Pambano Linaendelea

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(1 Samweli 17, 2 Samweli 11-12, Nehemia 1-2)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
1
Lesson Number: 
5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Mungu anakuhitaji ufanye nini? Mika 6:8 inajibu kuwa “Kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.” Mifano tuliyojifunza juma hili na juma lililopita kuhusu viongozi wa Mungu wa zamani, inaweza kukufanya upigwe butwaa kwamba ni kwa jinsi gani inaendana na jibu la Mika. Kitu kinachotujia mawazoni mwetu kwa nguvu ni kwamba tunatakiwa kusimama imara kumtii Mungu katika nyakati za changamoto. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi juu ya kile ambacho Mungu anatutaka tujifunze!

  1. Daudi
    1. Soma 1 Samweli 17:20-24. Unadhani Daudi alifikiri kuwa anaweza kuendelea mbele kidogo kupigana kwenye vita ambavyo hakuruhusiwa?
      1. Unadhani mwitikio wa Daudi ulikuwaje alipowaona Waisraeli wakimkimbia Goliathi kwa woga? (Soma 1 Samweli 17:26. Daudi anaona kwamba huu ni udhalilishaji. Mungu amedhalilishwa na hawa watu waoga.)
    2. Soma 1 Samweli 17:28. Eliabu anaashiria nini kumhusu Daudi? (Kwamba Daudi sio wa muhimu, ana kiburi, na kiukweli yeye ni mwoga anayeogopa kupigana, anataka tu kushuhudia vita.)
      1. Kwa nini Eliabu anasema mambo hayo ya kutisha kwa ndugu yake? (Anafahamu kwamba hivyo ndivyo Daudi anavyomchukulia (na kimsingi jeshi lote), hivyo Eliabu anamdhihaki Daudi kwa kutumia dhana hiyo hiyo.)
    3. Soma 1 Samweli 17:31. Hii inatuambia nini kuhusu Sauli? (Alikuwa amekata tamaa. Kwa nini mfalme amwite kijana mdogo mchungaji?)
    4. Soma 1 Samweli 17:32-37. Daudi anaweka matumaini yake kwa nani? (Kwa Mungu. Imani yake ni kubwa kupita kiasi.)
    5. Soma 1 Samweli 17:40-44. Goliathi ana mtazamo gani juu ya changamoto inayotolewa na Daudi? (Aliona kwamba anadharauliwa. Tuna ukubali wa pamoja mahali kote juu ya ushindi wa Daudi. Hata inaonesha kwa wazi zaidi hitaji kuu la Mfalme Sauli.)
    6. Soma 1 Samweli 17:45-47. Daudi ameingiza jambo gani kwenye pambano? (Jambo lisilo la kawaida. Kwa dhahiri Daudi anasema kuwa Mungu ndiye atakayeshinda hili pambano. Daudi hachukui sifa kwa ushindi wake unaotarajiwa.)
    7. Soma 1 Samweli 17:48-51. Soma tena 1 Samweli 17:43. Goliathi ameshindwa kutambua kitu gani? (Kombeo. Anatarajia mpambano wa mkono kwa mkono, Daudi atakapotumia “fimbo.”)
      1. Je, Goliathi anaomba kwa kutumia nguvu zisizo za kawaida? (Ndiyo. “Mfilisti alimlaani Daudi kwa miungu yake.”
      2. Tuna nini cha kujifunza maishani kutoka kwa Daudi? Una maoni gani kumhusu Daudi?
    8. Soma 2 Samweli 11:1. Kuna jambo gani tofauti kwa Mfalme Daudi? (Kwa dhahiri amepoteza tamaa yake ya kupambana na watu wabaya.)
      1. Kwa nini? Umri? Uvivu? “Maisha bora?”
  2. Soma 2 Samweli 11:2. Je, huwa unakuwa na wakati mgumu zaidi kupata usingizi unapokuwa huna kazi zinazoshughulisha viungo vya mwili?
    1. Je, Bathsheba anafahamu kuwa mtu yeyote juu ya dari la jumba la mfalme anaweza kumwona? Unadhani anafahamu kuwa Daudi anazungukazunguka darini wakati wa usiku?
  3. Soma 2 Samweli 11:3-4. Ni wakati gani ambapo Daudi anatenda dhambi? Je, ni wakati anapoagiza mwanamke huyo akaletwe wakati akijua kuwa ameolewa? Au, wakati anapolala naye?
  4. Soma 2 Samweli 11:5. Jambo gani limebadilika katika maisha ya Daudi? (Dhambi ya siri ya Daudi inakaribia kuwa dhambi ya dhahiri kwa watu wote.)
  5. Bila mafanikio, Daudi anajaribu kuficha hii dhambi. Kisha Daudi anafanya mipango ili mume wa Bathsheba auawe vitani, pamoja na askari wengine. Soma 2 Samweli 11:26-27. Unadhani ni kwa jinsi gani kijana Daudi anakuwa Mfalme Daudi mtu mzima?
  6. Soma 2 Samweli 12:7-10 na Waebrania 11:32-34. Ni kwa namna gani Daudi anajumuishwa kama mmojawapo wa mashujaa wa imani?
    1. Ni kwa jinsi gani Daudi anafananishwa na Samsoni, ambaye naye pia anaorodheshwa kama shujaa? (Wote walikuwa na tatizo la tamaa ya wanawake.)
  7. Soma 2 Samweli 12:11-14. Tunajifunza nini kuhusu kutenda dhambi dhidi ya “jirani yetu?” (Dhambi zetu dhidi ya watu wengine zinaturudia na kutudhuru. Aina hii ya dhambi ina matoke mabaya ya kutisha.)
