Somo la 13: Kumngoja Bwana

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 20, Zaburi 27, 92, 126, na Mathayo 12
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
1
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Kumngoja Bwana

(Ufunuo 20, Zaburi 27, 92, 126, na Mathayo 12)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unamtazamia Yesu arejee na kukuchukua mbinguni? Hili ni somo letu la mwisho katika kitabu cha Zaburi. Kinaishia na ujumbe kwamba tunapaswa kungojea ujio wa Yesu Mara ya Pili.

Ninaposubiria jambo huwa ninatarajia lolote linalonifanya nisubirie. Chakula kizuri? Uzoefu wa kufurahisha? Kupandishwa cheo? Uzoefu mbaya usioepukika? Unapokuwa ukisubiria, je, huwa unafikiria litatokea jambo gani ikiwa mambo hayatatendeka kama ilivyotarajiwa? Ikiwa ujio wa Yesu Mara ya Pili ndio unaopaswa kuwa kiini cha maisha yetu, inaonekana kuwa na mantiki kuzingatia mbadala. Uzima wa milele katika utukufu au kuchomwa moto.

Kwa nini tunasita kubainisha sehemu ya kuchomwa moto?  Ningependa kufahamu kuhusu suala hilo kama ningepewa uchaguzi huo mara ya kwanza. Huenda kutozingatia matokeo ya mwisho kunahusiana na ukweli kwamba watu hawajali sana mambo yajayo kuliko wanavyojali mambo ya sasa. Watu wanaopambana na saratani wanafuata ushauri wa daktari kwa umakini. Watu wanaokabiliana na ugonjwa wa kisukari wanajali sana juu ya kufurahia chakula chao cha sasa. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusiana na maswali haya!

I.  Matokeo ya Aina Mbili

A.  Soma Ufunuo 20:4-5. Hii inafafanua jambo gani? (Ufufuo wa aina mbili. Wenye haki wanafufuliwa mwanzoni mwa miaka elfu na “hao wafu waliosalia” hawafufuliwi hadi baada ya miaka elfu.)

B.  Soma Ufunuo 20:6. Ungependa kuwa sehemu ya ufufuo gani? Je, wale waliofufuliwa katika ufufuo wa kwanza watakufa tena? (Hapana. “Mauti haina nguvu.”)

C.  Soma Ufunuo 20:7-9. Wenye haki wako wapi? (Wapo katika Yerusalemu Mpya (“mji huo uliopendwa”) pamoja na Yesu.)

1.  Waovu wapya waliofufuliwa wako wapi? (Huku wakiongozwa na Shetani, wanaishambulia Yerusalemu Mpya na kuwashambulia wenye haki.)

a.  Nini kinawatokea waovu? (“Moto ukashuka kutoka mbinguni ukawala.” Walikufa kwa kuchomwa moto.)

II.  Je, Kumngoja Yesu ni Jambo Rahisi?

A.  Soma Zaburi 27:1-3. Vifungu hivi vya Daudi vinaendanaje na vifungu vya Ufunuo tulivyovisoma hivi punde? (Vinaendana kwa usahihi kabisa. Jeshi la “watenda mabaya” linamshambulia Daudi.)

B.  Hebu turuke hadi chini na tusome Zaburi 27:10-13. “Nchi ya walio hai” ni kitu gani? (Daudi anamtafuta Mungu amwokoe hata kama watu wengine wote wamemwacha. Hatma ya nchi ya walio hai ipo mbinguni na katika nchi mpya.)

C.  Soma Zaburi 27:14. Mfalme Daudi anatuambia “tumngoje Bwana.” Kwa nini? Bwana anakuja na nini? (Zaburi 27 inahusu kuokolewa kutoka kwa watenda mabaya. Daudi anatuambia tungoje kuokolewa.)

1.  Kwenye utangulizi nimewalinganisha wenye tatizo la afya na wale wenye uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la kiafya miaka ya mbele. Kungoja gani kunaelezewa hapa? (Kungoja kote kuwili (both). Daudi anamwomba Mungu amwokoe sasa hivi na kumwokoa katika nchi ya walio hai.)

