Mteswa na Mfufuka

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mathayo 26)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
2
Lesson Number: 
13

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Wakati umefika kwa ajili ya kujifunza habari za kafara ya Yesu kwa ajili yetu. Maneno hayatoshi kuielezea kafara hiyo kwa ukamilifu. Upendo wa ajabu kiasi gani! Rehema ya ajabu kiasi gani! Kutokuwa na ubinafsi kwa ajabu kiasi gani alikotuonesha! Hebu tuchimbue Biblia zetu ili tushuhudie kafara ya Yesu ya ajababu na yenye kushangaza kwa ajili yako na mimi!

 

I.                   Yuda

 

A.                Soma Mathayo 27:1-3. Tukio gani lilimfanya Yuda ajute? (Kwamba Yesu “alihukumiwa.” Hiyo inatilia mkazo fikra yangu kwamba Yuda hakudhania kabisa kuwa Yesu ataruhusu kukamatwa na kuhukumiwa.)

 

B.                 Soma Mathayo 27:4-5. Je, viongozi wa dini walimfariji Yuda kwa kumwambia kuwa alitenda jambo sahihi?

 

1.                  Je, viongozi wa dini walidhani kwamba walikuwa na wajibu gani?

 

C.                 Soma Mathayo 18:7-9 na uyalinganishe mafungu haya na hali ya sasa ya Yuda. Unadhani Yuda alidhani kuwa atanufaika na nini kwa kumsaliti Yesu? (Bila shaka angepata sifa kwa kitendo cha Yesu kuudai ufalme wake hapa duniani. Lakini, angalao pia angekuwa na vipande thelathini vya fedha. Alidhani kuwa atanufaika.)

 

1.                  Jambo gani hasa lililomtokea Yuda? (Alipoteza fedha zake, ufalme na uhai wake. Na kwa kuongezea, inaonekana ameukosa ufalme wa milele. Katika Mathayo 18 Yesu anatuambia kwamba tunadhani tutanufaika na dhambi, lakini kimsingi ni kwamba ni heri kupoteza mkono, mguu au jicho, kuliko vile ambavyo dhambi itakugharimu.)

 

II.                Pilato

 

A.                Soma Mathayo 27:11 na Luka 23:3-4. Mathayo anashindwa kuonesha hisia za Pilato. Hiyo inamaanisha nini kwa Yesu? (Inamaanisha kuwa Yesu anapaswa kuachiwa huru.)

 

B.                 Soma Mathayo 27:12-14 na Luka 23:13-16. Viongozi wa Kiyahudi wanaleta mashtaka (sio mashahidi) dhidi ya Yesu, na anatumia haki yake ya kutokujibu (kukaa kimya). Kwa nini hajibu? (Nchini Marekani tunaiita “Haki ya Tano ya Mabadiliko,” haki ya kukaa kimya bila kuhatarisha kujitia hatarini (kujiponza). Hesabu 35:30 na Kumbukumbu la Torati 19:15 zinaonesha kuwa watu wa Mungu walikuwa na sheria kama hiyo kwamba majuto mepesi (kukiri kwa urahisi tu) hayakutosha kumtia mtu hatiani.

 


C.                 Kama tunavyoona kutoka kwa Luka, haya mashtaka ya uongo na ukimya wa Yesu havitoshi kumshawishi Pilato au Herode kwamba Yesu ametenda kosa lolote. Soma Mathayo 27:19. Ujumbe huu una umuhimu gani kwa Pilato? (Nukuu za Barne zinasema “Ndoto zilichukuliwa kama ishara ya mapenzi ya Mungu, na miongoni mwa Waruni na Wayunani, na kwa Wayahudi pia, ndota zilitegemewa kwa hali ya juu sana.” Mawazo ya Pilato sasa yameimarishwa na ujumbe wa Mungu!)

 

D.                Soma Mathayo 27:15-18 na Mathayo 27:20-23. Ungefanya nini endapo wewe ndiye ungekuwa Pilato? Unayo mawazo yako mwenyewe, ambayo yameimarishwa zaidi na Mungu, dhidi ya mapenzi ya makutano yasiyokuwa na sababu wala msingi wowote.

