Kupitia Kwenye Kioo, kwa Jinsi ya Fumbo
Utangulizi: Hivi sasa ninasoma kitabu kinachoitwa Antifragile kilichoandikwa na Nassim Taleb. Isipokuwa kwenye eneo la fizikia, Taleb anadhani kwamba wasafiri, badala ya wanasayansi, ndio wanaowajibika na maendeleo ya aina nyingi ya “kisayansi.” Mhusika mkuu katika nadharia ya Taleb ni Steve Jobs, mtu aliyeacha elimu ya chuo na kuanza kutengeneza tarakirishi aina ya Apple katika karakana yake. Linapokuja suala la mgongano kati ya sayansi na Biblia, sina uhakika sana kama inasaidia kuwaambia wapagani, kama ambavyo Taleb angewaambia, “Nyie sio werevu vya kutosha na mnaongopa kuhusu mafanikio yenu!” Hata hivyo, kuna jambo kwenye madai ya kwamba sisi sio werevu sana kama tunavyodhani – hususan pale wanadamu wanaposhindana/wanapopingana na Mungu. Somo letu juma hili linahusu sababu za kuwepo kwa maarifa yetu yenye ukomo, kwa hiyo hebu tuzame kwenye somo letu ili tujifunze zaidi!
- Kama Mungu
- Soma Mwanzo 1:26 na Mwanzo 3:4-5. Angalia lugha ya “mtakuwa kama Mungu.” Je, Mungu na Shetani wana lengo moja kwa wanadamu? (Wote walisema kwamba wanadamu wanapaswa kuwa kama Mungu.)
- Mara kwa mara tunasema kwamba Hawa alitenda dhambi kwa sababu ya kiburi/majivuno na tamaa kwa sababu alitaka kuwa “kama Mungu.” Je, hii inawezaje kuwa dhambi wakati Mungu alitangaza kwamba alikuwa amewafanya wanadamu “kwa mfano wa Mungu?”
- Je, malengo ya Shetani na Mungu yanatofautianaje? (Mungu aliwafanya wanadamu kwa kufanana naye kwa kuwafanya wawe watawala na kuwapa uwezo wa kuunda maisha. Shetani aliwafanya “kufanana na Mungu” kwa kuwafungulia maarifa ya uovu.)
- Mada ya somo letu ni “Kupitia Kwenye Kioo, kwa Njia ya Fumbo.” Soma 1 Wakorintho 13:9-12. Kiyunani ambacho tafsiri ya Mfalme Yakobo (KJV) imetafsiri kuwa “kupitia kwenye kioo kwa njia ya fumbo,” wakati tafsiri ya NIV imetafsiri kuwa “uakisi hafifu kama unavyoonekana kwenye kioo.” Kwa nini njozi ya Mungu inayohusu sisi kuwa “kama Mungu” inajumuisha ukomo wa maarifa yetu?
- Soma 1 Wakorintho 13:13. Je, kauli hii ina chochote cha kujihusisha na jibu la swali lililotangulia?
- Soma Mwanzo 1:26 na Mwanzo 3:4-5. Angalia lugha ya “mtakuwa kama Mungu.” Je, Mungu na Shetani wana lengo moja kwa wanadamu? (Wote walisema kwamba wanadamu wanapaswa kuwa kama Mungu.)
- Njozi Ndogo
- Soma 1 Wakorintho 1:10-12. Je, asili ya tatizo ni ipi? (Wakristo wanaojihusisha na mtu badala ya kujihusisha na Yesu.)
- Kwa nini watu wana tabia ya kujihusisha na mtu badala ya kujihusisha na Mungu?
- Soma 1 Wakorintho 1:17. Ninapenda sana mahubiri mazuri. Je, Paulo anazungumzia nini hapa? (Hatutaki kuwaweka wanadamu kwenye nafasi ya Mungu.)
- Paulo anatumia kauli ya kufurahisha sana, “msalaba wa Kristo usije ukabatilika.” Je, uwezo wa msalaba ni upi?
- Soma 1 Wakorintho 1:18-20. Tumerejea kwenye mada yetu ya maarifa. Ninapowaangalia Musa na Paulo, ninawafikiria kama watu wawili werevu sana. Kwa nini Mungu awe kinyume na watu wenye busara na akili?
