Wanawake na Mvinyo

(Mithali 31)
Swahili
Year: 
2015
Quarter: 
1
Lesson Number: 
13

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kauli ya “Wanawake na mvinyo” inaonekana kama ni wimbo, sawa? Wanawake, huku wakidhani kwamba jambo hili linaweza lisiwe linajielekeza kwenye uelekeo utakaowaweka kwenye njia sahihi, wanauliza, “Kwa nini isiwe Wanaume na Bia?” Mithali imetupatia ushauri chanya ili kuboresha maisha yetu, na ushauri unaotolewa katika somo hili ambalo ni la mwisho katika mfululizo wa masomo yetu ya robo hii, hautakuwa tofauti. Hatutajifunza ushauri chanya wa Mungu kwa wanawake pekee, bali tutaanza na hekima ya mwanamke. Hebu tuzame kwenye Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!

  1. Hekima ya Mama Yake Lemueli!
    1. Soma Mithali 31:1. Chanzo cha hekima hii ni kipi? (Mama yake Lemueli!)
    2. Soma Mithali 31:2-3. Kwa nini mama yake Lemueli anatabanaisha mambo aliyoyasema katika mafungu haya mawili? (Anamkumbusha Lemueli juu ya ukaribu wao – yeye ni mama yake, ambaye alimzaa na kuweka nadhiri juu yake. jina lake linamaanisha “kwa ajili ya Mungu,” kwa hiyo hii inaashiria kwamba alimuweka wakfu kwa Mungu.)
      1. Lemueli anapewa onyo gani na mama yake katika Mithali 31:3? (Asitumie “nguvu” zake kwa wanawake wala “moyo [juhudi]” wake kwa “wale waharibuo wafalme.”)
        1. Kwa nini “nguvu” na “juhudi” vinarejewa? (Nadhani dhana nzima iliyopo ni kwamba hupaswi kutumia muda wako mwingi na wanawake au yale mambo (au watu) yatakayokuangamiza wewe kama mtawala. Kimsingi watu wengi wanadhani kwamba “Lemueli” ni Selemani. Kwa kuwa Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300 (1 Wafalme 11:3), tunaweza kuelewa wasiwasi uliopo juu ya nguvu na moyo wake.)
    3. Soma Mithali 31:4-5. Kwa nini wafalme na watawala pekee ndio wanaotajwa na wala si watu wengine? (Wasiwasi uliopo ni kwamba wataacha kufuata “utawala wa sheria.” Badala ya kutawala kwa mujibu wa sheria, mfalme ataisahau sheria na kutenda tu kile anachoona kuwa ni sahihi wakati asipotafakari kwa makini sana.)
      1. Je, umewahi kutenda jambo lisilo sahihi wakati ambapo fikra zako hazikuwa vizuri zaidi?
    4. Soma Mithali 23:20-21. Mafungu haya yanasema kuwa kuna tatizo gani linalotokana na ulevi au ulaji wa kupindukia? (“Kuwa wenye kusinzia.” Kwa mara nyingine, tunaona tatizo ni kwamba unapoteza uwezo wako wa kufikiri vizuri wakati ambao ni wa muhimu kutenda mambo kwa usahihi.)
    5. Soma Mithali 31:6-7. Mama yake Lemueli anadhani kwamba ni vyema kumpatia mtu gani bia (kileo) na mvinyo? (Wale wanaokaribia kufa, wale walio na uchungu nafsini.)
      1. Kwa nini wazo hili ni jema? (Hatutaki mfalme asahau kanuni/sheria, lakini kwa watu wengine ni bora wakaisahau.)
        1. Je, ushauri huu unaonekana kuwa na mantiki? Ninaelewa ushauri wa kupunguza maumivu ya mtu anayekaribia kufa, lakini je, litakuwa ni jambo la msaada kwa kuwapatia kileo watu wenye uchungu na msongo wa mawazo? (Halionekani kuwa suluhisho la muda mrefu.)