 

E.                 Soma Mathayo 27:24-26. Hii inatufundisha nini kuhusu mustakabali wa uhuru wa dini? (Serikali inafungua njia kwa kundi la wendawazimu, wanaoongozwa kwa nguvu za pepo. Mtu mwovu anaachiwa huru na mtu asiye na hatia anahukumiwa kifo.)

 

III.             Mateso

 

A.                Soma Mathayo 27:41-44. Unakabilianaje na kebehi na matusi yanayokudhihaki katika nyanja ambazo una uwezo nazo mkubwa sana? Kama wewe una sura nzuri sana, mtu mwingine anasema kuwa wewe ni mbaya. Kama una nguvu sana, mtu mwingine anasema kuwa wewe nidhaifu. Ikiwa una akili sana, mtu ambaye ni mbumbumbu anakuita mpumbavu.

 

B.                 Soma Mathayo 27:45-46. Je, matusi hayo yanamwingia Yesu?

 

1.                  Soma Zaburi 22:1-2. Tunaona kwamba Yesu ananukuu Zaburi – au yumkini Zaburi inatabiri kile ambacho Yesu atakisema. Je, Yesu anadhihirisha uhaba wa imani kwa Baba yake? (Kwanza, ni vigumu sana kwa kitendo hiki kuwa dhambi kwa sababu Biblia isingeweza kubashiri kauli ya dhambi kutolewa na Yesu. Pili, si dhambi kusema, “Mungu, kwa nini hujibu? Mungu, unakuwa wapi wakati ninapokuhitaji?” Sababu ni kwamba unamtizama Yesu kwa ajili ya kupata msaada. Ni pale ambapo unapojitumaini wewe mwenyewe, au kugeuka na kumwacha Mungu ndipo dhambi inapokuja.)

 

2.                  Soma Isaya 59:1-2. Hii inapendekeza kuwa sababu ya kauli ya Yesu ni ipi? (Yesu alibeba dhambi zetu. Alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Dhambi zetu zilimtenganisha na Mungu.)

 

3.                  Kejeli kuu ya matusi yaliyovurumishwa na viongozi wa dini ni ipi? (Ilhali Yesu angeweza kuwaua wote na kusitisha mateso makubwa dhidi yake, aliteseka kwa kuzifia dhambi zao. Sio tu kwamba mashtaka yalikuwa ya uongo kabisa, bali pia Yesu aliteseka kwa matusi haya na maumivu kwa sababu ya dhambi za wanadamu.)

 

C.                 Soma Mathayo 27:50-51. Pazia linahusianaje na kifo cha Yesu? (Yesu alitimiza mfumo wa kafara wa hekalu. Waebrania 7:25-28. Mfumo wa hekalu haukuwa na thamani yoyote tena. Nafasi yake ilichukuliwa na Yesu, damu yake inatutetea katika hekalu la mbinguni. Ukweli kwamba pazia lilipasuka toka juu hata chini inaonesha kuwa kitendo hiki kilikuwa si cha kawaida kwa kutumia akili ya kawaida.)

 

D.                Soma Mathayo 27:52-54. Tafakari hofu waliyokuwa nayo viongozi wa dini walioshuhudia watu wakifufuliwa na Warumi wakikiri kuwa Yesu alikuwa Mungu!

 


1.                  Kwa nini Mungu aliwafufua watu kipindi hicho? Kwa nini hakusubiri hadi Yesu afufuke siku ya Jumapili? (Wakati wa kifo chake, Yesu aliishinda dhambi na kukishinda kifo. Huu ni uthibitisho mkuu kwamba Yesu alipumzika kaburini siku ya Sabato ili tu kusherehekea ushindi wake dhidi ya dhambi na kifo. Kama ambavyo Sabato inavyosherehekea kazi ya Uumbaji (Kutoka 20:1) na kuwekwa huru kutoka utumwani Misri (Kumbukumbu la Torati 5:15), sasa Yesu anasherehekea maisha yetu mapya na kuwekwa kwetu huru dhidi ya utumwa wa dhambi na kifo kwa pumziko la Sabato.)

 

IV.             Ufufuo wa Yesu

 

A.                Soma Mathayo 27:65 na Mathayo 28:1-3. Wapinzani wa Yesu wangeweza kulilinda kaburi ili liwe salama kwa kiwango gani? (Wasingekuwa na uwezo wa kutosha kulilinda!)

