Somo la 5: Ushuhuda wa Wasamaria
Somo la 5: Ushuhuda wa Wasamaria
(Yohana 4)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kila jamii ina watu ambao wana sifa mbaya, watu wanaochukuliwa kuwa na hadhi ya chini kutokana na sababu fulani fulani. Utakumbuka kwambea Nathanaeli, mwanafunzi mtarajiwa, aliuliza swali kumhusu Yesu, “Je, laweza neno jema kutoka Nazareti?” Yohana 1:46. Tunaona katika Tito 1:12 kauli isemayo “Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.” Katika somo hili Yohana anatufungua macho kwenye ukweli kwamba Wayahudi waliwachukulia Wasamaria kuwa watu duni (wa hadhi ya chini). Kwa nini? Mababu wa Wayahudi wa Kisamaria hawakuchukuliwa na watu wa Babeli kama watu wanaostahili kuchukuliwa watumwa, na wale waliooana na wasio Wayahudi ambao baadaye waliingia kwenye dini tofauti! Mtu anapokuchukulia kuwa wewe ni duni, mwitiko wako wa kawaida ni kumchukia. Hii inajenga msingi kwa ajili ya somo letu leo – Wayahudi na Wasamaria walichukiana. Hebu tuzame kwenye somo letu na tuone kile tunachoweza kujifunza jinsi ambavyo Yesu anavyowaendea watu wenye uhasama!
- Safari
-
- Soma Yohana 4:1-3. Kwa nini Yesu anaondoka wakati ambapo mafanikio yake yanakua na kuongezeka? (Kwa dhahiri Yesu alidhani ilikuwa ni mapema mno kwa viongozi wa Kiyahudim kumzingatia. Aliondoka kwenda Galilaya ambapo palikuwa mbali na Yerusalemu.)
-
- Soma Yohana 4:4. Je, hiyo ni kweli? Je, Yesu alikuwa na haja ya “kupita katikati ya Samaria?” (Kama tutakavyoona, Yesu alikuwa na sababu ya msingi ya kupitia njia fupi, badala ya kuzunguka kupitia Samaria. Lakini kwa mujibu wa the Believer’s Commentary, “mara nyingi” Wayahudi walipita kando ya Samaria ili kuepuka kukabiliana na Wasamaria.
- Kisima na Mwanamke
-
- Soma Yohana 4:5-6. Je, Mungu anaweza kuchoka? (Hii ni sehemu ya uthibitisho kwamba Yesu ni mwanadamu kamili na Mungu kamili.)
-
-
- Kila mtu anafahamu “saa sita” ni muda gani? (Ilikuwa ni majira ya adhuhuri (saa sita mchana).)
-
-
- Soma Yohana 4:7-9 na Yohana 4:27. Una maoni gani; je, mwanamke huyu anajenga uhasama au ni mdadisi tu? (Binafsi naona ameshangazwa sana. Wanafunzi wa Yesu “walistaajabu” kwamba Yesu alikuwa anazungumza na mwanamke, achilia mbali mwanamke wa Kisamaria. Mojawapo ya mwanamaoni alisema kuwa rabi halisi/mkali (a strict rabbi) asingeongea na mwanamke hadharani, si hata kwa mkewe au mwanamke yeyote katika familia yake.)
-
- Soma Yohana 4:10-11. Ungekuwa na mwitiko gani kwa kile alichokisema Yesu kama ungekuwa mwanamke huyu? (Anaonekana kuwa na wazimu. Kisima hiki ni kirefu, Yesu hakuwa na chombo cha kuchotea maji, licha ya hayo mgeni huyu wa Kiyahudi anamwambia mwanamke kuwa kama angelikuwa na ufahamu zaidi angekuwa anamwomba Yesu maji.)
-
- Soma Yohana 4:12. Kwa nini mwanamke huyu anaanza kumzungumzia Yakobo, Myahudi? Anahusikaje na kuyapata maji? (Yesu alimtambulisha Mungu kwenye mjadala na kwamba “karama” ya Mungu ingeweza kumpatia “maji yaliyo hai.” Kwa dhahiri mwanamke huyu anadhani kuwa Yakobo aliwapa zawadi ya kisima hiki kwa ajili ya mahitaji ya maji.)
