Somo la 3: Kisa Usuli: Utangulizi

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 1 & 17
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
4
Lesson Number: 
3

Somo la 3: Kisa Usuli: Utangulizi

(Yohana 1 & 17)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kama unasoma somo hili, uwezekano mkubwa ni kwamba unamwamini Yesu. Hiyo inamaanisha nini kwako? Unajua na kufahamu kwa kiasi gani habari za utangulizi wa Yesu? Unauelewaje wajibu wake ulimwenguni? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone jinsi Yohana anavyotutambulisha kwa Yesu. Utambulisho wa Yohana unatutambulishaje mtazamo mkubwa na mpana wa Yesu? Twende zetu!

  1.    Neno
    1.    Soma Yohana 1:1. Mara moja tunaingia kwenye tatizo. “Neno” linawezaje, vyovyote iwavyo, “kulikuwako” na Mungu na “alikuwako” kwa Mungu?
    1.    Kabla hatujaanza kutatua suala hili la “kulikuwako/alikuwako,” hebu tusome Yohana 1:14 ili tumwangalie huyu Neno ni nani. Neno ni nani? (Yesu. Yohana anapoandika Neno kufanyika mwili na kukaa kwetu, anaweza tu kuwa anamwelezea Yesu.)
      1.    Utaona kwamba Yesu anarejelewa kama “Mwana Pekee” ambaye “anatoka kwa Baba.” Sasa tumeongezea “anatoka” kwenye fumbo letu la “kulikuwako/alikuwako!”
    1.    Soma Yohana 1:2. Neno amekuwa na Mungu kwa muda gani? (Tangu mwanzo.)
      1.    Katika Yohana 1:14 na Yohana 1:18, miongoni mwa sehemu nyinginezo nyingi katika Biblia, Yesu anaelezewa kama “Mwana” na Mungu anaelezewa kama “Baba.” Hiyo inaashiria kwamba kwa namna fulani Mungu Baba alimuumba Yesu Mwana. Je, hiyo ni kweli? (Isingeweza kuwa kweli kama kiuhalisia Yesu alikuwapo mwanzo pamoja na Mungu.)
        1.    Je, kuwapo tangu mwanzo kunafafanua suala la “alikuwako” na Mungu la Yohana 1:1? (Nadhani kunafafanua. Yesu alikuwako na Mungu Baba tangu mwanzo.)
    1.    Angalia tena Yohana 1:1. Sasa tuna uelewa mzuri wa kauli ya “alikuwako” na Mungu. Unaelewaje namna ambayo Yesu kuwa “Mungu” inaendana na Yesu “kuwako” na Mungu? (Sheria ya Marekani ina kanuni ambayo kimantiki inatumika hapa. Sheria mbili hazikinzani ikiwa zote mbili zinaweza kutumika kikamilifu. Kwa dhahiri Yesu anaelezewa kuwa “Mungu” na “kuwako na Mungu.” Hiyo inaelezea utambulisho wa pamoja.)
      1.    Kwa kuwa hilo sasa limeshatatuliwa, tunapaswa kuelewaje sehemu ya ufafanuzi ya “alikuwako?” (Yesu alikuja kwetu kutoka mbinguni, hiyo inafafanua kauli ya “alikuwako.”)
  1.   Muumba wa Vyote
    1.    Soma Yohana 1:3. Yesu amefanya nini? (Yeye ni Muumba wa “vyote.” “Vyote vilifanyika kwa huyo.”)
    1.    Hebu tusome kifungu cha kwanza kati ya vifungu viwili vinavyofanana. Soma Mwanzo 1:1-3. Yesu aliumbaje? (Kwa kunena na vitu vikawepo.)
      1.    Hii inatoaje maana kamili kwenye sababu ya kumuita Yesu “Neno?” (Neno la Yesu liliumba vitu vyote.)
    1.    Kifungu kinachofuata ni Warumi 1:18-20. Kumwamini Yesu kumefafanuliwaje hapa? (Kuuangalia Uumbaji na kuamini kuwa Yesu yupo na kwamba alifanya Uumbaji.)
      1.    Romans 1:18 inawarejelea wasio na haki (waovu) waipingao kweli. Je, unamfahamu mtu yeyote anayeipinga kweli huu? (Kila anayeutangaza uibukaji (evolution) badala ya uumbaji ni mpinga kweli.)
        1.    Hiyo inatusaidiaje kufafanua vizuri zaidi kinachomaanishwa “kumwamini Yesu?” (Hili si tu suala la kuamini uwapo wake, bali tunatakiwa kuikubali kama kweli kile anachojinenea.)
        1.    Chukulia kwamba nimemwandikia barua mwajiri wako kuwa kazi yako inaweza kutekelezeka vizuri tu endapo ungefukuzwa kazi na kazi yako kuachwa kutekelezwa kwa nasibu na asili kuchukua mkondo wake (chance and natural selection). Je, utaudhika? (Naam. Na kwa kuongezea, usipokuwa kama wewe ni mwanasiasa, haitakuwa kweli!)
  1.      Nuru
    1.    Soma Yohana 1:4-5. Tunaona ukinzani gani hapa? (Kuna nuru na kuna giza duniani. Yesu ni nuru, na upinzani haujamshinda.)
    1.    Soma Yohana 1:9-12. Tunaona mgawanyiko gani miongoni mwa watu? (Kuna wale ambao hawampokei Yesu, na hawaamini kuwa aliufanya ulimwengu, na kuna wale wanaompokea na kuamini katika uwezo wake na tabia yake. Wale wanaoamini wana haki ya kudai kuwa ni watoto wa Mungu.)