    6. Soma Mithali 31:8-9. Unapoendelea kutafakari mafungu tuliyoyasoma hivi punde katika Mithali 31, je, unadhani jambo la msingi linahusu unywaji na kutumia muda mwingi na wanawake? (Jambo linaloonekana kuwa la msingi ni kutenda jambo sahihi. Kinachotarajiwa kutoka kwa wafalme ni kwamba watatawala kwa mujibu wa utawala wa sheria bila kujali hadhi ya mtu anayesimama hukumuni. Wale wasio wasomi na wanaoweza kujieleza kwa ufasaha, wale walio maskini na wasioweza kumsaidia mfalme, watu wa aina hiyo wote wanastahili kupata haki kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote yule.)
  2. Mwanamke Anayetafutwa
    1. Soma Mithali 31:10. Nadhani msitari wa kwanza, “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?” ni swali lisilohitaji jibu. Jibu linapaswa kuwa lipi? (Wanawake wa aina hiyo ni adimu – kama vito vya thamani.)
    2. Soma Mithali 31:11. Fungu linaposema mume wa “mke wa thamani” “hatakosa kupata mapato,” je, inamaanisha kwamba mke wa thamani huingiza fedha nyingi? (Hapana. Ikiwa una mke mwema, basi una kila kitu unachokihitaji.)
    3. Soma Mithali 31:12. Je, unajuaje kwamba unaye mke wa thamani? (Anamtendea mumewe mambo mema na wala hamdhuru.)
      1. Wake wa thamani wanaonekana kuwa wachache. Je, ni vigumu kiasi gani kutenda mema na kutomdhuru mwenzi wako?
      2. Unadhani njia ya kuweza kutimiza jambo hili ni ipi? (Kuishi kwa kuutegemea uongozi wa Roho Mtakatifu ndilo hitaji la kwanza. Lakini, kwangu mimi inaonekana kwamba lengo ni kutokuwa na ubinafsi.)
    4. Soma Mithali 31:13–15. Je, wanawake wa thamani hudamka? (Ndiyo!)
      1. Unafikiria nini juu ya ulinganifu wa mke wa thamani na “merikebu za biashara?” (Merikebu zibebazo mizigo ya biashara huleta utajiri mkubwa na bidha za aina mbalimbali. Inaonekana kuwa ni sifa kubwa kumlinganisha mke mwema na mapinduzi haya ya kibiashara.)
    5. Soma Mithali 31:16. Hii ni kauli ya kushangaza sana katika muktadha wa kihistoria. Utagundua kwamba mara kwa mara wanawake wamekuwa wakinyimwa haki ya kumiliki mali. Fungu hili linasema kuwa lengo la mke ni lipi? (Kufanya maamuzi yake binafsi ya kibiashara (“huangalia shamba”), kumiliki fedha zake binafsi na mali (“akalinunua kwa mapato yake”), na kujishughulisha na biashara (“hupanda mizabibu”).)
    6. Soma Mithali 31:17-18. Mafungu haya yanasema nini kuhusu taswira ya wanawake walegevu na tegemezi? (Yanasema kinyume chake (tofauti na mke wa thamani).)
      1. Huyu mke wa thamani anajihusisha na biashara gani nyingine? (Anafanya biashara yenye kuingiza faida.)
      2. Jambo hili linazungumzia nini kuhusu mtazamo wa Biblia juu ya shughuli huru za biashara? (Biblia inaipendekeza biashara hiyo na inapendekeza kwamba wanawake wawe sehemu ya hiyo biashara.)
    7. Soma Mithali 31:19 na Mithali 31:22 & 24. “Kazi za kike” (msitari wa 19) si sehemu ya msamiati wangu. Watoa maoni mbalimbali kuhusu Biblia hawako wazi juu ya hasa kinachomaanishwa kwenye fungu hili, lakini wengi wanaamini kwamba hiki ni aina ya kifaa kinachotumika kushona nguo. Mafungu ya 22 na 24 yanaunga mkono wazo hili.)
