Wimbo wa Kifalme wa Mapenzi
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Moja ya “majira ya familia” ni huruma. Hivyo ndivyo tunavyopata familia, sawa? Juma hili tunajifunza raha na ukomo wa huruma. Kuna jambo la kufurahisha zaidi ya hilo? Hebu tuzame kwenye Biblia na tuone kile inachotufundisha!
- Huruma
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 1:1-2. Busu lina uzuri gani? (Ni bora zaidi ya divai.)
-
-
- Kitabu cha Wimbo Ulio Bora kinaposema “upendo” unafurahisha zaidi ya divai, je, kinazungumzia kuhusu upendo au kinaelezea busu? (Busu ni kielelezo cha upendo.)
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 1:3. Nani amejipulizia manukato? (Mwanaume.)
-
-
- Kwa nini harufu inabainishwa? (Upendo unahusisha mguso wa busu na raha ya harufu nzuri.)
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 1:10. Mikufu inaonekanaje kwenye maelezo ya Biblia juu ya urembo? (Hii inaashiria kwamba inamfanya mtu aonekane mrembo zaidi.)
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 1:12-14. Nani mwingine amejipulizia manukato? (Mwanamke.)
-
-
- Mwanaume anazungumziwa kama “manemane iliyolazwa maziwani mwangu” na “kishada cha hina kilichochanua.” Unapojipulizia manukato mapya, je, unakuwa unasikia harufu yake siku nzima? (Kwa kawaida, marashi mapya yanatoa harufu siku nzima. Mwanamke anakuwa na ufahamivu na mwanaume muda wote.)
-
-
-
-
- Tunapata fundisho gani kutokana na hili? (Tunapaswa kuwawaza wapendwa wetu!)
-
-
-
-
- Hii inafanyaje kazi kwenye ndoa? Je, unaendelea kubusu? Je, unamuwaza mwenzi wako siku nzima? Je, hayo ni mawazo mazuri, kama yale ya maua? Je, bado unafanya hivi baada ya miongo ya kuwa kwenye ndoa?
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 1:15-16. Tunaona ushauri gani mzuri hapa? (Mwambie mwenzi wako kwamba amependeza!)
-
-
- Zingatia sehemu ya mwisho ya kifungu cha 16. Je, maneno ya “kitanda chetu ni majani” yanamaanisha nini? Kwamba una mashuka ya kijani? (Kitu kilicho chanikiwiti kinasitawi na kina uhai. Hii haimaanishi kwamba unalala na wanyama wako vipenzi (pets) au kwamba kamwe hufui mashuka yako. Inamaanisha kwamba yafanye maisha yako ya upendo yawe mabichi.)
-
- Hali ya Uchanya (Positivity)
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 5:9. Umewahi kujiuliza jambo hili kuhusu mwenzi wako?
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 5:10-11 na Wimbo Ulio Bora 5:13-15. Je, kweli kichwa chake kinafanana na dhahabu na kiwiliwili chake kimenakishiwa kwa yakuti samawi? (Kimsingi hapana, ilimradi yeye ni mwanadamu.)
-
-
- Kwa hiyo, kitu gani kinazungumzwa? (Mwanamke huyo anatoa maelezo ya kupendeza kupita kiasi kwa mwanaume huyo.)
-
-
-
- Akina dada mnapokutana pamoja, na kuwajadili waume wenu, je, mnatoa maelezo mengi kupita kiasi jinsi walivyo wazuri au mnatoa maelezo mengi kupita kiasi juu ya kasoro zao?
-
-
-
-
- Vipi kuhusu nyie, waume, mnawazungumziaje wake wenu?
-
-
-
-
-
- Kuelezea matatizo yako kunaifanyia nini akili yako? (Kunaimarisha mtazamo hasi. Unapaswa kuzungumza mambo chanya kumhusu mwenzi wako.)
-
-
-
- Soma Mwanzo 4:1. Tafsiri ya NIV inazungumzia “kulala” na mkeo na tafsiri ya NKJV inazungumzia “kumjua” mkeo. Neno msingi la Kiebrania linamaanisha kujua kwa kuona. Kwa nini kujamiiana kunaelezewa kama “kujua?” (Ni urafiki wa karibu sana (intimacy). Hakuna siri tena.)
-
-
- Nilikuwa nikisoma juu ya habari za “ndoa za wazi,” ikimaanisha kwamba wenzi wanaruhusiana kufanya ngono na watu wengine. Siku hizi ni nadra sana kusoma habari hizi. Ikiwa aina hizi za ndoa zinapotea, ni kwa nini? (Inafanya kosa la kudhani kwamba unaweza “kumjua” mtu kwa ukaribu sana bila kubadilishwa. Kwa ujumla ndoa hizo hazidumu.)
-
-
-
- Soma Mwanzo 2:24-25. Upande chanya wa “kumjua” mwenzi wako ni upi? (Hii ni sehemu ya kuwa “mwili mmoja.” Kujamiiana huwaleta pamoja. Husitawisha ndoa na kuifanya iwe na afya. Hiyo ndio sababu uzinzi unararua uhusiano wa ndoa.)
-
- Muda Mwafaka
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 8:1-2. Anataka nini ili aweze kumtendea [mwanamke]? (Kumbusu.)
