Somo la 10: Umoja na Uhusiano Uliovunjika

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Filemoni 1, Mathayo 18)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
4
Lesson Number: 
10

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.                           

 

Utangulizi: Unashughulikiaje uhusiano uliovunjika miongoni mwa washiriki wenzako wa kanisa? Je, unawaepuka tu hao washiriki wa kanisa? Je, unajaribu kupatana nao? Je, unajitahidi kutofikiria jambo hilo? Somo letu juma hili linahusu jitihada za kuponya uhusiano uliovunjika. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza!

 

  1.    Filemoni na Onesimo

 

    1.    Soma Filemoni 1:1-3. Paulo yupo wapi anapoandika barua hii? (Ni mtumwa wa Rumi. Kiyunani kinaashiria kwamba Paulo amefungwa mnyororo.)

 

      1.    Soma Waefeso 1:1. Hapa Paulo anajitambulishaje? (Anasema kuwa yeye ni “mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu.”)

 

        1.    Kwa nini Paulo anatumia utambulisho tofauti kabisa katika kitabu cha Filemoni? Badala ya kusema kuwa yeye ni “mtume wa Yesu” anasema kuwa ni “mtumwa” aliyefungwa mnyororo? (Tutaona kwamba Paulo anaandika kwa niaba ya mtumwa aliye mafichoni aitwaye Onesimo. Kwa kuanza na njia hii, Paulo anajinasibisha na Onesimo.)

 

    1.    Soma Filemoni 1:4-7. Tunajifunza nini kuwahusu Filemoni, Afia, Arkipo na kanisa la nyumbani kwao? (Ni watu wema.)

 

      1.    Je, wana uhusiano? (Barua haibainishi wazi uhusiano uliopo kati ya Filemoni, Afia na Arkipo. Inawezekana kwamba Afia ni mke wa Filemoni na Arkipo ni mwana wao. Kwa kuwa Paulo anasema kuwa kanisa linakusanyika nyumbani kwao (Filemoni 1:2), kuna uwezekano mkubwa kwamba wana uhusiano wa namna fulani. Kwa kurahisisha mambo, nitakuwa tu ninamrejea Filemoni kuanzia sasa.)

 

    1.    Soma Filemoni 1:8-11. Sasa tunyumbilishe jambo hili. Kwanza, Paulo anasema kuwa angeweza kumwagiza Filemoni naye angefuata aliloagizwa, badala yake anamsihi kwa upendo. Utakuwa na mwitiko gani kwenye kauli kama hiyo? (Hii inaakisi namna Paulo anavyoanza kuandika barua yake kwa kusema kuwa yeye ni mfungwa, badala ya kwamba ni mwakilishi wa Mungu.)

 

      1.    Paulo alikutanaje na Onesimo? (Onesimo aliongolewa kwenye Ukristo Paulo alipokuwa mfungwa.)

 

      1.    Paulo anasema kuwa hapo awali Onesimo hakuwa na maana yoyote kwa Filemoni. Hiyo inatuambia nini kuhusu Onesimo mfungwa? (Alikuwa muasi, au mvivu au vyote viwili.)

 

        1.    Unadhani Onesimo alikutanaje na Paulo, ukizingatia kwamba Paulo alikuwa mfungwa? (Inawezekana mara ya kwanza Paulo alikutana na Onesimo alipokuwa anamtembelea Filemoni na Onesimo akiwa mtumwa wa Filemoni.)

 

    1.    Soma Filemoni 1:12-16. Filemoni anahitaji kufanya uamuzi gani kumhusu Onesimo? (Endapo atabaki na Onesimo au kumrudisha kwa Paulo.)

 

      1.    Ikiwa Filemoni atabaki na Onesimo, tunapaswa kumtendeaje? (“Kama ndugu mpendwa katika Bwana.”)

 

    1.    Somo letu linahusu kurekebisha uhusiano uliovunjika. Unadhani Filemoni alijisikiaje kumhusu Onesimo kabla hajasoma barua hii? (Nina uhakika Filemoni alilipa fedha kwa ajili ya Onesimo, na hivyo kudhani kwamba Onesimo alikuwa amemwibia. Ukweli kwamba Paulo anasema kuwa hapo awali Onesimo hakuwa mtu wa “maana,” inaashiria kuwa tayari Filemoni alikuwa na maoni hasi kumhusu Onesimo. Kuwekeza kwa Onesimo ilikuwa uwekezaji mbaya.)

