Somo la 7: Utume kwa Jirani Yangu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Luka 10, Yakobo 2, Mathayo 7
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
4
Lesson Number: 
7

Somo la 7: Utume kwa Jirani Yangu

(Luka 10, Yakobo 2, Mathayo 7)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Katika Luka 10:27 Yesu alifundisha kuhusu “kumpenda jirani yako kama nafsi yako.” Mtazamo huu, ambao unarejelewa kama “Golden Rule,” unatumiwa na dini nyingi. Kuifuata kanuni hii ya msingi sio jambo rahisi. Inahitaji fikra. Chukulia kwamba mtu asiye na makazi (ombaomba) anakuomba fedha. Kwa haraka haraka unaweza kuamua kwamba endapo majukumu yako yatabadilishwa ungependa kupokea fedha hizo. Ukiangalia jambo hili kwa kina, kama ungekuwa ombaomba kutokana na matumizi ya dawa za kulevya au kutokana na uvivu, je, ungependa kusalia katika hali hiyo? Binafsi nisingependa. Katika mazingira hayo, kukataa kumpatia ombaomba fedha na hivyo kusaidia kushinikiza mabadiliko linaweza kuwa jambo bora zaidi kwa mtu huyo – ambalo ndilo jambo ambalo ungelipenda kwa upande wako. Hebu tuzame kwenye Biblia yetu ili tuone kile anachotufundisha Yesu kuhusu jibu la swali hili!

I. Kumjaribu Yesu

A. Soma Luka 10:25. Je, kweli mwanasheria huyu anataka kujua jibu la swali hili? (Hapana. Mwanasheria alidhani kuwa tayari alikuwa anafahamu jibu la swali, alitaka kuona kama Yesu alikuwa na jibu sahihi.)

B. Soma Luka 10:26-28. Nani anayeishia kujaribiwa? (Mwanasheria! Yesu anabadili hali ya mambo.)

1. Sehemu ya swali hili inaonekana kuwa na makossa. Mwanasheria anauliza “nifanye nini” ili nipate kuokoka? Je, hili ni swali sahihi kwa kuwa tu bado Yesu hajafa msalabani?

2. Chunguza jibu la Yesu katika kifungu cha 26 kisha uniambia endapo Yesu anatoa jibu la kijanja? (Yesu anauliza mwanasheria anasemaje kuhusu uzima wa milele. Sheria inahusu matendo. Yesu anahusisha neema.)

3. Zingatia Luka 10:28. Ingawa Yesu amehamisha swali, anamwambia mwanasheria kuwa endapo atatenda jambo fulani (Mpende Mungu na jirani yako) “ataishi.” Hii inaendanaje na Wagalatia 2:16 na kutegemea kile ambacho Mungu amekitenda kwa ajili yetu badala ya kuyategemea matendo yetu kwa ajili ya wokovu?

C. Soma Luka 10:29. Unadhani kuwa bado hili ni jaribu? Au Yesu amemvuta mwanasheria kwenye mjadala wa dhati kuhusu uzima wa milele wa mwanasheria? (Nadhani mwanasheria amevutwa ili kuyatafakari maisha yake mwenyewe.)

II. Kumjaribu Mwanasheria

A. Soma Luka 10:30-32. Je, hawa viongozi wawili wa dini walimwona mtu aliyejeruhiwa? (Yesu anabainisha kuwa walimwona na kuamua kuachana naye.)

1. Walikuwa na sababu gani ya kutokumsaidia mtu yule? (Kama walikuwa wanakwenda hekaluni Yerusalemu inawezekana walidhani kuwa kumgusa mtu huyu kungeweza kuwafanya wawe najisi (angalia kwa ujumla Mambo ya Walawi 15 kuhusiana na damu), na hilo lingesababisha tatizo katika kazi yao ya Mungu.)

B. Soma Kumbukumbu la Torati 22:4. Sheria iliwataka viongozi hawa wa dini wafanye nini? (Kama walitakiwa kumsaidia mnyawa wa thamani wa ndugu, kwa hakika walitakiwa kumsaidia ndugu yao.)

C. Rejea kwenye Luka 10:30. Ni nini falsafa ya wanyang’anyi hawa? (Nina haki ya kuchukua kilicho chako.)

D. Soma Luka 10:33-35. Una maoni gani, je, mwanasheria angefanya kile alichokifanya Msamaria?

E. Soma Zaburi 139:21-22. Mtu aliyetoa msaada alikuwa Msamaria. Kama mtu aliyejeruhiwa alikuwa Msamaria, je, mwanasheria angemsaidia Msamaria katika mazingira haya? (Jibu ni, “hapana,” kwa sababu Wasamaria walikuwa maadui.)

F. Soma Luka 10:36-37. Kwa kuzingatia mjadala wetu hadi kufikia hapa, unadhani katika siku zijazo mwanasheria atatii kile alichokisema Yesu?

1. Katika sehemu ya utangulizi nilipendekeza kuangalia kwa kina mazingira yaliyopo. Hii ilikuwa barabara hatari. Je, mtu yule aliyejeruhiwa anapaswa kulaumiwa kwa kusafiri peke yake katika barabara hiyo?

a. Je, atapata fundisho la msingi kama utamwacha tu hapo? (Fundisho lolote la kujifunza kuhusu usalama binafsi tayari lingekuwa limefanyika.)

