Somo la 2: Suala Kuu: Upendo au Ubinafsi?

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Luka 19, Matendo 2-5, Waebrania 11
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Suala Kuu: Upendo au Ubinafsi?

(Luka 19, Matendo 2-5, Waebrania 11)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Katika wikiendi ya Pasaka nilianza kuandika somo hili. Upendo usiopimika kiasi gani ambao Mungu ametuonesha! Unakumbuka juma lililopita tulijifunza kuhusu vita mbinguni na pambano kati ya Mungu na Shetani juu ya utii wa Adamu na Eva? Shetani alikuwa na mwenendo gani wakati huo dhidi ya Mungu? Tulijadili kwamba Shetani alikuwa anaendelea vizuri sana. Alishawishi theluthi ya malaika na wanadamu wote wawili kumfuata. Kama ungekuwa Mungu, ungefanya nini? Je, ungetumia nguvu kwenye tatizo hili kwa kumwangamiza Shetani na wafuasi wake? Au, ungejitoa wewe mwenyewe? Cha kushangaza akilini mwa mwanadamu ni kwamba Mungu aliamua kujitoa yeye mwenyewe. Hivyo, Mungu alitumia nguzo ya upendo kama silaha yake. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Akalia

A.  Soma Luka 19:36-38. Yesu anaingia Yerusalemu kwa ushindi. Watu wanamaanisha nini kwa kumwita Yesu “Mfalme ajaye kwa jina la Bwana?” (Wanamuita Yesu Masihi. Watu wa Yerusalemu wanamuita Masihi na Mfalme mtarajiwa.)

B.  Soma Luka 19:39-40. Yesu anamaanisha nini anaposema kuwa mawe yatapiga kelele? Nini kitasababisha hilo litokee? (Yesu anasema kuwa sifa zitatoka kwenye vyanzo vya kimiujiza (supernatural). Yesu anathibitisha kuwa yeye ni Masihi.)

C.  Soma Luka 19:41-42. Yesu anakurejelea “wewe” ambaye ulipaswa kujua nini kinaleta amani. Huyo wewe ni nani? (Raia wa mji.)

1.  Yesu anazungumzia “amani” gani? Amani na Warumi?

D.  Soma Luka 19:43-44. Yesu anapozungumzia kuhusu “kutembelea,” je, anarejelea Warumi kuishambulia Yerusalemu? Wayahudi hawakujua lini hilo litatokea. (Hapana. Yesu anasema hawakumfahamu na kutambua kuwa alikuwa Masihi! Mawe yalimtambua, lakini watu wa Mungu hawakumtambua. Hili halihusiani na Warumi.)

E.  Hebu turejee kwenye Luka 19:38. Angalia rejea ya “amani mbinguni.” Yesu analetaje amani mbinguni? (Fikiria juu ya mjadala wetu wa juma lililopita. Kitendo cha Yesu kujitoa yeye mwenyewe sio tu kwamba kilishinda pambano duniani, bali pia kilitatua suala lililokuwa mawazoni mwa wale wote waliopo ulimwenguni.)

F.  Hebu turejee kwenye Luka 19:41. Kama mtu akikukataa, je, utalia kutokana na kitendo hicho au kitendo hicho kitakukasirisha? (Yesu anaonesha upendo wake kwa kulia juu ya upotevu unaokuja wa watu wake.)

G.  Angalia tena Luka 19:43-44. Nani anayefanya uangamivu? (“Maadui.” Shetani yuko nyuma ya shambulio hili kwa Wayahudi.)

1.  Hilo linatendekaje? Yesu ana upendo kwa watu wake, lakini Shetani anawaangamiza – hadi watoto. Kwa nini? (Watu walimkataa Yesu na hivyo waliukataa ulinzi wake.)

