa kusahau.)
-
-
-
- Roho Mtakatifu anatatuaje tatizo letu la neno? (Roho Mtakatifu si tu kwamba anatusaidia kuyakumbuka maneno ya Yesu, lakini pia anatusaidia kuelewa kwa kutufundisha.)
-
-
- Soma Yohana 16:7. Hivi punde tumejifunza kwamba Roho Mtakatifu aliwasaidia wanafunzi kuyakumbuka maneno ya Yesu. Kwa kuzingatia hilo, ilikuwa ni jambo la msaada kiasi gani kwa Yesu kuondoka? (Roho Mtakatifu ni mzalishaji wa kani/nguvu. Roho anaweza kuwepo kila mahali kwa wakati mmoja. Yesu alikuwepo mahali pamoja kwa wakati mmoja alipokuwepo hapa duniani.)
-
- Soma Yohana 16:8. Ni muhimu kiasi gani kwamba Roho Mtakatifu anauhakikisha (convict) ulimwengu? Je, hiyo inakutoa nje ya msitari unapopeleka injili kwa wengine? (Sidhani kama tuliwahi kuwa “nje ya ndoano” linapokuja suala la uhakikisho (conviction) tofauti na kuwashirikisha wengine. Lakini hili ni jambo ambalo nina shida ya kuliweka bayana. Ninadhani kimakosa kwamba ninahitaji kutia hatiani kwa sababu kazi yangu kama mwanasheria ni kuwashawishi wengine.)
-
- Soma Yohana 16:9 je, inaonekana ajabu kwako kwamba dhambi inafafanuliwa kama kutomwamini Yesu? (Kwa miaka mingi masomo yangu yamenishawishi kwamba Yohana Mbatizaji na Yesu walipowaita na kuwaleta watu katika toba walikuwa hawazungumzii dhambi mahsuai. Walikuwa wanazungumzia kuhusu kubadili mawazo yako, kubadili njia yako ya wokovu.)
-
- Soma Yohana 16:10. Uhakikisho (conviction) kuhusu haki una nini cha kujihusisha na Yesu kurejea mbinguni? (Yesu alifufuka kutoka kaburini na kurejea mbinguni kwa sababu aliishinda dhambi. Alilipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. Haki yake inakuwa haki yetu.)
-
- Soma Yohana 16:11. Je, si hukumu yetu ambayo tunataka kuiepuka? Kwa nini tunajali kuhusu hukumu ya Shetani? (Anachokimaanisha Yesu ni kwamba Yeye alishinda na Shetani alishindwa. Tunatakiwa kumchagua Yesu, mshindi, ili kuepuka hukumu.)
- Maneno ya Kufungia (Closing Words)
-
- Soma Yohana 17:1-3. Ni nini msingi wa uzima wa milele? (Kumjua Mungu. Unamjua Mungu kwa kumjua Yesu.)
-
- Soma Yohana 17:8-9. Je, Yesu anakutafuta? (Yesu anasema kuwa anawaombea wafuasi wake, na si ulimwengu kwa ujumla.)
-
- Soma Yohana 17:20-23. Sasa Yesu anamwombea nani? (Wale watakaomchagua katika siku zijazo. Yesu anataka watu wote wamjue Mungu na kuwa wamoja pamoja naye.)
-
- Rafiki, je, utawasaidia wengine kumjua Mungu kwa kuwaelekeza kwa Yesu? Je, utafanya kila uwezalo kumdhihirisha Mungu kwa wengine?
- Juma lijalo: Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo!