Somo la 9: Mitafaruku Yerusalemu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Marko 11 & 12
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
3
Lesson Number: 
9

Somo la 9: Mitafaruku Yerusalemu

(Marko 11 & 12)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unapenda kitabu kilicho na maelezo yenye kona kona? Maelezo ya Marko sasa yanageukia mahala kwingine. Utakumbuka alianza na uthibitisho kuwa Yesu ni Mungu. Kisha Marko akageukia kwenye ukweli wa kutisha kwamba Yesu atakufa na kufufuka. Muda wote huo Yesu aliwaambia wale aliowaponya kwa kurudiarudia kwamba wafanye uponyaji huo kuwa siri. Aliwaambia wanafunzi wake waufanye mustakabali wake wa siku zijazo kuwa siri. Sasa, muda wa kutunza siri umekwisha. Yesu amedhamiria kwamba sasa muda umefika kwa yeye kudhihirisha kwa nguvu zote kuwa yeye ni nani. Na anafanya hivyo Yerusalemu! Hebu tuzame kwenye kitabu cha Marko na tuungane na Yesu kwenye ufunuo mkubwa!

  1.    Sasa Hakuna Siri
    1.    Soma Marko 11:1-2. Nilipokuwa mdogo tulikuwa na “uwindaji wa kuokoteza.” Mtu mmoja aliorodhesha vitu vya kipekee kabisa, na kisha tuliunda timu na kuanza kuzunguka na kuvipata vitu vilivyokuwa kwenye orodha na kuvirejesha. Timu iliyokuwa ya kwanza kupata kila kitu kwenye orodha ndiyo ilikuwa mshindi. Je, huu ni uwindaji wa kuokoteza? (Ni vigumu kuwa hivyo. Yesu anawaambia wanafunzi mahali mahsusi ambapo watampata mwana-punda, na hata kuwaambia kuwa mwana-punda huyo hajapandwa na mtu bado.)
      1.    Tunapaswa kuhitimisha nini kutokana na ufasaha wa uelewa wa Yesu?
    1.    Soma Marko 11:3-6. Kama ulidhani kuwa wizi unafanyika hapa, je, hili ni jibu la kuridhisha? (Maoni ya John MacArthur yanasema kuwa Yesu alikuwa anajulikana sana katika eneo hilo. Watu walioleta changamoto kwenye kumchukua mwana-punda waliposikia kuwa jambo hili lilikuwa ni kwa ajili ya Yesu, walikubaliana nalo.)
    1.    Soma Marko 11:7-10, Zaburi 118:26, na Luka 19:38-40. Utakumbuka kuwa Yesu ndiye ameanzisha jambo hili. Yesu anawaambia nini watu katika Yerusalemu? (Kwamba yeye ni Masihi. Ndio maana viongozi wa Kiyahudi walidhani kuwa karipio lilikuwa sahihi kulitenda. Yesu anajibu kuwa ujumbe si wa kiulimwengu (supernatural) – mawe yatapiga kelele.)
    1.    Soma Marko 11:11. Je, hii ni kinyume na hali ya tabia ya nchi? Mara moja Yesu anaenenda kama mtalii? (Ni kinyume chake tu. Yesu analikagua hekalu. Tutarudi kwenye matokeo ya ukaguzi huo katika sehemu inayofuata.)
  1.   Kusafisha Hekalu
    1.    Hebu turuke vifungu kadhaa hadi chini (Tutarejea baadaye.) Soma Marko 11:15-18. Je, hekalu limefaulu ukaguzi wa Yesu baada ya Yesu kufanya ufuatiliaji? (Kwa dhahiri hapana.)
