Somo la 8: Kutimiza Unabii wa Agano la Kale

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 2, 3, 5, 8 & 19
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
4
Lesson Number: 
8

Somo la 8: Kutimiza Unabii wa Agano la Kale

(Yohana 2, 3, 5, 8 & 19)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Uliyafurahiaje masomo yetu katika majuma machache yaliyopita kuhusu ushuhuda kwamba Yesu ni Mungu? Juma hili tuna ushahidi mpya na mwenye nguvu, Agano la Kale la Biblia. Uthibitisho gani bora zaidi ya huu kwamba Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa, Mungu aliyekuja duniani, kisha unabii wa kale? Ukweli kwamba unabii ni wa kale si suala la msingi sana. Bali, suala la msingi ni imani yetu kwamba Mungu aliivuvia Biblia yote. Hivyo basi, shahidi huyu ni Mungu! Hebu tuzame na tuangalie jinsi Yesu anavyotimiza unabii wa kale!

  1.    Macho Kuwa Wazi
    1.    Soma Yohana 5:37-39. Yesu anaashiria kuwa ni nini kiwango cha uelewa wa Biblia cha wasikilizaji wake? (Yesu anasema kuwa wao ni wajinga wa Biblia (“wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu”), na hivyo hawamtambui kama Masihi.)
      1.    Je, unadhani kuwa hadhira itakubali kwamba wao ni wajinga wa Biblia? (Hawatakubaliana kwa nguvu zote. Mafarisayo walikariri Torati (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia).)
      1.    Ikiwa si kweli kwamba viongozi wa Kiyahudi walikuwa wajinga wa Biblia, Yesu anasema nini? (Anasema kuwa hawako makini. Hawako tayari kuelewa kwamba Agano la Kale “linanishuhudia.”)
    1.    Angalia tena Yohana 5:39. Ni nini sababu ya Wayahudi kujifunza Maandiko? (Walidhani kuwa wao ndio njia ya uzima wa milele.)
      1.    Kwa hiyo, jambo gani lilikwenda ndivyo sivyo? Walikuwa wasomi, lakini bado hawakuelewa. Kwa nini?
    1.    Soma Yohana 5:40. Yesu anasema kuwa sababu ni ipi kwa wao kutoyaelewa Maandiko? (“Hamtaki kuja kwangu.”)
      1.    Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Inamaanisha kuwa wanaruhusu chuki zisizo na sababu (prejudice), dhana potofu, au kutokuelewa kwao kuwazuie kuuona ukweli wa Maandiko. Tusiwe kama wao. Hebu leo tuyaangalie Maandiko kwa macho ya wazi kabisa.)
    1.    Soma Yohana 8:17-19 na Yohana 8:23. Yesu anawaambia viongozi wa Kiyahudi kwamba kama wangemjua kwa ukamilifu Yeye na Baba wake wangetambua kuwa Yesu ni nani. Yesu anatoa sababu gani nyingine kwa kushindwa kwao kumtambua? (Hawawasikilizi mashahidi wawili - Mungu Baba na Yesu. Sababu ya wao kutosikiliza ni kwamba wamejikita kwenye mambo ya dunia. Hawezi tu kuwa anasema kwamba wanaishi duniani na Yeye alishuka kutoka mbinguni, vinginevyo hakuna mwanadamu atakayeweza kuelewa kamwe.)
      1.    Kwa nini wanauliza, “Yuko wapi Baba yako?” (Wanamdhihaki Yesu kuhusiana na swali la kuumeni (paternity) kwake. Huo ni uthibitisho zaidi kuwa wao ni “wa ulimwengu huu.”)
  1.   Kuinuliwa
    1.    Soma Yohana 3:14-15. Unafahamu Yesu anarejelea jambo gani?
    1.    Soma Hesabu 21:4-5. Hii ni safari iliyofanywa na watu wa Mungu kutoka kwenye nafasi yao ya utumwa nchini Misri kuelekea katika nchi waliyoahidiwa kupitia kwa Ibrahimu. Madai yao kuhusu chakula na maji yana uhalali gani? (Walikuwa na chakula walichopewa na Mungu, lakini kwa dhahiri hawakukipenda. Kama wasingekuwa na maji, wangekuwa wameshakufa.)
