Somo la 9: Huduma Katika Kanisa la Agano Jipya

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Matendo 2, 4 & 5, 2 Wakorintho 8)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
3
Lesson Number: 
9

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Juma hili tunaanza somo letu kwa taarifa ya kile ambacho Wakristo wa awali kabisa walikifanya kwa mali zao. Hakuna kitu kama hicho kimetaarifiwa katika Agano la Kale, na hakuna kitu kama hicho kimetaarifiwa tena katika Agano Jipya. Kwa nini hivyo? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

 

  1.    Kusanyiko la Pentekoste

 

    1.    Soma Matendo 2:5-11. Kwa nini tunao watu kutoka duniani kote ndani ya Yerusalemu? (Ni katika kusherehekea “Sikukuu ya Majuma” (Kumbukumbu la Torati 16:10), ambayo sasa tunaiita “Pentekoste.”)

 

    1.    Ikiwa hukifahamu kisa cha Pentekoste, soma Matendo 2:1-40. Ikiwa tayari unakifahamu, soma Matendo 2:41. Matokeo ya ujumbe wa injili kutolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ni yapi? (Watu elfu tatu walibatizwa kanisani siku hiyo.)

 

    1.    Soma Matendo 2:42. Hao “wakawa” wanaozungumziwa katika “wakawa wakidumu katika fundisho la mitume” ni akina nani? (Ni wale elfu tatu walioongolewa.)

 

      1.    Watu elfu tatu walikuwa wanafanya nini? (Mitume walikuwa wakiwafundisha hawa waumini wapya. Walikuwa, wakiomba na kufurahia kuwa pamoja.)

 

    1.    Soma Matendo 2:43-46. Tatizo la dhahiri ni lipi? (Wao ni wasafiri, wanakaa Yerusalemu kwa muda mrefu zaidi ya walivyotarajia, wapo shule na hawafanyi kazi – wanaishije? Wanapataje chakula?)

 

      1.    Unapoyazingatia mazingira hayo, je, hii ni hali ya pekee, au kwa kawaida hivi ndivyo Wakristo wanavyopaswa kuishi? (Hii ni hali ya pekee. Kama umewahi kuhudhuria “mkutano wa makambi,” fikiria kwamba mkutano huo umeendelea kwa miezi kadhaa bila kutarajia, na si kwa juma moja au majuma mawili. Ili kuhakikisha kwamba kila mtu amepata chakula, ungetakiwa kuuza ulichokuwa nacho kilichokuwa cha thamani ili kusaidia kuwalisha watu chakula.)

 

      1.    Unapotafakari kwamba njia hii ya kuishi haijataarifiwa mahali popote kwenye Biblia, hii inazungumzia nini kuhusu kuishi kijumuiya? (Kwa kawaida, Wakristo hufurahia heshima na nidhamu ya kazi. Hiki ni kipindi maalumu cha maelekezo. Ninatarajia kwamba baada ya mafundisho ya kutosha, hawa waongofu wapya walirejea nyumbani ili kushiriki injili mahali walipokuwa wakiishi.)

 

    1.    Soma Matendo 2:47. Je, tatizo la kuwalisha watu linatatuliwa au linakuwa baya zaidi? (Habari njema ni kwamba watu wengi wanaokolewa. Habari mbaya ni kwamba waongofu wapya pia wanahitaji kulishwa, ingawa inawezekana tayari waongofu hawa wanaishi Yerusalemu.)

 

    1.    Soma Matendo 4:4. Sasa tupo kwenye sura mbili za ukuaji wa kanisa. Hatujui muda gani umepita baada ya Pentekoste. Sasa tunao waumini wangapi Yerusalemu? (Idadi kamili ya wanaume, wanawake, na watoto haijulikani, lakini tunafahamu walikuwepo wanaume elfu tano.)

 

    1.    Soma Matendo 4:32-35. Je, bado hii ni hali ya dharura iliyokuwepo mara baada ya Pentekoste? (Inaonekana jibu ni “hapana.”)

 

      1.    Kwa nini hawa waumini wa awali wana mtazamo wa kwamba hakuna kitu chochote “walichonacho kilicho mali yake mwenyewe?” (Ilitatua tatizo la wahitaji kwa wakati huo.)

 

      1.    Matendo 4:34 inasema kuwa waliomiliki viwanja na nyumba waliviuza na kuleta mapato yaliyopatikana kwa wanafunzi (mitume) ili vigawanywe upya. Hii inajenga hoja dhidi ya hali hii kuwa ya dharura. Jumuiya hii inaweza kuendelea na ufadhili wa aina hii kwa muda gani?

 

    1.    Soma Matendo 4:36-37. Tunafahamu nini kumhusu Barnaba? (Baadaye anakuwa kiongozi maarufu katika kanisa la awali. Utaona kifungu hiki kinasema kuwa yeye ni “Mlawi.”)

 

      1.    Soma Hesabu 18:20-21. Barnaba anafanya nini kwa kumiliki mali? (Baadhi ya maoni yanaashiria kwamba katazo la Walawi kumiliki mali lilishakoma.)

 

      1.    Barnaba aliuza sehemu gani ya mali yake?

 

    1.    Soma Matendo 5:1-4. Hebu tujadili maswali ambayo Petro anamwuliza anania. Ni wajibu gani alio nao anania kuuza mali yake na kuipeleka kanisani? (Kilichopo ni kwamba Anania hakuwa na wajibu wa ama kuuza kiwanja chake au kutoa mapato ya mauzo yake.)

