Mpambano (Ugomvi) na Mtafaruku : Waamuzi

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Waamuzi 4, 6, 7 & 14-16)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
1
Lesson Number: 
4

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unakabiliana na hofu? Je, unapambana sana dhidi ya kutokuwa na imani au kuwa na imani hafifu na unapungukiwa uaminifu? Mimi nafahamu kwamba ninao upungufu huo. Miezi kadhaa iliyopita, nilipangiwa kutoa utetezi kwenye Mahakama na Rufaa ya Marekani – mahakama ambayo moja kwa moja ipo chini ya Mahakama Kuu ya Marekani. Ratiba hiyo ilinisababishia hofu. Hata hivyo, muda mfupi kabla sijatoa utetezi wangu nilihubiri kuhusu kumtumaini Mungu na hubiri hilo lilinipa nguvu kubwa. Mungu alinisaidia na mjadala ulienda vizuri. Somo letu juma hili linawahusu wanaume na wanawake wanaokabiliana na hatari kubwa. Hebu tuchimbue somo letu la Biblia ili tuone kama tunaweza kupata ushujaa wa kukabiliana na matatizo yetu na hofu zetu!

  1. Mwamuzi Debora
    1. Soma Waamuzi 4:1-3. Hapa “watu wabaya” ni akina nani? (Mfalme Yabini na amiri wa jeshi, Sisera.)
      1. Jambo gani liliwapa mamlaka juu ya watu wa Mungu? (Mungu “aliwauza” kwa sababu hawakuwa waaminifu. Pia kuna suala la magari 900 – faida kubwa ya kijeshi dhidi ya watu wabaya.)
    2. Soma Waamuzi 4:4-5. Nani anayewaongoza watu wa Mungu katika kipindi hicho? (Debora.)
      1. Vigezo vyake hadi kuwa kiongozi ni vipi? (Yeye ni nabii wa Mungu. Watu wa Mungu wanamwendea ili kutatua mitafaruku yao – hii inaonesha kuwa waliyatambua mamlaka yake.)
  2. Mpango wa Pambano
    1. Soma Waamuzi 4:6-7. Mungu amempa Debora mpango gani wa pambano? (Baraka anatakiwa kukusanya askari 10,000 na kwenda katika mto wa Kishoni.)
      1. Unaona udhaifu wowote kwenye huu mpango wa vita? (Tofauti na kutumia “mtego,” hauelezei mkakati wa vita. Vipi kuhusu magari? Mungu anasema kuwa atawapa ushindi.)
    2. Soma Waamuzi 4:8-10. Unadhani kwa nini Mungu alimchagua Baraka kuongoza majeshi?
      1. Tafakari maneno yake. Je, yuko radhi kutomtii Mungu? (Ndiyo! Anasema kuwa atafanya hivyo ikiwa tu Debora ataambatana naye.)
        1. Jambo hili linaonesha kuwa Debora ni mtu wa namna gani? (Ana imani na ujasiri na ni mtu mwenye kuwatia hamasa watu wengine.)
          1. (1) Je, kuna maelezo mengine ya jambo hili ambayo yanampa Baraka upendeleo? (Inawezekana Baraka anajali na kuthamini uaminifu wa Debora. Anaona kwamba ikiwa Debora yu radhi kuhatarisha maisha yake, basi hasemi uongo kuhusu maelekezo ya Mungu.)
        2. Hatujajadili jambo lisilo la kawaida la Debora kuwa kiongozi wa Israeli. Debora anathibitishaje hili tatizo la kiutamaduni? (Anasema kuwa Mungu atamwuza Sisera kwa mkono wa mwanamke – kana kwamba hilo ni jambo lisilotarajiwa au jambo hasi.)
    3. Soma Waamuzi 4:14-16. Nini kilitokea licha ya manufaa makubwa ya kijeshi ikiwemo farasi na magari dhidi ya askari wa ardhini? (Waisraeli wanashinda. Wanaua jeshi lote la adui na kuchukua magari mengi!)
