Somo la 13: Hitimisho : Kumjua Yesu na Neno Lake

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 21
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
4
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Hitimisho : Kumjua Yesu na Neno Lake

 

(Yohana 21)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Hivi karibuni, mkufunzi wangu alinisaidia kujifunza na kuboresha ujuzi wangu. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuepuka kusababisha madhara. Lengo la mkufunzi wangu lilikuwa ni kunifundisha kufanya mambo kwa usahihi na usalama. Kama nilikuwa na mwenendo mbaya, alitaka kurekebisha tabia hizo mbaya. Baada ya Yesu kufufuka katika wafu na kushangiliwa Mbinguni, alirejea duniani ili kuwapa wanafunzi wake maelekezo ya mwisho. Ilikuwa jambo la muhimu kuyafanya mambo hayo kwa usahihi. Petro na Yohana ni watu muhimu miongoni mwa wanafunzi na Petro anahitaji hatua za kufanyiwa marekebisho. Hebu turejee kwenye somo letu la mwisho katika kitabu cha Yohana na tuone jinsi Yesu anavyowasaidia watu kama sisi wanaohitaji maboresho!

  1.    Kuoka Samaki
    1.    Soma Yohana 21:1-3. Je, hili linakushangaza? Baada ya kifo na kufufuka kwa Yesu wanafunzi wamerejea kwenye uvuvi? (Soma Marko 16:7. Yesu aliwaelekeza warejee Galilaya. Tiberia ulikuwa mji mkuu wa Galilaya.)
      1.    Unadhani wanafunzi walijisikiaje wakati wa asubuhi? (Walivunjika moyo kwamba wamevua usiku kucha bila kupata chochote. Hii ni nyongeza ya kutokuwa kwao na uhakika kwa ujumla kuhusu mustakabali wao.)
      1.    Je, bado Petro ni kiongozi miongoni mwa wanafunzi?
    1.    Soma Yohana 21:4-5. Kwa mtazamo wa wanafunzi mawazoni mwao, unadhani walipenda kuitwa “wanangu?” (Robertson’s Word Pictures inataarifu kuwa hii ni sawa na Yesu kusema, “Vijana wangu.” Na Robertson anasema Yesu pekee ndiye aliyetumia neno hilo kwa wanafunzi wake.)
    1.    Soma Yohana 21:6. Kwa nini wanafunzi wanakubali ushauri wa kuvua kutoka kwa mtu aliyesimama ufukweni? (Bado walikuwa hawajatambua kuwa huyu ni Yesu. Lakini neno alilolitumia Yesu kuwaita ni neno linalotumiwa na mtu mkubwa kwa watu wa chini. Inawezekana wanafunzi walidhani kuwa huyu ni mtu mzima mwenye busara aliyejua mambo mengi ya uvuvi. Hivyo walitii.)
      1.    Na kwa nini upande wa chombo liwe jambo la kuzingatiwa? (Pande za chombo hazikuwa na maana yoyote. Kilichokuwa cha muhimu ni endapo wanafunzi walikuwa wanatenda kazi chini ya maelekezo ya Yesu au walikuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia kipawa chao.)
      1.    Unadhani kwa nini wanafunzi hawakumtambua Yesu? (Kulikuwa na giza.)
    1.    Soma Yohana 1:4-5. Je, hili ni “kumbusho” la mwanzo wa injili ya Yohana?
    1.    Soma Yohana 21:7. Unadhani ni kwa nini Yohana pekee (“mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda”) ndiye aliyemtambua Yesu? Je, ni kwa sababu yeye ndiye mdogo kuliko wote na macho yake yanaona vizuri? (Yohana alipewa ishara mbili za kumpa sababu ya kumwangalia mgeni huyu kwa ukaribu. Kwanza, aliongea nao kama alivyofanya Yesu. Pili, walipata samaki wengi kimaajabu kutokana na kufuata ushauri wa mtu huyu mgeni.)
