Jesus’ Teaching and the Great Controversy

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Matthew 7, 11 & 12)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
1
Lesson Number: 
7

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umewahi tu kuliangalia suala la “Pambano Kuu” kwa juujuu? Pambano hilo ni kati ya wema na uovu, kati ya Yesu na Shetani. Lichunguze kwa kina zaidi. Je, pambano kuu halizungumzii kuhusu uelewa wa asili ya Mungu? Je, hicho sicho ambacho “pambano” linakihusu? Somo letu juma hili linaashiria hivyo. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

  1. Mwamba wa Upendo
  • Soma Mathayo 7:24-27. Sote tunafahamu tatizo la kujenga nyumba karibu na mkondo wa maji kwenye msingi ulio juu ya mchanga. Je, jambo hili linahusikaje katika maisha yetu ya Kikristo? (Yesu anasema kuwa msingi imara wa maisha ni kuyaweka maneno yake katika vitendo.)
    1. Ni maneno gani hayo? (Tunatakiwa kuujua muktadha kwa sababu jambo hili linaonekana kuwa la muhimu sana.)
  • Soma Mathayo 7:21-23. Ikiwa nitakuuliza kuwa, “Je, ni kutokana na mapenzi ya Mungu kwamba unatabiri, kuondoa pepo na kutenda miujiza,” utajibuje? (Ndiyo!)
    1. Je, maisha yako hayapungukiwi kwa kuzingatia maisha ya Wakristo wanaotenda haya matendo makuu?
    2. Endapo ungeweza kutenda jambo moja tu kati ya yale mambo, je, ungedhani kuwa Roho Mtakatifu alikuwa nawe kwa kukupatia uwezo?
    3. Hebu tuutafakari muktadha huu kidogo. Ikiwa kuyaweka maneno ya Yesu kivitendo si sawa na haya matendo makuu, na kuyatekeleza maneno ya Yesu kivitendo ni ufunguo wa msingi wa maisha ya Kikristo, je, “kuyatenda mapenzi ya Mungu” ni sawa na kufanya nini? (Kumjua Mungu – au angalao Mungu kukujua wewe.)
  • Bado ninapata shida kulifahamu jambo hili akilini mwangu. Soma tena Mathayo 7:21 na Mathayo 7:23. Fungu la kwanza linazungumzia kuyatenda mapenzi ya Mungu na fungu la pili linazungumzia Mungu kumjua mwanadamu. Unadhani “kuyatenda” mapenzi ya Mungu inamaanisha nini kivitendo? (Lazima iwe ni kumjua Mungu.)
    1. Je, hicho ndicho unachokifanya sasa unapojifunza Biblia? (Hii ni njia ya muhimu ya kumjua Mungu vizuri zaidi.)
  • Bado tunajitahidi kufahamu muktadha zaidi. Hebu turejee nyuma zaidi katika hii sura. Soma Mathayo 7:7-8. Je, unaiamini hii ahadi?
  • Soma Mathayo 7:9-12. Kwa nini Yesu anajenga hoja kwamba tunapaswa kuamini kuwa Mungu atatupatia mambo mazuri tunayoyaomba? (Yesu anasema hata wazazi huwapatia watoto wao vipawa vyema. Fikiria mtazamo wako dhidi ya wanao. Huo ni chini ya mtazamo wa Mungu dhidi yako.)
    1. Utakumbuka tulianza kujifunza kwamba “kuyatenda” mapenzi ya Mungu ni kumjua Mungu – au angalao kutambua kwamba Mungu anatujua. Ulinganifu wa Mungu na wazazi unatusaidiaje kuelewa kinachomaanishwa kumjua Mungu? (Nadhani sasa ninaelewa! Msingi imara wa maisha ya Mkristo ni kujua kwamba Mungu anakupenda na anakupatia vipawa vyema. Sio kutenda matendo makuu. Yesu anasema hayo matendo makuu hayaoneshi kwamba mtu anamjua Mungu kama mzazi mwenye upendo.)