III. Kujaribiwa Kwetu

A. Hadi kufikia hapa tunatakiwa kujadili ambacho Yesu anamfundisha mwanasheria pamoja na sisi.

1. Je, anafundisha kuwa utii wa sheria hauwezekani kwa wanadamu wadhambi, na hivyo jibu halisi la kuupata uzima wa milele ni kuyategemea matendo ya Yesu badala ya kuyategemea matendo yetu?

2. Au je, Yesu anafundisha kuwa tunapaswa kuwasaidia maadui wetu na wale wanaoingia matatizoni kipumbavu?

3. Au je, ni jambo jingine kabisa? (Nadhani Yesu anatufundisha falsafa ya Kikristo ya maisha ni kuwaonesha wengine upendo, hata kama watu hao ni maadui. (Sidhani kama anafundisha maridhiano na uovu.) Wakati huo huo, kwa kuwa mwanasheria aliona kuwa jambo hili haliwezekani kiuhalisia, nadhani Yesu anafundisha neema.)

4. Yesu hafundishi nini? Falsafa zipi za maisha zimekataliwa? Falsafa ya mnyang'anyi: kama una vitu vingi kuliko mimi, nina haki ya kuchukua mali yako. Huu ni ujamaa au ukomunisti wa kisasa. Yesu pia anakataa njia ya viongozi wa dini wanaotaka kutunza kile wanachokimiliki (muda na fedha). Hili ni kweli hata kama wataweka hadithi ya kidini kwenye njia yao. Huo ni mtazamo wa kwamba nimetafuta fedha zangu mwenyewe na sitawapa watu wengine fedha zangu kwa sababu nao wanatakiwa kuwa kama mimi kwa kutafuta fedha zao wenyewe.)

B. Angalia tena Luka 10:37. Unadhani amri ya Yesu ya “enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo” ilikoma msalabani? (Soma Mathayo 5:17. Yesu aliturehemu! Yesu hakuitangua torati, alitenda kile tusichoweza, ambacho ni kuitii sheria kikamilifu. Hiyo haiondoi wajibu wetu wa kujaribu kuishika sheria. Haiondoi wajibu wetu wa kumpa Mungu utukufu kwa matendo yetu. Angalia Mathayo 5:16.)

C. Soma Yakobo 2:14-16. Kama unakubaliana na alichokiandika Yakobo, vipi kama badala yake mtu atasema, “nitakuombea?” (Ombi sio, na wala halipaswi kuwa, kauli tupu. Ni jambo lenye ufanisi sana tunaloweza kulifanya. Swali ni endapo Mungu anatuita kuwa wasaidizi wake?)

D. Soma Yakobo 2:17-18. Hiki ni mojawapo ya vifungu vinavyofahamika sana katika Biblia. Unadhani Yakobo anamaanisha nini kwa kubainisha kuwa anadhihirisha imani yake kwa matendo yake?

E. Soma Mathayo 7:21. Je, Yesu na Yakobo wanaonekana kusema jambo linalofanana?

F. Soma Mathayo 7:22-23. Sasa tunalo tatizo, sawa? Yakobo alituambia kuwa atadhihirisha imani yake kwa matendo yake na huo ndio hasa utetezi unaoibuliwa na watu hawa. Je, hii inaonesha kuwa Yakobo hayuko sahihi? Kwamba hatimaye akimwambia Yesu kile alichotuambia, “uthibitisho” wake hautoshi?

1. Je, kuna namna ya kupatanisha alichokisema Yesu katika Mathayo 7:22-23 na alichokisema Yakobo kuhusu kuthibitisha imani yake kwa matendo yake? (Ndiyo. Kwa yenyewe, matendo hayaithibitishi imani. Warumi 3:28. Hata hivyo, imani kwa Mungu inayoakisi uelewa wa upendo wake huzaa matendo. Kumwelewa Yesu hubadili maisha yako.)

G. Hebu tuwe na uhalisia. Unapowalinganisha watu katika Luka 10:30 na Luka 10:34-35, je, umeridhika na wajibu wako wa kuwasaidia wengine kwa kuwapigia kura maafisa wa serikali wanaotumia fedha za kodi kuwasaidia maskini? (Msamaria alitumia fedha zake mwenyewe kumsaidia mtu aliyejeruhiwa. Wale wanaowalazimisha wengine kuwasaidia wahitaji wanapaswa kusoma kisa hiki kwa umakini. Taarifa zilizopo zinabainisha kuwa watu wanaosaidia sana kwa kutumia fedha za watu wengine, wanatoa fedha kidogo sana kutoka mifukoni mwao ili kuwasaidia maskini.)

H. Rafiki, je, utakichukulia kwa dhati kisa cha Msamaria? Je, utamwomba Roho Mtakatifu, sasa hivi, akuongoze kuwasaidia wale watakaonufaika na msaada wako?

IV. Juma lijalo: Utume kwa Mhitaji.