Somo la 1: Mungu Aliumba

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mwanzo 1-3, Mithali 14)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
3
Lesson Number: 
1

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Karibu kwenye mfululizo mpya wa masomo kuhusu wajibu wetu wa Kikristo wa kuwahurumia wale wanaotuzunguka. Biblia inatoa wito wa kutumia zaidi ya njia rahisi na ya kawaida. Kumbukumbu la Torati 28 inafundisha kwamba uaminifu kwa Mungu huleta baraka za mali. Hiyo inaashiria kwamba inawezekana wale wanaohitaji msaada hawakuwa waaminifu kwa Mungu. Wakati huo huo, sheria ya Musa inajumuisha amri kadhaa kuhusu kuwasaidia wale wanaojikuta kwenye mazingira magumu kiuchumi. Hiyo inatuambia kuwa matendo mema yanaweza yasiwe kipimo cha kutoa msaada. Kisa cha Ayubu na Waebrania 11 kinabainisha kwamba si mara zote kanuni za jumla zinatumika. Sabato iliyopita nilisikiliza hubiri lililohusu kisa cha Yesu kuhusu mwana mpotevu (Luka 15:11-32). Nilifikiria juu ya mfululizo huu wa masomo niliposikia Luka 15:16 – “hapana mtu aliyempa [mwana mpotevu] kitu” alipokuwa na njaa. Matokeo yake, katika Luka 15:17, ni kwamba mwana mpotevu “alizingatia moyoni mwake.” Je, mwana mpotevu angerejea nyumbani endapo mtu mmoja mwema angemsaidia katika uasi wake kwa kumpatia chakula? Hebu tuanze uchimbuzi wetu juu ya kile ambacho Biblia inakifundisha kuhusu wajibu wetu wa kuwa na huruma!

 

  1.    Uumbaji

 

    1.    Soma Mwanzo 1:26. Kifungu hiki kinasema kuwa kwa nini Mungu aliwaumba wanadamu? (Aliwaumba ili wawe watawala wadogo. Walifuatia baada ya Mungu, na wakatawala chini ya mamlaka yake.)

 

      1.    Wajibu wao ulikuwa ni upi? (Kuwatawala wanyama.)

 

    1.    Soma Mwanzo 1:27-28. Mungu aliwapa wanadamu uwezo gani mwingine? (Uwezo wa kuumba. Amri ilikuwa ni kuwaumba wanadamu wengine, kuijaza na kuitiisha nchi, na (Mungu anarudia) kuwatawala wanyama.)

 

      1.    Fikiria kwamba umeajiriwa kazi mpya na hayo ndio maelekezo ya kazi yako. Inamaanisha nini “kuijaza” dunia na “kuwatawala” wanyama? (Hayo ni mamlaka makubwa sana, na wajibu wa pekee.)

 

        1.    Dunia kamilifu inahitaji nini ili “kujazwa?” (Kwa kuwa dunia kamilifu isingekuwa kwenye uasi, nadhani inamaanisha kwamba wanadamu wangependelewa zaidi ya wanyama. Kama wangekuwa kwenye mtafaruku, wangetakiwa kufungua njia kwa wanyama.)

 

      1.    Tafakari tatizo hili ili kujaribisha njia yako kwenye jambo hili. Ikiwa wanadamu walihitaji mavazi ili kujihifadhi na kujipatia joto, je, utamuua mnyama na kutumia ngozi yake? Au, ungetangaza amri kwamba hakuna mnyama ambaye angeweza kudhuriwa kwa manufaa ya mwanadamu? (Angalia Mwanzo 3:21.)

 

    1.    Soma Mwanzo 2:15. Je, wanadamu walikuwa na wajibu wa kuwa baraka kwa nchi?

 

      1.    Je, ungejisikiaje kuwa na wajibu, kama mtawala, kutenda kilicho sahihi?

 

      1.    Unadhani wanadamu walikuwa wanafanya nini katika “kuilima” bustani?

 

        1.    Hiyo inatofautianaje, kama tofauti ipo, na “kuitunza” bustani ambayo waliishimo?

 

    1.    Soma Mwanzo 2:16-17. Hebu tuanze na shauri kwamba Mungu ana wajibu wa kuwatunza wanadamu kama wanadamu walivyo na wajibu wa kuwatunza wanyama na kuitunza nchi. Kwa nini Mungu aruhusu mti wa hatari kiasi hicho – mti uliokuwa na simu – uwepo bustanini?

 

      1.    Fikiria njia nyepesi: hebu tupige kura kama tunapaswa kuruhusu mti bustanini ulio na tunda lenye sumu? (Jambo sahihi si mara zote jambo la dhahiri kwa juujuu. Suala hili ni tatanishi.)

 

  1.   Utata wa Dhambi

 

    1.    Soma Mwanzo 3:1-5. Nyoka anapendekeza nini kumhusu Mungu? (Hasemi ukweli, kwa sababu anataka wanadamu wasipate taarifa muhimu.)

 

      1.    Utaona nyoka anatoa fursa ya “kuwa kama Mungu.” Eva alipaswa kusema nini kuhusu hilo? (Tayari alikuwa kama Mungu. Alikuwa mtawala.)

 

    1.    Soma Mwanzo 3:6. Walikuwa na matunda mengine mengi sana kwa ajili yao, kwa nini atake tunda “zuri” zaidi lililopendeza? (Nadhani kauli hii inahusiana na kauli yake ya uongo (Mwanzo 3:3) kwamba wasingeweza kuligusa tunda. Hamasa ya kweli ilikuwa ni ya “kupata maarifa.”)

