Somo la 12: Ibada Isiyokoma

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Zaburi 15, 24, 134, Isaya 53
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
1
Lesson Number: 
12

Somo la 12: Ibada Isiyokoma

(Zaburi 15, 24, 134, Isaya 53)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Makanisa mengi nchini Marekani yana washiriki mia moja au chini ya hapo. Huo ndio uhalisia katika kanisa langu la sasa. Ingawa makanisa madogo yana manufaa, hasara kubwa ipo katika eneo la ibada. Mara kadhaa maishani mwangu nimekuwa katika makundi makubwa yanayoimba sifa za kumtukuza Mungu. Nguvu ya sauti nyingi ni uzoefu wa pekee unaotoa hisia za furaha kubwa! Hii inanipatia kidokezo cha jinsi ibada itakavyokuwa mbinguni. Je, kuna sababu yoyote kwa nini ibada katika kanisa dogo inapungukiwa furaha? Ninajisikia furaha wakati wa ibada katika kanisa langu dogo. Nguvu ya sauti nyingi ndio inayokosekana. Je, kuna jambo jingine linalokosekana? Je, tunapaswa kuwa makini kutochanganya sauti na imani? Hebu tuzame kwenye somo letu la Zaburi ili tujifunze zaidi kuhusu ibada sasa hivi na mbinguni!

I.  Kusifu Kunakochangamsha

A.  Soma Zaburi 134:1. Inamaanisha nini kusema kwamba wanasifu usiku? (Kitendo hicho kilikuwa kinaendelea hekaluni usiku. Mambo ya Walawi 6:9 inarejelea sadaka ya kuteketezwa wakati wa usiku na 1 Mambo ya Nyakati 9:33 inatuambia kuwa waimbaji walikuwa kazini hekaluni wakati wa usiku. Zaburi 134:1 inawarejelea “enyi watumishi wa Bwana,” hivyo inawarejelea waabudu wa kawaida wa kila siku. Nadhani kinachomaanishwa ni kwamba hawa ni wafuasi wa Mungu wenye juhudi.)

B.  Soma Zaburi 134:2. Ninapata furaha ninapoinua mikono yangu pale ninapoimba nyimbo za sifa, lakini kamwe hakuna aliyefanya hivyo kanisani nilipokuwa nikikua. Hata pale nilipokuwa Mchungaji Mlei wa kanisa langu mahalia nilipokea malalamiko kwamba hatupaswi kuwa wa “Kipentekoste.” Je, washiriki wanainua mikono yao wanapoimba nyimbo za kusifu kanisani kwako?

1.  Unadhani kuinua mikono yako ni jambo lisilofaa? Je, hiyo inakufanya ufikirie mikusanyiko ya ki-Nazi?

C.  Soma Zaburi 63:4, Maombolezo 3:41, Zaburi 141:2, na 1 Timotheo 2:8 kuhusu mada ya kuinua mikono yetu tunapoimba nyimbo za sifa au kumwomba Mungu. Unavielewaje vifungu hivi? (Kuna rejea kadhaa katika Biblia kuhusu kuinua mikono yetu.)

D.  Soma Zaburi 134:2-3. Je, hii inaashiria kwamba tukiinua mikono yetu kumbariki Mungu, Mungu naye atatubariki?

E.  Katika kipindi cha kufurahisha cha TED Talk kuhusu kufanya mawasilisho kwa kujiamini, mwasilishaji alisema kuwa kabla hajaenda jukwaani anainua mikono yake hewani. (Alionekana kama umbo “Y” alipofanya hivyo.) Alidai kuwa kitendo hicho kilimpa ujasiri na kujiamini. Sikudhani kama manufaa haya yaliyotokana na kuinua mikono ilikuwa ni nasibu (coincidence) – ingawa hakuwa akimsifu Mungu. Una maoni gani? (Ninaamini kwamba Mungu aliyetuumba “aliweka” (engineered) ndani yetu baraka zinazojiendesha zenyewe (automatic). Kuinua mikono yako wakati wa maombi au kusifu ni mojawapo ya hizo njia zilizowekwa za kusababisha ujasiri na imani.)