  • Soma Mathayo 7:15-20. Yesu anatuonya dhidi ya jambo gani? (Manabii wa uongo. Watu wanaoonekana kuwa watumishi wa Mungu lakini mafundisho yao na maisha yao hayauakisi ukweli.)
    1. Kutokana na kile tulichojifunza, mafundisho na maisha ya aina gani yanaakisi “tunda jema?” (Huduma inayotangaza taswira ya Mungu mwenye upendo ambaye mtazamo wake ni ule ule dhidi yetu kama ulivyo mtazamo wa wazazi wenye upendo kwa watoto wao!)
  • Kwa kuwa tunatembea kuelekea nyuma kwenye hii sura, hebu tusome Mathayo 7:1-5. Kwa nini tunatakiwa kutokuhukumu? (Tunahukumiwa kwa viwango vyetu wenyewe.)
    1. Kwa nini jambo hili ni ukweli? Jambo hili linahusianaje na kumjua Mungu? (Ikiwa mtazamo wa Mungu dhidi yetu ni sawa na mzazi mwenye upendo, basi mtazamo wa kuhukumu haumuwakilishi Mungu. Ni sawa na mwalimu wa uongo azaaye matunda mabaya. Ikiwa tunafahamu kwamba Mungu ni sawa na mzazi mwenye upendo, basi hatutajikita kwenye “vumbi chafu la mbao” kwenye jicho la mshiriki mwenzetu wa kanisa. Wazazi wangapi wenye upendo wanajikita kwenye vipengele chanya kwa watoto wao badala ya vipengele hasi? Wazazi wenye upendo wana mtazamo chanya.)
    2. Nira ya Upendo
  • Soma Mathayo 11:27. Tumeona kwamba msingi imara wa maisha yetu katika Kristo ni kumjua Mungu na kuuelewa upendo wake kwetu. Ni vigumu kiasi gani kuelewa jambo hili? (Fungu hili linasema kuwa asili ya Mungu hufunuliwa kwa wale ambao “Mwana apenda kumfunulia.”)
    1. Je, tunapaswa kushangaa kwamba watu wengi wanamtazama Mungu kuwa ni mkatili na kutoelewa kilicho cha muhimu zaidi katika maisha ya Mkristo?
  • Soma Mathayo 11:28. Asili ya huu mzigo ni ipi? (Biblia haisemi chochote. Lakini inaonekana kuwa mizigo maishani. Huenda pia ni mzigo wa kutoyaelewa mapenzi ya Mungu maishani mwako, kutokuwa na msingi imara.)
  • Soma Mathayo 11:29. Je, ungependa kuvaa nira? (Nira inaunganisha nguvu za ng’ombe wawili ili kurahisisha kuvuta mkokoteni.)
    1. Je, kuna mkokoteni wowote umebainishwa hapa? (Tulijadili kuhusu kuwa na “mzigo.”)
    2. Nira hii inatoa pumziko. Hilo linawezekanaje? (Nadhani Yesu anatufundisha kwamba anatusaidia kutatua matatizo yetu maishani. Hii inatupatia “pumziko” dhidi ya kujaribu kutekeleza sisi wenyewe. Yesu ananyoosha mkono ili tuweze kuushikilia atusaidie.)
  • Soma Mathayo 11:30. Je, huu ni mzigo tofauti na ule uliozungumziwa katika Mathayo 11:28? (Lazima uwe tofauti. Mzigo wa awali unatuchosha. Tunatakiwa kupumzika kutokana na mzigo huo. Lakini mzigo mwingine ni “mwepesi.”)
    1. Kwa nini mzigo wa pili ni mwepesi sana? (Tunaungana na Yesu.)
    2. Hebu turejee kwenye kile tulichojifunza: mtazamo wa Mungu dhidi yetu ni sawa na mtazamo wetu dhidi ya watoto wetu. Je, wazazi wema watawafanyia watoto wao kila kitu? (Hapana. Mtoto hatajifunza ikiwa mzazi atafanya kila kitu. Taswira ya kiakili ya “nira” ni kwamba Yesu anatenda kazi pamoja nasi ili kukabiliana na matatizo maishani.)