2.  Kama tunapeleka injili kwa wale wasiojua au wasioamini, tunapaswa kusema nini kuhusu muda wa uamuzi wao? (Kumchagua Mungu huleta tofauti sasa hivi na katika siku zijazo. Tunaweza kuwa tumechelewa ikiwa tutufanya uchaguzi baadaye.)

D.  Soma Warumi 8:18-19. Hebu subiri kidogo! Je, tutateseka sasa hivi hata kama tutamchagua Yesu? (Kama ambavyo Daudia anatuambia kuwa watenda mabaya wanamfuatilia, vivyo hivyo kifungu hiki kinasema kuwa kuishi katika hii dunia kunatuletea mateso.)

1.  Mke wangu huniambia kuwa mimi ni mtu mwenye matumaini mema (optimist). Hilo ni kweli. Mtazamo wangu ni kwamba maisha ni mazuri sana. Hata hivyo, hivi karibuni nilizungumza na kundi la watu wenye chuki kali lililonifanya niwe na wasiwasi juu ya usalama wangu. Gari langu lenye mwendo mdogo lilikuwa na tatizo kubwa la kiufundi. Mtu wangu wa karibu sana katika familia amepatwa ugonjwa mbaya (fatal disease). Pia mimi na mke wangu kwa sasa tunapitia tatizo la kutembea kwa taabu. Je, ninapitia mateso?

E.  Soma Warumi 8:20-21. Nani aliyesababisha “tusiwe na lolote la maana” kwa sasa? (Soma Mwanzo 3:17-19. Eva na Adamu walifanya uamuzi wa kutomwamini na kutomtii Mungu. Mungu aliilaani ardhi, jambo lililofanya maisha yawe magumu kwao. Warumi 8:20-21 inatuambia kuwa kutokana na hili litakuwepo tumaini kwamba tutakuwa huru na “kutolewa katika utumwa wa uharibifu.”)

III.  Jinsi ya Kungoja (Kusubiri)

A.  Soma Zaburi 126:1-3. Je, hili limeshatokea? (Soma Zaburi 126:4. Hapana. Hivi ndivyo watu wa Mungu wanavyodhani mustakabali utakavyokuwa.)

1.  Utaona kwamba Zaburi 126:1 inasema kuwa ni kama “ndoto.” Je, huwa unaota kuwa mbinguni kutakuwaje? Katika dunia mpya?

2.  Je, umewahi kuota juu ya gari jipya, nyumba mpya, au safari nzuri? Ikiwa ndivyo, uhalisia ukoje? (Mara nyingi ndota huwa nzuri kuliko uhalisia. Hilo halitakuwa kweli kule mbinguni, lakini uzoefu katika kutarajia kwetu unaonesha kuwa tunaweza kuwa na furaha kubwa katika ndoto.)

B.  Soma Zaburi 126:5-6. Utaona kwamba mara mbili vifungu hivi vinarejelea upandaji. Kifungu kimoja kinasema, “wapandao kwa machozi,” na kingine kinasema, “mbegu za kupanda.” Kwa nini hapa maisha yanafananishwa na upandaji? (Utakumbuka tumesoma Mwanzo 3:17-19 inayobainisha kuwa maisha ya hapa duniani ni magumu zaidi kwa sababu ya dhambi. Katika maisha yetu ya kila siku tunafanya kazi chini ya laana ya dhambi. Tukimchagua Yesu, basi mavuno yatakuwa “kelele za furaha” mbinguni.)

1.  “Mbegu” na “miganda” ni kitu gani hasa? (Kwa kuwa hatuwezi kupeleka mali zetu mbinguni, lazima miganda itakuwa inawarejelea wale tuliowashawishi kumpokea Yesu. Lazima mbegu zitakuwa juhudi zetu za kuwashawishi wengine kumpokea Yesu. Inaweza pia kurejelea mateso yetu hapa duniani ambayo ni sehemu ya juhudi yetu ya kuitangaza injili.)

