Uzoefu wa Umoja Katika Kanisa la Awali

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Matendo 1-5, 2 Wakorintho 9)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
4
Lesson Number: 
5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Unapotaka kutekeleza jukumu fulani, je, unaangalia jinsi watu wengine walivyolitekeleza katika siku za nyuma? Au, je, unaangalia mawazo bunifu yanayoweza kukusaidia kulitekeleza jukumu hilo vizuri zaidi? Inaonekana kwamba mara kwa mara huwa tunapuuzia mafundisho yanayotokana na historia. Juma hili somo letu linahusu mchanganyiko wa uwezo, utajiri, na umoja katika kanisa la awali. Tunaweza kujifunza nini kutokana na historia? Hebu tuchimbue Biblia yetu na tuone kile tunachoweza kujifunza!

 

  1.    Mfarakano

 

    1.    Soma Matendo 1:3-6. Wanafunzi wanataka nini? (Wanataka Israeli iwe na uwezo wa kisiasa na kijeshi kiasi cha kuuangusha utawala wa Rumi.)

 

    1.    Soma Matendo 1:7-9. Je, huo ndio ujumbe ambao Yesu anawataka wausambaze baada ya yeye kurejea mbinguni?

 

    1.    Zingatia Matendo 1:8. Wanaomba uwezo wa kisiasa na kijeshi. Yesu anazungumzia uwezo gani kwenye jibu lake? (Yesu anazungumza nao kwa kuzingatia uwezo halisi: uwezo wa Roho Mtakatifu.)

 

      1.    Hii inaashiria nini juu ya Roho Mtakatifu na umoja? Yesu na wanafunzi wake hawakuwa wameunganishwa katika lengo lao. (Roho Mtakatifu ndio nguvu iliyo nyuma ya umoja katika Kanisa.)

 

      1.    Roho Mtakatifu alikuwa wa muhimu kiasi gani katika hali hii? (Kama ningekuwa Yesu, ningeghafirishwa na kuhuzunika sana kwa swali hili. Ni kana kwamba wanafunzi hawajajifunza chochote. Yesu anamtegemea Roho Mtakatifu ili kutatua tatizo hili zito.)

 

        1.    Je, somo hili ni muhimu kwa mifarakano inayotokea leo?

 

  1.   Njia ya Kuuelekea Umoja

 

    1.    Soma Matendo 1:12-14. Mada ya maombi yao ni ipi? (Kwa kuwa Yesu aliwaambia katika Matendo 1:4-5 kwamba wanapaswa kuusubiri ubatizo wa Roho Mtakatifu, nadhani hiyo ndio mada ya dhahiri ya maombi yao.)

 

    1.    Soma Matendo 2:1-4. Kwa nini kelele, upepo na moto ni vya muhimu? (Tafakari kuwepo mahali pale! Hii ni nguvu kubwa sana. Uvumi wa upepo wa nguvu ni uwezo mkubwa. Moto ni nguvu. Walihitaji uwezo (nguvu) na Yesu aliwapatia – lakini kwa namna tofauti na walivyotarajia.)

 

      1.    Je, wangepaswa kutarajia uwezo wa aina hii? (Tafakari uwezo alioutumia Yesu wakati alipokuwa pamoja nao duniani. Huu ndio uwezo alioutumia Yesu. Wanafunzi ndio kwanza walikuwa wanaanza kuelewa somo hili.)

 

    1.    Soma Mwanzo 11:5-7. Utakumbuka hivi karibuni tulijadili kisa cha Mnara wa Babeli. Tulijifunza kwamba waliungana ili kumpinga Mungu. Mungu anasema nini hapa kuhusu uwezo wa lugha moja? (Hakuna kitakachoshindikana.)

 

      1.    Je, unaona uhusiano uliopo kati ya Pentekoste na Mnara wa Babeli? (Mungu anageuza kile alichokifanya. Mara hii umoja unatafutwa ili kuutangaza Ufalme wa Mungu.)