 

B.                 Soma Mathayo 28:5-7. Je, wanatakiwa kuliamini neno la malaika? (Hapana! Malaika anawaonesha kaburi lililo tupu na kuwaambia kuwa Yesu atawatokea Galilaya.)

 

C.                 Soma Mathayo 28:8-10. Kwa nini Yesu hasubiri kuwaona Galilaya, kama alivyosema malaika? (Ninalipenda tukio hili! Kwa dhahiri Yesu hawezi kusubiri! Anataka kuwaona wanawake waliokaa pamoja naye katika kipindi chote cha kuteswa kwake (Mathayo 27:54-56) na kushiriki nao habari njema!

 

D.                Soma Mathayo 28:16-17. Mtu anawezaje kuona shaka ikiwa walimwona Yesu akiwa hai? (Soma 1 Wakorintho 15:6 na Yohana 20:24-25. Tunaona maelezo ya Tomaso kuwa mgumu kuamini (kwa sababu hakuwepo pamoja na wanafunzi wenzake), na tunaona kundi kubwa la wanafunzi. Suala lililopo ni kwamba wafuasi wa Yesu walitokea kuamini katika nyakati tofauti tofauti.)

 

1.                  Kwa nini mashaka yanatajwa? Ikiwa lengo la Mathayo kuandika injili yake ni kutufanya tuamini kuwa Yesu ni Mungu, kuna manufaa gani kubainisha kwamba mashahidi walikuwa na mashaka? (Hii inatupatia ujasiri wa kuyaamini maelezo ya Mathayo aliyoyaandika kwa dhati na uaminifu. Endapo angekuwa anazusha mambo yote haya, asingebainisha suala la kuona shaka. Jambo la msingi zaidi ni kwamba, Mathayo anatutaka tufahamu kwamba suala la Yesu kuuawa na kufufuka ni jambo linaloweza kuchukua muda kulikubali.)

 

E.                 Soma Mathayo 28:18. Yesu ana nafasi gani ulimwenguni? (Amepewa mamlaka yote!)

 

F.                  Soma Mathayo 28:19-20 na Mathayo 24:45-46. Utakumbuka tulipojifunza Mathayo 24 tulihitimisha kwamba wakati tukisubiri kurejea kwa Yesu, kazi yetu ni kulisha watu – kuuendeleza Ufalme wa Mungu. Je, Mathayo 28:19-20 inaongezea taarifa gani mahsusi kwa kina zaidi? (Tunatakiwa kuwafanya (kutengeneza) wanafunzi wapya, kuwabatiza na kuwafundisha.)

 

G.                Soma tena Mathayo 28:20. Yesu anaahidi kutoa msaada gani? (Kwamba atakuwa pamoja nasi hadi ujio wake wa Mara ya Pili.)

 

1.                  Hilo ni kweli kwa kiasi gani? Nilidhani kuwa Yesu alirejea mbinguni? (Soma Yohana 14:16-20 na Yohana 16:5-7. Yesu anarejea mbinguni, lakini Yesu yupo pamoja nasi kwa njia ya Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu! Kwa kuzungumzia kuhusu Yesu kuwa pamoja nasi – Anakaa pamoja nasi ikiwa tuko tayari.)

 

2.                  Je, umewahi kusema, “Natamani ningekuwa mfuasi wa Yesu ili kwamba ningeweza kumwuliza maswali?” Je, swali hilo limejengwa juu ya dhana zisizo sahihi? (Nadhani hivyo. Kwa kuwa Yesu yupo na anapatikana kwa ajili ya kukaa pamoja nasi kwa njia ya Roho Mtakatifu, ikiwa unamwomba Roho Mtakatifu akuelekeze, basi upo kwenye nafasi sawa na mwanafunzi wa Yesu! Wazo la kupendeza kiasi gani!)

 


H.                Rafiki, Yesu alivumilia matusi, maumivu na kifo ili kutupatia fursa ya uzima wa milele. Je, unafanya nini ili kushiriki hizo habari njema na watu wengine? Kwa nini usijitoe leo ili kushiriki habari njema na watu wengine?

 

V.                Juma lijalo: Tutaanza mfululizo mpya wa masomo juu ya Wajibu wa Kanisa Katika Jamii.