Somo la 1: Baadhi ya Kanuni za Unabii

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yeremia 9, Mathayo 13, Danieli 12, Ufunuo 22
Swahili
Year: 
2025
Quarter: 
2
Lesson Number: 
1

Somo la 1: Baadhi ya Kanuni za Unabii

(Yeremia 9, Mathayo 13, Danieli 12, Ufunuo 22)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Tunaanza mfululizo mpya wa masomo kuhusu unabii. Una mtazamo gani juu ya unabii wa Biblia? Unadhani kuwa unauelewa, wakati wengine wengi hawauelewi? Unadhani ni kupoteza muda kujifunza unabii huo? Hoja bora kabisa ya kujifunza unabii wa Biblia ni sura ya pili ya kitabu cha Danieli. Katika sura hiyo Danieli anatafsiri njozi ya Mfalme Nebkadreza inayoweka bayana historia yote ya sayari dunia! Wakati historia yetu bado haijakamilika, miaka 2,000 ya kwanza baada ya njozi ilitabirika kikamilifu! Hoja bora ya kuwa mtu wa kushuku, au angalao kuwa na tahadhari kuhusu unabii wa Biblia, ni kwamba sehemu kubwa ya somo letu la robo hii inahusu ujio wa Yesu Mara ya Pili. Wasomi wa Biblia walikosea ujio wa Yesu mara ya kwanza, hivyo kwa nini tudhani kuwa tunaweza kuupatia ujio wake wa Mara ya Pili? Bila kujali mtazamo wako wa sasa juu ya unabii wa Biblia, fuatana nami tunapochimbua mada hii!

  1.    Kumwelewa Mungu
    1.    Soma Yeremia 9:23. Mungu anasema kuwa tusijisifu juu ya nini? (Hekima, nguvu, au fedha zetu.)
    1.    Soma Yeremia 9:24. Tujisifie nini? (Kwamba tunamjua Mungu.)
      1.    Unadhani inamaanisha nini “kumjua Mungu?” Kwamba sisi ni marafiki? Au, tunajua kwamba Mungu anafurahia upendo, haki, na usawa? (Kwa sababu Mungu anaelezea taarifa za kina kuhusu tabia yake, inaonekana anamaanisha yote mawili.)
    1.    Soma Isaya 55:6-9. Tuna matatizo ya namna gani katika kumtafuta na kumjua Mungu? (Fikra yake haipo katika ligi yetu. Ni mwerevu zaidi kuliko sisi.)
      1.    Kwa nini basi Mungu anatupatia wito wa kutafuta kumjua?
    1.    Soma Mathayo 13:10-11. Unalielewaje jibu la Yesu kwenye sababu ya yeye kuzungumza na watu kwa mifano? (Yesu anataka baadhi waelewe na wengine wasielewe.)
      1.    Kwa nini Yesu atake mtu yeyote asielewe bayana? (Soma Mathayo 13:14-15. Yesu hashangilii suala la kushindwa kuelewa. Bali anasema kuwa baadhi ya watu hawataki kuelewa.)
    1.    Soma Mathayo 13:12-13. Je, Yesu anasema kuwa baadhi ya watu si werevu sana, wagumu kusikia, au wana uoni hafifu? Ikiwa hilo ni kweli, basi kwa hakika si kosa lao kwamba hawaelewi, sawa? (Si kweli. Yesu anasema kuwa uwezo wa kuelewa kile anachokifundisha kinageukia kwenye mtazamo wa wasikilizaji. Kama wanasoma ili kujifunza, basi watapewa uelewa mkubwa. Lakini kama hujali kuhusu uelewa, basi utapoteza hata uelewa mdogo ulio nao.)
    1.    Soma Matendo 1:6-9. Una maoni gani juu ya swali lililoulizwa na wanafunzi mara Yesu alipokuwa anakaribia kurejea mbinguni? (Kama ningekuwa Yesu ningeanza kuwafokea! Baada ya kipindi chote walichokuwa pamoja naye, bado hawakuelewa kwamba hakuwa akielekea kuwaangusha Warumi na kuirejesha Israeli kama bwana juu ya wakandamizaji wao wa Kirumi.)