      1.    Unadhani ni kwa nini Petro pekee ndiye aliyejitupa majini na kuogelea hadi ufukweni ili kukutana na Yesu?
    1.    Soma Yohana 21:8. Kwa nini wanafunzi wengine walipendelea kuwaleta samaki nchi kavu? (Yohana anaandika maelezo haya. Ndiye aliyemtambua Yesu kwanza, lakini hakujitupa majini kama alivyofanya Petro. Ninadhani maoni ya Yohana kwamba “hawakuwa mbali na nchi kavu” ndio sababu yake ya kutoenenda kama Petro. Hawakuchelewa sana, na waliweza kuwahifadhi samaki.)
    1.    Soma Yohana 21:9-10. Tayari Yesu anaandaa kifungua kinywa. Kwa nini? (Anatimiza mahitaji ya kimwili ya wanafunzi.)
    1.    Soma Yohana 21:11. Kwa nini Petro anarejea chomboni kuwavuta samaki? (Hii inaashiria walihitaji nguvu zake au ujuzi wake.)
      1.    Kwa nini tunaambiwa kuhusu ukubwa na idadi ya samaki waliovuliwa? (Hizi ni taarifa zinazobainisha kuaminika kwa maelezo yaliyotolewa.)
    1.    Soma Yohana 21:12-13. Unaelezeaje maoni ya kwamba hakuna aliyeuliza kuhusu utambulisho wa Yesu? Tayari Yohana amekwishamtambua Yesu. (Huenda bado wanaendelea kuzoea suala la Yesu kufa na sasa yu hai. Huenda Yesu amebadilika kwa namna fulani baada ya kurejea mbinguni.)
      1.    Tofauti na wanafunzi kuwa na njaa, je, unaweza kufikiria sababu nyingine yoyote ya Yesu kuwaokea samaki? Je, kuna fundisho lolote kwa kufanya hivyo? (Hii inaturejesha kwenye suala la endapo Yesu amefufuka. Yeye si mzimu. Anakula chakula kama alavyo mwanadamu.)
    1.    Soma Yohana 4:48. Je, hii ndio sababu Yesu alipangilia uvuaji huu mkubwa – ili waweze kuamini kuwa ni yeye?
  1.   Petro
    1.    Soma Yohana 21:15. Hiki ndicho wanasheria wanachokiita “leading question.” Jinsi swali lilivyoulizwa linaashiria jibu. Yesu anaashiria jibu gani? (Kama Petro angejibu tu kwamba, “Ndiyo,” angedai kuwa anampenda Yesu zaidi kuliko wanafunzi wengine.)
      1.    Hivi punde tu Yesu amejitupa wa kwanza kutoka chomboni ili kumwona Yesu. Tumeona kwamba alihitajika katika kulivuta jerife. Tunakumbuka kuwa hapo awali Petro aliamini kuwa alimpenda Yesu zaidi kuliko wanafunzi wengine. Mathayo 26:33. Je, mtazamo wa Petro wa upendo wake wa hali ya juu umebadilika? (Kwa busara Petro analiweka upya swali la Yesu ili kusema tu kwamba anampenda Yesu.)
    1.    Soma Yohana 21:16. Je, Yesu anamdhihaki Petro? Yesu anatoka kumkumbusha Petro kwamba alikuwa akidai kuwa alipenda zaidi, hadi sasa kuashiria kuwa Petro hampendi Yesu kabisa!
    1.    Soma Yohana 21:17. Yesu anakuwa na mjibizo gani kwa kuulizwa mara ya tatu kuhusu kumpenda Yesu? Kumbuka kwamba mara mbili zote za awali Petro alimwambia Yesu kuwa anampenda. (Petro “anahuzunika.” Hafurahii kwamba Yesu haonekani kuliamini jibu lake.)
      1.    Kwa nini Yesu alimwuliza Petro mara tatu? Je, alikuwa anamwadhibu Petro kwa majivuno yake ya awali kwamba alimpenda zaidi? (Utakumbuka katika Yohana 13:38 Yesu alitabiri kwa usahihi kwamba Petro atamkana mara tatu.)
