Siku za Mwisho za Yesu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mathayo 26)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
2
Lesson Number: 
12
 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Somo letu la Mathayo juma hili linawamulika wasaliti wawili na mwanamke mmoja aliyejitoa kikamilifu kwa Yesu. Je, inamaanisha nini hasa kumsaliti Yesu? Inamaanisha nini kujitoa kikamilifu kwa Yesu? Kwa nini matokeo ni tofauti sana kwa msaliti mmoja kuliko mwingine? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

 

I.                    Wapanga Njama na Mwanamke

 

A.                Soma Mathayo 26:1-2. Kwa dhahiri hizi ni habari zenye kukatisha tamaa sana. Kwa nini uwaambie wanafunzi? (Yesu alitaka kuwaonya (kwa mara nyingine tena).)

 

1.                  Hiyo inaashiria nini kuhusu umuhimu wa matukio ya siku za mwisho? (Yesu atatuonya kuhusu matukio ya muhimu na yale yenye changamoto.)

 

B.                 Soma Mathayo 26:3-7. Tunazo taswira mbili kinzani. Taswira ya kwanza ni ya kundi linalopanga kumwua Yesu na nyingine ni ya mwanamke ambaye anajitoa kwa hali ya juu kwa ajili ya Yesu. Kutokana na Yesu kuelewa mustakabali wa mauti yanayomkabili kitambo kifupi kijacho, unadhani alijisikiaje kuhusu huyu mwanamke? (Hii ni nyota inayong’aa kwenye mazingira ya giza. Ningemshukuru sana mwanamke huyu.)

 

C.                 Soma Mathayo 26:8-9. Unauelezeaje mwitiko wa wanafunzi? Wameambiwa kwamba Yesu anakaribia kufa, je, hawapaswi kushiriki katika kumfanyia jambo la pekee? (Nadhani wanafunzi walipingana na uhalisia kwa kutokubali kuamini kile alichowaambia Yesu. Hawakutaka kuamini kuwa atakufa.)

 

1.                  Je, ungekuwa na mwitiko gani endapo wewe ndiye ungekuwa huyu mwanamke na kusikia ukosoaji huu? Umejitoa kwa kununua hii marhamu, na sasa wanafunzi wanakukosoa!

 

2.                  Kuna dhana katika fungu hili ambayo nataka uiangalie. Wanafunzi hawakusema kwamba mwanamke alipaswa kutoa fedha kwa masikini badala ya kununua marhamu, bali walisema kuwa angeweza kuiuza hiyo marhamu. Hii inatuambia nini kuhusu jinsi mwanamke huyu alivyoipata hii marhamu? (Ilikuwa ni zawadi. Kwa uthibitisho, hakikuwa kitu ambacho angeweza kumudu kukinunua.)

 


D.                Soma Mathayo 26:10-13. Hii ilikuwa ni zawadi, kuna mtu alidhamiria mwanamke huyu aweze kuitumia zawadi hiyo. Badala yake, alichagua kujikana nafsi kwa kutoitumia kama walivyopendekeza wanafunzi. Je, wanafunzi walikuwa na haki ya kumwambia kufanya matumizi anayopaswa kujikana nafsi ili kutoyafanya? (Hawana ushauri sahihi. Yesu anasema kuwa alichokifanya mwanamke huyu kitaongelewa katika kumbukumbu lake na historia yote.)

 

1.                  Je, zipo fursa zinazokuzunguka kuinua mioyo ya watu waliokata tamaa kwa kuwatendea wema?

 

2.                  Je, pia watazungumzia duniani kote kuhusu habari ya wanafunzi kumkosoa mwanamke huyu aliyejikana nafsi?

 

3.                  Kuna tofauti gani kati ya mtazamo wa mwanamke na ule wa wanafunzi? (Alikuwa amejitoa kwa Yesu kikamilifu. Wanafunzi walijitoa kufanya uamuzi wa matumizi bora ya marhamu yake.)

 

II.                 Yuda

 

A.                Soma Mathayo 26:14-16. Je, Yuda ndiye aliyemkosoa mwanamke?

 

1.                  Unadhani kwa nini Yuda alimsaliti Yesu? Je, sasa aliamua kumchukia Yesu? (Ninazo nadharia mbili. Kwanza, hakuamini kwamba Yesu angeweza kuuawa – na kwamba angeweza pia kupokea fedha kama thawabu kwa kumlazimisha Yesu kujitangaza kuwa Mfalme. Pili, kwamba Yesu alimaanisha sana juu ya kifo chake, kiasi kwamba alistahili fedha kwa muda alioupoteza kwa kuzunguka kwake kote kwa muda wa miaka mitatu. Katika nadharia zote mbili, alijitumainia yeye mwenyewe na wala hakumtumaini Yesu.)

 

2.                  Soma Mathayo 18:7. Je, maelezo haya yanazungumzia hali aliyo nayo Yuda?

 

B.                 Soma Mathayo 26:17-22. Wanafunzi walichukulia kwamba bado usaliti ulikuwa haujaanza kufanyika. Kwa nini? (Kwa sababu wote, isipokuwa Yuda, walikuwa hawajamsaliti Yesu.)

 

1.                  Tumejadili mawazo yangu kuhusu njama ya Yuda. Wanafunzi wengine walikuwa wanafikiria nini – je, mawazoni mwao waliwaza kwamba wangeweza kutengeneza fedha kiasi katika hiki kizungumkuti cha kubadilika kwa matukio? (Walikuwa na masikitiko kuhusiana na habari hii, na walikuwa na wasiwasi kwamba wanaweza wasiwe watu wa kutegemewa.)

