Somo la 6: Nitainuka

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Zaburi 1, 12, 82 & 76, Mithali 22
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
1
Lesson Number: 
6

Somo la 6: Nitainuka

(Zaburi 1, 12, 82 & 76, Mithali 22)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Utaiitaje nadharia ya kibinadamu inayoonekana kuwa na mantiki lakini haijajengwa juu ya Biblia? Utaiitaje nadharia ya kibinadamu inayokinzana na Biblia? Uabudu sanamu katika Biblia ni kitendo cha mwanadamu kutengeneza sanamu kisha kuiabudu. Je, itakuwa na mantiki kuamini kwamba kuzikubali dhana na hoja fulani za kibinadamu inaweza kuwa uabudu sanamu? Je, kuiabudu dhana ni dhambi kama ilivyo kuiabudu sanamu? Somo letu juma hili linahusu uovu, vitendo visivyo vya haki, na ukandamizaji. Imani nyingi za sasa kuhusu uovu, vitendo visivyo vya haki, na ukandamizaji hazijajengwa kwenye mafundisho ya Biblia na baadhi yake zinakinzana na Biblia. Hebu tuchimbue hili zaidi kwa kuzama kwa mara nyingine tena kwenye somo letu la Zaburi!

I.  Miongozi/Mihimili Sahihi

A.  Soma Zaburi 1:1-2. Kuna uhusiano gani kati ya kubarikiwa na kupokea ushauri kutoka kwa waovu? (Tunabarikiwa tunapoyaongoza maisha yetu kwa neno la Mungu. Tunapowasikiliza waovu, tunapojihusisha na wadhambi, au kuungana na wadhihaki, tunajielekeza kwenye taabu.)

B.  Soma Zaburi 1:3. Je, wenye haki wanajihusisha na kazi? (Ndiyo, na wale wanaomfuata Mungu wanasitawi.)

1.  Kwa nini mtunga Zaburi anamlinganisha mwenye haki na mti uliopandwa kando ya vijito vya maji? (Maji huumpa mti nguvu. Analojia iliyopo ni kwamba kuishi katika mazingira ya sheria ya Mungu, tofauti na kuishi kwa kufuata ushauri wa wadhambi, huwafanya wenye haki wasitawi.)

C.  Soma Zaburi 1:4-6. Waovu wanaweza kutarajia maisha ya namna gani? (Maisha yanawapeperusha. Maisha hayana huruma kwao. Hatimaye wanaangamia.)

D.  Utaona kwamba Zaburi ya kwanza inaweka kipimo: ishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu yaliyodhihirishwa, vinginevyo upate mateso na kuangamia. Uchaguzi ni wako!

II.  Kushughilika na Maskini na Wahitaji

A.  Soma Zaburi 12:2-4. Hawa ni watu wa namna gani? (Watu wanaoamini kuwa wanaweza kuzungumza jambo lolote. Watu wanaoamini kuwa wao ni mabwana wa wengine kutokana na maneno yao ya ushawishi.)

1.  Je, unawafahamu watu kama hawa? Watu ambao ama wanajipendekeza au kuwakashifu wengine kwa kuwa maneno yana nguvu?

a.  Hivi karibuni, mwanaume aliyesema kuwa anapendelea kuishi kama mwanamke alitajwa kama “Mwanamke wa Mwaka” na jarida maarufu. Je, hiyo inaendana na kile tunachokijadili?

B.  Soma Zaburi 12:5. Jambo gani linasababisha tatizo kwa maskini na wahitaji? (“Wametekwa nyara” na wale wanaowalaghai. Wanenaji hawa wanasababisha madhara kwa maskini.)

1.  Utaona kwamba neno “maskini” linamaanisha, kwa mujibu wa Strong, “waliokandamizwa kimawazo au kimazingira.” Unadhani hii inawajumuisha vijana wanaojaribu kujipenyeza kimaisha na “wanatekwa nyara” na wale wanaowadanganya?

2.  Hebu tuwazungumzie wale walio maskini kwa kuzingatia mazuri ya dunia. Uovu gani unawasilishwa? (Wazungumzaji wako hivyo tu, hawafanyi mambo yoyote ili kuwasaidia maskini.)