-
-
- Tatizo ni lipi? (Jamii. Utamaduni hautaidhinisha. Lakini, kama angekuwa kaka wake, anasema hakuna ambaye angefikiria jambo lolote kuhusu suala hili.)
-
-
-
- Tunajifunza nini? (Kuna vizingiti vya nyakati, mahali, na uhusiano kwenye uhusiano wa karibu sana na watu wengine.)
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 8:4. Hii inatuambia nini kuhusu muda mwafaka? (Wale ambao bado hawajaoa/hawajaolewa wanaweza na wanapaswa kudhibiti suala la muda. “Kuyaamsha mapenzi” muda usiofaa ni hatari.)
-
-
- Utamaduni mpya nchini Marekani unasema kwamba hii si kweli, kwamba vijana hawawezi kujidhibiti pale “wanapoyaamsha” mapenzi. Unasemaje? (Utamaduni mpya hautaki kuashiria suala la udhibiti. Nilipokuwa mdogo hapakuwepo na akina mama wasio kwenye ndoa, na ilikuwa nadra sana kuwa mjamzito dhahiri kabla ya ndoa. Hiyo haikutokana na matumizi mazuri ya njia za kudhibiti mimba, na si kwa sababu ya utoaji mimba. Badala yake, ulikuwa ni “udhibiti” uliosababishwa na shinikizo la jamii.)
-
-
-
- Je, “udhibiti” unatofautiana ndani ya kanisa? (Bi harusi mpya alimtaarifu mke wangu kwamba alijamiiana kabla ya ndoa, na kwamba kila mtu alifanya hivyo. Hii inaashiria kwamba mtazamo umebadili kabisa uelekeo ndani ya kipindi cha kizazi kimoja.)
-
-
-
- Kutokuwepo kwa baba kunafanya nini kwenye “majira ya familia?” (Kamwe mtoto hana uzoefu sahihi wa kuwa na uhusiano na baba.)
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 8:8. Nani anazungumza hapa? (Maumbu.)
-
-
- Wanataka kufanya nini? (Kumsaidia mdogo wao wa kike kujiandaa kwa ajili ya ndoa.)
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 8:9. Umbu mdogo ana uchaguzi gani? (Kuwa ukuta au mlango. Ama atakubali au atakataa kujamiiana kabla ya ndoa.)
-
-
- Matokeo yanabadilikaje kutokana na uamuzi wa umbu? (Ama ni “mnara” wenye “fedha,” au “amehifadhiwa” kwenye eneo dogo.)
-
-
-
-
- Unadhani hii inamaanisha nini? (Nadhani moja inazungumzia majivuno na mali wakati nyingine inazungumzia uchaguzi wenye ukomo.)
-
-
-
- Soma Wimbo Ulio Bora 8:10. Umbu mdogo anachukua uamuzi gani? (Yeye ni “ukuta.” Hajamiiani kabla ya ndoa.)
-
-
- Hilo linamuathirije mwenzake wanayetaka kufunga naye ndoa? (Hilo linasababisha ushindani.)
-
-
-
-
- Kwa nini hilo ni kweli? (Hawalinganishwi na watu wengine.)
-
-
- Mtazamo wa Mungu
-
- Soma Mambo ya Walawi 20:10. Uzinzi ni mbaya kiasi gani machoni mwa Mungu?
-
- Soma Mambo ya Walawi 20:13. Dhambi gani inaelezewa hapa? (Kujamiiana wanaume kwa wanaume (ushoga).)
-
-
- Dhambi hii ni mbaya kiasi gani machoni mwa Mungu? (Kama ilivyo kwa uzinzi, ni dhambi yenye adhabu ya kifo.)
-
-
-
- Angalia kauli ya, “damu yao itakuwa juu yao.” Hiyo inamaanisha nini? (Nadhani inamaanisha kuwa wamefanya uchaguzi mbaya. Mungu anauchukulia kama uchaguzi.)
-
-
- Soma Mambo ya Walawi 20:22-24. Hii inatufundisha nini kuhusu utamaduni mpya? (Utamaduni mpya una viwango tofauti na vile vya Mungu. Mungu anauchukia sana utamaduni huu.)
-
-
- Hakuna utamaduni wa kisasa wa kimagharibi unaotekeleza hukumu ya kifo kwa kosa la uzinzi na ushoga. Tunapaswa kujali jambo gani kuhusu mtazamo wa Mungu? (Hukumu ya Mungu kwenye mambo haya ni ya mwisho.)
-
-
- Je, hivi ni viwango tu vya Agano la Kale? (Soma Warumi 1:26-27 na 1 Wakorintho 6:9-10. Mtazamo wa Mungu ni ule ule katika Agano Jipya. Kama una muda, soma Warumi 1. Inafuatisha maendeleo ya dhambi, na hilo lina mafunzo ya kufurahisha.)
-
- Rafiki, Mungu alibuni ngono. Anatuambia kwamba mahaba na ngono ni vitu vizuri sana. Hata hivyo, Mungu anaweka vipimo vya muda na namna ya kuendana navyo. Je, utachukua uamuzi, sasa hivi, kwa msaada wa Roho Mtakatifu, kuyatii mapenzi ya Mungu kwenye mada hii?
Juma lijalo: Mambo Muhimu Katika Kuwa na Umoja wa Familia.