      1.    Ninawasikia watu nchini Marekani wakisema kuwa “hatujawahi kugawanyika.” Je, hilo ni kweli? (Mara zote pamekuwepo na mgawanyiko kati ya watoto wa Mungu na giza. Giza linafafanuliwa kama wale wasioamini katika uwezo wa Mungu.)
    1.    Soma Yohana 1:17. “Neema na kweli” zinatofautianaje na torati? (Nuru kamili ya Mungu ni kwamba Yesu alikuja kutuonesha ukweli wa asili ya Mungu. Kiini cha ukweli huo ni kwamba tunaokolewa kwa neema na si kwa matendo ya sheria. Angalia Wagalatia 3:10-14.)
    1.    Soma tena Yohana 1:10-11. Kwa dhahiri Yohana anaangalia nyuma katika kipindi alichokuwa na Yesu. Unadhani Yohana anamuwazia nani anapowaelezea “watu wake mwenyewe” ambao “hawakumpokea?” (Viongozi wa Kiyahudi waliopanga njama ya kumwua Yesu. Na Yuda, ambaye alikuwa mmojawapo wa wanafunzi.)
      1.    Kwa dhahiri Yuda na viongozi wa Kiyahudi walimwamini Yesu. Kasoro yao ilikuwa ni ipi? (Yuda ni mfano mzuri wa kile tunachokizungumzia. Alidhani kuwa alikuwa mwerevu kuliko Yesu. Alidhani kuwa angemlazimisha Yesu kuwa mfalme wa taifa la Kiyahudi. Mkristo anaweza kuamini katika uwapo wa Yesu, lakini kama huamini na kuamini katika kile anachokisema Yesu, unafuata giza na si nuru.)
      1.    Je, viongozi wa Kiyahudi na Yuda walidhani kuwa walikuwa watu wa kidini? Je, walitumia muda wao kutangaza mitazamo yao ya kidini? (Ndiyo. Kutokana na hili tunajifunza kuwa kudhani kuwa sisi ni watu wa kidini, hata kuwa na kazi inayotangaza dini, inaweza kuwa jambo lisilo na maana. Jambo la msingi ni endapo unaamini kile anachokisema Yesu na kinachosemwa na Biblia, au kama unatengeneza dira yako mwenyewe ya maadili.)
  1.   Utukufu
    1.    Soma Yohana 17:1-2. Yesu anazungumzia “saa” gani? (Soma Yohana 16:32. Yesu anarejelea kauli yake kuhusu wanafunzi kumtelekeza. Hiyo ni rejea ya kukamatwa kwake iliyoishia kwenye kusulubiwa kwake.)
      1.    Kwa utangulizi huo, “utukufu” kwa Yesu na Baba ni upi? (Wamefungiwa kwenye pambano dhidi ya Shetani. Pambano hilo lilihusisha kama sheria ilikuwa ya haki, endapo Shetani alikuwa bwana wa ulimwengu, na endapo Yesu atatimiza wajibu wa wanadamu kuishika sheria, na kuzibeba dhambi zetu kwa kifo chake. Yesu alishinda pambano kwenye nyanja zote hizi.)
    1.    Soma Yohana 17:3. Yesu anaifafanuaje njia ya uzima wa milele? (Kumjua Mungu Baba na Yesu.)
      1.    Hii inaashiria kuwa tunawezaje kumjua Baba? (Tunamjua Baba kupitia kwa Yesu.)
    1.    Hebu turuke hadi mbele na tusome Yohana 17:7-8. Ni kwa jinsi gani hasa Yesu anatusaidia kumjua Mungu Baba? (Kwa njia ya maneno na matendo ya Yesu.)
      1.    Je, ungetarajia kwamba Mungu Baba ni mkali zaidi kuliko Yesu, Mwana? (Hii inaonesha kuwa hayuko hivyo.)
    1.    Soma Yohana 17:4-6. Unadhani ni nani hasa ambaye Yesu anamzungumzia pale anaporejelea “watu wale ulionipa,” ambao “neno lako wamelishika?” (Lazima hii inawajumuisha wanafunzi.)
      1.    Kama ulikuwa pamoja nami katika mfululizo wa masomo yaliyopita ya kitabu cha Marko, unafahamu kuwa wanafunzi walikuwa na matatizo makubwa katika kumwelewa na kumfuata Yesu. Unaweza kuelezeaje kile ambacho Yesu amekisema hivi punde? (Hii ni faraja kwetu. Yesu anatoa kikolezo chanya kwa kile inachomaanisha kulishika neno la Mungu.)
    1.    Angalia tena Yohana 17:7-8. Ni lipi lililo jambo la msingi kwa wanadamu wanaotamani kumpa Mungu utukufu? (Kuamini kuwa Mungu alimtuma Yesu. Kuamini kuwa alichokisema na kukitenda Yesu kinaakisi kile alichopewa kutoka kwa Baba wake mbinguni.)
    1.    Rafiki, je, unaamini kuwa Yesu aliumba kila kitu? Kwamba Yeye ni mmoja pamoja na Mungu Baba? Kwamba alichokisema na kukitenda Yesu duniani kinaakisi asili ya Mungu? Ikiwa ndivyo, basi wewe ni sehemu ya utukufu wa Yesu! Wewe ni sehemu ya wale wanaomwamini Yesu kwa dhati. Kama huamini, jambo gani litakufanya uamini?
  1.    Juma lijalo: Mashuhuda wa Kristo Kama Masihi.