    1.    Utaona kwamba kuanzia Yohana 21:15 mara tatu Yesu anamwambia Petro awalishe kondoo wake. Unalihusisha hili na umuhimu gani, ikiwa upo? (Yesu anamrejesha Petro kwenye kiongozi. Kazi ni kuwalisha kondoo na Petro anastahili kazi hiyo.)
      1.    Tulianza kwa maelekezo ya Yesu baada ya kufufuka. Petro amefundishwa nini? (Unyenyekevu na msamaha.)
  1.      Fokasi (Focus)
    1.    Soma Yohana 21:18-19. Hii inaonekana kama utabiri kwa watu wengi wanaozeeka. Je, Yesu anamwambia Petro kwamba atazeeka sana? (Hapana. Yesu anamwambia Petro kuwa atasulubiwa.)
      1.    Yesu anamaanisha nini anaposema, “Nifuate?” (Petro atamfuata Yesu hadi msalabani.)
      1.    Yesu anamfundisha nini Petro kuhusu mustakabali wake usiofanana na siku zake za nyuma? (Petro atasalia kuwa mwaminifu kwa Yesu. Atakufa kwa ajili ya Yesu, kama alivyoahidi Petro hapo kabla.)
    1.    Soma Yohana 21:20-21. Kwa nini Petro aliuliza swali hili? (Tafakari kwamba Yohana ndiye mwanafunzi pekee aliyemfuata Yesu hadi msalabani. Ingawa hapo awali Petro alidai kumpenda Yesu zaidi kuliko wanafunzi wengine, bado Yohana anajiita “mwanafunzi aliyependwa na Yesu.” Ubashiri wangu ni kwamba Petro anamchukulia Yohana kama mshindani wa upendo wa Yesu na anataka kujua jinsi mambo yatakavyombadilikia Yohana.)
    1.    Soma Yohana 21:22. Ungeliwekaje jibu la Yesu katika lugha ya leo? (Endelea kujizingatia (stay focused). Baki kwenye msitari wako. Usiwe na wasiwasi juu ya mustakabali wa Yohana.)
      1.    Je, bado huo ni ushauri mzuri kwetu? Usijihangaishe na mafanikio ya Wakristo wengine? (Hili ni fundisho muhimu kwa kila mtu na fundisho gumu kwangu. Mara zote nimekuwa mshindani. Lengo ni kufanya vizuri kuliko wengine. Biblia inafundisha ubora binafsi kwa njia ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Jikite katika kuboresha kazi yako kwa ajili ya Mungu.)
    1.    Soma Yohana 21:23. Je, Yesu anaashiria kuwa anaweza kurejea katika kipindi cha uhai wa Yohana? Kwa nini?
  1.   Hitimisho
    1.    Soma Yohana 21:24. Kwa nini Yohana anasema kuwa tunapaswa kuamini kile alichokiandika katika injili yake? (Yeye ni mtu mwaminifu.)
      1.    Unamtafakarije Yohana kutokana na kujifunza injili yake? (Ni mtu mwema. Nina hisia mchanganyiko juu ye yeye kujiita, “mwanafunzi aliyependwa na Yesu.”)
    1.    Soma Yohana 21:25. Yesu anatuambia kuwa mambo mazuri aliyoyafanya Yesu ni mengi sana kuweza kuandikwa yote. Hiyo inaashiria nini kuhusu alichokiandika Yohana? (Kwamba aliandika mambo ya muhimu zaidi kwa ajili ya sisi kuyafahamu.)
    1.    Rafiki, Tulianza Injili ya Yohana kwa mtazamo kwamba Yohana alitaka kutushawishi kuwa Yesu ni Mungu aliyekuja duniani. Yesu ni Masihi aliyesubiriwa kwa muda mrefu. Je, umeshawishika? Kwa nini usiwe mtiifu kwa Yesu sasa hivi?
  1.    Juma lijalo: Tunaanza mfululizo mpya kuhusu asili ya upendo wa Mungu. Mfululizo wa masomo hayo una kichwa kisemacho, “Upendo na Haki ya Mungu.”