Somo la 5: Kuimba Wimbo wa Bwana Katika Nchi ya Ugenini

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Zaburi 37, 41, 74 & 77
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
1
Lesson Number: 
5

Somo la 5: Kuimba Wimbo wa Bwana Katika Nchi ya Ugenini

(Zaburi 37, 41, 74 & 77)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Utajisikiaje kama watu wengi wanaupinga Ukristo na kudhani kuwa Ukristo una mafundisho hatarishi? Kwa kuwa wasomaji wa masomo haya wametapakaa duniani kote, baadhi wanafahamu kiuhalisia jinsi dhana hiyo ilivyo. Lakini kwa wale tuliopo nchini Marekani hatujui lolote. Nilipokuwa kijana mdogo nikiishi Michigan, watu wengi walidai kuwa ni Wakristo. Ama kwa hakika, palikuwepo na waasi wachache. Lakini hakuna aliyedai kuwa Ukristo una madhara, mambo yalijikuta tu kuwa katika “wakati mzuri.” Hilo sasa linabadilika. Idadi kubwa ya Wamarekani hawaiamini tena Biblia, badala yake wanaamini kuwa mafundisho yake ni sumu kwa uhusiano wa binadamu. Hata ndani ya kanisa watu wengi wanajenga hoja kuwa watu wamedhuriwa kwa namna ambavyo baadhi ya Wakristo wamekuwa wakipeleka (share) ukweli kwa wengine. Malalamiko halisi ni yepi kuhusu kupeleka ukweli kutoka kwa wale wanaodai kuwa wao ni watu wa Mungu? Kwamba ukweli unashirikishwa bila kuwataka radhi? Au kwamba wale wanaowashirikisha wengine ukweli hawana ubunifu? Zaburi zetu juma hili zinajadili juu ya kuishi kwa ajili ya Mungu katika mazingira ya chuki. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia!

I.  Wito wa Msaada

A.  Soma Zaburi 74:3-4. Janga gani linaelezewa hapa? (Soma Zaburi 79:1. Hii ni rejea ya uangamivu wa kwanza wa helaku (la Sulemani) na mji mkuu wa Yerusalemu. Kila kitu ndani ya hekalu la Mungu kimeangamizwa kabisa.)

1.  Nini kinamaanishwa (Zaburi 74:4) katika maneno “Watesi wako wameunguruma?” (Wamefurahia katika ushindi kwa Mungu. Mambo yote yaliyojielekeza katika uwezo wa Mungu yote yanajielekeza kwenye uwezo wa maadui wa Mungu.)

B.  Soma Zaburi 74:5-6. Ni kwa jinsi gani maadui wa Mungu wanafananishwa na wakataji miti? (Maadui wa Mungu wamechukua njia ile ile kwenye mbao nzuri zilizotiwa nakshi katika hekalu kwa kukata miti msituni!)

C.  Soma Zaburi 74:7-8. Jambo gani baya kabisa limetokea katika mahali pa ibada? (Pote pamechomwa moto!)

D.  Soma Zaburi 74:9. Jambo gani linakatisha tamaa? (Hawajui lini Mungu ataingilia kati ili kuwasaidia.) 

II.  Kukata Tamaa na Fedheha

A.  Soma Zaburi 74:10-11. Unapojikuta umeshindwa jambo, je, unafurahia kudhihakiwa na kilichokushinda? Je, unafurahia fedhedha ya kushindwa? (Jibu ni dhahiri: Hapana!)

1.  Mtunga Zaburi anamuuliza Mungu kwa nini anaruhusu afedheheshwe? Unadhani huu ni mkakati mzuri? Kama ungekuwa Mungu, je, ungefurahia maoni ya namna hii?

B.  Hebu tuangalie Zaburi nyinginezo ili kujua sababu za kwa nini tunamlaumu Mungu kwa kutotatua matatizo yetu. Soma Zaburi 77:7-9. Sababu gani zinapendekezwa hapa? (Mungu amemkataa mtunga Zaburi milele. Mungu hatupendi tena. Ahadi za Mungu zina tarehe ya kuchotora (expire) na tumeshaipita tarehe hiyo. Mungu amekasirika na amesahau kuwa Mungu wa neema.)

1.  Kama ungekuwa Mungu, je, ungependezwa na madai hayo?

C.  Soma Zaburi 74:12. Mtunga Zaburi anapendekeza kuwa sababu ya Mungu kutochukua hatua ni ipi? (Mtunga Zaburi anajibu swali lake mwenyewe. Mungu ni Mungu mwenye uzoefu. Amekuwa akifanyia kazi wokovu wa watu kwa muda mrefu. Lazima Mungu atakuwa na mkakati wa kuwaokoa watu katika jambo hili.)

D.  Soma Zaburi 77:14-16 na Zaburi 77:19-20. Hapa tunaona mtazamo gani chanya wa utayari wa Mungu kutoa msaada? (Kutenda maajabu ni sehemu ya asili ya Mungu. Aliwachukua watumwa Misri na akawapitisha katika bahari!)

E.  Soma Zaburi 74:13-17. Mtunga Zaburi hajumuishi sababu ipi ya Mungu kutochukua hatua? (Kuchelewa kwa Mungu hakuakisi kutokuweza kwake kuchukua hatua au udhaifu wake. Mungu ana uzoefu wa kuvunjavunja vichwa vya madubwana (monsters). Zaidi ya hayo, anadhibiti majira!)