      1.    Wanafunzi walikuwa na uelewa kiasi gani juu ya mustakabali ujao? (Walikataa kuachana na imani yao ya kinabii ya kawaida ya Wayahudi kwamba Masihi ataanzisha ufalme wa kidunia.)
        1.    Ninawafahamu watu wengi ambao wana uhakika kabisa kuwa wanaelewa unabii kuhusu matukio ya siku za mwisho. Wanafunzi walitumia zaidi ya miaka mitatu wakimsikiliza Yesu. Ikiwa hilo halimfanyi mtu kuwa na tahadhari juu ya kiburi chake katika kuuelewa unabii, hiyo inakuambia nini kuhusu mtu huyo? (Mtu huyo ni mpumbavu.)
    1.    Unadhani ni nini ulio msingi wa kuuelewa unabii? (Mathayo 13:12 inaashiria kuwa tuwe makini nao na kuuchukulia kwa dhati. Kufanya kazi kwa bidi kuuelewa. Wakati huo huo Mungu ni Mungu na sisi si Mungu. Lazima tuelewe mipaka yetu.)
  1.   Nyamaza au Funguka?
    1.    Soma Danieli 12:1-3. Jambo gani linajadiliwa hapa? (Ujio wa Yesu Mara ya Pili.)
    1.    Soma Danieli 12:4. Unadhani inamaanisha nini “kuyafunga maneno na kukitia muhuri kitabu?” (Soma Isaya 29:11. Hii inamaanisha kuwa kitabu hakipaswi kueleweka hadi katika kipindi fulani kijacho.)
    1.    Soma Danieli 12:8-9. Je, Danieli alielewa? (Hapana. Alitaka kuelewa, lakini aliambiwa maneno yalikuwa “yamefungwa na kutiwa muhuri hata wakati wa mwisho.”)
      1.    Tunaposoma kuwa “maneno” yatatiwa muhuri, je, ni ya kitabu chote cha Danieli? (Soma Danieli 2:44-45. “Maneno” hayawezi kuwa yanarejelea kitabu chote cha Danieli kwa sababu njozi muhimu ya unabii wa Nebukadreza “inajulikana” dhahiri, na tafsiri yake ni “thabiti.”)
    1.    Soma tena Danieli 12:1. Je, “wakati wa taabu” ni sehemu ya maneno yaliyotiwa muhuri na kunyamazishwa? (Sijui. Kilicho dhahiri ni kwamba kitabu chote cha Danieli hakikutiwa muhuri.)
    1.    Soma tena Danieli 12:3. Hii inamwelezea nani? (Kabla tu ya kauli inayohusu kutia muhuri, tunasoma kauli hii inayohusu “nyota” inayowaongoa wengine. Aina fulani ya uelewa wa Mungu inaongezeka.)
    1.    Soma Mathayo 24:15-16. Nani anayezungumza? (Yesu.)
      1.    Yesu anamnukuu nani? (Analihusianisha hili na Danieli. Ninapendekeza Danieli 9:27.)
      1.    Hii inatuambia nini kuhusu kitabu chote cha Danieli kutiwa muhuri? (Yesu anasema kuwa wasikilizaji wake wanapaswa kuangalia unabii wa Danieli wa kuponyesha Rumi kuliangamiza hekalu la pili la Kiyahudi!)
    1.    Mwanamaoni mmoja alibainisha kazi ya kinabii ya William Miller, ambaye alitabiri dunia itafikia ukomo wake mwaka 1843-44, kama mfano wa muda wa kutengua muhuri pale ambapo “maarifa yataongezeka” (angalia Danieli 12:4). Una maoni gani? Je, kuelewa unabii isivyo sahihi kwa dhahiri (kwa sababu ujio wa Mara ya Pili haukutokea mwaka 1843-44) ni mfano wa maneno kutiwa muhuri au kutotiwa muhuri?