    4. Soma Waamuzi 4:17-21. Wanaume: je, wanawake wanaaminika? (Utagundua kwamba Mungu anawaamini.)
      1. Je, hii ndio sababu wanaume wengi siku hizi wanaishi kwenye nyumba na si kwenye mahema?
      2. Soma tena Waamuzi 4:9. Nilidhani Debora alimaanisha kuwa Mungu atampeleka Sisera kwake. Inamaanisha nini Mungu kumpeleka Sisera kwa Yaeli? (Suala hili linahusu masuala ya jinsia.)
        1. Nini kinamaanishwa? (Inaonekana kwamba ikiwa wanaume hawataongoza, Mungu atawachagua wanawake kuongoza. (Huenda ni kutokana na Mwanzo 3:16, ambayo tuliisoma hivi karibuni.) lakini, hatimaye Mungu anamchagua mtu anayemtumaini yeye (Mungu), bila kujali jinsia.)
    5. Soma Waamuzi 4:22-24. Je, hapa wanawake wamebadili historia ya kijeshi? (Ndiyo, walimtumaini Mungu na matokeo yake ni kulishinda jeshi kubwa na lenye nguvu lililokuwa linawapinga watu wa Mungu.)
  3. Mwamuzi Gideoni
    1. Soma Waamuzi 6:1-2. Sasa watu wabaya ni akina nani, na kwa nini wana udhibiti wa kimamlaka? (Kwa mara nyingine watu wa Mungu walimwangusha Mungu, kwa hiyo Mungu anawaruhusu Wamidiani kuwanyanyasa watu wake.)
    2. Soma Waamuzi 6:3-6. Wamidiani wanatumia mkakati gani kuwadhibiti watu wa Mungu? (Ama wanaharibu au wanakula chakula chote.)
    3. Soma Waamuzi 6:7-10. Watu wanapomwita Mungu, je, anawapuuzia? (Hapana, Mungu anamtuma nabii anayewaelezea sababu ya kutokea kwa matatizo yao.)
    4. Soma Waamuzi 6:11. Kwa nini Gideoni anapepeta ngano ndani ya shinikizo? Matumizi ya chombo hicho yanaashiria ugumu gani? (Shinikizo ni chombo kikubwa mfano wa pipa kilichotengenezwa kwa mbao. Upepo unatakiwa kuvuma ili kuondoa takataka (makapi) wakati ngano inapopepetwa. Kwa hakika pipa sio chombo cha kukitumia wakati unapopepeta. Tunaweza tu kuhitimisha kwamba Gideoni anafanya hivi ili kuficha chakula chake dhidi ya Wamidiani.
    5. Soma Waamuzi 6:12. Je, malaika anamdhihaki Gideoni? “Pipa zuri, ee shujaa!”
    6. Soma Waamuzi 6:13. Gideoni anamlaumu nani kutokana na ukweli kwamba “shujaa” amejificha kwenye pipa? (Anaonekana kusema, “Nitakuwa mwerevu zaidi ikiwa Mungu atatokea na kutenda jambo kuu.” Gideoni, kama ilivyo kwa Adamu, anaonekana kumlaumu Mungu.)
    7. Soma Waamuzi 6:14-16. Je, Gideoni, kama ilivyo kwa Baraka, anamhitaji mwanamke ili kumtia hamasa?
      1. Niambie unadhani Mungu anasema nini katika fungu la 16? (Mungu anasema “Unachokihitaji ili kushinda si kitu kingine bali Mimi. Unasema kuwa sikuwa wa msaada? Nipo hapa, hebu tutekeleze jambo hili pamoja.”)