F.  Soma Zaburi 74:19-23. Unadhani mtunga Zaburi ana wasiwasi juu ya nani hasa? (Hapa ndipo tunapouona ukweli. Maneno “hua,” “mnyonge,” “aliyeonewa,” na “mhitaji” yote yanawarejelea watu wa Mungu. Ingawa pasi na shaka yoyote mtunga Zaburi anawazia sana kuhusu jina la Mungu (ikizingatiwa kuwa yeye ni Mungu wa mtunga Zaburi), kiuhalisia anachokijali ni kuhusu yeye mwenyewe! Usitusahau, Mungu!)

1.  Je, hilo ni jibu la kibeuzi (cynical), au kuna mantiki katika jibu hilo? (Mantiki ni kwamba Mungu anaweza kujihudumia mwenyewe. Watu wa Mungu hawawezi kujihudumia wenyewe.)

G.  Soma Zaburi 41:7-9. Tunatakiwa kustahamili chanzo gani kingine cha fedheha pale ambapo Mungu haingilii kati ili kuwashinda watu wabaya? (Watu wengine wanatulaumu! Wale wanaotuchukia “wanatuwazia mabaya,” lakini hili pia ni kweli kwa “rafiki yangu wa karibu niliyemtumaini.”)

H.  Soma Zaburi 41:10. Mtunga Zaburi ana wazo gani zuri baada ya Mungu kuingilia kati kwa ajili yake? (“Atawalipa” wale wote wanaomchukia na, kwa dhahiri, rafiki yake anayemwamini.)

1.  Unadhani anawazia malipo gani? (Soma Zaburi 41:11. Jibu chanya zaidi ni kwamba malipo yanakuja katika mfumo wa wao kumwona akirejea madarakani.)

III.  Tunachokistahili

A.  Soma Zaburi 41:12. Mtunga Zaburi anadai kuwa Mungu amemwokoa “kutokana na ukamilifu [wake].” Una maoni gani? Je, hiki si kiini cha madai ya kwanza (original) – kwamba mtunga Zaburi hakuwa amelindwa kutokana na udhaifu wake?

1.  Soma Zaburi 41:4. Mtunga Zaburi anakiri juu ya jambo gani? (Kwamba yeye ni mdhambi!)

2.  Soma Zaburi 38:3-5. Maoni ya Albert Barnes yanasema kuwa kifungu hiki kinamwelezea mtunga Zaburi yule yule aliyeandika Zaburi 41:12 ambaye anazungumzia “uadilifu” wake. Biblia inatufikishia ujumbe gani? Tunapaswa kujifunza nini? (Hatuwezi kujiamini ili kujifanyia tathmini ya kweli ya uadilifu wetu.)

B.  Soma Luka 13:1-5. Yesu anasema nini kuhusu imani yetu kwamba wema wetu wa kawaida unatulinda? (Yesu anasema kuwa bila yeye dhambi zetu zitasababisha mauti ya milele. Sote tunastahili kifo. Sisi sote ni wadhambi.)

1.  Je, hiyo inamaanisha kuwa mtazamo wa kwamba dhambi inasababisha madhara na matokeo ya kutisha sio sahihi? (Hapana. Dhana ya jumla kwamba utii na ulinzi vinahusiana ni dhana ya kweli. Hiyo ndio sababu mojawapo ya kwa nini Mungu alitupatia sheria zake – kutulinda. Alichokimaanisha Yesu ni kwamba hatuwezi kudai kuwa sisi ni wema. Tusipotubu, yaani tusipo utegemea wema wa Yesu, sote tunastahili kifo. Na, hatuwezi kutegemea tathmini yetu wenyewe kuhusu uadilifu wetu.)

IV.  Njia ya Kuuelekea Ushindi

A.  Soma Zaburi 37:1-2. Ni nini hatima ya wale wanaotutaabisha? Hatima ya watendao uovu? (Watanyauka na kufa.)

B.  Soma Zaburi 37:3-4. Matokeo ya asili ya kuwa na uhusiano na Mungu ni yepi? (Atakupa haja za moyo wako.”)

C.  Soma Zaburi 37:5-7. Jambo gani ni la muhimu sana kwetu kulitenda wakati wa taabu? (Mtumaini Mungu. Kuwa mvumilivu. Jitahidi usiwe na wasiwasi.)

D.  Soma Zaburi 37:8-9. Unakumbuka habari za mtunga Zaburi katika Zaburi 41:10 aliyesema kuwa Mungu atakapomrejesha juu “atawalipiza” wale wanaosema mambo mabaya juu yake? Hii inaashiria kuwa jibu zuri zaidi ni lipi? (Usikasirike. Kwa wakati wa Mungu utakuwa juu.)

E.  Soma Zaburi 37:12-15. Jambo gani litawatokea waovu? (Watateseka juu ya kile wanachokiwazia kwa ajili ya watu wa Mungu.)

1.  Muda si mrefu tumetoka kujadili kisa cha Esta. Jambo gani linakujia akilini? (Hamani alinyongwa katika mti wa mikono hamsini alioutengeneza kwa ajili ya kumnyongea Mordekai. Esta 7:9-10.)

F.  Soma Zaburi 37:16. Tunapaswa kujifariji na jambo gani hadi Mungu atakapotuokoa? (Kidogo tulicho nacho ni bora kuliko vitu vyote vinavyomilikiwa na waovu.)

G.  Rafiki, Mungu atashinda! Hatustahili kushinda, lakini Mungu anatenda na kwa neema zake amejitolea kutufanya nasi pia tuwe washindi. Je, utatubu na kukubali ofa yake sasa hivi? Je, utasubiria uokozi wa Mungu kwa subira?

V.  Juma lijalo: Nitainuka.