Somo la 7: Tatizo la Wokovu
Somo la 7: Tatizo la Wokovu
(Mwanzo 1-4, Ayubu 1 & 23, Warumi 8)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Katika sheria ya Marekani tunaiita “usimamizi wa kizembe.” Inamaanisha kuwa mtu au kampuni inayosimamia eneo fulani imeshindwa kuwalinda kikamilifu watu waliopo katika maeneo hayo wasipate madhara. Suala linajitokeza katika eneo la kazi, katika maduka makubwa ya biashara, au mahala popote ambapo mtu fulani anasimamia mazingira uliyopo. Je, Mungu ana hatia ya usimamizi wa kizembe? Tuna uovu wa kutisha ulimwenguni na Mungu ndiye mwenye mamlaka ya ulimwengu. Je, wajibu unakoma kwake? Je, tuko kwenye nafasi ya kuhukumu? Mungu anasema nini juu ya usimamizi wake wa ulimwengu na tatizo la uovu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujionee! Kumbuka kwamba hatutaingia kwa kina kuhusu chanzo cha uovu ulimwenguni, bali uovu unaodhuru dunia yetu.
- Janga Edeni
-
- Soma Mwanzo 1:31. Dunia ilikuwa na hali gani Mungu alipoiumba kwanza? (“Ilikuwa njema sana.”)
-
- Soma Mwanzo 3:1-3. Nani alimfanya nyoka huyu? Nani aliyemfanya Eva? Nani aliyeufanya mti uliokatazwa? (Mungu alivifanya vyote vitatu.)
-
- Soma Mwanzo 3:4-7. Enyi wanafunzi wa Biblia, jambo gani limetokea hapa? (Dhambi imeuingia ulimwengu wa wanadamu. Huu ndio mwanzo wa uovu kwa wanadamu.)
-
- Soma Mwanzo 4:3-8. Ni nini nia ya Kaini ya kumwua nduguye Habili?
-
-
- Hawa ni watoto wa kwanza wa Adamu na Eva. Uovu wa mauaji unajionesha katika kizazi cha kwanza baada ya ukamilifu!
-
- Jinsi Janga Lilivyoibuka
-
- Hivi punde tumesoma taswira ya jinsi wanadamu walivyotenda dhambi na hivyo kuukaribisha uovu duniani. Uovu huu unajidhihirisha wenyewe pale mzaliwa wa kwanza anapomwua mzaliwa wa pili wa wanandoa wa kwanza waliokuwa wakamilifu! Unalielezeaje jambo hili?
-
- Soma Mwanzo 2:9. Miti hii miwili ilichipushwa sehemu gani? (Katikati ya Bustani ya Edeni.)
-
-
- Nini lililokuwa lengo la mti wa uzima?
-
-
-
- Nini lililokuwa lengo la mti wa ujuzi wa mema na mabaya?
-
-
-
-
- Kwa nini miti hii ilikuwa sehemu moja?
-
-
-
-
-
- Kwa nini unavutiwa kwenda karibu na mti uliozuiliwa unapotaka kula kutoka kwenye mti wa uzima?
-
-
-
-
-
- Kwa nini Mungu hakuuweka mti uliokatazwa nje ya bustani? Au angalao sehemu ya mbali ya bustani?
-
-
-
-
- Kama utaliangalia jambo hili kwa mantiki, utatoa jibu gani kuhusiana na eneo ilipowekwa miti hii miwili? (Hii haikuwa ajali. Mungu aliiweka pamoja kwa makusudi.)
-
-
-
-
- Je, hii inamaanisha Mungu aliibuni Edeni ili wanadamu waanguke?
-
-
- Ayubu
-
- Ayubu anatupatia taarifa nyingi kuhusu jinsi Mungu alivyouumba ulimwengu. Hebu tuangalie Ayubu anatufundisha jambo gani jingine kuhusu mwanzo. Soma Ayubu 1:6-8. Kwa nini Mungu alimwuliza Shetani swali hili? (Kwa sababu Shetani alidai kuwa aliitawala dunia.)
-
- Soma Ayubu 1:9-12. Shetani anajenga hoja kwamba utii wa Ayubu kwa Mungu unatokana na sababu gani? (Mungu anamlinda na kumbariki Ayubu.)
-
-
- Shetani anasema jambo gani hasa? (Ayubu hampendi Mungu, Ayubu anapenda mafanikio.)
-
-
- Vifungu hivi vinatuambia nini kuhusu mitazamo ya Mungu na Shetani kuhusiana na ulimwengu? (Mitazamo inashindana. Inashindania utii wa wanadamu.)
-
-
- Kitabu cha Ayubu kiliandikwa katika kipindi kipi? (Kiliandikwa baada ya Adamu na Eva kutenda dhambi kwani hiyo ndio sababu Shetani anadai utawala wa ulimwengu. Wakati huo huo inaonekana kuwa ni kipindi cha awali cha utawala wa Shetani, kwani inaonekana kuwa ni baada ya taarifa ya Ufunuo 12:7-9 kwamba Shetani alitupwa kutoka mbinguni, lakini bado aliruhusiwa kutembelea.)
-
-
-
- Je, mitazamo ya Mungu na Shetani ni udhihirisho wa mitazamo ya Mungu na Shetani wakati wa uumbaji wa Bustani ya Edeni?
-
-
-
-
- Je, mahali palipochipushwa miti miwili pale Edeni ni shindano lililokubaliwa kwa pamoja kama ilivyokuwa kwa mashambulizi juu ya Ayubu?