 

      1.    Hii inatoa mwanga gani kwenye hali ya mali ya kijumuiya ambayo tumekuwa tukiijadili? (Haikuwa hitaji la Mungu au viongozi wa kanisa la awali. Hata hivyo, kwa kuishi kwa njia hii hakuna aliyepata njaa.)

 

    1.    Soma Matendo 5:5. Tatizo ni lipi? (Kusema uongo!)

 

      1.    Je, hii si adhabu iliyopitiliza kwa kusema uongo?

 

      1.    Hebu tuchimbue jambo hili kwa kina. Kitu gani kilimhamasisha Anania kusema uongo? (Unakumbuka maelezo ya Barnaba? Anania na mkewe walitaka kuchukuliwa kama watu wenye haki kama Barnabas na kila mtu aliyekuwa akishiri mali yake.)

 

      1.    Nini kingetokea kanisani kwako, nini kingekutokea, endapo adhabu ya kifo ingetolewa kwa kila mtu ambaye angejaribu kuonekana mwenye haki zaidi kuliko uhalisia wake?

 

    1.    Hebu turuke mbele na tusome Matendo 5:9 na tuilinganishe na Matendo 5:3. Kwa nini Petro anamwingiza Roho Mtakatifu kwenye jambo hili? (Sasa tumegusia tatizo halisi – kuamini kwamba Roho Mtakatifu hakuwa na uwezo kiasi cha kutokuujua ukweli.)

 

    1.    Soma Matendo 5:11. Washiriki wapya walikuwa wanaogopa nini? Kuficha vitu vyao kwa uchoyo? (Ilikuwa heshima kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kanisa lilikuwa katikati ya muda usio wa kawaida wa utendaji wa Roho Mtakatifu.)

 

      1.    Hii inatufundisha nini kuhusu kuwaongoza miongoni mwa hawa walio wadogo? (Hii inaturejesha kwenye jambo ambalo tumekuwa tukilijadili. Kwa nini umpe maskini suluhisho la muda mfupi wakati unaweza kufanya “vizuri zaidi” kwa kumruhusu Roho Mtakatifu kuponya chochote kilicho mzizi wa tatizo lao?)

 

        1.    Je, panaweza kuwepo na nia ya ubinafsi nyuma ya “kufanya vizuri zaidi” – huna haja ya kushiriki vitu vyako ikiwa Roho Mtakatifu anafanya kazi kubwa?

 

  1.   Jaribu

 

    1.    Soma 2 Wakorintho 8:7. Paulo anawaandikia waumini wa Korintho. Paulo anasifia nini kuwahusu Wakorintho? (Imani, usemi, elimu, bidii yote, na upendo.)

 

      1.    Paulo anapendekeza kuwa jambo gani linahitaji maboresho? (“Hii neema ya utoaji.”)

                          

    1.    Soma 2 Wakorintho 8:1 na 8:3-4. Paulo anauzungumzia mfano wa nani? (Watu wa Makedonia ambao walikuwa wanatoa msaada kwa ukarimu kwenye mpango wa utoaji msaada.)

 

    1.    Soma 2 Wakorintho 8:8. Hebu subiri kidogo. Paulo anawezaje kusema kwamba kuwasaidia watu wengine si “amri,” bali utoaji huthibitisha kwamba upendo wako ni wa “dhati?”

 

      1.    Je, kughushi upendo wako si dhambi? (Wafikirie tena Anania na mkewe.)

 

    1.    Soma 2 Wakorintho 8:9. Yesu anatoa mfano gani? (Kiwango cha juu kabisa cha kutokuwa na ubinafsi.)

 

  1. Baraka

 

    1.    Soma 2 Wakorintho 8:10. Paulo anatupatia “maoni” yake kwamba kuwa mkarimu kutamnufaisha mtoaji. Una maoni gani katika hili? (Soma Malaki 3:10-12. Hiki ndicho kilichopo katika Biblia yote. Ukiwa mkarimu kwa Mungu, Mungu anakuwa mkarimu kwako.)

 

    1.    Soma Matendo 4:34. Tafakari hili katika mwanga mpya. Badala ya kufikiria jinsi itakavyokuwa vigumu kutoa mali yako, jikite kwenye ukweli kwamba hakuna mtu aliyeishia kuwa “mhitaji.” Unakumbuka kwamba tulijadili kama huu utoaji wa kijumuiya ungeweza kudumu? Jibu sahihi ni lipi? (Mungu akiendelea kubariki utoaji huo unawezekana!)

 

    1.    Soma Matendo 9:36-38. Unadhani wanafunzi walifikiri kuwa Petro anaweza kufanya nini kuhusu kifo cha Dorkasi?

 

    1.    Soma Matendo 9:39-40. Endapo Dorkasi angekuwa tu mshiriki wa kawaida akaaye kwenye benchi la kanisa kila juma, unadhani Petro angeitwa? (Hapana. Dorkasi angezikwa.)

 

      1.    Biblia inamaanisha nini kwenye kisa hiki? (Ukiwa mkarimu kwa wengine, utabarikiwa. Huu ni mfano mwingine tena wa msururu wa mambo kwenye Biblia kwamba kumtii Mungu, na kumpenda jirani yako, huboresha maisha yako. Kinyume chake pia ni kweli, kutokuwa mtiifu na ubinafsi huyafanya maisha yako kuwa mabaya zaidi.)

 

    1.    Soma Mithali 11:24. Rafiki, ungependelea nini – kufanikiwa (kusitawi) au kuwa maskini? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu akuoneshe jinsi ya kuwa baraka kwa wengine?

 

  1.   Juma lijalo: Kuiishi Injili.