    8. Soma Waamuzi 6:17. Unaichukuliaje imani ya Gideoni?
  4. Soma Waamuzi 6:20-23. Gideoni anasema, “Tafadhali usiondoke hapa, nataka kuleta sadaka.” Mungu anamtendea nini Gideoni? (Anampa ishara. Angalia subira ya Mungu na jinsi anavyoshughulika na mashaka ya Gideoni.)
    1. Tunaruka mambo mengi sana kuhusu kisa hiki cha kufurahisha mno. Soma Waamuzi 6:33 na Waamuzi 7:19-22. Watu wangapi wapo pamoja na Gideoni katika kulishambulia jeshi la Midiani? (Watu mia moja.)
      1. Washambuliaji mia moja wameshika nini mikononi mwao? (Kifaa cha muziki na mienge.)
      2. Soma tena Waamuzi 6:15. Gideoni alikuwa na wasiwasi gani kuhusu kukabiliana na Wamidiani? (Alikuwa mnyonge na walikuwa wachache.)
      3. Kuna fundisho gani kwetu leo? (Kilicho cha muhimu katika kuwashinda watu wabaya ni Mungu pamoja na wewe kufanya kazi pamoja.)
  5. Samsoni
    1. Soma Waamuzi 14:1-2. Kwa nini Samsoni anadai kwamba wazazi wake wampatie mke? (Soma Kutoka 22:17. Akina baba walitakiwa kuidhinisha ndoa.)
    2. Soma Waamuzi 14:3. Je, wazazi wa Samsoni wanaidhinisha? Je, wanapaswa kuidhinisha? (Soma Kumbukumbu la Torati 7:1-3. Hawapaswi kuidhinisha kwa sababu Samsoni anataka kumwoa mtu ambaye hamwabudu Mungu wa kweli.)
    3. Soma Waamuzi 14:4. Wazazi wanaweza kujifunza nini kutokana na jambo hili? Kwamba kila amri inakuja na tanbihi (maelezo ya ziada), maelezo yanayosema kuwa Mungu anafanya jambo lisilo la kawaida katika mazingira fulani?
    4. Soma Waamuzi 14:5-9. Kwa nini Samsoni hakujigamba kwa kitendo cha kumwua simba na asali ya ziada aliyoipata kutoka kwenye mzoga wa simba huyo? (Mambo ya Walawi 11:39-40 inabainisha kuwa wazazi wa Samsoni wangechukulia kwamba kula asali hiyo kungewafanya kuwa najisi.)
      1. Je, haya matukio mawili yanatufundisha nini? (Samsoni hajali sheria.)
    5. Soma Waamuzi 13:6-8 ili kufahamu kisa kinachohusu kuzaliwa kwa Samsoni. Unadhani wazazi wa Samsoni wanajisikiaje kuhusu mtazamo wake wa kutokuwa mwangalifu dhidi ya amri za Mungu? (Nina uhakika hawafurahii hata kidogo, na wanadhani kuwa wanamwangusha sana Mungu.)
    6. Soma Waamuzi 15:20 na Waamuzi 16:1. Samsoni ni Mwamuzi! Je, Samsoni ni mtu wa namna gani?
    7. Samsoni anaishia kukamatwa na kutiwa upofu na maadui zake. Soma Waamuzi 16:25-30. Je, Mungu anasikia maombi ya wadhambi? (Ndiyo.)
    8. Soma Waebrania 11:32-33. Unaelezeaje kitendo cha watu hawa kuorodheshwa kwenye orodha ya “mashujaa wa imani?”
      1. Watu wa Mungu walibadilika na kuwa watu wabaya pale waliposhindwa kumfuata Mungu. Watu hawa wana tofauti gani? (Suala la msingi ni kumtegemea Mungu. Matendo yao yalikuwa legelege (au mabaya sana), lakini kwa ujumla walimtegemea Mungu.)
  6. Rafiki, je, utadhamiria leo kumtegemea Mungu – kumtumaini siku zote?
  7. Juma lijalo: Mpambano Unaendelea.