Somo la 4: Mashuhuda wa Kristo Kama Masihi
Somo la 4: Mashuhuda wa Kristo Kama Masihi
(Yohana 1 & 3)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Katika mahakama za Marekani njia kuu ya kutafuta uthibitisho ni kwa njia ya mashahidi. Njia nyingine ya msingi ya kuthibitisha jambo ni kwa njia ya nyaraka. Nyaraka nyingi hazijithibitishi zenyewe, hivyo pia lazima uthibitisho wake utokane na mashahidi. Kuna njia kadhaa za kuujaribu ukweli unaosemwa na mashahidi chini ya kiapo. Ninakumbuka kesi iliyochukua siku 53 ambapo ushahidi wa moja kwa moja uliwasilishwa kwa njia ya hati ya viapo (affidavits), na takriban ushahidi wote uliotolewa na watu niliuthibitisha kwa kuwahoji (cross-examined) mashahidi waliowasilisha hati za viapo. Hilo si jambo la kawaida kabisa, lakini lilifanyika ili kufupisha muda wa kesi! Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone ni mashahidi gani anaowaita Yohana ili kutoa ushahidi kumhusu Yesu. Kwa kuwa nina uzoefu wa kuwahoji mashahidi, nitashiriki nanyi nguvu ya ushahidi kana kwamba mimi ni mkosoaji, jambo ambalo si tabia yangu (mimi si mkosoaji).
- Shahidi wa Kwanza: Yohana Mbatizaji
-
- Soma Yohana 1:19-20. Hii inaashiria kuwa viongozi wa Kiyahudi walidhani kuwa Yohana Mbatizaji ni nani? (Walidhani anaweza kuwa Masihi.)
-
-
- Yohana anakana kuwa yeye si Masihi. Kama ungetakiwa kuujaribu ushuhuda wa Yohana, ungewaza jambo gani akilini mwako? (Msingi mkuu wa kumjaribu shahidi ni upendelevu (bias) unaozingatia maslahi binafsi. Watu wanapenda kuamini kuwa wao ni wa muhimu zaidi, si vinginevyo. Hii inaufanya ushuhuda wa Yohana kwenye jambo hili kuwa wa kuaminika.)
-
-
- Soma Yohana 1:21. Utaona kuwa Kumbukumbu la Torati 18:15 inaandika kwamba Musa alitabiri kuwa “nabii” kama yeye atakuja. Je, Yohana angebainisha kuwa alikuwa mtu wa muhimu kwa kusema kuwa yeye ni “Eliya” au “Nabii?” (Kwa mara nyingine, upendelevu wa kujiona muhimu ungeunga mkono madai kuwa yeyote kati ya hao watu muhimu kihistoria. Kwa hiyo Yohana anasema ukweli.)
-
- Soma Yohana 1:23 na Isaya 40:3. Je, Yohana anatoa madai ya wajibu tofauti, lakini ambao bado ni wa muhimu? (Ndiyo. Lakini bado hii inaashiria kuwa Yohana ni mwaminifu. Kama utadanganya, kwa nini usijikite kwenye uongo ambao viongozi wa Kiyahudi wana mwelekeo wa kuukubali?
-
- Soma Yohana 1:24-25. Sasa Yohana anapewa changamoto na mawakala wa viongozi wa Kiyahudi kwa sababu hadai kuwa yeye ni mmojawapo wa watu muhimu ambao wamekuwa wakimuulizia habari zake. Kwa nini wajibu mdogo wa Yohana uufanye ubatizo uwe jambo lisilofaa? (Maoni ya Albert Barnes yanatufahamisha kuwa wapagani walioongoka na kuingia kwenye dini ya Kiyahudi walibatizwa. Kamwe Wayahudi hawakubatizwa. Hata hivyo, mtu aliyetoka mbinguni angeweza kudai kuwa na mamlaka ya kuwabatiza Wayahudi.)
-
- Soma Yohana 1:26-27. Je, huu unaonekana kama ushuhuda wa kweli? (Naam. Yohana anabainisha kuwa yeye hastahili.)