IV.  Mtazamo wa Sabato

A.  Soma Zaburi 92:1. Zaburi hii imeandikwa kuhusiana na muda gani? (Sabato.)

1.  Nimesoma Zaburi 92 yote na mwanzoni ilionekana kama wimbo wa ajabu sana wa Sabato. Haizungumzii chochote kuhusu uumbaji. Haizungumzii chochote kuhusu pumziko. Je, tuna mtazamo usio sahihi kuhusu Sabato? Au, huyu mtunga Zaburi ana mtazamo mbaya?

B.  Soma Mathayo 12:10. Viongozi wa Kiyahudi wanamuuliza Yesu swali hili. Wanatarajia kuwa Yesu atajibuje? (Kwamba ni halali. Hii itawapa msingi wa kumshtaki Yesu.)

C.  Soma Mathayo 12:11. Jibu la Yesu ni kuwauliza swali viongozi kwanza. Je, hili ni swali la msingi? (Hapana, angalao sio kwa dhahiri. Yesu anauliza juu ya hali ya dharura. Mtu mwenye mkono uliopooza halikuwa jambo la dharura. Angeweza kusubiri kuponywa baada ya Sabato.)

D.  Soma Mathayo 12:12. Hii inatufundisha nini juu ya mtazamo wa Yesu kuhusu Sabato? (Kipengele cha dharura kwenye swali la kondoo sio cha muhimu. Yesu anasema kuwa wanadamu wana thamani zaidi kuliko kondoo, unapaswa kuwatendea wema wanyama na wanadamu siku ya Sabato. Yesu anatufundisha kuwa Sabato inahusu urejeshaji.)

E.  Soma Mathayo 12:13-14. Linganisha mtazamo wa Yesu na viongozi wa Kiyahudi linapokuja suala la urejeshaji? (Yesu alifanya urejeshaji siku ya Sabato. Viongozi walipanga uangamivu siku ya Sabato.)

F.  Huku tukiwa na mtazamo huu wa Sabato akilini, hebu turejee nyuma na tusome Zaburi 92:1-2. Tunaimba kuhusu jambo gani siku ya Sabato? (Upendo na uaminifu wa Mungu. Hii inaleta mantiki tukiwa na mtazamo sahihi wa Sabato.)

G.  Soma Zaburi 92:4-6. Wakati tukingojea ujio wa Mara ya Pili, tunaweza kuelewa nini kumhusu Yesu ambacho wapumbavu hawawezi kukielewa? (Mungu ana matendo na mawazo makubwa. Uelewa wa viongozi wa Kiyahudi juu ya Sabato haukuwa mkubwa. Hawakuelewa kuwa siku ya Sabato ilikuwa kwa ajili ya kufanya urejeshaji.)

H.  Soma Zaburi 92:9-11. Tunapaswa kuzingatia nini tunapongojea marejeo ya Yesu? (Kwamba Mungu atashinda. Tutashinda. Uovu utaangamizwa.)

1.  Hilo linapaswa kutufanya tutende jambo gani? Tunapaswa kuwa na mtazamo gani? (Kwa kuwa huu ni wimbo wa Sabato, tunapaswa kujitahidi kuwarejesha watenda mabaya. Hatuna haja ya kuwa na shaka kwamba tutarejeshwa.)

I.  Soma Zaburi 92:12-15. Mustakabali wako ukoje? (Wewe si sawa na nyasi, bali unafanana na mti mkubwa “utakaositawi katika nyua za Mungu wetu.”)

J.  Soma Zaburi 30:5. Asubuhi huwa furaha! Je, utatazamia kwa furaha urejeshwaji wako wa mwisho?

K.  Rafiki, usingependa kushindwa. Usingependa kuchomwa moto. Kwa nini usifurahie sasa hivi na baadaye kwa kumchagua Yesu? Kwa nini usichague furaha?

V.  Juma lijalo: Tunaanza mfululizo wa masomo yenye mada “Pambano Kuu.” Tutajifunza mgongano wa jumla kati ya wema na uovu.