      1.    Je, watu hawa wanasema uongo? (Nadhani. Inawezekana hapakuwepo “chakula na maji” katika jangwa lile, lakini Mungu alikuwa akiwapa chakula na maji. Kwa uaminifu wasingesema kuwa wako ukingoni mwa kifo.)
    1.    Soma Hesabu 21:6-7. Je, hii inakufanya utafakari kuwa Mungu ni yule yule katika Agano la Kale na Agano Jipya? Uliza swali kuu, “Yesu angefanya nini?”
      1.    Je, unadhani mashambulio ya nyoka ni jambo lililotokea kulingana na jambo jingine (coincidence)? (Sidhani. Shetani ni joka wa Edeni, baba wa uongo. Yohana 8:44. Watu walikuwa wanasema uongo kumhusu Mungu, waligeuzwa mawazo yao (distracted) kwa uasi na malalamiko yao, na nyoka walioishi katika maeneo yale wakawashambulia. Wangekuwa makini na mahali walipokuwa wanatembea, wangeweza kuliepuka hili.)
    1.    Soma Hesabu 21:8-9. Kwa nini, kati ya mambo yote, Mungu afanye kitendo cha kuiangalia sanamu ya nyoka kuwa njia ya uponyaji? (Nyoka aliwakilisha dhambi.)
      1.    Je, kisa hiki ni ushuhuda wa Yesu kama Masihi wetu? (Naam, kwa dhahiri kabisa. Yesu alifanyika dhambi kwa ajili yetu (2 Wakorintho 5:21), alichukua dhambi zetu. Alipoinuliwa msalabani, alikufa kwa ajili yetu (Warumi 5:8). Tunapolielewa hili na kumkiri Yesu kama mbadala wetu, tunaokolewa dhidi ya “kung’atwa” na dhambi.
  1.      Siku Tatu
    1.    Soma Yohana 2:14-16. Je, hii inaonekana kama Mungu ambaye tumekuwa tukisoma habari zake? (Hii inaonekana kama kisa cha nyoka tulichokisoma hivi punde.)
    1.    Soma Yohana 2:17 na Zaburi 69:9. Jambo gani linaendelea mawazoni mwa wanafunzi? (Wanadhani kuwa huku ni kutimia kwa msemo wa Agano la Kale.)
    1.    Soma Yohana 2:18-20 na 1 Wafalme 8:12-13. Viongozi wa Kiyahudi wanadhani kuwa Yesu anarejelea uangamivu halisi na ujenzi upya wa jengo la hekalu. Yesu anarejelea nini?
      1.    Ikiwa umejibu, “mwili wake,” je, hiyo inaakisi dhana ya Agano la Kale? (Ndiyo. Hekalu ni mahala ambapo Mungu alikaa ili awe na watu wake. Si nasibu kwamba Yesu anajilinganisha na hekalu, kwa sababu alikuwa Mungu. Alikaa ndani yake mwenyewe.)
  1.   Mifupa
    1.    Soma Yohana 19:31-33 na Yohana 19:36. Ni upi unabii wa Agano la Kale uliotabiri kuwa mifupa ya Yesu haitavunjwa? (Soma Yohana 1:29 na kisha usome Kutoka 12:46 na Hesabu 9:12. Hii inatuonesha kwamba Yesu alitimiza vigezo vya kuwa Kondoo wa Pasaka, kondoo aliyemfanya mwangamizaji kugeuka. Angalia Kutoka 12:21-23.)
    1.    Soma Yohana 19:34, Yohana 19:37, na Zaburi 22:16-17. Utabiri gani wa Agano la Kale unatimia hapa? (Kwamba Yesu “atachomwa.” Hili linatokea mikononi mwake, miguuni mwake, na ubavuni mwake. Lakini hakuna mifupa inayovunjwa.)