-
- Soma Yohana 1:29-30. Yohana anathibitisha kuwa Yesu ni Masihi. Anamuunganisha Yesu na huduma ya kafara ya Kiyahudi. Je, kauli hii ni ya kuaminika? (Tayari Yohana ameshaweka mazingira mazuri ya kuaminika. Kauli hii haina chochote cha kuhafifisha kuaminika huko.)
-
-
- Tafakari tena dhana ya kwamba sababu ya kuuamini ushahidi ni pale ushahidi huo unapoenda kinyume na maslahi binafsi ya mnenaji. Je, Yohana ana maslahi yanayotofautiana na Yesu kuwa kondoo wa kafara? (Dhahania ni kwamba, Yohana, kama ilivyo kwa mtu yeyote yule, alidhani kuwa Masihi atakuja ili kuwaangusha Warumi. Kuja ili afe haiendani na tumaini hilo.)
-
- Shahidi wa Pili: Roho Mtakatifu
-
- Soma Yohana 1:32-34. Yohana anasema kuwa nani anathibitisha ushuhuda wake? (Roho ashukaye kutoka mbinguni. Lazima huyu atakuwa Roho Mtakatifu.)
-
-
- Hebu tujadili ushahidi wa kusikia kidogo. Jambo la kusikia ni lile ambalo shahidi alimsikia mtu mwingine akilisema. Kwa ujumla ni ushahidi usiokubalika kwa sababu, pamoja na mambo mengine, mzungumzaji hawezi kuhojiwa (cross-examined), lakini mengi ya yale ambayo Roho aliyasema Yohana aliyaona yakitokea.)
-
-
-
- Zingatia tena Yohana 1:34. Yohana anadai kuwa anashuhudia nini? (“Ameona” kuwa Yesu “ni Mwana wa Mungu.”)
-
- Shahidi wa Tatu: Andrea
-
- Soma Yohana 1:35-37. Bado Yohana Mbatizaji anaongea, lakini angalia mwitiko wa wanafunzi. Hawa ni wanafunzi wa nani? (Wa Yohana!)
-
-
- Kwa nini wamwache Yohana na kumfuata Yesu? (Kwa sababu walimwamini Yohana. Utaona kwamba wamehitimisha kuwa Yesu ni mkuu kuliko Yohana.)
-
-
- Soma Yohana 1:38-39. Je, wanafunzi hawa wawili wamejibu swali la Yesu kwa akili? (Kwa haraka haraka linaonekana jibu la kipumbavu. Huenda wamepigwa butwaa, ikimaanisha kuwa hawajui nini cha kumwambia mtu wa muhimu sana katika historia. Maoni ya Albert Barnes yanaashiria kuwa wanafunzi hawa wanaamua tu kuwa wapole. Hawataki kumwingilia (interrupt) Yesu, lakini wanataka kufahamu wanaweza kwenda wapi baadaye na kujadili juu ya kuwa wanafunzi wake.)
-
- Soma Yohana 1:40-41. Unajenga hoja gani kuhusu uaminifu wa Andrea? (Ingawa Andrea anaweza asiwe sahihi, kwa dhahiri anasema jambo analoliamini. Kwa nini? Alibadili kazi kutokana na kile alichomsikia Yohana akikisema na kile alichokiona wakati akimfuata Yohana.)
- Shahidi wa Nne na wa Tano: Filipo na Nathanaeli
-
- Soma Yohana 1:43-46. Andrea, na huenda Petro, walikuwa wanamfuata Yesu ili kuona kama wangeweza kuwa wanafunzi wake. Hili ni tofauti kivipi kwa Filipo? (Yesu anamuita.)
-
-
- Filipo anathibitisha kuwa Yesu ni Masihi. Filipo anajenga hoja gani ili kuunga mkono kauli yake? (Anasema kuwa Yesu anaendana na kile ambacho Musa alikitabiri katika Kumbukumbu la Torati na kile ambacho manabii wa Agano la Kale walikitabiri.)
-
-
-
-
- Je, Filipo amebadili kazi yake kutokana na imani yake?
-
-
-
-
- Filipo anajenga ushuhuda wake juu ya nini? (Utaona kwamba hahoji ukweli wa kile alichokiongea na Nathanieli. Anazingatia tu ushahidi.)
-
-
- Soma Yohana 1:47-49. Yesu anasema nini kumhusu Nathanaeli? (Ni mtu mwaminifu.)