    3. Rehema
  • Soma Mathayo 12:1-2. Kwa nini wanafunzi walivunja masuke na kuyala siku ya Sabato? (Kwa sababu walikuwa na njaa.)
    1. Je, Mafarisayo wanakuwa na tabia ya kuhukumu? Soma tena Mathayo 7:1-3. (Ndiyo.)
  • Soma Mathayo 12:3-4. Kwa nini Yesu anatumia mfano ambao anakiri kuwa “sio halali?” (Je, hiki si kielelezo kamili cha mtazamo wa Mungu kama mzazi mwenye upendo akinyanyua mzigo kutoka kwa wanaye? Daudi na watu wake wana njaa. Wanafunzi wa Yesu wana njaa. Yesu anasema ninayatanguliza mahitaji ya wafuasi wangu mbele badala ya kuitanguliza sheria.)
    1. Hadi kufikia hapa yumkini ukawa unaziangalia sana sheria. Sheria iliyokuwa inaangaliwa ni kufanya kazi siku ya Sabato (Kutoka 20:10). Kwa nini Yesu hakusema, “Wanachokifanya wanafunzi wangu sio kazi?” Kwa nini anaonekana kukiri kwamba walichokuwa wanakifanya ni kazi na badala yake anajenga hoja kuwa, “Daudi alifanya hivyo!”
  • Soma Mathayo 12:7-8. Sidhani kama tunatakiwa kukomea kwenye “Daudi alifanya hivyo.” Sababu gani ya kweli inamfanya Yesu aseme kuwa hii ni sahihi? (Kwa sababu inaonesha rehema. Sheria za Mungu zipo kwa ajili ya manufaa yetu. Kwa kuwa Mafarisayo hawakumjua Mungu, kwa kuwa hawakuuelewa upendo wa Mungu, walipendelea sheria dhidi ya rehema. Yesu anasema “Nataka rehema, wala si sadaka.”)
    1. Je, hii inamaanisha kuwa “upendo huishinda sheria?” Kama ndivyo, kwa nini Mungu alitupatia sheria? (Sasa tunaanza kumjua Mungu vizuri zaidi. Lengo la sheria ni kuboresha maisha yetu. Kwa kawaida, kufuata sheria ya Mungu ni njia bora ya kufurahia maisha dhidi ya matatizo yasiyo ya lazima. Lakini, kuna nyakati ambazo sheria zinakinzana na upendo ambao mzazi angeuonesha kwa mtoto.)
    2. Utaona kwamba Yesu anasema, Mimi ndiye “Bwana wa Sabato.” Je, hiyo inamaanisha nini? (Anachokisema Yesu kinamaanisha jinsi sheria inavyopaswa kutumika.)
      1. Tunaidhinishwa kusema kuwa, “Achana na ile sheria kwa sababu inakinzana na upendo?” (Kuna jambo la muhimu hapa. Mungu alitengeneza sheria, hatuna haki ya kuzitengua. Kwa upande mwingine, Yesu anaonya dhidi ya kuwa watu wa kuhukumu. Tunatakiwa kumwomba Roho Mtakatifu kuyaongoza mawazo yetu pale ambapo matumizi ya sheria hayaakisi upendo wa Mungu.)
  • Rafiki, je, unauelewa mtazamo wa Mungu dhidi yako? Je, unafahamu kwamba katika kila hali atatenda kwa ajili yako, ikiwa utamruhusu, kile ambacho wazazi wenye upendo watamtendea mtoto wao? Je, utafanya uamuzi leo kumtumaini Mungu na kuuakisi upendo wake?
    1. Juma lijalo: Ndugu Wakiwa Pamoja.