    1. Mungu anaonekana kujali jambo gani kwa dhati zaidi? (Maadui wa Mungu wanadhihirisha dharau kubwa.)
    2. Soma tena 2 Samweli 12:13. Je, unakubaliana na Daudi, kwamba amemfanyia Mungu dhambi? (Hiki ndicho tulichokijadili juma lililopita. Nusu ya kwanza ya Amri za Mungu, huduma yetu kwa Mungu ni jambo la muhimu sana. Watu wengi wanadhani Daudi alitenda dhambi dhidi ya mume wa Bathsheba na askari wengine waliouawa. Lakini, Daudi na Mungu wanaelewa kuwa suala la msingi ni jinsi jambo hili linavyomwathiri Mungu, jinsi linavyoathiri pambano kati ya wema na uovu. Unaepuka kukiuka nusu ya pili ya Amri Kumi za Mungu kwa sababu wewe si punguani na hutaki kuteseka. Unatii amri tano za kwanza kwa sababu ya utiifu kwa Mungu.)
      1. Ni kwa namna gani hizi sehemu mbili, yaani, nusu ya kwanza na nusu ya pili ya Amri Kumi zinaathiriana? (Wote wawili, yaani Daudi na Samsoni walimfanya Mungu aonekane mbaya kutokana na dhambi yao ya zinaa.)
  • Hezekia
    1. Soma 2 Wafalme 19:9-13. Unauelewaje umuhimu wa ujumbe wa barua ya Mfalme Senakeribu kwa Mfalme Hezekia? (Hakuna mungu ambaye ameweza kusimama dhidi yangu, na Mungu wako hatakuwa na lolote jipya.)
    2. Soma 2 Wafalme 19:14-16. Kwa nini Mfalme Hezekia hasemi “watu wenu wengi watakufa ikiwa hamtatenda jambo fulani? Taifa lenu litaangamizwa ikiwa hamtaingilia kati? (Hezekia amepatia kabisa, suala lililopo ni kuhusu heshima kwa Mungu. Anamwambia Mungu kuwa hii ni “dhihaka” kwako.)
    3. Soma 2 Wafalme 19:17-19. Hii inakufundisha nini kuhusu maombi yako unapokuwa kwenye matatizo?
    4. Soma 2 Wafalme 19:20-22 na 2 Wafalme 19:27-28. Je, Mungu anafahamu mahali wanakoishi maadui wetu?
    5. Soma 2 Wafalme 19:32-34. Kwa nini Mungu ataiokoa Yerusalemu na watu wake? (Kwa ajili yake na kwa ajili ya Daudi.)
    6. Soma 2 Wafalme 19:35-36. Je, Mfalme Hezekia ana haja ya kuhatarisha maisha yake vitani? (Hapana.)
      1. Hii inakufundisha nini kuhusu matatizo unayokabiliana nayo – ikiwa utasimama imara kwa kumheshimu Mungu?
  • Nehemia
    1. Mafungu ya kwanza ya Nehemia yanaelezea hali ya kutisha ya Yerusalemu baada ya kuangamizwa na Babeli. Soma Nehemia 1:4-7. Nehemia anaanzaje maombi (sala) yake? (Kwa kumtukuza Mungu.)
      1. Watu wa Mungu wamemwangushaje? (Sehemu ya utukufu wa Mungu ni kwamba anatunza ahadi zake, tatizo ni kwamba hatusimamii upande wetu wa mkataba.)
    2. Soma Nehemia 1:8-9. “Maelekezo” haya kwa Musa yalitolewa muda mrefu sana hapo zamani. Je, ahadi hiyo bado inahusika?
      1. Kama ndivyo, kwa nini inahusika? (Nehemia anaiunganisha ahadi iliyotolewa kwa Musa na utukufu wa Mungu. Anairejea Yerusalemu kama mahali alipopachagua “ili kuliweka jina langu hapo.”)
    3. Soma Nehemia 1:10-11. Ikiwa unayachukulia maombi ya Nehemia kama hoja, elezea mantiki ya maombi hayo? (Anajenga hoja kwamba Mungu ana mkataba (“agano”) na wale wanaompenda na kumtii. Mkataba huo ni kwamba ikiwa unamtii Mungu, maisha yatakuwa bora, na kitendo hiki kitaleta utukufu kwa jina la Mungu. Anakiri kwamba watu walimwangusha Mungu, lakini anasema kuwa yeye pamoja na kundi la watu wengine wanataka kuingia tena kwenye huu mkataba.)
      1. Je, mkataba huu uko wazi kwa ajili yako? (Nadhani.)
        1. Bila shaka kila mkataba una lengo la jumla, na manufaa kwa pande zote mbili katika mkataba huo. Lengo la jumla la mkataba huu ni lipi? (Kuutangaza utukufu wa Mungu.)
        2. Kuna manufaa gani kwa wanadamu? (Wafuasi wa Mungu wanapofanya vizuri, Mungu anatukuzwa.)
          1. (1) Je, hii ni kanuni isiyo na ukomo? (Hapana. Wakati mwingine Mungu anatukuzwa tunapokuwa waaminifu kupitia kwenye dhiki na taabu.)
    4. Rafiki, lengo la maisha yetu linapaswa kuwa ni kumpa Mungu utukufu. Maisha yako yanampaje Mungu utukufu? Ikiwa ni vigumu kusema, kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu ayafungue macho yako kwenye fursa za kumpa Mungu utukufu?
  • Juma lijalo: Ushindi Nyikani.