Mtume Paulo Akiwa Rumi
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, umewahi kupanga kusafiri kwenda mahali fulani na hali ya maisha ikakuwia vigumu kuweza kufanya safari hiyo? Hatimaye ulipofanikiwa kuifanya safari hiyo, ulifurahia sana, sawa? Au pengine hapana. Vipi ikiwa safari ilihusisha kuwaona ndugu ambao kamwe hukuwahi kuonana nao, au ndugu ambaye hamjaonana kwa miaka mingi? Je, utatafakari kwa makini jinsi ya kuwaendea na kuhusiana nao? Je, ungependa kuwaonesha mvuto bora? Tunaanza mfululizo mpya wa masomo ya barua ya Paulo kwa Warumi. Juma hili tunataka kuangalia baadhi ya mambo ambayo yumkini yalikuwa yakiendelea akilini mwa Paulo alipokuwa akitafakari barua yake na safari yake. Tukiwa na hilo mawazoni mwetu, hebu tuzame kwenye somo letu la Warumi ili tujifunze zaidi!
- Safari
-
- Soma Warumi 15:20-21. Paulo analenga kundi gani kwa ajili ya kulipelekea injili? (Wale wasiofahamu chochote kuhusu habari za Yesu.)
-
-
- Je, hilo pia ndilo lengo lako binafsi?
-
-
-
- Sababu ya Paulo kulilenga kundi hilo ni ipi? (Hataki kujenga juu ya msingi uliojengwa na mtu mwingine.)
-
-
-
-
- Unadhani Paulo anamaanisha nini kwa kauli hiyo?
-
-
-
-
- Ikiwa lengo lako linafanana na la Paulo, je, sababu yako ya kulilenga kundi hilo ni sawa na ile ya Paulo? (Lengo la Paulo kupeleka injili kwa wale ambao hawajasikia habari za Yesu ni ya muhimu sana. Ingawa sina uhakika kama ninaielewa sababu ya Paulo kwa ukamilifu, inaonekana anapendelea kazi ya waanzilishi. Kwa kuwa kwa ujumla masomo haya yanaelekezwa kwa wale ambao tayari wanafahamu habari za Yesu, nadhani tunafanya kazi tofauti kidogo.)
-
-
- Soma Warumi 15:22. Kwa nini Paulo hajaweza kuwatembelea Warumi, ingawa anataka kuwatembelea? (Kazi yake ya uanzilishi ndio ilikuwa ya kwanza. Ilimchelewesha kwenda Rumi.)
-
- Soma Warumi 15:23-24. Paulo ana mipango gani ya safari ya kwenda Rumi? (Atapitia Rumi na kupiga kituo atakapokuwa akielekea Spania.)
-
- Soma Warumi 15:25-26. Kituo cha kwanza cha Paulo ni kipi katika safari yake ya Spania? (Yerusalemu. Anawapelekea msaada wa kifedha washiriki wa hapo.)
-
- Soma Matendo 21:27-33. Nini kinamtokea Paulo alipokuwa Yerusalemu? (Ghasia inaanza. Wayahudi wanamwona Paulo na wanaijua kazi yake – ambayo wanaamini inahafifisha dini ya Kiyahudi.)
-
- Baada ya kukamatwa kwa Paulo, anapitia mfululizo wa masuala ya kisheria wakati akiwa jela kwa miaka kadhaa. Hebu tuangalie jambo hili mwishoni mwa wasilisho la kisheria pale Yerusalemu. Soma Matendo 25:10-12. Unadhani Kaisari alikuwa anaishi wapi? (Rumi! Badala ya Paulo kupitia na kupiga kituo kwa muda Rumi kama sehemu ya mpango wake wa safari, sasa anapelekwa Rumi kama mfungwa kutokana na rufaa yake ya kisheria.)
- Mwisho wa Safari
-
- Soma Matendo 28:16-20 na Matendo 28:30-31. Mungu anatendaje kazi ili Paulo aweze kusambaza injili Rumi?
-
-
- Vipi kuhusu mpango wa kuweka mvuto bora kabisa kuanzia mwanzo?