      1.    Kwa kutokuwa na uhakika juu ya lini sehemu ipi ya kitabu cha Danieli haitatiwa muhuri, tunapaswa kuwatizamaje wale wanaodai kuwa sahihi kuhusu unabii wa siku za mwisho? (Kama historia haitoshi (kwamba watu wa Mungu hawakuelewa vizuri ujio wa Yesu mara ya kwanza), kifungu hiki kinachohusu utiaji muhuri kinatoa tahadhari ya ziada dhidi ya kuwa na kiburi kuhusu unabii wa Biblia.)
    1.    Soma Ufunuo 22:10-11. Malaika alimwambia nini Yohana kuhusu kutia muhuri unabii wa Ufunuo? (Aliambiwa asiutie muhuri. Unabii huo unapaswa kueleweka sasa hivi.)
      1.    Kwa nini kitabu cha Ufunuo hakitiwi muhuri na Danieli kinatiwa muhuri? (Yohana anaandika kuwa “wakati umekaribia.”)
        1.    Je, hiyo inamaanisha kuwa Danieli anapaswa kueleweka baada ya kipindi cha kuandikwa kwa Ufunuo?
        1.    Danieli na Ufunuo vinaelezea mada zinazofanana kwa kiasi fulani. Kwa nini mmoja atiwe muhuri na mwingine asitiwe muhuri?
    1.    Hivi karibuni nilisikiliza mhadhara unaohusu maneno “wakati umekaribia” na kauli zinazofanana na hiyo zilizotolewa katika Agano Jipya. Kwa mtazamo wa kibinadamu kipindi cha ujio wa Mara ya Pili ni angalao miaka elfu mbili baadaye. Mhadhiri alijenga hoja kwamba neno “umekaribia” halikurejelea chronology – mfuatano wa muda -  (kuhesabu muda), bali lilirejelea kutotarajiwa. Hoja yake ilijengwa juu ya tafsiri ya kiutamaduni ya lugha ya asili. Alionekana kuwa na ushawishi, na ninauelewa mdogo sana kiasi cha kuweza kutathmini uelewa wake wa lugha ya asili. Lakini uelewa huo unaendana na kile kilichotokea tangu awali. Kama hutarajii Yesu kuja sasa hivi, na akaja, muda umekaribia.
  1.      Wajibu Wetu Katika Kufunguka
    1.    Soma 2 Petro 1:19-20. Kama tunapaswa kuepuka kiburi kuhusu unabii, tunatakiwa kufanya nini? (Tunapaswa kuwa makini!  Tunapaswa kujifunza unabii ili kuuelewa na kubainisha kile ambacho hakijatiwa muhuri.)
      1.    Ni wapi mahala petu pa kuanzia kama wanafunzi wa unabii? (Ni kama vile tuna taa mahali penye giza.)
        1.    Hilo lina ufanisi kiasi gani katika kuona taswira yote? (Si sana. Lakini ni mwanzo.)
      1.    Taa yetu inakuwaje? (Pambazuko la asubuhi.)
        1.    Hii inaashiria nini kuhusu maarifa yetu yaliyoongezeka? (Uelewa wetu uliongezeka kwa kasi!)
    1.    Angalia tena 2 Petro 1:20. Katika kujifunza unabii, hii inatoa mwelekeo gani? (Unabii wa Biblia umevuviwa na Mungu. Tunatakiwa kuweka msitari wa wazi unaotofautisha kati ya kile kinachosemwa na Biblia na kile ambacho mtu anayeitafsiri biblia anakisema.)
    1.    Soma 2 Petro 1:21. Tunawezaje kuwa na ujasiri katika unabii wa Biblia? (Umetoka kwa Mungu. Tunaweza kujiamini sana. Tafsiri ya unabii ni jambo jingine. Tunatakiwa kuwa na Roho Mtakatifu akimvuvia mtafsiri.)
    1.    Rafiki, tunatakiwa kuwa wanafunzi makini na madhubuti wa unabii ambao Mungu ametupatia. Je, utaungana kwenye safari hii ili kuuelewa unabii wa Biblia vizuri zaidi?
  1.   Juma lijalo: Msingi wa Kitabu cha Mwanzo.