Somo la 10: Njia, Kweli na Uzima

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 13 & 14
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
4
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Njia, Kweli na Uzima

(Yohana 13 & 14)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kamwe maishani mwangu sijawahi kuwa na mwanafamilia aliyefahamu kuwa atafariki hivi karibuni, na kutokana na hilo akatoa maelekezo ya kutekelezwa atakapofariki. Bila shaka baadhi ya wasomaji wa somo hili wamepitia uzoefu huo. Sikuweza hata kuwashawishi wazazi wangu kujadili kwa dhati suala la maeneo ya maziko. Matokeo yake ni kwamba wazazi wangu hawakuzikwa katika eneo zuri la makaburi, badala yake wamezikwa katika eneo linalotazamana na duka la vifaa vya ujenzi! Kimsingi wazazi wangu hawajali juu ya hilo. Kwa dhahiri mimi ninajali kwa sababu ninaandika juu ya suala hilo! Juma hili tunaona kwamba Yesu anajali kuhusiana na ustawi wa wanafunzi wake baada ya kuondoka kwake. Anachowafundisha Yesu pia ni ushauri mzuri kwetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuuchukue ushauri wa Yesu!

  1.    Kujitoa Kafara
    1.    Soma Yohana 13:1. Inamaanisha nini kwamba Yesu aliwapenda wanafunzi wake “upeo?”
      1.    Kwa nini Yesu asiwapende wanafunzi wake “upeo?” (Yesu alikuwa mbioni kukabiliana na nyakati za kutisha na kuogofya. Ilikuwa ni jambo la kawaida kudhani kuwa angevurugwa mawazo (distracted) na masuala hayo.)
    1.    Soma Yohana 13:2-5. Tafakari vifungu hizi. Je, vinaleta mantiki yoyote? Ngoja niliweke suala hili katika lugha ya kisasa, “Paulo, hali akijua kuwa alikuwa anakaribia kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni kubwa kabisa nchini kwake, alienda kwenye ghala/stoo ya bidhaa na kuanza kupanga makasha.” Je, hiyo inaleta mantiki?
    1.    Soma Yohana 13:6-8. Hatimaye, tunamwona mtu mwenye mantiki! Huku tukiendelea na analojia ya kisasa, mkuu wa uzalishaji katika kampuni, kama ilivyo kwa Petro, anamwona Afisa Mtendaji Mkuu mtarajiwa akipanga makasha na kusema, “Acha kufanya hiyo kazi! Tuna wapanga makasha wengi, tunahitaji ufanye jambo litakalohakikisha kuwa biashara yetu inaendelea kuwa na mafanikio!” Je, Petro yuko sahihi?
    1.    Angalia tena Yohana 13:8. Kwa nini Petro “asiwe na shirika” na Yesu ikiwa Petro anasisitiza kuitunza heshima ya Yesu? (Kila kitu kimepinduliwa juu chini. Kinachoendelea hakina mantiki yoyote kwa mtazamo wa kawaida wa kibinadamu.)
    1.    Angalia tena Yohana 13:7. Yesu anasema kuwa matendo yake ya sasa hayana mantiki kwa sasa, lakini yatakuwa na mantiki katika siku zijazo. Tunaishi katika siku zijazo, unayaelezeaje matendo ya Yesu ya kuosha miguu ya wanafunzi?
    1.    Soma Mathayo 20:20-24. Hii inatuambia nini juu ya mtazamo wa wanafunzi kuhusu mustakabali wao katika ufalme wa Yesu? (Bila shaka ndugu wale walitaka “Mama” azitie kufuli kwa kuhifadhi nafasi za juu kwa ajili yao. Wanafunzi wengine wanapolisikia jambo hili wanakasirika. Kwa nini? Kwa sababu wanataka kupata nafasi za juu.)
      1.    Unadhani hili ni tatizo kubwa kwa mustakabali wa wanafunzi? Je, ni tatizo kubwa kwa mustakabali wa kanisa la awali?
    1.    Soma Yohana 13:9-11. Je, hili linaonekana kuwa jambo la ajabu kwako? Kwa nini Yesu anaanza kuzungumzia habari za Yuda kwa muktadha wa kutawadha miguu? (Kama umefuatilia masomo haya hapo kabla tulijadili nia ya Yuda kumsaliti Yesu. Nia ya dhahiri, kupewa rushwa, haileti mantiki. Kwa nini Yuda anachukua kiasi kidogo cha fedha wakati alikuwa ukingoni kabisa kuwa msimamizi wa hazina katika Israeli mpya iliyokombolewa? Uwezekano mkubwa wa jambo linaloendelea mawazoni mwake ni kwamba yeye ni mwerevu kuliko mtu yeyote yule katika chumba, na atamlazimisha Yesu kutangaza ufalme wake.)
    1.    Soma Yohana 13:12. Unadhani wanafunzi walimjibuje Yesu?
      1.    Yuda na wanafunzi wengine waliosalia wana jambo gani linalofanana linalozuiwa na Yesu kwa kuwatawadha miguu yao? (Wote wanadhani wana hadhi ya juu na hivyo wanapaswa kuheshimiwa. Yesu anawafafanulia na kuwadhihirishia unyenyekevu halisi.)
    1.    Soma Yohana 13:13-15. Yesu anatangaza kuwa yeye ni “kielelezo.” Kielelezo cha nini? (Mtu mwenye mamlaka kuosha miguu ya wengine.)