 

    1.    Unadhani Onesimo alijisikiaje kumhusu Filemoni? (Ni vigumu katika utamaduni wetu, ambapo kwa pamoja utumwa unachukuliwa kuwa ni kitendo haramu na kinyume na maadili, tunapojiweka kwenye nafasi ya Onesimo. Lakini, tunaweza kuwa na uhakika kuwa alichukia kuwa mtumwa. Bila shaka ndio sababu kutokuwa mtu wa “maana” ilikuwa sehemu ya uasi wake dhidi ya hadhi yake. Kama Mkristo, alidhani kuwa utumwa ni kinyume na maadili.)

 

    1.    Kutokana na hili tunaweza kuhitimisha kwamba Filemoni alipoanza kusoma barua hii, alikuwa na hasira dhidi ya Onesimo na Onesimo alikuwa na chuki na hali ya uasi dhidi ya Filemoni. Paulo anawapatanishaje hawa watu wawili? Anatumia mbinu gani? (Nitauita huu kama wito mkubwa wa kupenda. Paulo “hamlazimishi” (kifungu cha 14) au “kumwagiza” (kifungu cha 8) Filemoni kupatana na Onesimo, lakini anataja huo uwezekano wakati akitoa wito wake uliojengwa juu ya upendo.)

 

      1.    Je, unadhani kwamba Paulo alimwendea Onesimo na kumtaka arejee bila kuwa na uhakika kwamba Filemoni atamtendea vizuri? (Paulo anamwambia Filemoni kwamba hata kama ataendelea kubaki na Onesimo, hawezi kuendelea kumtendea kama mtumwa kwa sababu sasa yeye ni “ndugu katika Bwana.”)

 

    1.    Soma Filemoni 1:17-21. Kwa mara nyingine, Paulo anajenga hoja yake juu ya sababu ya Filemoni kutakiwa kumtendea Onesimo vizuri. Hii inakuambia nini juu ya uhakika wa Paulo kwamba Filemoni atafanya kile anachokiomba? (Inaonekana kwamba Paulo hana uhakika.)

 

      1.    Unapoviangalia vifungu hivi, unaona kuwa Paulo anajenga hoja gani? (Kwanza anatoa wito kwake kama Mkristo – “kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe.” Baadaye Paulo anamwambia Filemoni kuwa anataka kuwa na “faida kwako katika Bwana.” Angalia jinsi jambo hili linavyobadili upepo. Filemoni anatakiwa kupata manufaa kutoka kwa Onesimo! Kisha Paulo anatoa fedha kwa Filemoni kwa ajili ya madhara yoyote yanayoweza kuwa yamesababishwa na Onesimo. Mwisho, Paulo anatoa wito wa “utii” kwa upande wa Filemoni.)

 

    1.    Soma Filemoni 1:22. Kwa nini Filemoni ahitaji kuandaa mahali pa kukaa wakati Paulo ni mtumwa? (Sidhani kama hili linahusiana na maandalizi ya mahali pa kukaa, nadhani ni ujumbe kwa Filemoni kwamba Paulo anaweza kufuatilia jinsi anavyomtendea Onesimo.)

 

    1.    Unapotafakari hoja za Paulo, je, kuna hoja zozote zisizofaa kwa ajili ya kuwapatanisha washiriki wa kanisa leo?

 

  1.   Wewe na Mtu Mwingine

 

    1.    Soma Mathayo 18:15. Hebu tuangalie kifungu hiki kwa undani zaidi. Kwanza, kundi gani linazungumziwa kama wadhambi watarajiwa? (Washiriki wa kanisa. Matumizi ya neno “ndugu” yanamaanisha kuwa Yesu hauzungumzii ulimwengu.)

