Somo la 6: Kwa Undani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Marko 7 & 8
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
3
Lesson Number: 
6

Somo la 6: Kwa Undani

(Marko 7 & 8)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Wale ambao mara kwa mara wanasoma masomo haya wanafahamu kwamba mara nyingi huwa ninanukuu Kumbukumbu la Torati 4:2 inayotuelekeza kuwa sio sahihi kutengeneza sheria na kudai kuwa Mungu anazitaka jinsi zilivyo kwa kuwaambia watu kuwa hawana haja ya kufuata sheria ambazo Mungu amezitoa. Kwa sehemu fulani somo letu juma hili ni ufafanuzi kamili wa suala hilo. Katika Marko 7 Yesu anaingia kwenye mjadala wa kina juu ya sheria na Mafarisayo, lakini kama tulivyokwishaona hapo awali, hoja za Yesu zinaonekana kutokuwa na mantiki hadi tutakapoingia kwa kina zaidi. Hebu tuanze kuingia kwa kina kwenye neno la Mungu!

  1.    Mikono Safi na Chakula Najisi
    1.    Soma Marko 7:1-4. Unadhani nani ana hadhi ya juu, viongozi wa dini waliounga mkono suala la usafi wakati wa kula, au wavuvi ambao wanakula kwa mikono michafu? (Kura yangu ninaielekeza kwa watu wanaounga mkono usafi wakati wa kula.)
    1.    Soma Marko 7:5-7. Je, Yesu anapingana na usafi? (Hapana. Hii inaturejesha hadi kwenye Kumbukumbu la Torati 4. Kuna mawazo mazuri mengi, kama vile kunawa mikono yako kabla ya kula na kusafisha vyombo vyako vya chakula, glasi, na sahani. Tatizo linaibuka pale unapodai kuwa mawazo yako mazuri yanatakiwa na Mungu.)
    1.    Soma Marko 7:9-12. Kutowaheshimu wazai wako kunahusianaje na kutonawa mikono yako? Hii inanikumbusha juu ya bosi anayemwambia mwajiriwa kuvaa kwa unadhifu, na mwajiriwa asiyejali anajibu, “Huwapendi wazazi wako!” (Kama ningekuwa ninahojiana hili na Yesu ningejaribiwa kusema, “usibadili mada.”)
      1.    Je, kuna yeyote ambaye angependa kutetea jibu la Yesu? Je, mtu yeyote anaweza kuhusisha mjadala juu ya mikono safi na kuwapenda wazazi wako?
      1.    Kama kweli suala ni matumizi ya Kumbukumbu la Torati 4:2, je, inajalisha kama suala linalohusika ni tofauti? (Hapana. Ukiangalia kwa kina kile ambacho Yesu anakijengea hoja kinaleta mantiki kamilifu. Analalamika kwamba viongozi wa dini wamajikita kwenye usafi kuhitajika na Mungu wakati huo huo wakihafifisha kabisa mojawapo ya matakwa halisi ya Mungu – Amri ya Tano kati ya zile Amri Kumi (Kutoka 20:12) – inayosema kuwaheshimu wazazi wako.)
        1.    Ninaweza kuelezea kwa ufupi hoja ya Yesu kwa maneno: “Mnatengeneza sheria bandia za dini, wakati mkizipinga sheria hasili.”
  1.   Asili ya Dhambi
    1.    Angalia tena Marko 7:6. Yesu anamnukuu Isaya ambaye anasema kuwa watu “wanamheshimu” Mungu kwa midomo yao, na si mioyo yao. Viongozi wa dini wanamheshimuje Mungu kwa midomo yao? (Wanaongea juu ya mambo yasiyo ya muhimu, wakati wakipuuzia mambo muhimu.)
    1.    Soma Isaya 6:1-3 na uilinganishe na jibu la Isaya katika Isaya 6:5. Kwa nini Isaya anazungumzia midomo? (Malaika wanamtukuza Mungu kikamilifu, lakini Isaya anajisikia huzuni kwa sababu hamtukuzi Mungu.)
      1.    Ni nini linalopaswa kuwa lengo la kila Mkristo? (Kumtukuza Mungu. Kumheshimu.)
      1.    Kwenye utamaduni wa heshima/fedheha, je, itakuwa jambo la fedheha kuwaacha wazazi wako wateseke wakati unaweza kuwasaidia? (Mtu ambaye kweli anamheshimu Mungu atawaheshimu wazazi wake. Kunawa mikono yako hakumheshimishi Mungu. Kunachofanya ni kuboresha afya yako.)
    1.    Soma Isaya 6:5-7. Je, Isaya ameokolewa kwa neema? (Ndiyo. Anatambua tatizo na Mungu anamsamehe katika maandalizi kwa ajili ya huduma ijayo.)
    1.    Soma Marko 7:14-15. Je, hii inaleta mantiki kwako? Chukulia kwamba mtu ni mlevi wa kutupwa ambaye kamwe hakuna muda ambao anakuwa hajalewa. Je, mtu huyo amenajisika?
      1.    Vipi kuhusu mtu ambaye ni mnene sana kiasi kwamba hawezi kutembea. Je, mtu huyo amenajisika?
      1.    Maoni ya Finis Dake yanasema kuwa Yesu hazungumzii pombe, dawa za kulevya, au tumbaku, badala yake anazungumzia chakula. Je, hiyo inapuuzia jambo la dhahiri ambalo Yesu alilisema? (Ndiyo. Hakuna msingi wowote katika kile alichokisema Yesu kuchora msitari kama huo.)
      1.    Muktadha unaashiria kuwa Yesu anazungumzia jambo gani? (Muktadha unahusu kunawa mikono. Lakini Yesu anazungumza kwa mapana na umadhubuti kabisa.)
