Kumhuzunisha na Kumpinga Roho Mtakatifu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, ungependa kukutana na Yesu uso kwa uso? Mimi ningependa! Wakristo wanasema kuwa wanatamani kama wangekuwa wanaishi kipindi Yesu alipokuwepo hapa duniani. Wanatamani kama wangekuwa mojawapo kati ya wanafunzi wa Yesu na kuzungumza naye moja kwa moja ili kupata maelekezo yake pamoja na majibu ya jinsi wanavyopaswa kuishi. Nina mashaka kama uhalisia unaendana na matamanio haya. Kwa nini? Kwa sababu mara nyingi huwa hatupendi kusikia ukweli. Watu wanapokuwa hawapendi kile kinachosemwa na Biblia, wanakataa hayo yasemwayo. Watu wanapokataa kile kinachosemwa na mitume, wanawakataa. Vipi pale watu wanapokataa kile anachokisema Roho Mtakatifu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza juu ya tatizo la kumpinga Roho Mtakatifu!
- Onyo la Stefano
-
- Baadhi ya maneno yanaweza kukufanya uuawe! Soma Matendo 7:51 ili uone alichokisema Stefano kwa viongozi wa Kiyahudi kabla hawajamuua. Kuna tatizo gani la kihistoria kwa watu wa Mungu? (“Siku zote wanampinga Roho Mtakatifu.”)
-
- Soma Matendo 7:52-53. Watu hawa wametenda jambo gani jingine? (Waliwatesa na kuwaua manabii, walimuua Yesu, na hawakuitii torati.)
-
-
- Kwa nini Stefano anayaweka pamoja haya mambo manne kwenye hoja yake? (Yesu, manabii, torati, na Roho Mtakatifu – vyote hivi ni njia anazozitumia Mungu kuwasiliana na watu wake.)
-
-
-
- Kwa nini watu hawa wanakasirika sana kutokana na maneno ya Stefano? (Huwa tunakasirika watu wanapotuambia mambo tunayofahamu kuwa ni ya kweli na hatutaki yawe ya kweli.)
-
-
- Soma Matendo 7:54-56. Nani anayemchochea Stefano kusema maneno haya? (Roho Mtakatifu!)
-
- Yafikirie maisha yako. Je, unaiheshimu Biblia, torati, manabii, na Roho Mtakatifu?
-
-
- Bila shaka unasema kwamba (na hii ni kweli), “Ninaokolewa kwa neema, hivyo sihitajiki kuishika sheria.” Fikiria mantiki ya kauli hii. Ikiwa Mungu ametupatia Biblia, manabii, torati, na Roho Mtakatifu ili kutupatia mwelekeo wa jinsi tunavyopaswa kuishi, kwa nini hatuishiki sheria?
-
-
-
-
- Mtazamo wa namna gani ni sahihi dhidi ya sheria kwa wale tunaookolewa kwa neema pekee?
-
-
-
-
- Ninapotafakari kwa uaminifu mtazamo wangu dhidi ya maelekezo ya Mungu, nina wasiwasi kwamba ninafanana na Wayahudi warusha mawe kuliko ninavyofanana na Stefano. Vipi kuhusu wewe?
-
-
- Nimekuwa nikijifunza kitabu cha Matendo na kikundi kidogo. Kama haufahamu yaliyomo kwenye Matendo 15, soma sura hiyo sasa hivi. Kisha soma Matendo 15:23-29 ili tuone hitimisho la mjadala huu. Ikiwa wewe ni mtu uliyedhamiria kuitii Biblia, manabii, na torati, je, utakuwa katika upande gani kwenye huu mjadala? (Soma Mwanzo 17:9-11 na Mwanzo 9:14. Ikiwa umedhamiria kumtii Mungu, utakuwa upande wa amri ya tohara kwa sababu hiyo ni amri iliyotoka kwa Mungu moja kwa moja. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba, hiyo ni amri inayohusu kuwa na uhusiano na Mungu.)
