Somo la 4: Mifano

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Marko 4
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
3
Lesson Number: 
4

Somo la 4: Mifano

(Marko 4)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unafurahia kuijua siri? Inakufanya uwe wa pekee, si ndio? Unakuwa mtu wa ndani (insider). Katika somo letu juma hili Yesu anawaambia wanafunzi wake kwamba “wameijua siri ya ufalme wa Mungu.” Marko 4:11. Je, haionekani kuwa ajabu kwamba injili inapaswa kuwa siri? Je, hii sio ajabu kama Yesu kumwambia mwenye ukoma kukaa kimya kuhusu uponyaji wake na pepo wachafu kuacha kudhihirisha kwamba Yesu ni Mungu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Marko ili tuone siri ya kwa nini Yesu anauelezea ujumbe wake kama siri!

I.  Mpanzi

A.  Soma Marko 4:1-2. Unadhani inamaanisha nini kufundisha kwa “mifano?” (Mfano ni kisa. Jaribu kukumbuka hubiri ulilowahi kulisikia siku za nyuma. Uwezekano mkubwa ni kwamba unachokikumbuka ni kisa kilichofafanua suala la maadili.)

1.  Unaona fundisho gani kwenye njia anayoitumia Yesu? (Mahubiri na mafundisho yetu yanapaswa kutegemezwa na visa. Kijana mmoja aliyekuwa akitembea pamoja nami afanya uamuzi wa kuniambia kuhusu kumbukumbu yake ya mahubiri. Kwa mshangao, alirejelea mahubiri ya hadi miaka kumi iliyopita. Alikumbuka visa.)

B.  Soma Marko 4:3. Kwa nini Yesu anaelezea kisa cha mpanzi? Kama ulitaka watu wakumbuke, kwa nini usielezee kuhusu mwovu mwenye uthubutu na uzoefu wake wa kuponea kifo chupu chupu? (Je, umewahi kusikia kuhusu Memory Palace? (Hii ni njia ya kukumbuka viwango vikubwa vya taarifa. Hivi ndivyo inavyofanya kazi. Fikiria jinsi unavyoingia nyumbani kwako na kisha kuingia kwenye vyumba vilivyopo nyumbani kwako. Unaweka kitu unachotaka kukikumbuka kila kona ya mahali utakapopita ndani ya nyumba yako. Mahali unapopafahamu nyumbani kwako panagundisha taarifa akilini mwako.)

C.  Soma Marko 4:4-7. Sehemu hii ya mfano inakufundisha nini?

D.  Soma Marko 4:8. Sehemu hii ya mfano inakufundisha nini?

E.  Soma Marko 4:9. Je, una masikio? “Umesikia” nini?

1.  Kisa hiki kinahusu nini? Je, kinahusu mbinu za kilimo? (Soma Marko 4:14. Yesu anatuambia kuwa anazungumzia “neno.” Maneno ya Mungu.)

2.  Ikiwa ulichokisikia ni, “usipande mbegu njiani, mwambani, au kwenye udongo wenye miiba,” na “upande mbegu kwenye udongo mzuri,” utalielewaje neno hili kama linavyotumika kwenye upelekaji wako wa injili? (Sina maoni yoyote. Watu gani ni njia, miamba, miiba au uchafu mzuri? Na unawezaje kujua bila uzoefu kwanza?)

3.  Ikiwa fundisho sio aina ya udongo, bali kitu kingine, ni kitu gani hicho? (Fundisho linahusu upandaji. Tunapaswa kupanda mbegu nyingi kadiri inavyowezekana na kwa upana mkubwa kadiri inavyowezekana.)

4.  Matumaini ya kila mwanasheria anayejali maslahi ya umma ni kupeleka kesi katika Mahakama Kuu ili kubadili sheria. Kwa takriban miaka 50 nimekuwa nikienda mahakamani kwa niaba ya the National Right to Work Legal Defense Foundation. Shirika hili limesaidia zaidi ya waajiriwa 20,000 kwenye kesi zaidi ya 2,500. Kati ya kesi zote hizi, tuliweza kufanikisha kesi 18 kuamuliwa kwa kupewa ushindi na Mahakama Kuu ya Marekani, na nyingine nyingi ziliamuliwa na Mahakama bila kwenda kwenye kesi ya msingi. Je, unakubaliana kwamba hii inaendana na mfano wa mpanzi?

II.  Kanuni za Mfano

A.  Soma Marko 4:10-12. Unaielezeaje kauli ya Yesu kwamba mifano inawasaidia watu kukanganyikiwa, kiasi kwamba hawabadiliki kuiacha dhambi na kusamehewa? Je, hiyo si kinyume na kila kitu tulichokisoma kuhusu Yesu katika Agano Jipya? Je, Petro hakusikia vizuri au Marko alikosea kuliandika?

B.  Soma Isaya 6:9-10. Je, Yesu anafafanua vifungu hivi katika kitabu cha Isaya? (Naam. Utaona kwamba kifungu katika kitabu cha Marko kina alama za kudondoa (“  ”).)

1.  Kwa hiyo Mungu alimaanisha nini alipoyasema haya kwa Isaya? (Huu ni unabii kuhusu jinsi ambavyo watu watapokea ujumbe wa Mungu utakaotolewa kupitia kwa Isaya.)

C.  Soma Isaya 6:11-12. Nini kitawatokea watu? (Wataangamizwa.)

1.  Je, mpanzi yupo kwenye kazi ya upumbavu?

2.  Je, Yesu anamnukuu Isaya ili kuwaonya watu? (Unapolitafakari hili, Yerusalemu iliangamizwa si muda mrefu sana baada ya Yesu kuwapelekea ujumbe wake.)

