Somo la 4: Kuusimamia Ukweli

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Matendo 5, 2 Timotheo 2, Ufunuo 3
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
4

Somo la 4: Kuusimamia Ukweli

(Matendo 5, 2 Timotheo 2, Ufunuo 3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unaogopa kukiri imani yako ya Kikristo kazini au hadharani? Kwa uelewa wangu, hakuna mtu nchini Marekani aliyeuawa hivi karibuni kwa kuwa Mkristo. Kwa ujumla, hali za kutisha kama hizo zipo nje ya Marekani ya Kaskazini. Kwa kuwa ninafundisha Sheria ya Kazi (Labor Law), ninafahamu kwamba “industrial capital punishment” inarejelea kitendo cha kufukuzwa kazini. Je, watu nchini Marekani wanafukuzwa kazi kwa sababu ya imani yao ya Kikristo? Naam, ni kweli! Kwa sasa kuna kesi inayoendelea ambapo Mkristo alifukuzwa kazi kwa sababu aliandika kuwa ilikuwa “chukizo” kwa kikundi shawishi cha mabasha/wasenge (homosexual lobby) kuteka alama ya upinde wa mvua, ishara ya Mungu kwamba kamwe hataiangamiza tena dunia kwa maji. Mwajiriwa huyu hakutambua kuwa kauli yake itaonwa na waajiriwa wengine. Mazingira kama hayo yanawafanya Wakristo nchini kwangu kuwa na wasiwasi juu ya kuusimamia ukweli. Biblia inasema nini kuhusu kuusimamia ukweli na jinsi tunavyopaswa kuendana nao? Hebu tuzame kwenye somo letu na tujifunze zaidi!

I.  Hotuba Iliyoidhinishwa

A.  Soma Matendo 5:16-18. Kitu gani kilihamasisha kukamatwa kwa wanafunzi? (Viongozi wa dini waliuonea wivu uwezo wa Roho Mtakatifu wa uponyaji. Walikuwa wanapoteza ushawishi wao kwa watu.)

B.  Soma Matendo 5:19-20. Nani ambaye kwa mahsusi amewaelekeza wanafunzi kufundisha juu ya habari za Yesu hekaluni? (Malaika aliyewaokoa kutoka gerezani.)

1.  Hii inaibua suala la kwanza kuhusu kuwainjilisha wengine katika eneo la kazi. Je, tunaombwa na Mungu kusambaza injili katika eneo la kazi?

a.  Kwa nini upo katika miliki ya mwajiri wako? (Uko hapo kwa ajili ya kufanya kazi. Kama usingekuwa hapo kwa ajili ya kufanya kazi ungekuwa mpita njia.)

b.  Je, ni kitendo cha uaminifu kutumia muda unaolipwa kwa ajili ya kufanya kazi na kuutumia katika shughuli za uinjilishaji? (Nadhani tunapaswa kusambaza injili kwa kutumia muda wetu binafsi. Hii tafsiri yake ni kwamba hulipwi kwa kusambaza injili.)

2.  Sheria inayohusu uhuru wa maoni wa mwajiriwa kwa ujumla ilitokana na suala la waajiriwa kutumia muda wa kazi kushawishi masuala ya vyama vya wafanyakazi. Je, unafahamu sheria zipi kuhusiana na uhuru wa maoni zilitokana na muda wa kazi kati ya mwajiriwa na mwajiri? (Waajiriwa wanaweza kuwashirikisha waajiriwa wenzao mawazo yao kihalali nyakati za mapumziko.)

C.  Soma Mathayo 10:5-7. Nani amewaidhinishia wanafunzi kushiriki na wengine habari njema za Yesu? (Yesu mwenyewe!)

D.  Soma Mathayo 10:14. Yesu anawashirikisha wanafunzi wake kanuni gani muhimu? (Msimbughudhi mtu yeyote kwa injili. Wasipowasikiliza, acheni suala hilo mikononi mwa Mungu.)

1.  Unadhani kanuni hii inatumika katika eneo la kazi? (Binafsi ninaamini hivyo. Kesi nyingi za uhuru wa dini zinazohusisha kusambaza injili katika eneo la kazi zinaibuka kutokana na madai kwamba waajiriwa wengine “wanabughudhiwa.” Kwa kuizingatia kanuni ya Yesu inapaswa kukuepusha dhidi ya mashtaka ya bughudha.)