 

2.                  Kwa nini Yesu alibainisha ukweli kwamba atasalitiwa? Unadhani alitaka kumfanya Yuda ajisikie hatia, au alitaka Yuda aachane na mpango wake, au Yesu alikuwa na wazo jingine mawazoni mwake?

 

C.                 Soma Mathayo 26:23-25. Hili ni tukio kubwa sana mawazoni mwa wanafunzi. Je, unadhani walielewa kwamba Yuda alikuwa anamsaliti Yesu?

 

1.                  Ikiwa ndivyo, kwa nini hawakumshambulia Yuda? Kwa nini wasimtishe ili asiweze kumsaliti? Kwa nini wasimzuie (wasimweke kizuizini) ili asiweze kumsaliti Yesu?

 

2.                  Yuda aliposema, “Ni mimi, Rabi?,” je, hiyo inatuambia nini kuhusu utayari wake wa kuachana na mpango wake? (Yuda alikuwa ameshafanya uamuzi. Sasa alisema uongo ili kuuficha uamuzi wake.)

 


III.              Mlo Wake wa Mwisho

 

A.                Soma Mathayo 26:26-30. Jiweke kwenye nafasi ya wanafunzi. Je, ungeweza kufahamu chochote ya kile ambacho Yesu alikuwa anakizungumzia? Kwanza anasema anakaribia kuuawa, na sasa kiishara anazungumzia kuhusu kuula mwili wake na kuinywa damu yake.

 

B.                 Angalia kile tulichojifunza hadi sasa. Wanafunzi wanadhani kuwa wana mawazo mazuri zaidi kuliko ya mwanamke. Yuda anadhani ana mawazo bora kuliko mawazo ya Yesu. Unadhani Mathayo anamaanisha nini kwa kuandika hapa haya maelezo ya Mlo Wake wa Mwisho?

 

IV.              Petro

 

A.                Soma Mathayo 26:31-35. Unadhani Petro anasema ukweli? (Soma Yohana 18:10-11. Katika maelezo ya Yohana juu ya kukamatwa kwa Yesu, Petro anachomoa upanga wake, yuko radhi kufa kwa ajili ya Yesu. Anasema ukweli.)

 

1.                  Petro anatofautianaje na Yohana? (Yesu haenendi ili kujinufaisha yeye mwenyewe.)

 

B.                 Hebu turuke mafungu kadhaa baada ya kukamatwa kwa Yesu. Soma Mathayo 26:57-58. Je, bado Petro anadhihirisha ujasiri mkubwa?

 

C.                 Soma Mathayo 26:69-75. Jana, nilimsikiliza mtu aliyekuwa na dhamira njema akisimulia jinsi ambavyo tunatakiwa kutia bidii kujiepusha na dhambi, kwamba tunakabiliana na Shetani, na kwamba bora tuwe tayari kwa ajili ya pambano dhidi ya dhambi (huku Yesu akitusaidia). Anguko la Petro ni lipi? Anadhihirisha kasoro gani kitabia? Kuna dosari gani kwenye haiba yake ni tatizo kubwa? (Petro alikuwa na Yesu muda wote tena kwa ukamilifu. Alikuwa radhi kupambana hadi kufa. Lakini, alichanganyikiwa kwa kitendo cha Yesu kutopambana na kitendo cha Yesu kuzungumzia kuhusu kuula mwili wake na kuinywa damu yake. Yesu hakujua nini cha kufikiri.)

 

1.                  Ni jambo gani basi ambalo Petro alipaswa kulifanya? (Kumtumaini Yesu tu.)

 

D.                Hebu turejee kwenye somo letu. Kwenye mjadala kati ya wanafunzi na mwanamke juu ya matumizi bora ya marhamu, nani alikuwa anamtumaini Yesu na nani alikuwa anayatumaini mawazo yake mwenyewe? (Wanafunzi walikuwa wanayatumaini mawazo yao wenyewe.)

 

E.                 Katika maelezo ya usaliti wa Yuda, je, Yuda anamtumaini nani? (Anajitumainia mwenyewe. Anadhani ana ufahamu (anajua) zaidi ya Yesu.)

 

F.                  Kwenye kumbukumbu ya Mlo Wake wa Mwisho, Yesu anamaanisha nini kuhusu kuula mwili wake na kuinywa damu yake? (Wokovu unapatikana kwa njia ya Yesu pekee. Yeye ndiye Kondoo wa kafara wa huduma ya patakatifu (hekalu). Yeye ndiye njia pekee ya kuufikia wokovu.)

 

G.                Petro hadhani kwamba yeye ni mwerevu zaidi ya Yesu. Ingawa yu radhi kufa, kwa namna fulani ameharibu mambo na kumkana (kumsaliti) Yesu. Je, Petro alipaswa kufanya nini ili kuepuka matokeo haya? (Soma tena Mathayo 26:31-33. Petro angeweka kando majivuno yake na kumwuliza Yesu, “Nawezaje kuepuka kufanya hivyo? Niambie ninachotakiwa kukifanya ili niweze kukusaidia kikamilifu badala ya kukukana.”)


 

H.                Rafiki, sidhani kama ni wazo jema kujiandaa kwa ngumi ili kupambana na Shetani. Sidhani kama ni wazo zuri kujikita kwenye kuchunguza na kukomesha kila dhambi maishani mwako. Kiini cha maisha yako lazima kiwe ni kumtumaini Mungu, hata pale dunia yote inapoonekana kuwa nje kabisa ya udhibiti. Unaweza kuanza kufanya hivyo sasa hivi kwa kumwomba Roho Mtakatifu kila siku, kuongoza kila uamuzi wako na kila wazo lako ili iweze kuwa tabia yako kumtumaini Mungu.

 

V.                Juma lijalo: Mteswa na Mfufuka.