 

      1.    Kwa nini leo wamisionari wanatakiwa kujifunza lugha za kigeni?

 

    1.    Viambato vya uwezo na umoja katika kanisa la awali vilikuwa ni vipi? (Tamaa ya kuwa na uwezo. Ombi la kuwa na uwezo wa Roho Mtakatifu. Kuwasili kwa uwezo huo.)

 

      1.    Ikiwa tuna mgogoro mkubwa Kanisani, je, huo ni uthibitisho kwamba tunapungukiwa uwezo wa Roho Mtakatifu?

 

  1. Kuulinda Umoja

 

    1.    Soma Matendo 4:32-35. Umoja ulikuwa na mizizi mirefu kiasi gani? (Ulifikia hadi kwenye mifuko yao!)

 

    1.    Soma Matendo 4:36-37. Je, baadaye Barnaba anakuwa mtu wa muhimu katika kazi ya kanisa? (Naam, hakika! Tulijifunza habari zake kwenye mfululizo wa masomo yetu uliopita.)

 

    1.    Soma Matendo 5:1-2. Je, ni sahihi kuzuia sehemu ya fedha zako?

 

      1.    Baaddhi ya watu wanabainisha tatizo hapa kama “tamaa/uchu.” Je, unaweza kutamani kitu ambacho tayari ni chako?

 

    1.    Soma Matendo 5:3-4. Tatizo ni lipi? (Kwamba Anania na Safira walidanganya.)

 

      1.    Kwa nini walidanganya? (Walitaka waonekane kuwa na wao ni wakarimu kama Barnaba! Kilikuwa kitendo cha kuwasilisha tabia isiyo yao. Huenda hapa ndipo tamaa inapojitokeza - walitamani kuwa na hadhi kama ya Barnaba.)

 

      1.    Petro anawezaje kusema kuwa Anania alimdanganya Mungu? (Sote tunafahamu kwamba Mungu anajua kila kitu. Mungu hakulaghaiwa kwa kitendo hiki.)

 

        1.    Kama kiuhailisia haiwezekani kumdanganya Mungu, je, Petro anamaanisha nini? (Anania hakuwa na uelewa sahihi juu ya uwezo wa Mungu. Aliamini kwamba Roho Mtakatifu asingejua. Vinginevyo, anachokisema Petro hakina mantiki.)

 

          1.   Je, hili ni suala lenye mgogoro kanisani leo? Upande mmoja (au pande zote mbili) haziuelewi uwezo wa Mungu?

 

    1.    Soma Matendo 5:5-6. Kwa nini jambo hili lilitokea? Je, “hofu nyingi” iliyotawala kwenye kanisa la awali ilikuwa sehemu ya mpango wa kulinda umoja?

 

    1.    Soma Matendo 5:7-9. Ni kwa jinsi gani hili ni “jaribu” kwa Roho Mtakatifu? (Kwa mara nyingine, inaonekana kwamba Safira hakuuelewa uwezo wa Roho Mtakatifu. “Alimjaribu” kwa kuchukulia kwamba Roho Mtakatifu angeweza kudanganyika.)

 

    1.    Soma Matendo 5:10-11. Kifungu hiki kinabainisha wazi kwamba “hofu nyingi” ililipata “kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.” Je, kuna cha kujifunza kwetu leo katika jambo hili?

 

      1.    Je, wale wanaotilia shaka uwezo wa Roho Mtakatifu wanapaswa kuwa na hofu? Je, tunapaswa kuwaadhibu waasi? Je, tunapaswa kumwachia Roho Mtakatifu adhabu?

 

    1.    Hebu tupitie suala la tamaa na umoja. Ingawa siamini kuwa dhambi ya Anania na Safira ilikuwa ni uchu wa fedha zao wenyewe, tulijadili kwamba walitamani kuwa na hadhi kama ya Barnaba. Unapofikiria matatizo ya umoja uliyoyaona kanisani kwako, ni matatizo mangapi kati ya hayo yaliwahusisha watu waliotamani uwezo na mamlaka ya viongozi kanisani?