3.  Mungu atafanya nini? (Ataandaa mahali salama kwa ajili ya maskini na wahitaji.)

C.  Soma Zaburi 12:6-7. Mungu anafanya nini ili kuwasaidia maskini na wahitaji? (Ana “maneno safi.” Mungu anasema ukweli. Kama wafuasi wa Mungu lazima tuseme ukweli.)

D.  Soma Zaburi 12:8. Ulimwengu unauchukuliaje udanganyifu wa waovu? (Uovu unatukuzwa.)

1.  Unaona taswira iliyopo hapa? Watu wa Mungu wanasema ukweli, lakini waovu wanazungukazunguka kila mahali wakitangaza mawazo yao potofu. Jambo la kawaida?

E  Hebu tubadili suala hili kidogo. Soma Mithali 22:7. Je, kifungu hiki kinaelezea ukweli, au suala hili linaakisi mapenzi ya Mungu? (Soma Mithali 22:4. Mungu anawapa thawabu ya utajiri, heshima na uzima wale wanaomtii. Matokeo yanayofuatia kwa wasio watiifu yanaendana na mapenzi ya Mungu.)

F.  Soma Mithali 22:9. Wale waliobarikiwa wanapaswa kuwatendea nini maskini? (Wawapatie chakula. Matokeo yake ni kubarikiwa zaidi.)

G.  Soma Mithali 22:3 na uilinganishe na Mithali 22:13. Vifungu vyote hivi viwili vinahusisha hatari. Mmoja anasema kuepuka ajali ni busara. Mwingine anasema kuepuka hatari hukufanya kuwa “goigoi.” Unadhani jambo gani linafundishwa hapa? (Mtu mwenye “busara” anadhihirisha matumizi ya akili ya kawaida (commonsense). Anaona tatizo linakuja na kuchukua hatua ya kuepuka kuumizwa na matatizo hayo. Goigoi, ikimaanisha mtu mvivu, kwa udanganyifu anadai kuwa anaogopa ili kuepuka kufanya kazi.)

1.  Je, umewahi kuwasikia watu wanaodai kuwa na hofu kwa sababu mtu fulani katika chumba hakubaliani na mawazo yao?

2.  Kama umejibu, “Ndiyo,” je, mtu huyo ni “goigoi?” (Badala ya kubadilishana mawazo juu ya kilicho sahihi na kisicho sahihi, wana uvivu mkubwa kimawazo kiasi cha kushindwa kutafakari mitazamo mingine.)

H.  Katika sehemu hii tumeangalia vifungu katika kitabu cha Zaburi na kuongezea vifungu kutoka katika kitabu cha Mithali. Tumejifunza kanuni gani? (Mpangilio wa asili wa mambo ni kwamba wale wanaotii wanabarikiwa. Wale wanaobarikiwa wanapaswa kuhakikisha kuwa maskini wanalishwa – kama sehemu ya wajibu wao kwa Mungu. Ulishwaji huu humaanisha kuusimamia ukweli na kuwasaidia maskini. Wale wanaotafuta matatizo kutoka kwa Mungu wanawadanganya maskini na kunufaika kupitia kwao. Kwa kiasi kikubwa wanafanya hivyo kwa kuwalaghai. Ukweli ni wa muhimu.)

III.  Hukumu Sasa Hivi

A.  Soma Zaburi 82:1-3. Unadhani kwa nini Zaburi hii inatumia neno “haki” badala ya “upendo?” (Dunia inawapendelea waovu. Mungu anasema kuwa anataka haki kwa wanyonge na wahitaji.)

1..  Ni nini haki kwa wale wanaodai kuwa wanaogopa jambo fulani ili kuepuka kufanya kazi? Ni nini haki kwa wale wanaoendelea kutotii sheria za Mungu na kuteseka kwa kitendo hicho cha kutotii? (Kwa miaka mingi nimewasikia Wakristo wakizungumza kuhusu “upendo thabiti.” Kwa jinsi ninavyolielewa neno hilo, inamaanisha kuwa haki ni sehemu ya kile tunachokifanya kwa upendo kwa ajili ya maskini na wahitaji.)