      1. Angalia tena Mithali 31:22. Unafikiria nini juu ya mavazi yake? (Hizi sio nguo za kawaida. Ni nguo nzuri na za thamani. Zinaashiria utajiri.)
      2. Soma 1 Petro 3:3-4. Je, maelezo ya mke wa thamani katika Mithali 31 yanakinzana na maelezo ya Petro juu ya mke wa Kikristo? (Mafungu haya mawili yanapaswa kusomwa kwa pamoja. Petro anasema urembo wa kweli hutokana na tabia na matendo. Soma sambamba na Mithali 31, Petro hasemi kwamba vito, mavazi mazuri na nywele zilizopambwa vizuri vinakatazwa, anasema tu kwamba havipaswi kuwa chanzo cha kweli cha uzuri/urembo wa mwanamke.)
    8. Soma Mithali 31:20. Mtazamo wake dhidi ya maskini ukoje? (Anawasaidia.)
      1. Unadhani rejea ya “mikono” inamaanisha nini? (“Mikono iliyokunjuliwa” inaonekana kuakisi mtazamo wa kuwakaribisha maskini, baada ya kuwaonea huruma. “Mikono” hutuambia kwamba mikono yake yote miwili inawasaidia wahitaji. Mtazamo wake unaungwa mkono na matendo ya “mikono yake miwili!”)
  3. Soma Mithali 31:23. Mumewe anahusikaje na jambo hili? Je, inamaanisha kwamba wake wa thamani wanaolewa vyema? (Mke anahusika kwenye mafanikio ya mumewe.)
    1. Soma Mithali 31:25. Je, mke huyu anakabiliana na ziku zijazo zenye kuchekesha? (Angalia mitazamo yake: nguvu, heshima/hadhi, na bila kuwa na wasiwasi juu ya wakati ujao.)
      1. Kwa kuwa hakuna mwanadamu awezaye kutabiri siku zijazo, je, mwanamke huyu ni mpumbavu na asiyejali (mzembe)? (Nusu ya mwisho ya Mathayo 6 ina maelekezo juu ya kutokuwa na wasiwasi kuhusu siku zijazo. Mungu atatulinda. Hata hivyo, Mithali 31 inaongezea jambo la msingi, tunatakiwa kuwa na bidii leo. Mungu hasemi kwamba, “kuwa mvivu na usiwe na wasiwasi.” Badala yake anasema kwamba, “kuwa na juhudi na unitumaini Mimi.”)
    2. Soma Mithali 31:28-29. Akina mama, je, ni mtazamo wa aina gani mnaotaka watoto na waume zenu wawe nao juu yenu? (Kuifuata kanuni hii hukupatia maangalizo mazuri kutoka kwa familia yako.)
    3. Soma Mithali 31:30. Wanaume, mtafanyaje ili kumpata mke wa thamani? Mtaangalia mambo gani? (Ucheshi, uzuri na uhusiano wake na Mungu.)
      1. Kipi kilicho cha muhimu zaidi? (Uhusiano wa mwanamke na Mungu. Mara kwa mara uzuri huwa unapotea kadri umri unavyozidi kuwa mkubwa. Baadhi ya wanawake huwa ni wema tu wakati wanapokuwa kwenye urafiki kabla ya ndoa. Lakini, uhusiano na Mungu unaweza kuwa tabia ya milele.)
    4. Soma Mithali 31:31. Waume wanapaswa kuwatendeaje wake zao wa thamani? (Kwa kuwapa thawabu na kuwasifia!)
    5. Rafiki, angalia mtazamo madhubuti wa Mungu dhidi ya wananake katika sura hii ya Mithali. Kwanza, Mungu anatuambia kuwa wao ni chanzo cha ushauri wa kuufanyia kazi. Pili, anatuambia kwamba wanapaswa kuruhusiwa kutumia uwezo wao mkubwa kuwabariki wale wanaowazunguka.
  4. Juma lijalo: Tutaanza kujifunza Injili ya Luka.