1.  Kama unashangaa ni aina gani hiyo ya dhana ya ajabu, jiulize kwa nini dawa za kupoza (placebos) kwenye majaribio ya dawa zinafanya kazi vizuri? Vipozauongo (placebos) havina dawa, lakini mara nyingi huwa na matokeo chanya. Ninapendekeza kwamba Mungu ameweka ndani yetu mjibizo wa imani.)

F.  Soma Zaburi 98:4-8. Kipengele kingine cha ibada kilichochukiwa nilipokuwa mdogo ilikuwa ni kupiga makofi kanisani na kuimba kulikochangamka sana. Je, mito pekee ndio inayoruhusiwa kupiga makofi?

1.  Je, kupiga makofi kanisani kunapaswa kuruhusiwa kwa ajili ya Mungu tofauti na mwanadamu?

2.  Je, umegundua kuwa vifungu hivi vinatumia neno “kelele” mara mbili na kubainisha “kuvuma” kwa bahari? Je, rejea hizi kuhusu kelele kubwa zinapaswa kuongoza fikra yetu juu ya ibada, au sehemu hii ya kauli ni kama ajali tu au haina umuhimu kwenye kusifu kwetu? (Neno la Kiebrania la “kelele” hapa linamaanisha ku “split the ear.” Nadhani rejea hii ni muhimu kwenye ibada yetu.)

G.  Soma Zaburi 149:3 na Zaburi 150:3-6. Ngoma ni kifaa kingine kilichozuiliwa kwa ajili ya ibada kanisani kwangu nilipokuwa mdogo. Hii inaashiria nini kuhusu ngoma kama sehemu ya kumsifu kwetu Mungu? (Vifungu hivi vinajumuisha tari (aina ya ngoma) na matuazi, ambacho ni kifaa kinachogonganishwa.)

1.  Unapotafakari kauli juu ya kuinua mikono katika kusifu, ear-splitting noise vikihusianishwa na kusifu, na matumizi ya ngoma na matuazi, tunapaswa kuhitimisha nini? Je, tunaweza kusema kuwa huu ni uchaguzi wa “kiutamaduni” na Waebrania walikuwa na utamaduni wa kupiga kelele na uchangamfu?

a.  Liweke hili katika muktadha mwingine. Baadhi ya tamaduni zinaonesha upendo kwa kubusu, kukumbatia, na kutoa kauli za kufurahisha. Tamaduni nyingine hazioneshi upendo kwa njia ya kugusana. Unadhani njia hizi tofauti zinaathiri kiwango cha upendo? (Ninaamini hii ina athari kwenye kiwango cha upendo. Ninadhani ibada zisizo na uchangamfu zinatufanya tukose vipengele muhimu vya kusifu. Lakini pia ninajua kwamba hii ni mada yenye mjadala mkubwa!)

II.  Wale Waliokubaliwa

A.  Soma Zaburi 15:1. Unadhani inamaanisha nini kusema “kilima kitakatifu?” (Hii ni rejea ya kwanza kabisa ya hekalu la Yerusalemu, lakini hatimaye rejea ya Yerusalemu Mpya katika dunia mpya.)

B.  Soma Zaburi 15:2-5. Je, unastahili kuishi katika Yerusalemu Mpya?

C.  Soma Zaburi 24:3-6. Angalia mambo mawili kuhusu vifungu hivi. Kwanza, hii inawaelezea wale wanaoingia (atakayepanda mlima) na wana uwezo wa kusalia (“watakaosimama”) katika Yerusalemu Mpya. Je, hii inakuelezea wewe?

1.  Mojawapo ya ukosoaji wa kusifu kunakochangamsha ni kwamba kunaakisi kanisa lisilo dhati kuhusu kutembea na Mungu. Haliko dhati kuhusu ibada ya kweli. Una maoni gani?

