Somo la 5: Miujiza Kando ya Ziwa

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Marko 4-6
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
3
Lesson Number: 
5

Somo la 5: Miujiza Kando ya Ziwa

(Marko 4-6)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kuna miujiza, halafu tena kuna miujiza! Unakumbuka somo letu majuma mawili yaliyopita ambapo Yesu alimponya mtu aliyepooza ili kuthibitisha kwamba anaweza kusamehe dhambi? Miujiza kama hiyo inakaribisha mashtaka ya kwamba inaweza kufanywa kuwa ya bandia. Vipi kuhusu miujiza isiyoweza kufanywa kuwa bandia? Miujiza inayoonesha kuwa misingi ya mambo ya asili iko chini ya udhibiti wa Yesu? Hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa uthibitisho wa Marko kwamba Yesu ni Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Kulala Katika Dhoruba
    1.    Soma Marko 4:35-38. Je, unapenda kulala wakati wa dhoruba? Kuisikiliza mvua inaponyesha ni jambo linalotuliza roho (soothing). Ni kitu gani kilicho tofauti hapa? (Chombo (boti) kinalemewa kwa kujazwa maji na wataalamu wa kushughulika na masuala ya boti wanadhani ya kwamba wanakaribia kufa.)
      1.    Una maoni gani juu ya namna ambavyo wanafunzi wanamwamsha Yesu na kumwomba msaada?  Je, hivi ndivyo ambavyo ungefanya? (Huu ndio mwitikio wa kawaida kabisa wa mwanadamu, wana wasiwasi juu ya maisha yao na wanataka kujua kama Yesu pia anawajali.)
      1.    Kama Yesu ni Masihi, je, jambo la kwanza ambalo walipaswa kulijali lisingekuwa juu ya usalama wake? Ustawi wake?
      1.    Unadhani wanafunzi walikuwa wanawazia nini? Je, ingetosha tu kama Yesu angesema, “Ndiyo, ninawajali. Pigeni makasia kwa nguvu! Toeni maji haraka!”
    1.    Soma Marko 4:39-41. Hii inaashiria kuwa wanafunzi walikuwa wanawazia nini? (Hawakuwazia suluhisho la Yesu. Walikuwa tu na hofu na wakamuita Yesu awasaidie.)
      1.    Je, Yesu alitaka wanafunzi wawe na mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji?
      1.    Hebu litafakari hili kidogo. Wanafunzi walikuwa wataalamu wa masuala ya boti. Walikuwa wameshapitia uzoefu wa kukabiliana na dhoruba nyingi hapo kabla. Hii inatufundisha nini pale tunapokabiliana na matatizo makubwa maishani? (Kuna matatizo ambayo hatuwezi kuyatatua wenyewe. Tunatakiwa kuwa watulivu na kumtumaini Mungu.)
      1.    Inaonekana kwamba kumwomba Yesu msaada lilikuwa jambo la mwisho kabisa walilolifanya. Je, kumwomba Yesu msaada inapaswa kuwa jambo letu la kwanza kwa kila tatizo? Hata kama sisi ni wataalamu wa suala linalohusika?
    1.    Angalia tena Marko 4:41. Unadhani Marko anataka tujifunze nini kutoka kwenye kisa hiki? (Yesu ni Mungu. Nani anayeweza kutoa wito kwa upepo na bahari, nguvu za msingi za asili, ziweze kutii?)
  1.   Mtu Mwenye Wazimu
    1.    Soma Marko 5:1-4 na Marko 5:6. Taswira niliyonayo ni kwamba mtu huyu mwenye wazimu anakimbia kumwelekea Yesu na wanafunzi mara baada ya kutia nanga baada ya kupona kutoka kwenye dhoruba. Je, wanafunzi wanapaswa kutuma maombi kwa ajili ya kazi nyingine?
      1.    Unadhani wanafunzi wako wapi? (Wanakimbia kuelekea uelekeo tofauti.)
    1.    Soma Marko 5:7-8. Pepo hawa wachafu wanasihi kupatiwa ulinzi kwa jina la nani? (Mungu! Tunaweza kuwa na kisingizio gani cha kujaribu kutatua matatizo kwa uwezo wetu wenyewe?)
    1.    Soma Marko 5:9-13. Hebu niambie, tukio hili linatufundisha nini kuhusu uchaguzi wetu kati ya wema na uovu? Uovu unatuwazia nini?
    1.    Ruka vifungu kadhaa chini na usome Marko 5:18-20. Tumeona mara kadhaa Yesu akiwaambia wanufaika wa miujiza yake wakae kimya juu ya miujiza hiyo. Kwa nini Yesu anatoa maelekezo tofauti hapa?
  1.      Imani Hungoja
    1.    Soma Marko 5:21-23. Unaposoma ombi la Yairo, baba, hali yake ni ya dharura kiasi gani? (Ni suala la uhai na kifo. Binti wake “yu katika kufa.”)
    1.    Soma Marko 5:24. Je, Yesu amekubali kutoa msaada?
    1.    Soma Marko 5:25-26. Unaweza kuelezeaje tatizo la kiafya la mwanamke huyu? (Lilikuwa tatizo sugu, sio suala la dharura.)
    1.    Soma Marko 5:27-30. Unajisikiaje unapokuwa na haraka na kujikuta kwenye msongamano wa magari barabarani? Je, mwanamke huyu anasababisha ucheleweshaji usio wa lazima kwenye suala la dharura?