    1.    Angalia tena Marko 11:17. Marko anasema Yesu “akawafundisha.” Anawafundisha nini? Je, anatufundisha jambo lolote?
      1.    Wakristo wengi wanajenga hoja, kutokana na maisha ya Yesu, kwamba hatupaswi kujiingiza katika kujaribu kulipeleka taifa letu kwenye njia ya maadili zaidi. Wanajielekeza kwenye ukweli kwamba kamwe Yesu hakujihusisha na siasa. Je, hilo linaonekana kuwa sahihi kwako? (Kuna tofauti mbili kubwa kati ya hali ya Yesu na yetu. Kwanza, sisi si Mungu. Lakini pili, Rumi haikuwa na demokrasia. Katika kisa hiki tunamwona Yesu akifanyia kazi kubadili kile anachoweza.)
      1.    Soma Marko 10:1-2. Unakumbuka tulipojifunza jambo hili? “Mtego” ulikuwa laana ya talaka ambayo itamchukiza Herode Antipa (ambaye aliamuru kuuawa kwa Yohana Mbatizaji). Je, Yesu alijizuia kutoa maoni kwenye maadili ya umma – hata pale ilipokuwa jambo la hatari? (Kama tulivyojifunza juma lililopita, Yesu alichukua msimamo thabiti kwenye suala la usafi wa ngono.)
    1.    Hebu tusalie kwenye Marko 11:17 kwa muda mrefu kidogo. Unadhani kwa nini Yesu alirejelea “mataifa yote” kwa muktadha wa hekalu la Kiyahudi? (Soma Isaya 56:6-7. Hii inatoa uthibitisho mkubwa kwamba Yesu hakuwa akisafisha ndani ya hekalu halisi, bali alikuwa katika “Mataifa Yote.” Mataifa yasingeweza kulikaribia hekalu kwa ukaribu kuzidi eneo hili. Hii inaimarisha hoja kuhusu “maadili ya umma.” Yesu anatetea nafasi ambayo Mataifa wanaweza kumwendea Mungu.)
  1.      Mamlaka Hekaluni
    1.    Hebu turuke vifungu kadhaa hadi chini tena. Soma Marko 11:27-28. Je, hili ni swali lenye mantiki? Nani aliyempa Yesu mamlaka ya kuvuruga kile ambacho viongozi wa Kiyahudi walikiruhusu?
    1.    Soma Marko 11:29-33. Kwa nini Yesu atake kulifanya hili kuwa siri? Je, hili si jambo ambalo lilihusu kuingia kwake Yerusalemu? (Soma Marko 4:11-12. Tumelijadili hili hapo kabla. Yesu anaufunua ukweli kwa wale wanaotaka kuujua. Sio kwa wenye chuki au wasio na hamu ya kuujua.)
  1.   Mtini
    1.    Hebu turejee na tuangalie vifungu tulivyoviruka. Zingatia kwamba ninadhani mpangilio wa Biblia ni sehemu ya utendaji wa Roho Mtakatifu. Soma Marko 11:12-14. Ooh mtini usio na matunda! Kwa nini Yesu anatafuta matunda ya tini wakati sio msimu wa matunda?
      1.    Kibaya zaidi, kwa nini Yesu anaulaani mtini kwa kufanana na mitini mingine yote? Na hata huu sio mtini wake!
    1.    Hebu tuangalie Marko 11:13 tena. Utaona kifungu kinasema kuwa mtini huu una majani. Je, hilo ni la muhimu? (Maoni kadhaa yanasema kuwa uwapo wa majani ni ishara kwamba kunapaswa kuwapo chakula – hata kama ni “machipukizi,” ambayo yanalika.)
    1.    Hebu turukie chini na tusome kisa chote kilichosalia kuhusu mtini. Soma Marko 11:20-21. Kwa nini jambo hili ni la muhimu? (Usingetarajia mti kunyauka mara moja. Huu ni muujiza wenye asili hasi.)
    1.    Soma Marko 11:22. Unadhani hili ni jambo la ajabu? Kama Yesu anataka kuhamasisha imani kwa Mungu, kwa nini aue mti ili kulitekeleza hilo? (Kuna jambo la ziada linaloendelea hapa. Kumbuka kwamba muktadha ni muhimu. Muktadha unaashiria kuwa Yerusalemu “imejaa majani,” inaonesha ishara kwamba ni mahali ambapo ujumbe wa Mungu unaweza kupatikana. Inaonekana kuwa Yerusalemu inakaribia kumuua Masihi wake, hivyo kuonesha kuwa haina matunda. Kama tunavyofahamu, muda mfupi baada ya tukio hili Yerusalemu iliangamizwa.)