-
-
- Ni nini msingi wa Ushuhuda wa Nathanaeli kwamba Yesu ni Mungu? (Yesu alimwambia Nathanaeli kile alichokuwa akikifanya.)
-
-
-
-
- Je, kwa upande wako huo unaonekana kama ushahidi wenye nguvu?
-
-
-
- Soma Yohana 1:50-51. Je, Yesu anautafakari ushuhuda huu wenye nguvu? (Hii inaashiria kuwa hauchukulii hivyo. Yesu anamwambia kuwa ataona ushahidi mkubwa zaidi.)
-
-
- Utajengaje hoja kuhusu kuaminika kwa Nathanieli? (Nathanaeli alianza na imani inayopingana na Yesu kuwa Masihi. Sasa ameshawishika kuwa hakuwa sahihi.)
-
- Shahidi wa Sita: Nikodemo
-
- Soma Yohana 3:1-2. Je, Nikodemo anaamini kuwa Yesu ni Masihi? (Hapana. Anamuita “Rabi,” na katikati ya hilo lazima Mungu atakuwa na Yesu. Hata hivyo, anakutana na Yesu muda ambao hakuna mtu atakayegundua.)
-
- Tutaruka baadhi ya vifungu na kujikita kwenye vifungu ambavyo vinazingatia mtazamo wa Nikodemo juu ya Yesu. Soma Yohana 3:8-10. Je, Yesu anaonesha heshima kwa Nikodemo? (Hapana. Anamdhihaki.)
-
- Soma Yohana 3:11-12. Je, hii pia ni dhihaka? (Ndiyo. Yesu anasema “wala hamnisadiki” kwenye mambo ya kawaida kabisa, kwa nini niwaambie juu ya mambo ya mbinguni?
-
- Soma Yohana 3:13-15. Je, hili lingekushawishi kwamba Yesu ni Mungu kama ungekuwa Nikodemo? (Yesu hatoi madai ya kwamba yeye ndiye mfalme ajaye, anasema yeye anafanana na nyoka “aliyeinuliwa.” Angalia Hesabu 21:8-9.)
-
- Soma Yohana 19:38-39. Je, hii inaandika kauli kutoka kwa Nikodemo kumhusu Yesu? (Hapana.)
-
-
- Kwa nini tumuite Nikodemo kuwa ni shahidi? (Anachokitenda mtu ni ushahidi mzuri wa kile anachokiamini. Yusufu wa Arimathaya anaelezewa kuwa mwanafunzi wa Yesu. Kumbukumbu hii ya kile anachokitenda Nikodemo inaashiria kuwa pia ameshafanya uamuzi kwa ajili ya Yesu.)
-
-
-
- Maoni mbalimbali yanatuambia kuwa Nikodemo ameleta kiwango kikubwa sana cha manukato ili kuuhifadhi mwili wa Yesu. Je, hiyo inazungumzia lolote kuhusu mtazamo wa Nikodemo? (Inatuambia kuwa Nikodemo ni tajiri, lakini pia inatuambia kuwa aliamini kwamba Yesu ni wa muhimu na alistahili sadaka hii. Inatuambia kuwa Nikodemo ameungana na Yesu, badala ya kuungana na Mafarisayo.)
-
-
-
- Mjadala wa awali wa Yesu katika kitabu cha Yohana 3 unatuambia nini kuhusu kuaminika kwa uamuzi wa Nikodemo? (Kwa kawaida, hatuwakubali au kuwaunga mkono watu wanaotudhihaki. Hii ni kweli hususan pale tunapokuwa na nafasi muhimu. Nikodemo alikuwa na sababu nyingi za kumkasirikia na kumkataa Yesu. Matendo ya Nikodemo yanatuambia kuwa amevishinda vikwazo hivi na sasa anamheshimu Yesu.)
-
-
- Rafiki, je, utawaamini mashahidi hawa? Je, kuwahoji kwako kumekufanya uwaamini? Kama kamwe hujawahi kutoa kauli ya imani kwamba Yesu ni Mungu, aliyeshuka duniani ili kuondoa dhambi zetu, kwa nini usikiri hivyo sasa hivi?
- Juma lijalo: Ushuhuda wa Wasamaria.