2.  Angalia muda wa kifungu cha 5. Kinasema kuwa wale wanaostahili (angalia kifungu cha 4) “watapokea ... haki kwa Mungu wa wokovu wake.” Hii inaniambia kuwa lazima nikidhi vigezo kwa ajili ya haki yangu kwa kuwa na mikono safi na moyo mweupe. Je, unakubaliana kwamba hicho ndicho inachokisema?

a.  Je, unakidhi vigezo?

b.  Nilisoma maoni juu ya vifungu hivi yaliyosema, “hii haihusiani na kupata upendeleo wa Mungu bali kuepuka mambo yatakayotutenganisha na Mungu.” Natamani hilo lingekuwa kweli. Lakini maoni hayo hayahusiani kimantiki na kile tulichokisoma hivi punde. Wanamaoni wengine wananukuu vifungu hivi na kuhitimisha kwamba sio rahisi kuwa “safi” na “halisi,” hivyo vifungu havimaanishi kile vinachokisema. Una maoni gani?

D.  Soma Yeremia 17:9-10. Je, hii inaelezea hali ya mioyo yote? 

1.  Ikiwa ndivyo, je, hii inamaanisha kuwa sote tumepotea?

E.  Soma Yeremia 17:14. Yeremia anatafuta nini? (Kuponywa na Mungu! Mponyaji wa moyo wake mchafu kiasi cha kutisha ni Mungu.)

F.  Soma Isaya 53:5-6. Lifikirie hekalu la Yerusalemu. Jambo gani liliruhusu wanadamu kutakaswa? (Walileta kafara ya mnyama. Watu hawakudai ukamilifu.)

1.  Kifungu hiki kinaashiria kuwa tutaingiaje katika Yerusalemu Mpya?

G.  Soma Zaburi 51:1-2 na Zaburi 51:10. Nani anayempa Mfalme Daudi moyo safi?

H.  Soma Wakolosai 2:13-14. Nani anayetupatia moyo safi?

I.  Hebu tulizungumzie hili kidogo. Zaburi 15 na 24 zinasema kuwa tunatakiwa kuwa wakamilifu ili kuingia mbinguni. Isaya 53, Zaburi 51, na Wakolosai 2 zinatuambia Mungu anatupatia huo moyo safi. Sio suala la matendo yetu au juhudi zetu katika kusafisha moyo wetu. Kwa nini basi Zaburi 15 na 24 zinasema kile zinachokifanya?

J.  Soma 2 Wakorintho 3:18. Tunaokolewaje? (Tunaokolewa kwa neema pekee. Ni karama ya Mungu.)

K.  Soma 1 Yohana 3:4-9. Unaweza kuliwekaje fundisho hili kwa maneno yako mwenyewe? Je, kuna wakati tunatarajiwa tuache kutenda dhambi? (Ingawa tunaokolewa kwa neema pekee, Mungu anatutarajia tubadilike. Badiliko hilo linatokana na utendaji wa Roho Mtakatifu. Hapa ndipo nitakapochomekea mawazo kutoka kwenye nukuu inayohusu kuepuka mambo yatakayotutenganisha na Mungu. Fundisho sio kwamba tunaufikia ukamilifu au kuacha kutenda dhambi kutokana na juhudi zetu. Kinachomaanishwa ni kwamba tunatakiwa kumchagua Mungu na sio Shetani. Tunatakiwa kuishi maisha yanayoepuka dhambi na kutulia kwa Yesu.)

1.  Kwa kuzingatia uchunguzi wetu wa vifungu vyote hivi vya Zaburi 15 na 24. Ni nini mtazamo wa wale wanaopanda kwenda Yerusalemu Mpya? (Wanampa Mungu sifa kwa kuwa na mioyo na mikono safi. Mioyo na mikono safi ndio tamaa ya maisha yao. Ndilo lengo lao.)

2.  Uelewa wa kwamba Mungu amekupatia uzima wa milele, haukuufanyia kazi, unaathirije sifa zako kwa Mungu? (Kama tunadhani kuwa tunawajibika, basi kwa asili kusifu kwetu kutanyamazishwa. Lakini kama tunaamini kuwa tumepewa uzima wa milele ambao hatukuustahili, hilo ndilo jambo la kulifurahia haswaa!)

L.  Rafiki, kama umeokolewa kwa neema, lakini matamanio yako hayaendani na mapenzi ya Mungu, je, utamwomba Roho Mtakatifu akuongoze kubadili mtazamo wako? Kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?

III. Juma lijalo: Kumngojea Bwana.