-
- Soma Warumi 14:1-4. (Ikiwa hauna uzoefu wa ujumbe huu, soma sura nzima ya Warumi 14.) Paulo anasema nini hapa kuhusu watu walio makini sana kujaribu kutenda kila lililoandikwa kwenye torati? (Anawaita wadhaifu. Hususani, ninaamini Paulo anasema kuwa maelekezo ya Matendo 15:29 kuhusu “kujiepusha na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu” hayatufungi. Suala la kula mbogamboga lilihusiana na kuepuka kula nyama kwa sababu yumkini ilitolewa sadaka kwa sanamu.)
-
- Hebu tutafakari zaidi haya mambo magumu. Nilianza kwa kukiri kwamba yumkini nimekuwa mtu wa “kutupa mawe” kwa sababu wakati mwingine huwa ninapingana na baadhi ya sheria. Lakini, baadaye tulijifunza kuwa Kanisa la awali lilitupilia mbali matumizi ya baadhi ya sheria kwa waumini wapya wa Mataifa. Baadaye, Paulo anawaita “wadhaifu” wale waliodhamiria kufuata kila sehemu ya sheria. Je, ni sahihi kupingana na baadhi ya sheria? Au, je, sisi ni kizazi kama cha watu ambao Stefano aliwaonya?
-
-
- Ikiwa unasoma masomo yangu mara kwa mara, unafahamu ninafundisha kuwa sheria zipo ili kuboresha maisha yetu! Watu wanaotafuta kuishi maisha bora wanawezaje kuitwa “dhaifu?” (Kwa dhahiri, kuna jambo la muhimu sana hatulielewi ambalo tunatakiwa kuligundua!)
-
- Uchunguzi Juu ya Kumhuzunisha Roho Mtakatifu
-
- Hebu tupitie tena uamuzi wa kutupilia mbali tohara kwa waumini wapya wa Mataifa. Soma Matendo 15:6-11. Hoja ya Petro ni ipi dhidi ya hitaji la tohara? (Kwamba Roho Mtakatifu aliwathibitisha wale ambao hawakutahiriwa. Watu hawa wa Mataifa walijawa Roho Mtakatifu.)
-
- Soma Matendo 15:12. Barnaba na Paulo wanajenga hoja gani kupitia kwenye hivi visa? (Hii inaonesha kuwa Roho Mtakatifu alikuwa sehemu ya kazi iliyofanywa miongoni mwa Mataifa.)
-
- Soma Matendo 15:28-29. Yakobo anamnukuu nani kwenye barua yake kwa Mataifa? (Yakobo anamnukuu Roho Mtakatifu kama msingi wa kubainisha kwamba maelekezo ya wazi kwa Ibrahimu na uzao wake hayakuwahusu waumini wapya wa Mataifa.)
-
-
- Utaona kwamba katika Matendo 7:8 Stefano anaitaja tohara kwa namna chanya.
-
-
-
- Utaona kwamba Mwanzo 17:12 inabainisha kuwa sheria ya tohara inatumika kwa watu wasio Wayahudi.
-
-
- Soma Wakolosai 2:9-12. Je, tohara bado ipo? Je, imechukua sura mpya? (Ndiyo, ule uhusiano wa pekee ambao Mungu aliuzungumzia kwa Ibrahimu, sasa unaendelea katika ubatizo!)
-
-
- Ubatizo unafananaje na tohara? (Ni kukatilia mbali asili ya dhambi. Katika ubatizo tunakufa pamoja na Yesu kwa ajili ya dhambi zetu. Tunapotoka ndani ya maji baada ya kuzamishwa tunaingia kwenye maisha mapya na uhusiano mpya pamoja na Yesu.)