E.  Hebu turejee kwenye kisa chetu katika Matendo 5. Soma Matendo 5:25-28. Je, kufundisha habari za Yesu hekaluni ni sawa na kufundisha habari za Yesu kazini?

F.  Soma Matendo 5:29. Je, hili ni jibu sahihi kwa ajili ya kusambaza injili kazini? (Jibu langu ni, “Hapana.” Wanafuzi hawakuwa wameajiriwa na viongozi wa dini. Wanafunzi walikuwa wanatumia muda wao wenyewe na walikuwa katika mazingira ya hadhara ya kidini. Kwa umahsusi walikuwa wameamriwa na malaika kuwashirikisha wengine habari za Yesu katika eneo lile mahsusi.)

G.  Soma Matendo 5:40-42. Je, utakuwa salama dhidi ya adhabu kama utasambaza injili?

1.  Wanafunzi waliichukuliaje adhabu hii?

II.  Hekima Katika Ushirikishaji

A.  Kwenye visa viwili tulivyovijadili hivi punde, wanafunzi walipewa maelekezo maalumu ya ushirikishaji. Mjadala wetu juu ya ukomo wa kusambaza injili kazini unaibua swali juu ya akili ya kawaida (common sense). Hebu tuendelee na mada hiyo kwa kusoma 2 Timotheo 2:1-3. Timotheo anaambiwa kufanya nini? (Anapewa maelekezo ya kuwafundisha walimu wa injili.)

1.  Je, mara zote ushirikishaji ni jambo rahisi? (Kwa mara nyingine tunaambiwa kuwa ushirikishaji unaweza kuleta mateso/taabu.)

B.  Soma 2 Timotheo 2:4-7. Paulo anabainisha mambo matatu mahsusi kwa Timotheo kuhusu kufundisha na kisha anamtaka Timotheo afanye nini? (Kuyatafakari mambo hayo. Hebu nasi tuyatafakari!)

C.  Soma tena 2 Timotheo 2:4. Utatumiaje ushauri huu katika kusambaza injili? (Usitoke nje ya mada. Kama unasambaza injili, hakikisha unasalia kwenye masuala ya dini na usijiingize kwenye ubishani mwingine.)

D.  Unaweza kuwa unatafakari, “Bruce, unapaswa kuusikiliza ushauri huu wa Kibiblia. Masomo yako yanatangatanga na kupotelea kwenye siasa. Kwa mfano, unarejelea bendera ya upinde wa mvua katika sehemu ya utangulizi.” Ingawa hii ni tahadhari nzuri kwangu, jiulize kama mjadala juu ya Biblia usiojikita kutumia ukweli kwenye masuala yanayoendelea sasa hivi yana umuhimu wowote kivitendo?

1.  Soma tena 2 Timotheo 2:5. Kanuni zipi zinatumika kwenye ushuhudiaji wa Kikristo tofauti na kanuni za shindano la riadha? (Kanuni zinazonijia mawazoni ni mafundisho ya Biblia. Hakikisha kwamba uinjilisti wako umejengwa juu ya Biblia.)

E.  Soma 1 Petro 3:15-16. Kanuni gani nyingine kuhusiana na ushirikishaji zinakujia akilini? (Kanuni ya pili ni jambo ambalo wanasheria wanaliita “weledi” (professionalism). Kuwa na heshima, mwema, na mwangalifu kuhusu ambavyo unasambaza injili.)

1.  Sababu halisi ya hili ni ipi? (Usipotendewa kwa weledi, hii itauaibisha upande wa pili.)

F.  Soma tena 2 Timotheo 2:6. Hapa tunaona kanuni gani ya ushuhuda wa Kikristo? (Usiwe mvivu! Jitahidi kuwa bora.)

G.  Soma 2 Timotheo 2:8. Unaona jambo gani muhimu kuhusiana na usambazaji wa injili kwenye kifungu hiki? (Hatutakiwi kupoteza uelekeo wa hoja ya kuvutia sana – Yesu alikufa kwa niaba yetu na amefufuka kutoka kaburini!)