    1.    Soma Marko 11:23-24. Kuua miti, kung’oa milima. Je, maombi yetu yanatakiwa kuwa ya mambo chanya? (Hoja ya mambo haya kuwa chanya ni kwamba mti ni mfano wa somo muhimu. Kwa ujumla milima inachukuliwa kama changamoto maishani.)
      1.    Ni nini kigezo cha ombi lililojibiwa? (Kuamini kuwa umepokea ulichokiomba.)
      1.    Rafiki, kauli hii haina masharti. Nimewaona Wakristo wanao “amuru” muujiza. Inaonekana kwamba Yesu anatoa jambo hilo bure. Una maoni gani? (Maoni ya Biblia (The Bible Knowledge Commentary) yanasema ahadi hii masharti yake ni ombi kuendana na mapenzi ya Mungu. Hicho sicho kinachosemwa na kifungu hiki.)
    1.    Soma Marko 14:35-36. Je, inawezekana Yesu aliamuru kwamba aondolewe kwenye mzigo wa mateso na kifo? (Ndiyo. Alichokiahidi Yesu katika Marko 11 hakina masharti kama kinavyoonekana. Lakini Mkristo mwenye mantiki anafahamu kuwa Mungu ndiye hakimu bora wa kilicho bora. Kwa nini ujaribu kuyapindua mapenzi ya Mungu? Ninaomba ili kupata majibu kwa mujibu wa mapenzi yake, na sijaribu “kuamrisha” ili kupata matokeo.
  1.    Onyo
    1.    Soma Marko 12:1-5. Hawa ni wapangani wa namna gani?
      1.    Ungefanya nini kama ungekuwa mmiliki?
    1.    Soma Marko 12:6-9. Je, unakubaliana na hukumu ya mmiliki? Je, hii ni tiba sahihi?
      1.    Mara kwa mara ninakutana na Wakristo wanaoamini kuwa Mungu hatekelezi hukumu dhidi ya wapinzani wake. Fundisho la mfano huu ni lipi? (Mungu anatekeleza hukumu. Na alitekeleza hukumu kwa Yerusalemu baada ya Yesu kusulubiwa.)
    1.    Soma Marko 12:10-11. Jengo linahusikaje na shamba la mizabibu? (Mwana aliyeuawa na kutupwa nje ya shamba la mizabibu, ni jiwe lililokataliwa ambaye sasa ni jiwe kuu la pambeni.)
      1.    Jiwe hili ni nani? (Yesu! Mungu amewezesha ushindi wake.)
    1.    Soma Marko 12:12. Je, huu ni mfano ambao viongozi wa Kiyahudi wanauelewa? (Ndiyo. Unawafanya waogope.)
  1.   Mbingu
    1.    Soma Marko 12:18-23. Masadukayo hawaamini katika ufufuo. Kwa nini waulize swali kama hili? (Kwa dhahiri, wanadhani kuwa ugumu (complexity) ni hoja dhidi ya ukweli.)
    1.    Soma Marko 12:24. Tunapaswa kuujenga ukweli juu ya nini? (Biblia na imani katika uwezo wa Mungu.)
    1.    Soma Marko 12:25-27. Je, Yesu anatangaza kuwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo wapo hai mbinguni? (Suala ni ufufuo. Yesu anajenga hoja juu ya ufufuo kwa kusema kuwa utatokea kwa sababu Mungu ana mpango wa siku zijazo kwa ajili yetu unaohusisha sisi kuishi milele.)
    1.    Rafiki, Mungu ameshinda na hatimaye atawaangamiza wale wanaomkataa. Je, utakuwa upande wa waishio? Kwa nini usiamue kumkiri na kumpokea Yesu sasa hivi?
  1.      Juma lijalo: Siku za Mwisho.