    1.    Angalia tena Marko 5:30. Kwa nini Marko anatuambia kuwa nguvu zimemtoka Yesu? (Huu ni uthibitisho zaidi kwamba Yesu ni Mungu.)
    1.    Soma Marko 5:34-35. Ungekuwa na mawazo gani kama ungekuwa Yairo?
      1.    Hiki ni kisa kizuri chenye mguso kuhusu mwanamke, lakini je, kinathibitisha kuwa Yesu hana vipaumbele?
      1.    Juma hili Rais wa zamani, Trump, alijeruhiwa na mtu mwingine akauawa kwenye mkutano wa kisiasa. Wafuasi wa Trump wanasema Mungu aliyaokoa maisha ya Trump na wapinzani wake wanajenga hoja kwamba Mungu hawezi kuokoa maisha ya mtu mmoja na kuruhusu mtu mwingine afariki. Je, hili ndilo swali lililomo mawazoni mwa Yairo – kwa nini mtu mmoja anaishi na mwingine anakufa?
        1.    Je, swali hili linaleta changamoto zaidi kwa sababu mwanamke huyu hakuwa kwenye mazingira hatarishi ya kufa?
    1.    Soma Marko 5:36-37. Sasa Yesu anaudhibiti mkutano. Kwa nini hakufanya hivyo hapo kabla?
    1.    Soma Marko 5:40-42. Je, kuchelewa kwa Yesu na udhahiri wa Yesu kutokuwa na vipaumbele kunaleta tofauti yoyote kwa Yairo na mkewe wakati huu? (Hii inajibu maswali yote ya msingi. Kwa dhahiri ucheleweshaji si tatizo.)
      1.    Tumia fundisho la kisa hiki katika kila mazingira ambapo mtu mmoja anaishi na mwingine anafariki. Kuna fundisho gani? (Imani hungoja. Yesu atawaponya wote wanaomchagua. Muda wa uponyaji utatofautiana, lakini tutakapokuwa mbinguni na wote wakiwa wameponywa, ucheleweshaji hautakuwa na maana tena.)
  1.   Imani Hula
    1.    Soma Marko 6:30-32. Yesu ana wasiwasi kwamba wanafunzi wake hawapati mapumziko ya kutosha. Je, hicho ndicho unachokijali maishani mwako? Au haufanyi kazi kwa bidi kiasi cha kutosha?
    1.    Soma Marko 6:32-34. Je, ungekuwa na mtazamo kama wa Yesu? Au ungesikitika kwamba walikuwa wanaingilia mapumziko yako?
    1.    Soma Marko 6:35-37. Je, hii ni haki? Muda mfupi tu uliopita Yesu alikuwa amekubaliana na ukweli kwamba wanafunzi walihitaji pumziko, na sasa anawapa kazi kubwa ya kuwalisha watu ambao kwa makusudi waliingilia mapumziko yao!
      1.    Ungekuwa na mtazamo gani juu ya hili kama ungekuwa mwanafunzi? (Ningedhani kuwa hili ni tatizo lililosababishwa na kundi la watu na wanaweza kutatua tatizo lao wao wenyewe.)
      1.    Una maoni gani juu ya mtazamo wa wanafunzi?  (Kwa nini wanamwambia Yesu nini cha kufanya? Kama walipata fundisho la kutumaini, wangesema, “Ungependa tufanye nini?”)
    1.    Soma Marko 6:38 na Yohana 6:8-9. Kwenye kundi lote hili la watu kuna chakula cha kumtosha mtu mmoja pekee! Je, hawa ni watu wasiowajibika kabisa? Je, hawastahili kushinda njaa?
    1.    Soma Marko 6:39-42. Maoni ya Finis Dake yanasema kuwa Yesu aliizidisha mikate ili ifikie takribani mikate elfu ishirini! Hii inaashiria kuwa Yesu alitaka wanafunzi wake wafanye nini alipowaambia katika Marko 6:37 kuwapa watu chakula?
      1.    Utakumbuka kwamba wanafunzi walimwambia Yesu kuwa itawagharimu fedha nyingi. Unapokabiliwa na wahitaji, je, huwa unarudi nyuma kwa sababu una wasiwasi juu ya gharama?
      1.    Kama ilivyokuwa kwenye kuituliza dhoruba, huu ni muujiza ambao usingeweza kufanywa kuwa bandia. Kwa nini Yesu aliamua kutenda muujiza mkubwa wakati ambapo watu wangeweza kufurahia baraka za kiroho za kufunga? (Hatutakiwi kusahau kwamba Yesu yuko radhi kutenda muujiza hata kwenye vitu vidogo. Ndiyo, unaweza kuomba (kusali) kwa ajili ya msaada ili kupata ufunguo wa gari lako!)
    1.    Soma Marko 6:43-44. Kwa nini Yesu atengeneze chakula kingi kupita kiasi?
      1.    Je, mitazamo yako ni ile ya kwamba Yesu anaweza kutenda mambo madogo sana?
      1.    Tafakari nyuma kwenye Yohana 6:8-9. Je, unaweza kuwa kama yule mvulana? Kama uko tayari kushiriki na wengine, je, mchango wako mdogo unaweza kuishia kuwa baraka kubwa mikononi mwa Mungu?
    1.    Rafiki, tumeruka visa kadhaa katika Marko 4-6. Visa tulivyojifunza vinatufundisha nini? Vinatufundisha kumtumaini Mungu. Kumtumaini Mungu pale tunapodhani kuwa tunaweza kufa, kumtumaini Mungu pale anapoonekana kutenda mambo bila kutumia mantiki, na kumtumaini Mungu katika kusaidia hata kwenye mambo madogo maishani. Je, utafanya uamuzi, sasa hivi, wa kumtumaini Yesu?
  1.    Juma lijalo: Kwa Undani.