H.  Soma Mathayo 24:15-20. Yesu anataka kumwokoa nani? (Wakristo wanaomsikiliza. Wale wanaoamini. Eusebius na Epiphanius, waliokuwa mapadre wa Kanisa katika karne ya nne, wanataarifu kuwa Wakristo wa Yerusalemu waliona fursa ya kuondoka baada ya kuanza kwa uvamizi wa Rumi. Kufuatia maelekezo ya Yesu waliondoka na kuuacha mji na wote waliokolewa.)

I.  Soma Matendo 1:6. Wanafunzi wa Yesu walimuuliza swali hili alipokuwa kwenye mchakato wa kupaa mbinguni. Walikuwa na maoni gani kuhusu mustakabali wa Yerusalemu? (Kwa dhahiri hawakuuelewa mustakabali wa Yerusalemu.)

J.  Hebu tuzungumzie vifungu tulivyovijadili ili tupate taswira ya kina. Ni nini mkakati wa Shetani katika hili? (Kwanza Shetani anawashawishi watu wengi wa Mungu kumkataa Yesu kama Masihi – hata kama asili (mawe) yalimtambua.)

1.  Mkakati wa pili wa Shetani ni upi? (Kuwaangamiza wale waliomchagua Yesu. Kutia mhuri hatima yao ya kudumu.)

2.  Kamwe hekalu halijajengwa upya. Kwa nini hilo linadumisha malengo ya Shetani? (Hilo linakatisha tamaa na kuwachanganya uzao wa Ibrahimu ambao hawajampokea Yesu kama Masihi.)

3.  Kwa nini Mungu aruhusu uangamivu huo wa kutisha? Je, hiki ni kitendo cha kulipiza kisasi kinachofanywa na Mungu? (Kinawezekanaje? Tunasoma juu ya Yesu kuulilia mustakabali wa hekalu na watu wake! Baada ya Yesu kuishi maisha makamilifu, kufa badala yetu, na akafufuliwa na kwenda mbinguni, hekalu halikuwa na maana yoyote. Shetani alitaka kuangamiza mahali ambapo Mungu alikuwa na uwapo wake na Mungu akamruhusu.)

4.  Sehemu ya kichwa cha habari cha somo letu ni “upendo au ubinafsi? Tofauti na kile ambacho Shetani anakifanya, je, kuna ubinafsi mwingine unaoonekana kwenye kisa hiki? (Soma Luka 19:47. Viongozi wa Kiyahudi walitafuta namna ya kumwangamiza Yesu kwa sababu alikuwa akiwapa changamoto kwenye kanuni za dini yao. Hawakuweza kukubali kwamba Mungu ataenenda kwa niaba yao kwa kujitoa yeye mwenyewe. Hata wanafunzi wa Yesu walidhani kuwa watakuwa watawala, wasiokabiliana na makundi ya watu wenye chuki maishani mwao mwote. Viongozi walimkataa Yesu kwa ubinafsi.)

a.  Je, tunafanana na viongozi wa Kiyahudi? Je, tunaukataa wito wa Yesu kwa sababu kwa upumbavu tunaamini maisha yetu yatakuwa bora bila yeye?

II.  Wakapenda

A.  Soma Matendo 2:42-44. Kwa nini walikuwa na “vitu vyote shirika?”

B.  Je, kuwa na vitu kwa ushirika ndio kanuni ya Biblia? Soma Kumbukumbu la Torati 19:14 na Mambo ya Walawi 25:13-17. Vifungu hivyo vinatufundisha nini kuhusu umiliki binafsi wa vitu? (Agano la Kale limejaa kanuni juu ya haki za umiliki mali binafsi. Mambo ya Walawi 25 inaonesha kuwa Mungu aliweka kipaumbele cha juu cha watu kubaki na mali zao.)

C.  Soma Kutoka 20:17. Hii inatufundisha nini kuhusu mali? (Hupaswi kutafakari juu ya kuchukua mali ya jirani yako!)

D.  Tunaielezeaje tabia isiyo ya kawaida katika kitabu cha Matendo sura ya 2?

E.  Soma Matendo 2:5, Matendo 2:41 na pitia kwa harakaharaka vifungu arobaini na vitatu vya kwanza vya Matendo 2. Tunao watu wangapi wapya katika mji? (Kuna wageni wengi kwa ajili ya Pentekoste ambao wanaongolewa na wanaobaki ili kujifunza zaidi habari za Yesu.)

