Somo la 2: Mpango kwa Ajili ya Ulimwengu Ulio Bora
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mara ngapi umemsikia kiongozi wa kisiasa akizungumza kuhusu namna ya kuifanya nchi yako kuwa bora katika siku zijazo? Mara ngapi umemsikia bwana mipango wa eneo lako akielezea jinsi ya kuboresha jamii yako? Somo letu juma hili linaashiria kwamba ikiwa tunataka kuwa na mustakabali bora, tunatakiwa kumwomba Mungu atuongoze. Mungu ameweka kanuni katika jambo hili, hivyo hebu tuchimbue kile ambacho Biblia inatufundisha!
- Uongozi
-
- Soma Kutoka 3:7. Mungu anasema nini juu ya kiwango anachofuatilia kile kinachowatokea watu wake? (Mungu anaona na kusikia kile kinachotutokea.)
-
- Soma Kutoka 3:8. Mungu anapendekeza nini katika kuponya mateso ya watu wake? (Atawapatia makao mapya.)
-
-
- Hebu subiri kidogo! Haya makao mapya tayari yamekaliwa watu. Vipi kuwahusu Wakaanani, Wahiti na wengineo? (Watafukuzwa.)
-
-
-
- Wakristo waliokimbia mateso Ulaya walikuja Marekani na kuwafukuza Wahindi wa asili ya Marekani. Wahindi walikuwa wapagani, si Wakristo. Je, hiki ni kitu kile kile kama kilichotokea kwenye kitabu cha Kutoka – wafuasi wa Mungu kuchukua nafasi ya wapagani wa nchi ile?
-
-
-
- Je, uchukuaji huu wa nafasi ya wakaazi wa asili unaakisi uongozi wa Mungu? Watu wengine wanapendekeza kwamba “vita vya ushindi” vinakatazwa na Mungu?
-
- Amri za Mungu
-
- Soma Mathayo 22:36. Swali hili linatoa nadharia gani? (Kwamba baadhi ya amri ni kubwa kuliko nyingine.)
-
-
- Je, unakubaliana?
-
-
- Soma Mathayo 22:37-39. Je, Yesu anakubaliana kwamba baadhi ya amri ni muhimu zaidi? (Ndiyo. Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote ndio muhimu zaidi kuliko jambo lolote.)
-
-
- Kuna matokeo gani yenye mantiki ya jambo hilo kwa mpango wa kuwa na dunia bora?
-
-
-
- Je, wazo hilo linaunga mkono utengano wa kanisa uliopindukia?
-
-
- Angalia tena Mathayo 22:39. Je, hii inamaanisha kwamba ni vyema kujipenda?
-
-
- Je, Yesu alitupenda zaidi kuliko alivyojipenda? (Ndiyo, alikufa kwa ajili yetu.)
-
-
-
- Hebu tuangalie jinsi jambo hili linavyoweza kutumika kwenye dunia salama. Je, unatumia kanuni hizi kwako binafsi – kutokuiba, kuua au kutamani?
-
-
-
-
- Ikiwa ndivyo, je, kanuni hizo zinapaswa kutumika kwa watu wengine? (Soma Mathayo 22:40. Yesu anasema kuwa amri zote (na torati na manabii) zinaakisi hizi kanuni mbili.)
-
-
-
-
-
- Je, huu ni mwongozo rahisi wa maisha: chochote ukiwazacho, jiulize kama ungependa mtu mwingine akutendee?
-
-
-
-
-
- Vipi kama tungekuwa na nchi, au dunia salama, ambayo inafuata hiyo kanuni?
-
-
-
-
-
- Hebu tuulize maswali magumu. Asubuhi ya leo nimesoma makala ya mtu aliyefanya kazi kwa bidii, akafanya chaguzi za kujikana nafsi kuhusu shule asomazo, akajitahidi kupata alama za juu ili aweze kupata ufadhili, na aliweza kupunguza mkopo wake wa shule (kwa ajili ya kugharamia masomo yake). Yuko kinyume na dhana ya kwamba wanafunzi wanapaswa kusamehewa mikopo yao na serikali. Je, anawapenda wengine kama anavyojipenda mwenyewe?
-
-
-
-
-
-
- Ikiwa msaada wa serikali (au msaada wa kanisa) unahamasisha changuzi mbaya, je, huo ni upendo?
-
-
-
-
- Soma Kutoka 20:13-17. Sehemu hii ya Amri Kumi inaelezea uhusiano wetu na watu wengine. Kuna kitu gani chenye mfanano miongoni mwa amri hizi? (Tusiwadhuru wengine.)
-
-
- Kama ungekuwa unaweka mipango ya kuwa na dunia salama, jambo hili lingebadilije sera yako ya sasa ya serikali yako?