-
-
- Kuelekea Kwenye kwa Nini
-
- Angalia tena Ayubu 1:9. Ni muhimu kiasi gani kwa Mungu kwamba msingi wa uhusiano kati ya Mungu na Ayubu ni “upendo” na si “vitu?”
-
-
- Chukulia kwamba changamoto hiyo iliibuliwa kwa kuzingatia mtazamo wa watoto wako kwako?
-
-
-
- Chukulia kwamba changamoto hiyo iliibuliwa kwa kuzingatia mtazamo wa mwenzi wako mwenye umri mdogo zaidi kuliko wewe? Jibu ni la muhimu kiasi gani?
-
-
- Soma Warumi 8:38-39. Upendo wa Mungu una nguvu kuliko nini? (Chochote kinachoweza kututenganisha naye.)
-
- Soma Warumi 8:31-34. Mungu amefanya nini ili kuwa na uhusiano wa upendo nasi? (Yesu aliteswa na kuuawa ili tuweze kuwa na uhusiano naye.)
-
- Soma Mwanzo 1:26-28. Sampuli ya asili ya wanadamu ni ipi? (Mungu!)
-
-
- Tusingepewa uhuru wa kuchagua, je, tungefanana na Mungu? (Roboti “haifanani” na sisi ikiwa ipo chini ya udhibiti wetu.)
-
-
-
- Rejea nyuma kwenye mjadala wetu kuhusu makubaliano ya shindano pale Edeni. Fikiria kuhusu makubaliano ya shindano kwa ajili ya Ayubu. Mungu alikuwa anatafuta nini katika kila moja kati ya mashindano haya mawili? (Kwamba Adamu, Eva, na Ayubu watamchagua Yeye kutokana na upendo, na si kwa sababu Mungu aliwapatia vitu.)
-
-
-
- Je, uhuru wa kuchagua ni wa msingi kwa ajili ya upendo wa kweli?
-
- Kwa Nini Isiyowezekana?
-
- Soma Ayubu 23:3-4 na Ayubu 31:35-37. Ayubu anataka nini? (Ayubu anasema anataka Mungu amsikilize. Baadaye anasema anataka kumshtaki Mungu. Tatizo ni kwamba Ayubu hana mtu aliye juu ya Mungu anayeweza kumfanya Mungu aelezee kwa nini Ayubu anateseka na kisha atoe uamuzi/hukumu. Ayubu anasema kuwa mateso yake si ya haki.)
-
- Soma Ayubu 38:1-3 na kisha upitie kwa haraka haraka sura yote na sura ya 39. Mungu anatoa jibu gani kwa mashtaka yaliyoibuliwa na Ayubu? Je, Mungu anaeleza kwa nini Ayubu anateseka? (Kimsingi Mungu anasema, “Mimi ni Mungu na wewe si Mungu.” Vifungu vinavyofuatia baada ya Ayubu 38:2 ni mwendelezo wa ufafanuzi wa kwa nini Ayubu ni mtu mjinga.)
-
- Soma Ayubu 40:1-5. Ayubu anajibuje? (Ayubu anakubali kwamba yeye si Mungu na atakaa kimya kuhusu kuleta mashtaka dhidi ya Mungu. Kisha Mungu anatumia sura ya 40 na sura ya 41 kuendelea kusema kuwa wanadamu hawana uwezo wa kuelewa kile ambacho Mungu anakielewa.)
-
-
- Una maoni gani juu ya jibu la Mungu? Je, yanafanana na kile walichokisema wazazi wako, “Fanya kwa sababu nimekuambia ufanye.” Hakuna ufafanuzi uliohitajika. (Kamwe Mungu hamwelezei Ayubu chochote zaidi ya ujinga wa Ayubu.)
-
-
- Hebu tutulie kidogo na tutafakari jambo hili. Je, Mungu alikuwa na jibu jepesi ambalo angeweza kumjibu Ayubu? (Ndiyo. Hili lilikuwa shindano lililokubaliwa na pande mbili.)
-
-
- Je, Ayubu angeweza kulitilia maanani jibu hili? (Sidhani kama angeweza.)
-
-
-
- Kitabu cha Ayubu ni sehemu ya Biblia kwa sababu Mungu anataka tujue jibu la kweli la kwa nini Ayubu aliteseka. Kwa nini anatupatia jibu na si Ayubu aliyeteseka zaidi?
-
-
- Tulianza somo hili kwa ahadi ya kujaribu kubaini sababu ya uovu kuwapo katika ulimwengu huu na endapo Mungu anawajibika kwa uovu huo. Kisha tukasoma vifungu kadhaa vilivyotupendekezea majibu. Jibu gani ni bora na la moja kwa moja? (Kaa chini na ukae kimya. Mungu ni Mungu na sisi si Mungu. Wakati Mungu anatuelezea mazingira ya Ayubu (ambayo kwa maoni yangu pia yanafafanua mazingira ya Edeni), jibu bora ni kwamba hatuna uelewa wa Mungu na tunatakiwa kufahamu tu kwamba anatupenda. Lazima tumwamini hata kama inaleta mantiki au haileti.)
-
- Rafiki, Mungu alikufa kwa ajili yako. Mungu alikuumba wewe pamoja na ulimwengu wako. Je, utamwamini?
- Juma lijalo: Uhuru wa Kuchagua, Upendo, na Majaliwa ya Mungu.