 

      1.    Hili linajidhihirishaje? Je, ni tamaa kudhani kwamba unapaswa kuwa unafanya maamuzi badala ya viongozi wa kanisa?

 

  1.   Kuulinda Utajiri

 

    1.    Unapowafikiria Anania na Safira, tatizo lao lina pande mbili. Walitamani hadhi ya kuwa wakarimu, lakini walitaka kuendelea kuwa na fedha zao. Je, inawezekana kuyafanya yote mawili? Je, walidanganya na hivyo kufa bila ya ulazima wowote? (Soma 2 Wakorintho 9:6. Hii inatuambia kuwa kama tutakuwa wakarimu, basi tutabarikiwa kifedha. Sio tu kwamba inawezekana kuwa mkarimu na tajiri, bali pia ni mapenzi ya Mungu.)

 

    1.    Soma 2 Wakorintho 9:7-9. Anania na Safira walitoa kile walichokuwa wameshaamua. Je, walitoa kwa “ukunjufu?” (Walidhani kwamba kudanganya zawadi yao itawafanya wajisikie vizuri.)

 

    1.    Soma Mathayo 6:2-4. Je, Barnaba alitenda dhambi? Zawadi yake imeandikwa (Matendo 4:36-37) ili sote tuione!

 

      1.    Ikiwa mchakato wa utoaji katika kanisa la awali ulikuwa siri, je, Anania na Safira wamejiingiza matatizoni? (Kama usiri ulizingatiwa, wasingejaribiwa kuendana na watu wengine, kama vile Barnaba.)

 

      1.    Je, makanisa na taasisi za kikanisa zifanyazo kazi pasipo kuwa na faida mara kwa mara zinakiuka Mathayo 6:3-4? (Tunayaona haya mara zote. Kanisa langu mahalia halifanyi hivi, lakini Chuo Kikuu cha Andrews kinachapisha jina langu, jina langu limechongwa na kunakshiwa ukutani mahali ninapofundisha, hata Billy Graham ana majina ya wachangiaji yaliyochongwa kwenye matofali katika kituo chake. Kwa dhahiri, ningeweza kudhibiti jambo hili, lakini sikufanya hivyo na sitafanya!)

 

        1.    Je, kitendo cha kuchapisha majina ya wachangiaji kinahafifisha umoja? Je, unafanana na Anania na Safira, na unatamani jina lako liwe miongoni mwa kundi la wachangiaji wakarimu zaidi?

 

      1.    Je, ninatia chumvi asili ya tatizo? Je, Yesu alisema (Mathayo 6:2-4) kwamba ilikuwa dhambi kuwa mchangiaji mwenye jina kubwa? Au, je, Yesu alisema tu kwamba jina lako kuchapishwa ndio thawabu yako?

 

    1.    Binafsi naona kwamba tuna mtazamo uliogeuzwa kuhusu utoaji. Soma 2 Wakorintho 9:10-11 na usome tena Mathayo 6:4. Nini kitakutokea endapo utatoa fedha kwa siri? (Mungu “atakutajirisha katika vitu vyote.”)

 

      1.    Je, unadhani watu wengine wataiona thawabu yako? (Naam, hakika.)

 

    1.    Rafiki, unaona jinsi wanadamu wanavyofanya mambo kinyumenyume? Wanafunzi walitaka uwezo wa kisiasa na kijeshi. Mungu akawapa jambo kubwa zaidi, uwezo wake, uwezo wa Roho Mtakatifu. Anania na Safira walitaka (walitamani) hadhi ya ukarimu, lakini hawakutaka kuwa maskini. Mungu anatuahidi kwamba kwa kadri tunavyozidi kuwa wakarimu, ndivyo tutakavyotajirika. Rafiki, hii ni sawa na kuhesabiwa haki kwa njia ya imani. Lazima umruhusu Mungu akupatie uwezo, hadhi na fedha, bila kujaribu kufanya mambo hayo yatokee kwa juhudi zako. Je, utamruhusu Mungu akubariki?

 

     Juma lijalo: Vielelezo vya Umoja.