-
-
-
- Ninaishi nchini Marekani. Asilimia moja ya watu katika daraja la juu la walipa kodi wote walilipa kodi kubwa zaidi kuliko asilimia 90 wa watu walio katika kundi la chini kabisa la ulipaji kodi kwa ujumla wao. Wale walipo katika kipato cha nusu ya kundi la chini walilipa takriban asilimia 3 ya kodi yote. (Chanzo: Tax Foundation.) Serikali pekee ndio inayofanya jambo kama hili. Ninapokwenda kula, ninapokwenda kufanya manunuzi, ninaponunua tiketi kwa ajili ya tukio fulani, kila mtu analipa kiasi kile kile ili kupata huduma ile ile. Je, sera yetu ya kodi inaendana na dhana ya kwamba tusiwadhuru wengine?
-
-
-
-
- Je, tunawadhuru matajiri kwa kuwa tu wana fedha zaidi?
-
-
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 14:22-23. Kisha soma kanuni inayotumika ikiwa iko mbali sana kwa wewe kuleta zaka yako ambapo Mungu ameelekeza: Kumbukumbu la Torati 14:25-27. Baadhi ya wasomi wanaamini hii ni “zaka ya pili,” ingawa rejea ya kuwategemeza Walawi inatilisha shaka kwenye hitimisho hilo. Hii inalinganishwaje na sera ya kodi nchini kwako? (Inaunga mkono wazo la kwamba wale wenye kipato kikubwa wanalipa zaidi. Lakini, kila mtu analipa sehemu ile ile ya kipato chake, tofauti na ilivyo nchini Marekani.)
-
-
- Nani anayenufaika na hii zaka? (Kimsingi ni yule anayeitoa. Dhana iliyopo ni kwamba kumbuka na furahia ukweli kwamba Mungu anakutunza!)
-
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 14:28-29. Huu mwaka wa tatu zaka ni kwa ajili ya manufaa ya nani? (Walawi, wageni, yatima, na wajane.)
-
-
- Je, wazo hili linavuka mipaka ya kanuni ya “usiwadhuru wengine” katika Amri Kumi? (Ndiyo. Hawa si watu ambao mtoa zaka amewadhuru. Hawa ni wahitaji.)
-
-
-
- Matokeo ya kuwasaidia wahitaji hawa ni yapi? (Mungu anawabariki wale wanaowasaidia wahitaji.)
-
-
- Hivi karibuni, nilipokuwa ninaelekea nyumbani kutokea kazini, nilimwona mtu kwenye alama ya barabarani. Alikuwa amekalia ndoo akivuta sigara huku ameshikilia bango lililoandika “nina njaa na sina makazi.” Alikuwa mdogo kuliko mimi kiumri, na alionekana kuwa na afya nzuri kimwili. Ombi lake la fedha linaendanaje na kanuni tulizoziangalia muda mfupi uliopita?
-
-
- Kimantiki unaweza kuchukulia kwamba kamwe wewe na mimi hatujamdhuru, na hakuonekana kuwa Mlawi, mgeni, au mjane. Je, “mgeni” na “mjane” ni njia nyingine tu ya kumzungumzia maskini? Au, je, hili linakusudiwa kuwa mahsusi?
-
-
-
- Amri ya Mungu ya kuwapenda wengine kama tunavyojipenda inatumikaje kwa yule mvuta sigara aliyekalia ndoo?
-
-
-
-
- Katika kutekeleza amri ya Yesu, je, tunapaswa kutilia maanani kanuni ya “usidhuru” ya Amri Kumi?
-
-
- Jubilii (Jubilee)
-
- Soma Mambo ya Walawi 25:8-10. Tukio hili, linalofanyika katika mwaka wa 50, linaanza katika Siku ya Upatanisho. Kuna upekee gani kuhusu Siku ya Upatanisho? (Ni siku ambayo watu waliwekwa huru dhidi ya dhambi zao. Angalia Waebrania 9:7.)
-
- Soma Mambo ya Walawi 25:25-28, na Mambo ya Walawi 25:35-41. Hii inafananaje na Siku ya Upatanisho? (Umekuwa kamili tena. Mali yako inarejeshwa kwako na uhuru wako unapatikana tena.)
-
-
- Hii inatuambia nini kuhusu mitazamo ya Mungu kiuchumi kwa maskini? (Mungu hapingani na mtu anayefanya makubaliano ya kuwa mtumwa au kuuza mali. Hata hivyo, uhuru na mali ya mtu haviwezi kuzuiliwa milele. Hii inaniambia kwamba Mungu anataka maskini kushikilia uwezo wao wa kujitegemeza maishani kwa uhuru.)
-
-
- Tuliruka Mambo ya Walawi 25:29-30. Isome. Kwa nini mali hii inatendewa tofauti? (Ardhi ambako unaweza kulima ni njia unayoweza kujipatia kipato cha kuishi. Watu wanaoishi kwenye miji yenye kuta huenda wanajitegemeza kimaisha kwa njia nyingine. Hivyo, Mungu anaunga mkono uhuru wa mkataba pale ambapo haiingilii kati uwezo wako wa kujipatia kipato maishani milele.)
-
- Rafiki, je, unaziweka kanuni za Biblia kivitendo sasa hivi unaposhughulika na watu wengine? Ikiwa sivyo, kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuanza kufanya hivyo leo?
- Juma lijalo: Sabato: Siku ya Uhuru.