    1.    Soma Marko 7:17-23. Nimetumia mifano kadhaa ya uraibu. Baadhi ya watu wanaweza kunikomalia na kujenga hoja, “Bruce, huko ni kudhoofishwa na sio kunajisiwa.” Unadhani Yesu anamaanisha nini anapotumia neno “kunajisiwa?” (Mifano anayoitoa Yesu ya unajisi ama ni sehemu ya kupanga kudhuru au kumdhuru mtu kiuhalisia.)
      1.    Rejea nyuma kwenye mjadala wetu juu ya wajibu wa Mkristo wa kumtukuza Mungu. Kama watu wa Mungu ni kundi la dhahiri linalotenda makosa ya jinai, je hii husababisha kutomheshimu na kumfedhehesha Mungu?
      1.    Rejea nyuma kwenye mjadala wa pombe, dawa za kulevya, na tumbaku. Je, unaweza kuchora msitari wa kutetea maoni ya Yesu? (Yesu anasema kuwa kinachoingia mwilini kinaingia tumboni na kinatolewa. Tunapowazungumzia walevi, waraibu, na wanene kupindukia, matatizo haya hufanya ulaji ambao hufikia kiwango ambacho matokeo yake ni kusababisha matendo yenye madhara. Hiki ndicho kinachoingia mwilini pamoja na matendo ya kipumbavu.)
    1.    Soma tena Marko 7:19. Tofauti kati ya vyakula safi na najisi inapatikana katika kitabu cha Mwanzo 7:2 kwa kuihusisha na gharika. Hapa ni zamani kabla maelekezo ya Walawi 11 hayajatolewa. Hiyo inaashiria nini kwako kuhusu kula chakula najisi?
    1.    Hebu subiri kidogo! Je, huu ni ushauri mzuri au ni amri? Kwani Mungu hakuamuru katika Mambo ya Walawi 11:7-8 tusile, achilia mbali kugusa, mizoga ya nguruwe?
    1.    Soma Marko 2:28. Je, Yesu pia ni Bwana wa uumbaji? (Kama Yesu anaeleza wazi au anabadili amri ya awali, anayo hiyo haki. Yeye ni Bwana. Hitimisho langu ni kwamba kula chakula najisi ni jambo baya. Lazima Mungu alikuwa na sababu madhubuti kwa kufanya utofauti huu kwenye wanyama. Sehemu kubwa ya sheria ya mapokeo ilihusu kuishi kiafya. Ninataka kuishi maisha ya kiafya, na nina uhakika kanuni hizi za muda mrefu zimejengwa juu ya sababu ambazo Mungu alidhani kuwa ni za muhimu kwa wanadamu.)
  1.      Chakula cha Mbwa
    1.    Soma Marko 7:25-27. Je, Yesu anamuita binti wa mwanamke huyu kuwa ni “mbwa?” (Ndiyo.)
    1.    Soma Marko 7:28. Kama Yesu amemuita mtoto wako “mbwa,” na msingi wake ni masuala ya mbari, je, ungejibu kama mama huyu?
      1.    Niambie kile ambacho hasa ungemwambia Yesu?  (Huyu ni binti mdogo ambaye hakufanya chochote ili kuwa na pepo mchafu. Mtu mwenye upendo hatatoa jibu kali, lenye ubaguzi wa kimbari.)
    1.    Soma Marko 7:29-30. Je, jibu la Yesu lisilo la upendo ni kipimo? (Ni kipimo cha mambo matatu. Kwanza, kama mama angesikiliza kwa umakini (tofauti na kukasirika tu), Yesu alirejelea suala la watoto kupewa chakula “kwanza,” hivyo kuacha nafasi wazi kwa binti wake. Pili, mbwa yoyote “chini ya meza” lazima akaribishwe na mmiliki wake. Angeweza kuondoka na tumaini hilo na kuachana na matusi. Mwisho, inahitajika kuwa na moyo kupuuzia matusi.)
      1.    Kwa nini Marko anajumuisha kisa hiki? Je, kinajengwa juu ya ushuhuda kwamba Yesu ni Mungu? (Sehemu ya kukiri kuwa Yesu ni Mungu ni kwamba sisi sio Mungu. Mwanamke huyu alijikita kwenye kile ambacho Yesu angeweza kukitenda kwa binti wake, na si kwenye matusi kwake binafsi.)
  1.   Chakula Chomboni
    1.    Soma Marko 8:14-16. Kama ungekuwa umekaa chomboni ukiyasikiliza haya, ungeona tatizo gani? (Yesu na wanafunzi wanazungumzia mambo mawili tofauti kabisa.)
    1.    Soma Marko 8:17-18. Je, Yesu amewakasirikia wanafunzi? (Ndiyo. Kama ningekuwa mwanafunzi ningeyachukulia maoni haya kuwa matusi kwenye uwezo wangu wa kufikiri.)
    1.    Soma Marko 8:19-21. Jibu swali la Yesu. Wanafunzi walipaswa kuelewa nini? (Hawana haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kuwa na chakula cha kuwatosha. Badala yake wanapaswa kujikita kwenye suala la Yesu kuonya juu ya fundisho baya la kidini.)
    1.    Unadhani kwa nini Marko alijumuisha kisa hiki? (Tulichojifunza kwenye somo hili kina jambo moja la kufanana: zingatia yale ambayo ni yaa muhimu. Zingatia kumtukuza Mungu na si kuzingatia mawazo mazuri, matusi, au mahitaji yako binafsi. Mungu atakutunza ikiwa utayaelekeza maisha yako kwake.)
    1.    Rafiki, je, utaazimia sasa hivi kujikita katika kumtukuza Mungu?
  1.    Juma lijalo: Kuwafundisha Wanafunzi: Sehemu ya 1.