D.  Soma Marko 4:13. Hii inadhihirisha nini kuhusu endapo Yesu anawataka wafuasi wake waelewe mifano? (Kinachomaanishwa kwa dhahiri ni kwamba anawataka waelewe.)

E.  Soma Marko 4:14-20. Yesu anafundisha nini kwa mfano huu? (Anafafanua kwa nini watu wengi wanaukataa ujumbe wa injili.)

1.  Utaona kwamba ufafanuzi unatolewa kwa wanafunzi. Kwa nini kwa wanafunzi pekee? (Ufafanuzi unaonekana kuwa mrahisi sana.  Tofauti kati ya wale wasioweza kuelewa na wale wanaoelewa ni kwamba wale wanaoelewa wako radhi kujifunza na kutenga muda wa kuutafakari ujumbe.)

2.  Unaweza kufikiria sababu nyingine ya kwa nini Yesu alifundisha kwa kutumia mifano? (Maadui wake wasingeelewa kwa sababu walimchukia na hawakutaka kuelewa. Kama maadui wake wangeelewa vizuri, wangejiandaa vizuri kumpinga.)

F.  Hebu turuke vifungu kadhaa. Soma Marko 4:24-25. Yesu anamaanisha nini hapa? (Sasa Yesu kwa dhahiri anasema, “Angalieni msikialo” ikiwa mnataka kuelewa. Mkianza kuelewa, uelewa wenu utaendelea kukua. Mkiacha uzingativu, mtakuwa wajinga zaidi kuhusiana na injili.)

G.  Utaelezeaje kwa ufupi kile tulichojifunza hadi kufikia hapa katika Marko 4? (Fungua moyo wako! Kuwa mzingativu! Kuwa makini. Tafakari anachokisema Yesu na utakua katika uelewa wako.)

III.  Taa

A.  Soma Marko 4:21. Kauli hii haikinzani na njia ya mfano? Watu fulani pekee ndio wanaoweza kuona? (Mojawapo ya mahitimisho unayoweza kuyafikia kutoka kwenye kisa cha mpanzi ni kuepuka kupanda mbegu katika maeneo fulani. Hii inasema kuwa, ikiendana na njia ya mpanzi, acha nuru iende kila mahali.)

B.  Soma Marko 4:22. Je, Yesu anatuambia kuwa sababu ya kuficha jambo fulani, sababu ya kufanya jambo fulani liwe siri, ni kulifanya lijulikane? Unaweza kulielezea hilo? (Je, una hamu ya kuijua siri?)

IV.  Furaha ya Mkulima

A.  Soma Marko 4:26-28. Habari njema kwa mpanzi ni ipi? (Kazi yake ni kupanda mbegu tu, inakua yenyewe. Mkulima hana haja ya kuelewa jinsi mbegu inavyokua kwa jambo hili kutekelezeka.)

1.  Je, hii inapaswa kuwa mwongozo wa kazi yetu ya kiinjilisti?

2.  Ninakumbuka mikutano ya injili ambapo watu kadhaa walibatizwa na mwaka mmoja baadaye mtu mmoja au wawili pekee ndio bado walikuwa wakienda kanisani. Tulipojikosoa tuligundua kwamba hatukuwa na ufuatiliaji wa kutosha. Je, ufuatiliaji hauna maana? (Kama ninapanda kitu, ninafanya ufuatiliaji kwa kushughulika na magugu.)

B.  Hebu turukie mbele na tusome Marko 6:10-11. Je, hili linafanana na ujumbe wa mpanzi – wajibu wetu ni kupeleka injili, na si kung’ang’ana kujaribu kuwaongoa wengine? (Tofauti moja ni kwamba watu hawa walikataa kusikiliza tangu mwanzo kabisa.)

C.  Soma Marko 4:29. Huyu “mtu (he)” hapa ni nani? Mpanzi au Mungu? (Mpanzi ndiye anayevuna mazao, lakini ninadhani hii inamrejelea Mungu. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa mtu binafsi ili kuleta mguso kamili, ukuaji kamili wa mbegu ya injili.)

D.  Soma Marko 4:30-32. Unapaswa kutazamaje juhudi zako binafsi ili kusambaza injili? (Usidharau mianzo midogo! Mungu anaweza kuchukua mbegu yako ndogo na kuifanya kuwa mti mkubwa.)

1.  Siwezi kujizuia bali kulitafakari somo hili. Nilipokuwa kijana mdogo nilifundisha darasa dogo la Shule ya Sabato. Kompyuta zilipoingia, niliandika somo langu kwenye kompyuta. Kompyuta zilipokuwa ndogo, nilifundisha darasa langu kwa kuangalia kwenye kioo. Intaneti ilipoingia, mimi na kijana wangu tuliweka somo mtandaoni. Leo makumi kwa maelfu wana masomo haya. Somo lilikuwa wakati nikiwa nimelala!)

E.  Soma Marko 4:33-34. Yesu hayuko hapa kutufafanulia kila kitu. Je, hatuna matumaini? 

F.  Soma Yohana 14:26. Siri zinafunuliwaje kwetu leo? (Bado Mungu anatufafanulia siri hizo. Katika zama zetu, Roho Mtakatifu ndiye ambaye “anatufafanulia kila kitu.” Bwana sifiwe!)

G.  Rafiki, Mungu atakufunulia kweli zake kwa njia ya Roho Mtakatifu! Je, utajitahidi kuwa mmojawapo wa “wandani” wanaozijua siri za ufalme wa Mungu? Kwa nini usifanye uamuzi huo sasa hivi?

V.  Juma lijalo: Miujiza Kando ya Ziwa.