-
-
- Kwa nini viongozi wa kanisa la Kikristo pale Rumi, wale ambao hapo awali Paulo aliwaandikia, hawajitokezi kumsalimia Paulo? (Biblia haibainishi kwa umahsusi. Kwa dhahiri Paulo hakuanzisha kanisa Rumi. Si kana kwamba Paulo anarejea kwenye kanisa alilolianzisha. Tunapoendelea kujifunza barua ya Paulo kwa Warumi, hebu tuone kama tunaweza kujibu swali hili vizuri zaidi.)
-
- Soma Matendo 28:21-22. Hii inaashiria nini juu ya athari ya kanisa pale Rumi? (Wayahudi wanafahamu habari hasi (mbaya) za “madhehebu” ya Wakristo. Kujua jambo ni bora zaidi kuliko kutokujua jambo.)
- Barua ya Paulo
-
- Soma Warumi 1:1 na Warumi 1:7. Walengwa (hadhira) wa barua hii ni akina nani? Je, ni Wayahudi waliopo Rumi, au Wakristo waliopo Rumi? (Kwa kuzingatia kile tulichojifunza hadi sasa, jinsi Paulo anavyojitambulisha, na rejea yake ya “watakatifu,” kwa dhahiri anawaandikia Wakristo.)
-
- Soma Warumi 1:1-3. Paulo anazungumzia nini kuhusu majukumu yake? (Paulo anasema (Warumi 1:1) kwamba yeye ni “mtumwa” na “mtume” ambaye “ametengwa aihubiri injili ya Mungu.”)
-
-
- Paulo analielewaje jukumu lake? Injili hiyo inafananaje? (Paulo anasema kuwa injili inazungumzia habari za Yesu. Siku zote imekuwa ikizungumzia habari za Yesu kwa sababu mitume wa Agano la Kale waliahidi kwamba Yesu alikuwa anakuja.)
-
-
- Soma Warumi 1:3-4. Paulo anaielewaje asili ya Yesu? (Anasema kuwa Yesu ana asili ya mwanadamu (kutoka ukoo wa Daudi) na asili ya Kimungu (kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Yesu ni Mwana wa Mungu).)
-
-
- Tunawezaje kuwa na uhakika kuhusu asili ya Kimungu ya Yesu? Wanadamu waliweza kuona kuwa Yesu alizaliwa na mwanamke. Waliona nini kilichothibitisha kwamba alikuwa Mwana wa Mungu? (Ufufuo wa Yesu kutoka katika wafu ni “uthibitisho” kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu.)
-
-
- Soma Warumi 1:5-6. Hii inathibitisha kuwa walengwa wa barua ya Paulo ni akina nani? (Paulo anasema kuwa kazi yake ni kushiriki injili na Mataifa. Kisha anasema kuwa wale wanaosoma barua yake ni “miongoni mwa wateule.” Hivyo, inaonekana kuwa Paulo anawaandikia waongofu wa Mataifa.)
-
-
- Unaelezeaje basi, kile tulichojifunza hapo awali, kwamba watu aliokutana nao Paulo kwanza kama mtumwa aliyepelekwa Rumi ni viongozi wa Kiyahudi (Matendo 28:16-17)? (Je, hili haliendani na njia aliyoipendelea Paulo – kuwapelekea injili wale wasiofahamu habari za Yesu?)
-
- Kanisa Katika Rumi
-
- Soma Warumi 1:8. Jambo gani linataarifiwa kuhusu kanisa katika Rumi? (Imani yake!)
-
- Soma Warumi 1:11-12. Paulo anataka kujenga nini Rumi kwenye ule msingi wa imani? (Karama ya roho.)
-
-
- Kanisa la Rumi linaweza kumfanyia nini Paulo? (Linaweza kuhamasisha imani yake.)
-
-
-
- Je, huu ndio uhai tunaopaswa kuuzingatia katika makanisa yetu mahalia? Je, tunapaswa kuangalia karama mahsusi na uthabiti wa kila mshiriki wetu, na kisha kutiana moyo na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu?