-
-
-
- Hii inatufundisha nini kuhusu sheria na kumsikiliza Roho Mtakatifu? (Hakuna kilichobadilika kuhusu lengo la kuwa na uhusiano wa pekee na Mungu. Utaratibu uliotumika umebadilika kutokana na kubadilika kwa mazingira. Hii inatufundisha kuwa tunatakiwa kuangalia kwa makini kabisa kile anachokitenda Roho Mtakatifu. Mungu ana kanuni zenye “mtazamo mpana” zisizobadilika. Hata hivyo, Roho Mtakatifu anaweza kutuonesha kwamba kile tulichodhani kuwa ni utaratibu sahihi kinaweza kubadilika ili kuthibitisha vizuri zaidi sheria kwa mtazamo mpana.)
-
-
-
- Soma Warumi 14:16-18. Kanuni zenye mtazamo mpana ni zipi kwenye hiki kifungu? (“Haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.”)
-
-
- Soma Waefeso 4:30-32. Hapa zinazungumziwa kanuni gani zenye mtazamo (taswira) mpana? Jambo gani linaakisi kuwa nje ya msitari wa Roho Mtakatifu, na jambo gani linaakisi kuwa ndani ya msitari wa Roho Mtakatifu? (Mapigano, hasira na nia mbaya vinaakisi maisha yaliyo nje ya msitari wa Roho Mtakatifu. Utu wema, huruma, na msamaha vinaakisi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu.)
- Kujichunguza
-
- Soma Waefeso 5:1-2. Tunaweza kujichunguzaje ili kuona kama tunaendana na Roho Mtakatifu? (Maisha yetu yanapaswa kuakisi upendo – utayari wa kuacha mambo yako mwenyewe kwa manufaa ya watu wengine.)
-
-
- Hebu turejee kwa Stefano. Soma Matendo 7:51-53. Je, watu hawa walikuwa wanaenenda kwa upendo usio na choyo? (Hapana! Walikuwa wanawapinga wajumbe wa Mungu kwa nguvu zote. Ukiliangalia jambo hili kwa namna hii, ni dhahiri kwamba wewe na mimi tusingekuwa mojawapo kati ya watu kwenye lile kundi la warusha mawe.)
-
-
- Soma Waefeso 5:3-5. Je, haya ndio maeneo tunayorudi nyuma dhidi ya Roho Mtakatifu? Je, haya ndio masuala yenye taswira pana yanayotuambia iwapo tunaongozwa na Roho Mtakatifu?
-
-
- Hebu tuangalie kwa mahsusi Waefeso 5:5. Paulo anagongelea msumari maonyo yote haya mahsusi hadi kwenye “uasherati, uchafu au ulafi (tamaa).” Kisha anauita huu kuwa ni uabudu sanamu. Je, hii inaleta mantiki yoyote kwako? Hii inahusishaje na uabudu sanamu? (Kuabudu sanamu ni kuabudu kitu ulichokitengeneza kwa mikono yako mwenyewe. Ni kuabudu juhudi zako mwenyewe, hivyo kujiabudu mwenyewe. Uasherati, uchafu na tamaa vyote vinamhusu mtu. Tunajiingiza kwenye mambo haya kwa sababu sisi ni wabinafsi.)
-
-
-
- Hebu turejeshe jambo hili kwenye tohara. Je, hoja inayopendelea tohara ni hoja inayohusu nafsi ya mtu? (Kwa kuwa ninaweza kuona hoja katika pande zote mbili za swali hili, hii inaimarisha umuhimu wa uongozi wa Roho Mtakatifu.)
-
-
- Soma 1 Wathesalonike 5:19-22. Tunatakiwa kujaribu nini? (Mambo yote. Tafuta uongozi wa Roho Mtakatifu ili kujaribu uelewa wako wote kuhusu mapenzi ya Mungu. Ukimkataa Roho Mtakatifu, kamwe hutaweza kutambua mapenzi ya Mungu.)
-
- Rafiki, je, unajaribu kila kitu? Je, unautafuta uongozi wa Roho Mtakatifu kwenye masuala ambayo hayako wazi kwako? Kwa nini usidhamirie sasa hivi na kumwomba Roho Mtakatifu aongoze uelewa wako.
Juma lijalo: Kazi ya Roho Mtakatifu.