-
- Soma Yohana 4:13-14. Je, Yesu anadai kuwa yeye ni mkuu/mkubwa kuliko Yakobo? (Anadai kutoa maji mazuri zaidi.)
-
- Soma Yohana 4:15. Je, mwanamke huyu amefikia uamuzi wa kwamba Yesu hana wazimu? (Ninadhani anaamini kuwa Yesu ana maji fulani hivi yenye hadhi ya juu, lakini bado hajaelewa anachokisema Yesu.)
-
- Soma Yohana 4:16-19. Je, mazungumzo kati ya Yesu na mwanamke huyu yamebadili mwelekeo? Je, mwanamke anadhani kuwa Yesu anazungumzia jambo zaidi ya maji ya kipekee? (Ukweli kwamba Yesu aliyajua yote haya kumhusu yanamfanya adhani kuwa Yesu ana uhusiano wa kipekee na Mungu.)
-
-
- Je, mwanamke huyu ni mtu anayehitaji uhusiano bora na Mungu? (Kumwendea kwenye kisima hiki hakukuwa kwa kawaida. Sio kawaida kwa sababu ni muda wa joto kali sana, na, kwa mujibu wa Life Application commentary, hakikuwa kisima kilicho karibu sana na nyumbani kwake. Anaonekana kukwepa kukutana na wanawake wengine wanaomfahamu, na sababu inaonekana kuwa bayana – historia yake ya uhusiano wa kingono.)
-
-
-
- Je, Yesu aliuliza kuhusu mumewe ili kumfanya ajisikie vibaya? (Katika jamii ile, kwa usahihi zaidi Yesu alipaswa kuwa anazungumza na mumewe badala ya kuzungumza naye.)
-
- Injili
-
- Soma Yohana 4:19-20. Kwa nini mwanamke huyu anahama kutoka kuzungumzia habari za maji yenye hadhi na kuanza kuzungumzia mahali ambapo watu wanapaswa kuabudia? (Sasa ametambua kuwa Yesu anazungumzia masuala ya kiroho, hivyo anazungumzia kuhusu suluhisho la msingi la kiroho kati ya Wayahudi na Wasamaria – wanapaswa kuabudia wapi?)
-
-
- Hebu subiri kidogo! Je, suala la kiroho si uovu wa mwanamke huyu badala ya mahala gani pa kuabudia? (Watu wanapenda kuepuka kujadili matatizo yao ya kiroho.)
-
-
-
- Kwa nini Yesu anaibua suala la historia ya kingono ya mwanamke huyu? (Hii si ajali. Dhambi zake hazikumzuia Yesu kumpelekea injili, lakini Yesu alidhani kuwa ni sahihi kumkabili kwa dhambi yake. Hii ni tofauti sana na njia inayotumiwa na wale wanaodai kuwa kanisa linapaswa kuwa kimya kuhusu dhambi fulani kwa sababu itawakatisha tamaa watu kwenda kanisani.)
-
-
- Soma Yohana 4:21. Yesu anawezaje kusema hivi? Kwa dhahiri Yerusalemu ni mahali sahihi pa kuabudia. (Sasa Yesu anazungumza kuhusu injili moja kwa moja. Yesu amekuja kutimiza ishara ya mfumo wa kafara Yesusalemu. Anafanya mfumo wa kafara wa hekalu kutokuwa na umuhimu.)
-
- Soma Yohana 4:22. Ni kwa jinsi gani wokovu unatoka kwa Wayahudi? (Yesu alikuja kwenye taifa la Kiyahudi kwanza. Mamaye ni Myahudi.)
-
- Soma Yohana 4:23-24. Unadhani Yesu anamaanisha nini alipomwambia mwanamke lazima aabudu “katika roho na kweli?” (Ninadhani inamaanisha kuwa tunapaswa kuwa na mtazamo sahihi unaojengwa na kweli za Biblia. Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha mtazamo sahihi. Wale wanaoyakataa mafundisho ya Biblia kwa ajili ya mitazamo ya “kisasa” wanashindwa katika idara ya ukweli (truth department).)