      1.    Kifungu cha 14 kinasema wanafunzi wanapaswa kutawadhana miguu, na kifungu cha 15 kinasema utaratibu huu unapaswa kufanyika pia katika siku zijazo. Wanafunzi wote ni viongozi watarajiwa, je, hili ni jambo la kufanywa na viongozi?
      1.    Niliwahi kwenda katika Kanisa Katoliki ambapo padri alianza kuwatawadha miguu washiriki. Je, hiki ndicho alichokikusudia Yesu?
    1.    Soma Yohana 13:16-19. Yesu anahusisha kitendo cha kusalitiwa na Yuda na suala la kuamini kuwa “mimi ndiye.” Kwa nini Yesu anayahusianisha mambo haya mawili? (Yuda aliamini kuwa Yesu atatwaa madaraka. Wanafunzi pia waliamini hivyo. Yesu alipopitia mateso kama mtumishi wa msalaba, ilikuwa vigumu kwa wanafunzi kujipanga upya mipango yao ya siku zijazo. Yesu anawataka wanafunzi wake waelewe alikuja ili kuyatoa maisha yake kwa ajili yao.)
    1.    Tafakari maswali mawili ya muhimu. Kwanza, katika zama za leo fundisho la kuenenda kama mtumishi ni la muhimu kiasi gani? (Umuhimu wa injili ni kuyatoa maisha yako kwa ajili ya wengine. Hicho ndicho alichokifanya Yesu kwa ajili yetu.)
      1.    Pili, kama tukikubaliana kuwa ni fundisho muhimu, je, kutawadha miguu ndio njia ya kujifunza somo hilo? (Sina uhakika kama Yesu anatoa amri kutawadhana miguu kwa vizazi vyote vijavyo. Katika milo hii mtu fulani, mtumwa [mtumishi], alitawadha miguu ya watu wote kwa sababu kuvaa kandambili/makubadhi kulimaanisha miguu ilikuwa michafu. Hakuna mtumwa anayetawadha miguu siku hizi. Mikono, na si miguu, ndio huoshwa kabla ya kula.)
        1.    Je, unaweza kutafakari wajibu wa mtumwa kuhusianishwa na kula ambao hii leo unafanana kwa ukaribu zaidi na utawadhaji miguu? (Wakati ambapo ishara ya kutawadha miguu ni muhimu, nadhani tunaangalia kwa hali ya chini sana. Kwa mfano, kijana anapochagua kazi ya utumishi wa umma badala ya kazi inayomfanya awe tajiri, huo ni utawadhaji miguu. Utawadhaji miguu wa Yesu ilikuwa ni kitendo cha kufa kifo kichungu ili kutupatia uzima wa milele. Huo ndio utawadhaji miguu wa kweli.)
    1.    Soma Yohana 13:33-35. Yesu alikuwa anakwenda wapi ambapo wanafunzi wake wasingeweza kumfuata mara moja? (Alikuwa anarejea mbinguni.)
      1.    Kwa nini, katika muktadha huu, Yesu anawaelekeza wanafunzi kupendana? (Hiyo ni mbingu. Watu hupendana. Tunapaswa kuishi kwa mtazamo wa kimbingu kwa kutumikiana/kuhudumiana.)
  1.   Njia
    1.    Katika Yohana 13:33 Yesu anasema kuwa anakaribia kuondoka, na wanafunzi hawawezi kumfuata katika Yohana 13:36-37 Petro anasisitiza kuwa anaweza kumfuata Yesu kwa sababu yuko tayari kufa kwa ajili ya Yesu. Katika Yohana 14 Yesu anaendelea na mjadala wake kuhusu kuondoka. Soma Yohana 14:3-5. Je, Tomaso yuko sahihi? Hana ramani ya mahali aendako Yesu?
    1.    Soma Yohana 14:6-8. Je, Tomaso anaamini kuwa anayo ramani mawazoni mwake? (Hapana. Tomaso haelewi kitu.)
    1.    Soma Yohana 14:9-11. Unaona ramani gani ya kuelekea mbinguni kwenye maneno haya kwa Filipo na Tomaso? (Hakuna njia halisi iendayo mbinguni, njia ya kwenda mbinguni wanaipata wale wanaoamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu.)
    1.    Soma Yohana 14:12. Je, Yesu anazungumzia utawadhaji miguu? (Hii inafungamanisha imani kwa Yesu na mtazamo wa huduma. Nadhani hiki ndicho kilikuwa mawazoni mwa Yesu alipoanzisha mjadala huu kwa kutawadha miguu ya wanafunzi.)
    1.    Soma Yohana 14:13-14. Je, hii ni ofa ya kufanya jambo lolote tunalomwomba Yesu? (Angalia muktadha tuliojifunza hivi Punde. Yesu anatuambia kwamba ikiwa, katika kuwahudumia wengine, tunaomba jambo lolote atatupatia. Hii ndio njia, kweli na uzima. Yohana 14:16.)
    1.    Rafiki, je, umekua ukiusikiliza ushauri wa Yeau kwa mtazamo wa kifo chake kinachokaribia? Kumwamini Yesu ni kuwasaidia wengine, na si tu kujihudumia mwenyewe. Hizi zilikuwa habari za kukatisha tamaa kwa wale waliodhani kuwa wanakaribia kuwa wakubwa wa taifa. Lakini hebu angalia hili, huduma ya Yesu kwa watu wengine ilimsukuma na kumsogeza mbele kwenye nafasi ya juu kabisa. Katika hili tunaona tofauti kati ya njia za Shetani na njia ya Yesu. Kwa nini usiamue kufuata njia ya Yesu ya kufikia mafanikio?
  1.      Juma lijalo: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.