 

      1.    Pili, asili ya tatizo ni ipi? (Dhambi ndio inayozungumziwa. Bila shaka ndio maana kuna mambo mengi yanayoweza kutufanya tusiwe na furaha yasiyo dhambi dhidi yetu.)

 

      1.    Tatu, ni nini asili ya tatizo? Jambo gani “linatatuliwa?” (Sio tu “dhambi,” bali mtu aliye kinyume nawe binafsi.)

 

      1.    Tuseme kwamba nimesoma kauli au hoja iliyochapishwa ambayo ina makosa. Je, hiyo ni dhambi dhidi yangu? (Hapana, ni hadi pale itakaponitaja kwa namna yenye nia mbaya.)

 

        1.    Je, niko huru kuandika kauli kwa umma ikisema kwamba nadhani kauli au makala ina makosa? (Ndiyo. Hii haizungumzii kutokubaliana katika mabishano ya wazi.)

 

    1.    Hebu tuangalie nusu ya mwisho ya Mathayo 18:15. Lengo la Yesu ni lipi? (Kuliweka tatizo baina yenu wawili.)

 

    1.    Soma Mathayo 18:16. Vipi kama ndugu yako anakuwa msikivu, lakini hakubaliani nawe? Bado utawaleta watu wengi kwenye kikao? Unadhani lengo la kuwaleta watu wengine ni lipi? Je, ni ili tu kumshawishi “mdhambi?” (Kwa uzoefu wangu ni kwamba mtu anayeamini kuwa yeye ni mwathirika, anaweza asiwe sahihi. Kama huwezi kuwatafuta watu wengine waambatane nawe, inawezakuwa ni kwa sababu wao pia wanadhani kuwa wewe si mwathirika.)

 

      1.    Kifungu kinaposema kuwa, “ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike,” hiyo inamaanisha nini? (Mara nyingi kweli zenye mgongano huwa zina ubishani. Hii inasaidia kuhakikisha kwamba mtu anayetuhumiwa na mdhambi wanapokutana, mabishano ya kweli yatashughulikiwa na kutatuliwa.)

 

    1.    Soma Mathayo 18:17. Hadi kufikia hapa, je, kuna makubaliano ya jumla kuhusu dhambi? (Ndiyo. Unapoleta pamoja makundi makubwa, wakikubaliana na mwathirika, inaonesha kwamba mdhambi ana makosa.)

 

      1.    Utamtendeaje mpagani au mtoza ushuru? Kuwafukuza kanisani?

 

    1.    Ili kupata muktadha, soma Mathayo 18:12-13, inayotoa kauli ya utangulizi. Je, mpagani na mtoza ushuru ni sawa na kondoo aliyepotea?

 

    1.    Ili kupata muktadha zaidi, soma Mathayo 18:18, kifungu kinachofuatia kisa chetu. Kuna uzito gani ikiwa kanisa litamfungia mtu ushiriki wa kanisa? (Kwa upande mmoja, tunaambiwa kwamba Yesu anawakimbilia wale wanaoliacha kundi (nasi tunapaswa kufanya vivyo hivyo), na kwa upande mwingine, Yesu anawaambia wanafunzi wake (Mathayo 18:1) kwamba maamuzi yao ya hapa duniani yana matokeo ya kimbingu.)

 

      1.    Unadhani kwamba kufungiwa au kufunguliwa inazungumzia uzima wa milele? (Wanadamu hawana uamuzi wa uzima wa milele kwa wenzao.)

 

    1.    Soma Mathayo 18:35. Kama una muda, soma Mathayo 18:21 ili kupata muktadha zaidi. Yesu anatoa kauli gani ya mwisho kuhusu migogoro kati ya washiriki wa kanisa wenzako? (Kwamba tunapaswa kusamehe kwa sababu Mungu ametusamehe zaidi na zaidi.)

 

    1.    Rafiki, ikiwa una mgogoro na ndugu mwingine kanisani kwako, je, utaongozwa na somo la leo ili kuutatua mgogoro huo?

 

  1. Juma lijalo: Umoja Katika Ibada.