- Masihi
-
- Soma Yohana 4:25. Je, mwanamke huyu ametoka mbali katika uelewa wake? (Anaonekana kutoka kwenye kudhani kuwa Yesu ana wazimu, hadi kudhani ya kwamba alikuwa na maji maalumu yatakayoboresha maisha yake, hadi kutafakari kumhusu Masihi.)
-
-
- Tafakari juu ya njia ya Yesu ya kushughulika na mtu mwenye uhasama/chuki.
-
-
- Soma Yohana 4:26. Yesu amemwambia nini? (Yeye ni Masihi. Maoni ya Albert Barnes yanabainisha kuwa hii ndio mara ya kwanza Yesu anakiri wazi kuwa yeye ni Masihi. Zingatia kwamba alitoa tamko hili kwa mwanamke wa Kisamaria.)
- Ujumbe
-
- Soma Yohana 4:28-30. Kwa nini tunaambiwa kuwa mwanamke huyu aliacha mtungi wake kisimani? (Hii inaonesha aliamini kuwa ni kipaumbele chake kikuu kupeleka habari za Yesu.)
-
-
- Yesu alimwambia kwa uwazi kabisa kwamba yeye ndiye Masihi. Kwa nini mwanamke anasema, “Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?” Je, anaonesha mashaka? (Unapouliza swali, kama tufanyavyo kwenye masomo haya, linahusisha msikilizaji kupata utatuzi wa suala. Linawafanya watafakari.)
-
-
-
- Swali lake lilifanyaje kazi? (Waliamua kuja na kuona kama Yesu ni Masihi.)
-
-
- Soma Yohana 4:31-33. Kwa nini Yesu anawaambia wanafunzi jambo ambalo kimantiki anajua kuwa hawatalielewa? (Yesu anawataka watafakari juu ya kile anachokisema.)
-
- Soma Yohana 4:34. Kwa nini Yesu anaiita kazi yake “chakula?” (Alitiwa nguvu kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu. Je, umewahi kujihusisha kwenye jukumu kwa dhati kiasi cha kusahau kama una njaa?)
-
- Soma Yohana 4:35-36. Kwa nini Yesu anaendelea kuzungumzia suala la chakula wakati kwa dhahiri anazungumza kuhusu watu? (Analojia hii si tu kwamba inatusaidia kuelewa asili ya injili, pia inaendana na kauli ya Yesu kwamba kupeleka injili humpa nguvu kama alavyo chakula.)
-
- Soma Yohana 4:37-38. Je, unatiwa moyo na analojia hii ya ukulima? (Hili ni jambo zuri sana! Hatuna haja ya kubeba mabegani mwetu mazungumzo halisi. Tunachokibeba mabegani mwetu ni sehemu ya mchakato wa kuwaongoa wengine.)
-
- Soma Yohana 4:39. Je, hii inamaanisha kuwa uelewa wa Yesu wa historia ya mwanamke yule uliwaongoa? (Huo ulikuwa ushuhuda wa mwanamke. Ushuhuda wake pamoja na swali lake kuhusu kama kweli Yesu ni Masihi ulisababisha usikivu na imani ya kutosha kiasi kwamba walitaka kufahamu zaidi.)
-
- Soma Yohana 4:40-42. Je, huu ni ufafanuzi wa Yesu wa analojia ya shamba? Inawahitaji mwanamke na Yesu kufanya kazi pamoja ili kuanza mchakato wa kuanzisha uongofu wa Wasamaria?
-
-
- Kati ya watu wote ambao Yesu angeweza kuwatumia kuwa washirika wake katika kuwaongoa Wasamaria, kwa nini alimchagua mwanamke huyu?
-
-
- Rafiki, kisa hiki kinatupatia mwelekeo (roadmap) wa kuwaongoa watu wanaotuchukia, lakini si lazima wawe na uhasama na Mungu. Kwa nini usiombe sasa hivi ili Roho Mtakatifu akusaidie kutumia kanuni zilizotumika kwenye kisa hiki katika ushuhudiaji wako?
- Juma lijalo: Shuhuda Zaidi Kuhusu Yesu.