B.  Soma Zaburi 82:4-5. Ni nini kinachopaswa kuwa sehemu ya juhudi zetu za uokozi? (Kuwaelimisha maskini na wahitaji. Tatizo ni kwamba hawana “uelewa” na “ufahamu.”)

1.  Ni maeneo gani ya dhahiri ambayo maskini na wahitaji wanahitaji elimu? (Wanahitaji kujifunza stadi za kazi. Wanahitaji kuongozwa katika masuala ya kisheria na jinsi ya kusimamia masuala ya fedha.)

2.  Vipi kama maskini na wahitaji wanakataa kujifunza, au kama wanajifunza, wanakataa kutenda? (Nilimsikiliza raia wa Puerto Rico akizungumza kuhusu masuala ya fedha ya kisiwa hicho. Spika aliongoza kufilisika kwa serikali ili kisiwa hicho kiwe na fursa mpya ya mafanikio. Spika, ambaye ni Mkristo na mwenye kuwahurumia watu wa kisiwa hicho, anatazamia mambo mabaya katika siku zijazo (pessimistic about the future). Ana wasiwasi kwamba watu hawako tayari kubadilika.)

3.  Utaona kwamba wanamaoni hawakubaliani nami juu ya nani anayeelezewa kuwa hana uelewa. Wanasema kuwa hao ni mahakimu wasiotenda haki. Una maoni gani?

C.  Soma Zaburi 82:6-8. Ni nini lengo la maisha yetu, na ni nini uhalisia wa maisha yetu? (Sisi ni wana na binti wa Mungu. Tunapaswa tuenende vivyo hivyo. Hii ilihusika kwa mahakimu na maskini na wahitaji. Tukishindwa, basi tunaenenda njia ya watu wote wasio na Mungu.)

D.  Soma Zaburi 76:2-6. Mungu anapoamua kuchukua hatua dhidi ya uovu, je, anaweza kuzuiliwa?

1.  Nini kinawatokea wale waliopata utajiri isivyo sahihi? (“Wananyang’anywa marupurupu yao.”)

E.  Soma Zaburi 76:7-9. Uwezo wa Mungu unajidhihirisha kutoka wapi? (Kutoka mbinguni!)

F.  Soma Zaburi 144:5-6. Je, hii dhana ya uwezo wa Mungu kushuka chini kutoka mbinguni inaongeza ukuu wa kuokolewa kwetu?

G.  Soma Zaburi 144:7-8. Ni nini kilicho adui wa kujirudiarudia (consistent) kwa wenye haki? (Kutokuwa na uaminifu (dishonesty)! Hiki kinatumika dhidi ya maskini na wahitaji, na kinatumika dhidi ya watu wa Mungu.)

H.  Hebu turejee kwenye Zaburi 76:9. Kifungu kinapowarejelea “wapole,” je, inamaanisha kuwa tunatakiwa kuwa wapole? (Muktadha ni kwamba watu wa Mungu wamenyenyekezwa na waovu. Mungu anawaokoa watu wake wanaodanganywa, wanaokandamizwa, na kunyanyaswa na waovu. Uokozi huo ni hukumu ya Mungu.)

I.  Rafiki, je, haionekani kwamba adui mkuu wa wenye haki na maskini ni udanganyifu na vitendo visivyo vya haki? Ulimwengu unapotupachika majina, au unapotufanya tuingie kwenye mipango ya utekelezaji iliyojengwa kwenye kanuni ambazo hazipo kwenye Biblia, tunatakiwa kuipinga. Tunatakiwa kuusema ukweli kwa upendo. Tunatakiwa kuwasaidia wale wanaoteseka, lakini kwa namna inayoakisi mapenzi ya Mungu. Tutashindwa katika nyanja mbalimbali, lakini Mungu atashuka chini kutoka mbinguni na atasahihisha mambo. Je, utadhamiria kutoishi kwa udanganyifu?

IV.  Juma lijalo: Rehema Zako Hufika Hadi Mbinguni.