H.  Soma Zaburi 19:7. Je, una wasiwasi kwamba hauna werevu wa kutosha kufanya kazi nzuri ya kusambaza injili? (Hii inatuambia kuwa kung’ang’ania kwenye mafundisho ya Biblia kutatufanya tuonekane wenye busara, hata kama sisi ni wa kawaida. Kila mtu anaweza kupeleka injili.)

III.  Kupita Kutoka Mautini Kuingia Uzimani

A.  Soma Yohana 5:24. Nini kinamtokea mtu anayeuamini ujumbe wako wa injili? (Wanatoka mautini na kuingia uzimani.)

1.  Hilo linatokea lini? Je, kifungu kinarejelea siku zijazo? (Ukisoma vifungu vifuatavyo (Yohana 5:25-29) vinarejelea tukio linalokuja (future event). Lakini sidhani kama hilo ni kweli kwa kifungu cha 24. Mara unapompokea Yesu kama Mwokozi wako unatoka sasa hivi kutoka mautini na kuingia uzimani.)

2.  Unaielewaje kauli ya kwamba wale wanaotoka mautini na kuingia uzimani “hawaingii hukumuni?” (Soma Warumi 8:1. Kifungu hiki kinasema wale walio katika Yesu hawaingii “hukumuni.”)

B.  Soma Ufunuo 20:11-15. Vitabu vingapi vya hukumu vinafunuliwa? (Biblia haisemi.)

1.  Vitabu vingapi vya uzima vinarejelewa? (Kitabu kimoja tu.)

2.  Unadhani kwa nini kuna kitabu kimoja tu cha uzima na idadi isiyotajwa ya vitabu vya hukumu? (Ufunuo 20:15 inarejelea majina kuandikwa kwenye kitabu cha uzima. Kwa mujibu wa Ufunuo 20:12, vitabu vinavyohusiana na hukumu vinaandika kumbukumbu ya matendo. “Sawasawa na matendo yao,” kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya hukumu, ndio msingi wa hukumu juu ya maisha yao. Kuandika kumbukumbu ya matendo huchukua nafasi kubwa kuliko kuandika kumbukumbu ya majina.)

3.  Ni nini hukumu kwa wale ambao matendo yao ndio msingi wa hukumu yao? (Kifo. Kwa mujibu wa Ufunuo 20:15 wanatupwa katika ziwa la moto.)

C.  Angalia tena Yohana 5:24. Je, dhana ya kwamba hutahukumiwa linaleta mantiki zaidi kwako unapojifunza juu ya kitabu cha uzima?

D.  Hebu tuangalie kwenye kipengele kingine cha kitabu cha uzima. Soma Ufunuo 17:8. Ni lini jina lako linaandikwa kwenye kitabu cha uzima? (“Tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.”)

1.  Je, kila mtu anaokolewa? Au Mungu tayari ameshaamua (predestined) watu fulani kuokolewa? (Yohana 5:24 inaashiria kwamba si wote watakaookolewa. Pia inatuambia kuwa wokovu ni suala la mtu binafsi. Hiyo inazuia uamuzi unaofanyika kabla.)

2.  Unaelewaje suala la jina lako kuandikwa kwenye kitabu cha uzima kabla hujazaliwa, na kauli ya Yohana 5:24 kuhusu kupita kutoka mautini kuingia uzimani? (Mungu anatupatia sote uwezekano wa wokovu. Uwezekano huo unategemeana na uchaguzi wetu wa uzima wa milele.)

E.  Soma Ufunuo 3:5. Je, jina letu linaweza kufutwa kutoka kwenye kitabu cha uzima? (Ndiyo.)

1.  Katika mazingira gani jina lako litafutwa? (Kushindwa kwako kuvaa vazi jeupe. Angalia Mathayo 22:1-14. Tunapofanya uamuzi uliorejelewa katika Yohana 5:24 tunapokea vazi la harusi. Tunapita kutoka mautini kuingia uzimani kwa sababu hilo vazi jeupe la haki linamaanisha kuwa kamwe Yesu hatafuta jina letu kutoka kwenye kitabu cha uzima.)

F.  Rafiki, tulianza kwa kuzungumzia juu ya hatari ya kusambaza injili. Kisha tukaingia kwenye kanuni za ushirikishaji, na tukaishia na baraka ibadilishayo maisha itokanayo na kuisikia injili. Je, utawashirikisha wengine kwa hekima?

IV.  Juma lijalo: Imani Pale Ionekanapo Kutowezekana.