- Nukuu hii inatoka katika kitabu cha Isaya 29. Hebu tusome Isaya 29:11-12. Mungu alimpa Isaya maono. Isaya akayaandika kwenye gombo. Je, unafikiria nini kuhusu watu walivyoyachukulia yale maono? (Waliibua masuala ya kiufundi. Yamefungwa. Siwezi kuyasoma.)
- Je, walipaswa kusema nini? (Hebu tuyafungue. Hebu tumtafute mtu anayeweza kusoma. Ooh, Isaya, hebu tuambie kile yanachosema.)
- Soma Isaya 29:13. Je, tatizo la watu ni lipi? (Hawako makini kuhusu kuwa na uhusiano na Mungu.)
- Nukuu hii inatoka katika kitabu cha Isaya 29. Hebu tusome Isaya 29:11-12. Mungu alimpa Isaya maono. Isaya akayaandika kwenye gombo. Je, unafikiria nini kuhusu watu walivyoyachukulia yale maono? (Waliibua masuala ya kiufundi. Yamefungwa. Siwezi kuyasoma.)
- Hebu turejee kidogo kwenye 1 Wakorintho. Soma 1 Wakorintho 1:21. Tunatakiwa kufunga sehemu zilizolegea hapa. Katika kitabu cha Mwanzo tulijifunza kwamba Mungu alizuia maarifa fulani kwa wanadamu. Fungu hili linatuambia kuwa upungufu huu wa maarifa ni sehemu ya mpango wa Mungu (“maarifa ya Mungu”) ambao maarifa ya wanadamu yana ukomo.
- Kwa nini? Je, Mungu ni mpingaji wa maarifa?
- Je, ni aina gani ya “maarifa” ambayo watu waliionyesha katika Isaya 29? (Walikuwa wanajikita kwenye taarifa za kina. Mambo madogo madogo. Upungufu/kasoro za kibinadamu.)
- Soma Isaya 29:14. Je, suluhisho la Mungu kwa aina hii ya fikra ndogo ya mwanadamu ni lipi? (Atawang’arisha kwa maajabu!)
- Angalia kile tulichokisoma hivi punde katika 1 Wakorintho 1 na Isaya 29. Je, onyo hili linahusikaje kwetu hivi leo? Je, tunaona jambo hili sasa hivi?
- Miaka mingi iliyopita gari jipya lilikuwa linatambulishwa kwenye maonyesho ya magari. Lilipokuwa kwenye eneo ambapo linazungushwa zungushwa pande mbalimbali, niliona michubuko chini ya mlango. Kitu fulani kwenye mlango hakikuwa sawa, na viatu vya dereva viliharibu sehemu ya gari. Je, unadhani wauzaji wa gari walifikiria nini kuhusu maoni yangu? (Wanaojiita wasomi wanaonyesha mtazamo wa kisayansi wa umri wa vitu, taarifa zinazoibua hoja kuhusu suala la uumbaji. Mungu anaonyesha ukuu wa kila kitu!)
- Soma 1 Wakorintho 1:10-12. Je, asili ya tatizo ni ipi? (Wakristo wanaojihusisha na mtu badala ya kujihusisha na Yesu.)
- . Faida ya Maono ya Kiwango Kidogo
- Soma 1 Wakorintho 1:22-24. Hebu subiri kidogo! Je, Yesu hakufanya miujiza mingi? Je, kauli za Yesu sio za busara? (Ndiyo, Yesu alitenda miujiza na alishiriki nasi maarifa. Lakini, hilo halikuwa suala la msingi. Suala la msingi lilikuwa ni kwamba alikufa kwa ajili yetu.)
- Soma 1 Wakorintho 1:25. “Upumbavu wa Mungu” unarejea mafungu yaliyopita. Busara ya Mungu ilikuwa ni kumtuma Mwanaye, busara ya Kiyunani ilikuwa ni mantiki, na busara ya Kiyahudi ilikuwa ni uthibitisho wa kimiujiza. Je, busara ya Mungu ni ya kiwango cha juu kwa namna gani? (Hatuhitajiki kukabiliana na mambo kwa mtazamo mgumu. Mungu alikufa kwa ajili yetu. Hatuhitajiki kuwa na uwezo wa kuuelezea kimahesabu. Hatuhitajiki kuuthibitisha kivitendo.)
- Hebu turejeleze fikra yetu Edeni na kuangalia uchaguzi wa Hawa katika kitabu cha Mwanzo 3:3-5. Vipi kama Hawa angejikita kwenye kila jambo ambalo Mungu alilifanya kwa ajili yake, zawadi zote nzuri ajabu alizompa, kinyume na kile ambacho Mungu angeweza kuwa amekizuia?