1.  Watu hao watamuduje kukaa Yerusalemu katika muda wa ziada ambao haukupangiliwa?

F.  Soma Matendo 2:45-47. Je, hii inakusaidia kuwa na mantiki na hiki kitendo kipya na kisicho cha kawaida katika kanisa la awali kabisa?

G.  Soma Matendo 4:32-35. Sasa tunaona kuwa kuna mambo mengi zaidi kwenye kisa hiki. Je, bado hii ni hali ya “dharura?” (Bado ilikuwa hali mpya, lakini inaonekana ilikwenda zaidi ya watu waliokuwa wakiutembelea mji kwa ajili ya Pentekoste na wakajisikia kubaki ili kujifunza zaidi kuhusu imani yao mpya.)

H.  Soma Matendo 5:3-5. Hiki ni kisa cha kusikitisha kuhusu wanandoa waliotaka kuonekana wakarimu zaidi kuliko uhalisia – na wako tayari kudanganya juu ya hilo. Petro anaweka kanuni gani ya kimaadili kwenye vifungu hivi? (Wanandoa hawa walikuwa na haki kamili ya kimaadili na kisheria ya kuendelea kumiliki mali yao. Ambacho wasingeweza kukifanya ni kudanganya kuhusu ukarimu wao.)

1.  Utachukua kanuni gani kutoka kwenye kile tulichokisoma kwenye sura za mwanzo za kitabu cha Kutoka katika kuishi maisha ya upendo wa Kikristo?

2.  Nchini Marekani kuna mwelekeo wa watu wanaotoa sehemu ndogo ya fedha zao kama sadaka ili kusaidia wenye shida, lakini wanaotangaza sheria zinazowataka watu wengine kulipa fedha zaidi serikalini ili serikali iweze kuzigawanya. Je, hii inafanana na kisa cha Anania – kutafuta utukufu pale usipostahili?

III.  Wakapigana

A.  Soma Waebrania 11:32-34. Tumekuwa tukiwajadili wafuasi wa Mungu waliodhihirisha upendo na ukarimu mkubwa. Je, nasi pia tunaweza kumtumikia Mungu kama wapiganaji mashuhuri? Au wapiganaji walifanya hivi kama matokeo ya kushindwa kwa imani? (Walifanya hivyo kwa sababu ya imani. Mungu alikuwa nyuma ya matendo haya makuu ya kishujaa.)

B.  Soma Waebrania 11:35-38. Je, mambo haya yanaorodheshwa kama sehemu chanya ya imani ya Kikristo? (Jambo chanya ni kwamba walibaki na imani yao.)

C.  Soma Waebrania 11:39-40. Ni nini lengo la Mungu kwa ajili yetu? (Ahadi yake ya “kilicho bora.”)

D.  Je, tunaweza kuwa na mantiki ya kile tulichojifunza? Je, tunaweza kuja na kanuni inayotuambia wakati gani wa kupambana na kushinda na wakati gani wa kushinda kwa kujitoa wenyewe kwa ajili ya wengine kwa upendo?

1.  Kwani Mungu hakufanya yote mawili?

E.  Rafiki, Mungu anakutaka uwe mwaminifu. Bila kujali kama unajitolea mali zako au unajitoa wewe mwenyewe, bila kujali kama unasimama na kupambana kwa njia ya Imani, au bila kujali kama unapitia mateso kwa kutotendewa haki kutokana na imani yako, Mungu anatuita tumwamini. Mungu anatuwazia jambo jema. Shetani anawazia udanganyifu na uangamivu. Kwa nini usimchague Mungu sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Nuru Hung’aa Gizani.