-
-
-
-
- Ikiwa unakubaliana na jambo hili, je, utalitendaje kivitendo? (Hapa ndipo palipo na umuhimu wa vikundi vidogo vidogo kanisani kukutan)
-
-
-
- Soma Warumi 15:14. Tabia gani nyingine tunaziona katika kanisa la Rumi? (Watu wamejaa wema, wamejaa maarifa, na wana uwezo wa kufundishana.)
-
-
- Ikiwa wana maarifa kamili, kwa nini wafundishane? (Hii inaturejesha mahali ambapo kila mshiriki ana uthabiti au karama fulani, na kushirikiana humsaidia kila mmoja wao.)
-
-
- Soma Warumi 1:13. Hapo awali tulihitimisha kwamba Paulo hakuanzisha kanisa Rumi. Je, kuna ushahidi wowote kuthibitisha vinginevyo? Je, unadhani kuwa hapo awali alikuwepo mahali hapo? (Paulo hasemi kwa umahsusi, lakini kila anachokiandika kinaonekana kuashiria kuwa kamwe hajawahi kuwepo Rumi hapo kabla.)
-
-
- Paulo anaweza kuwa anamaanisha nini pale anapoandika kwamba anataka kuwa na “matunda kwenu ninyi?” Hivi punde tu tumesoma kwamba washiriki wa kanisa la Rumi “wamejaa wema” na wana “maarifa kamili.” (Paulo anapendelea kujenga msingi halisi wa kanisa. Lakini, hiyo haimaanishi hana ujuzi wa kujenga kanisa. Mpango wake ni kuwaongoa washiriki wapya katika kanisa la Rumi.)
-
-
- Soma Warumi 1:14-15. Tafsiri ya Biblia ya NIV inapunguza makali ya kile anachokisema Paulo. Anasema kuwa injili ni kwa ajili ya Wayunani na washenzi, wenye hekima na wapumbavu. Unadhani hadhira ilidhani kuwa wao ni akina nani? (Hii ni Rumi! Bila shaka walidhani kuwa wao ni kundi la watu wa kisasa na wastaarabu. Kama palikuwepo na Wayahudi kwenye hiyo hadhira, walijua kwamba walikuwa na hadhi ya juu, hata kama Wayunani wangewachukulia kuwa ni washenzi.)
-
-
- Kanisa lako linafanya kazi ya aina gani katika kuyafikia matabaka yote ya jamii?
-
-
-
- Je, Paulo anaweza kushinda tuzo kwa kuwa sahihi kisiasa? (Kuwa sahihi kisiasa huficha asili ya kazi. Vipi ikiwa umekiri kwamba baadhi ya makundi ya walengwa wako ni ya kisasa na kistaarabu na makundi mengine ni ya washenzi? Wengine werevu (wana hekima) na wengine ni wapumbavu? Je, utafanya uinjilisti kwa kutumia njia tofauti ikiwa utakuwa mkweli kwa nafsi yako katika hali hii?
-
-
- Soma Warumi 1:16. Kwa nini Paulo anakanusha kutoionea haya injili? (Kwa sababu ni kawaida kuona haya kumtangaza mtu aliyeteswa kwa kutenda kosa la jinai.)
-
-
- Kwa nini Wayahudi wanakuwa wa kwanza kwenye suala la wokovu?
-
-
- Soma Warumi 1:17. Nini kilicho cha “kwanza na cha mwisho,” kuanzia A hadi Z katika injili? (Haki kwa imani. Paulo haonei haya kusulubiwa kwa Yesu, kwa kuwa kifo chake ndicho kiini cha injili. Yesu alikufa kwa ajili yetu. Yesu aliishi maisha makamilifu kwa ajili yetu. Kwa hiyo, injili yetu ni mojawapo ya mambo ya imani pekee.)
-
- Rafiki, kushiriki injili na watu wengine ni muhimu kiasi gani kwako? Je, umetafakari jinsi unavyoweza kushiriki injili na watu wengine? Kwa nini usitafakari jambo hili kwa kina na umwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuwa na mpango wa utekelezaji?
- Juma lijalo: Pambano.