    1.    Soma Yohana 19:23-24 na Zaburi 22:18. Kwa nini Agano la Kale linatabiri hiyo habari ndogo kabisa ya kusulubiwa kwa Yesu? (Taarifa hizi ni za muhimu. Wakristo hawatoi tu madai haya ya jumla kwamba Agano la Kale lilitabiri kusulubiwa kwa Yesu, wanaelezea taarifa mahsusi kabisa.)
  1.    Kusifu na Punda
    1.    Soma Zekaria 9:9 na Zaburi 118:25-26. Ungetarajia Masihi afanye nini kama ungekuwa mwanafunzi wa Agano la kale? (Soma Yohana 12:12-15. Yesu pia anatimiza unabii huu.)
    1.    Hebu tuendelee na unabii wa Zekaria na tusome Zekaria 9:10. Hili lilitokea lini? (Halijatokea. Hili ni mojawapo ya mambo magumu ambayo tunatakiwa kukabiliana nayo kwa uaminifu. Viongozi wa Kiyahudi na wanafunzi wa Yesu walikuwa na msingi wa kinabii kuamini kuwa Yesu atawaondoa mabwana wa Kirumi na Kiyahudi na kuleta amani ulimwenguni.)
      1.    Unauelezeaje unabii huu uliofeli? Au, huu si unabii uliofeli? (Endelea kwa kusoma Zekaria 9:14-16. Wakristo wengi wanaamini kuwa unabii wa “nguvu” kumhusu Yesu, tofauti na unabii wa kuteseka kwa kondoo, unahusika na tukio tofauti. Tukio hilo ni ujio wa Yesu Mara ya Pili ambalo ni tukio la nguvu.)
      1.    Juma hili nilimsikiliza mmojawapo wa wahubiri maarufu kabisa katika madhehebu yangu. Alisema hatuamini kwamba Israeli haina umuhimu wowote tena. Kama Israeli haina tena umuhimu wowote kwenye matukio yajayo, je, hiyo inamaanisha kuwa huu ni unabii uliofeli?
    1.    Soma Warumi 11:11-12 inayozungumzia “kujumuishwa kwa Israeli kikamilifu,” na Warumi 11:17-18 na Warumi 11:24. Je, unadhani kuwa Israeli na watu wake hawatakuwa na sehemu yoyote katika matukio ya siku za mwisho?
    1.    Soma Warumi 11:25-29. Inamaanisha nini kusema kwamba “karama za Mungu na mwito wake” “hazina majuto?” (Ninatilia shaka kwamba Israeli si ya muhimu tena. Sidhani kama unabii wa “nguvu” wa Agano la Kale ulishindwa. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba, juma lililopita nilipokuwa sehemu ya mjadala kuhusu mustakabali ujao (future), nilitahadharisha dhidi ya majivuno ya maoni na kupendekeza kwamba unyenyekevu ni jambo bora zaidi kwa sababu wataalamu waliokuwepo katika nyakati za Yesu waliishia kuwa “wajinga” lilipokuja suala la kuuelewa unabii.)
    1.    Rafiki, ninatumaini kwamba baada ya somo hili uthabiti wako kwamba Yesu ni Masihi umeimarishwa na ushahidi wa unabii na matukio ya Agano la Kale. Wakati huo huo, kwa kuwa Yesu anabainisha kuwa wataalamu wa teolojia wa kipindi hicho hawakuuelewa ujio wake, ninapendekeza unyenyekevu katika kuelewa juu ya kutimizwa kwa unabii kuhusu ujio wa Yesu Mara ya Pili. Badala yake, “kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.” Mathayo 24:42. Je, utadhamiria, sasa hivi, kuwa mnyenyekevu na kuwa macho?
  1.   Juma lijalo: Chanzo cha Uzima.