- Tumia dhana hii kwenye mjadala wa uumbaji/uibukaji. Je, hoja gani inaendana na suala la uumbaji? (Kila kitu tukionacho – uwezo wa ajabu na umahiri ulio nyuma ya uendeshaji wa mbingu, dunia na miili yetu wenyewe.)
- Je, ni hoja gani iliyo nyuma ya uibukaji? (Nadharia ya kina iliyojengwa zaidi kwenye mambo tusiyoyaona.)
- Hebu tupitie tena 1 Wakorintho 1:17. Je, uumbaji unatuambia kuwa ni kwa jinsi gani tunapaswa kuhubiri injili? (Hatupaswi kuifanya kuwa ngumu. Hatupaswi kuifunika kwa “maarifa ya kibinadamu.” Badala yake, tunapaswa kuihubiri kama zawadi ya Mungu kwa wanadamu.)
- Soma 1 Wakorintho 1:26-28. Asante Paulo! Wengi wenu sio werevu, sio wenye ushawishi, sio watu wa kisasa, sio watu wenye nguvu. Nyie ni kundi la watu wenye akili dhaifu, miili yenye misuli dhaifu. Je, haya ni matokeo ya asili ya kuhubiri injili inayokinzana na usomi? Je, hili ndilo lengo, kuipelekea kwa watu wa jamii ya chini?
- Soma 1 Wakorintho 1:29. Je, sababu ya Mungu inayopingana na usomi, utamaduni, na uwezo/nguvu ni ipi? (Ili kwamba wanadamu wasijisifu.)
- Kwa nini Mungu anajali kama tunajisifu? (Kujisifu kunageuza mtazamo wetu mbali naye.)
- Soma Isaya 29:16. Je, ni kitu gani kinachotufunua kujifanya/kujisingizia kwetu? Kujisifu kwetu?
- Nadharia Kuu Yenye Kuunganisha Maono Hafifu
- Hebu tutafakari baadhi ya matumizi ya kile ambacho tumekuwa tukikijadili. Je, ni aina gani ya fikra iliyomfanya Hawa ahatarike kwa Shetani? (Fikra ya kwamba alihitajika kuwa na ufahamu zaidi. Fikra ya kwamba alipaswa kujikita kwenye uelewa (maarifa) wake, sio uelewa wa Mungu.)
- Je, ni aina gani ya fikra iliyofanya utendaji wa Yesu dhidi ya ule wa Wayahudi kuwa mgumu? (Walikuwa wanajiangalia wao wenyewe, na mkakati waliohitaji kuufuata ili waweze kuishi na kustawi. Angalia Yohana 11:49-50.)
- Soma 1 Wakorintho 1:30-31. Je, ni kitu gani ambacho kingewaokoa Hawa na Wayahudi? (Kuacha kujiangalia wao wenyewe na kumgeukia Mungu. Kama Hawa angeanza kuyasifia yale mambo ambayo Mungu aliyafanya, badala ya kujikita kwenye kile ambacho angekuwa na uhitaji nacho, Shetani angeshindwa.)
- Kama tulivyoona, waumini wengi wapya wa Paulo walikuwa wanatoka katika tabaka la chini la jamii. Je, hilo ni jema? (Faida nyingine ya ujumbe mwepesi kwamba Mungu alijitoa kwa ajili yetu, ili kwamba kila mtu aweze kuelewa hilo.)
- Kwa nini wasomi, matajiri na watu wenye nguvu wawe na uwezekano mdogo wa kukubali ujumbe rahisi wa injili? (Kwa sababu wana uwezekano mkubwa zaidi wa kujikita kwenye mambo yao. Wamezoea kuona watu wengine wakijikita kwao. Wanataka ujumbe unaojikita kwenye mambo yao, sio ujumbe rahisi unaoweza kueleweka na mtu yeyote na wenye kujikita kwa Mungu.)
- Rafiki, ujumbe wa Mungu ni kuwa ametupa uthibitisho wa kutosha kuamini kwamba yupo. Ametuonyesha upendo wake kwa kufa ili tupate uzima wa milele. Je, utadhamiria kumtumaini Mungu na hutasisitiza kwamba kila jambo lielezewe kwako? Je, utakubali kwamba wewe ni udongo na sio mwenye kuchezacheza na kazi bila kuwa na umakini?
- Juma lijalo: Yesu, Mfadhili na Mhimili.