 

      1.    Eva alipogusa tunda, lakini hakufa, hiyo ilikuwa na madhara gani kwenye uamuzi wake wa kula tunda? (Ilimhamasisha kulila. Naamini hii ndio sababu Kumbukumbu la Torati 4:2 inatuambia tusiwaambie watu kwamba jambo fulani ni dhambi wakati kiuhalisia si dhambi. Ni sawa na kuwaambia watu jambo fulani si dhambi ilhali ni dhambi. Nilipokuwa mdogo, nilifundishwa kwamba sipaswi kuingia kwenye ukumbi wa sinema kwa sababu malaika wangu asingeweza kuingia. Kile ambacho ningepaswa kufundishwa ni kuwa makini juu ya kile nilichokiruhusu kunishawishi.)

 

    1.    Soma Mwanzo 3:14. Ni kwa msingi gani Mungu Mtawala wetu alimlaani nyoka?

 

      1.    Je, hii iko ndani ya mipaka ya kuwatawala wanyama?

 

    1.    Soma Mwanzo 3:16. Utakumbuka kwamba mojawapo ya wajibu wa uumbaji-mdogo ilikuwa ni kuumba wanadamu wengine. Mungu anasema nini kwenye hili badiliko katika mazingira ya mtoto kuzaliwa?

 

      1.    Adamu na Eva wote wawili walitenda dhambi. Kwa nini adamu anapewa wajibu wa kipaumbele katika kufanya uamuzi? (Ukipitia “taarifa baada ya kitendo’ kwa Mungu katika Mwanzo 3:12-13, utaona kwamba Eva anasema kuwa nyoka alimdanganya na Adamu alisema Eva alimpa tunda. Maelezo haya yanaweka tuhuma ndogo kwa Adamu.)

 

    1.    Soma Mwanzo 3:17-19. Utawala wa wanadamu kwa nchi umebadilikaje? (Chakula si tena tunu na starehe. Sasa ni uchungu kutafuta chakula.)

 

      1.    Tafakari hili katika mtazamo wa “wajibu wa mwanadamu kwa nchi.” Hapo awali, mimea ilikuwa chini ya udhibiti wa wanadamu kabisa. Inaonekana wanadamu walikuwa na wajibu wa usimamizi kwa mujibu wa vifungu tulivyovisoma hapo kabla. Sasa, mimea haina ushirikiano. Inaleta upinzani. Kupata chakula kunatokana na jasho na uchungu. Kutokana na kwamba sasa mimea ni viumbe waasi, je, hii inabadili asili ya wajibu wetu wa usimamizi?

 

        1.    Nani ana hatia katika badiliko hili?

 

      1.    Tafakari suala hili katika mtazamo wa utawala. Kila kitu kimekuwa kigumu. Unadhani kwa nini Mungu alifanya hivi? Je, lilikuwa ni jambo lililotokea “moja kwa moja” kutokana na kuingia kwa dhambi? Je, ilikuwa ni adhabu kwetu? Je, ilikuwa tu ni kushiriki matatizo tuliyoyasababisha, kwa sababu sasa Mungu alikabaliana na matatizo mengi zaidi na nchi?

 

  1. Pamoja Katika Hili

 

    1.    Soma Mithali 22:2 na Mithali 14:31. Unaona kanuni gani kutokana na hivi vifungu viwili? (Mungu ni Muumbaji wetu, bila kujali kama sisi ni matajiri au maskini. Hiyo inamaanisha tuna wajibu kwa wanadamu wengine.)

 

    1.    Hebu tuangalie kwa ukaribu zaidi Mithali 14:31. Kwanza, tunaamriwa “tusiwakandamize” maskini. Hebu turejee kwenye utangulizi wetu. Kama mwana mpotevu angekuwa katika eneo lako, na akawa na njaa wakati akiwalisha nguruwe, je, “ungemkandamiza” kwa kumwacha peke yake? (Ukandamizaji wake ulitokana na uamuzi wake mwenyewe. Kwa kuzingatia kwamba siifanyi hali yake kuwa mbaya zaidi, ni vigumu kuona jinsi ninavyomkandamiza.)

 

      1.    Hebu tuangalie nusu ya pili ya Mithali 14:31. Pia tunaambiwa kwamba ikiwa tutawahurumia wahitaji, “tunamheshimu” Mungu. Je, kumheshimu Mungu ni suala la hiari?

 

      1.    Je, kuwa na huruma kunahitaji uamuzi fulani kwa upande wetu? Kwa mfano, kama tunamlisha mwana mpotevu mwenye njaa kiasi kwamba kamwe haguswi kurejea kwa baba yake, je, tunakuwa “wema” kwake?

 

        1.    Jibu lako linaashiria nini kuhusu hitaji la kuwafahamu watu unaofikiria kuwasaidia?

 

    1.    Rafiki, nadhani tunaweza kuanza kuona kwamba wajibu wetu kwa dunia na kwa watu wengine si jambo la miito myepesi (simple slogans) na fikra nyepesi-nyepesi. Tunatakiwa kumwomba Roho Mtakatifu atusaidie kuyaelewa mapenzi ya Mungu linapokuja suala la kuonesha huruma. Je, utafanya hivyo sasa hivi?

 

  1.   Juma lijalo: Mpango kwa Ajili ya Ulimwengu Ulio Bora.